Ukweli ni upi : Alexander the Great akiwa INDIA

View attachment 814513
Habari za jioni wakuu bila kupoteza muda niende moja kwa moja kwenye mada

Natumaini wote tumeshasikia mengi sana kuhusu alexander the great ila kuna mambo machache yananitatiza na tusaidiane kujuzana kuhusu mtawala huyu.

ALEXANDER NI NANI
View attachment 814519

Alexander III wa Macedonia alizaliwa 20/21 July 356 BC na kufariki 10/11 June 323 BC (Miaka 33) maarufu kama Alexander the Great aliyekuwa mfalme wa nchi ya makedonia iliyokuwa ndani ya ufalme wa kigiriki na alitumia muda wake mwingi wa maisha kupigana vita za kuteka miji mbalimbali ili kuongeza ufalme wake

UMAARUFU WAKE
View attachment 814517

Umaarufu wake ulikuja baada ya kuwa mwanajeshi asiyewahi kushindwa vitani na kufikia umri wa miaka 30 alikwisha angusha falme zote kubwa zilizokuwa tishio kati ulimwengu wa kale akitandika mataifa makubwa kuanzia ulaya,Afrika hadi Asia hivyo anatazamiwa kuwa commander bora zaidi wa kijeshi katika historia.

ALEXANDER AKIWA INDIA
baada ya kupata picha kidogo ya nani anazungumziwa twende moja kwa moja kwenye swali langu JE NINI KILITOKEA KWA ALEXANDER INDIA
View attachment 814512


Alexander baada ya kuvamia ufalme wa uajemi na kuutandika alielekea India akiwa na ndoto za kuifikia china hivo kutawala Asia nzima. Lakini kuna vita ilipiganwa kati yake na mfalme Puru/porus iliyozaa utata mkubwa.

1. Kwa upande wa wazungu wanadai Alexander alimpiga mfalme Porus na kwamba aliposhinda alimuona Porus ni mzuri vitani sababu alimpa ushindani hivyo akaamua kumrudishia ufalme wake wa hilo eneo aliloteka na alexander akaamua tu kugeuza kurudi uajemi baada ya wanajeshi wake kuweka mgomo kuwa wamechoka!!

2. Kwa upande wa wahindi wanadai alexander alipigwa sana na Puru hivyo akaamua kuomba poo na kusaini naye mkataba wa amani maana alisikia kwamba huko mbele kuna falme zina jeshi la tembo elfu 5000 wakati Puru alitoa upinzani kwa tembo 100 tu hivyo akaogopa sana na kuamua yaishe na arudi alipotoka maana wanadai kama alexander alishinda kwanni ageuze?? Kwanni ampige Puru alafu asimuue wala kumpora utawala wake??
View attachment 814518

Maswali ya kujiuliza GT
1. Alexander the Great anafahamika kwa ukatili wake awamo kwenye uwanja wa vita ssa iwaje hapa aliguswa na huruma ilihali alichomwa mkuki ambao ungeweza muua ila bado akamsamehe Porus na kumuachia eneo hilo alitawale????!!!

2. Kingine kabla ya vita hyo alexander alikwisha ingia ubia na mfalme Ambhi wa taxila ambaye aliahidiwa kama atamsaidia kumpiga mfalme porus watagawana utawala na mfalme Ambhi sasa najiuliza kama walishinda vita kivipi huyu Ambhi hakupewa huo ufalme alioahidiwa ila huyo huyo aliyepigwa yaani Porus ndio aliambiwa aendelee kutawala?? Na wala hakuna ushahidi wa kishitoria unaoonyesha mfalme ambhi akilalamika kunyimwa ahadi na alexander je kama kweli alexander alishinda kivp nchi hakupewa Ambhi.

3. Hoja nyingine ni kwamba wanadai jeshi la alexander liliamua tu baada ya kushinda kugeuza nyumbani eti kisa wamechoka?? Swali langu ni hili maeneo yote ambayo wanajeshi wake waligoma walinyongwa na pia jeshi lilikuwa na utaratibu wa kubadilisha wanajeshi ambapo waliokaa muda mrefu walirudishwa na vijana fresh wabichi kabisa walichukuliwa kuongeza nguvu sasa waliochoka ni wakina nani?? Pia kabla ya hapo ukimgomea alexander unachinjwa sasa ni muujiza gani walitumia hao askari kumpinga alexander na hakuwachinja??

HITIMISHO
Baada ya vita hii alexander alijeruhiwa vibaya sana na alifia akiwa huko babeli alipokuwa anarudi kutoka India na hata farasi wake alifia kwenye vita hiyo ya India!! Na baada ya hapo utawala wake ulimeguka baada ya wanajeshi wake kugombea madaraka hivyo jeshi kugawanyika na utawala kuporomoka na mpaka anakufa wazungu wanadai alexander hakuwahi kupigwa na hata kuna muda ulifika akaanza kulia sababu amekosa wapinzani wa kupigana nao hapa dunia!!! Je Great thinker unafkiri kuna historia inapotoshwa kuhusu mtawala huyu wa kipekee au historia yake ina usahihi 100% bila chumvi yeyote

Naomba kuwasilisha
View attachment 814515
umenikumbusha season ya porus
Huyo anajiita Alexander MKUU
wakati yupo India alichezea kichapo heavy
ni vile wazungu wanapenda kupotsha as walivyopotosha hist Yetu
 
Alexa
Nia na lengo la Alexandre the Great ilikuwa kutawala dunia. Falme alizoziteka aliingiza utamaduni wa Kigiriki akichanganya na wa nchi husika.
Yeye ndiye sababu ya kuwa na mji wa Alexandria nchini Misri na alioa watoto wa wafalme aliowateka. Malkia na watoto wake waliendeleza utawala wake.
Hakuwahi kuwa na watoto
 
Nimekusoma mkuu ila cha kujiuliza je ni kwanni aliposhinda hakuchukua huo mji wala hakumuua huyo mfalme?? Yaani kwanni ashinde vita alafu ageuze bila kuweka mtawala wake kwenye ufalme ule?? Hilo swali linanitatiza zaidi yaani kwanni ashinde alafu ufalme bado ulibakia kwa Porus

Pia kama unakubali aliogopa kusonga mbele je kwanini anaitwa THE GREAT alafu wanadai hakuwahi kupigwa maishani mwake ilihali aliogopa wahindi na wachina??? Kipi hasa kinamfanya great kwa muktadha huu
Walimpa binti wa kihindi akamwoa na yeye kuwaachia mamlaka yao ya ndani lakini kwa makubaliano kuwa watakuwa chini ya himaya yake. Lakini alivyotoka tu huko Hindukush hakuwa na maisha marefu. Akapatwa mauti akiwa Babylon ambayo alikuwa ameifanya kuwa mji wa himaya yake kuu.
 
who knows folded codes?
hakuna mwenye uhakika 100 since ni unabii
Wenye Imani thabiti wana uhakika. Wale wasiofata mkumbo ila waliamini kwa kuitwa na Mungu. Tatizo sayansi imeshawajaza watu ujinga wa kudai, "without proof, you know nothing about it" huu ndo ujinga uliowakaa wengi wapenda sayansi kuliko Mungu. Kitu kimoja nachoweza sema kuhusu Mungu, ni Roho. Hutoichunguza kwa nyama wala mitambo
 
Nitatufa
Aisee, ndo mzigo umefika season ya 392 wallah! Vipande vingine hadi next week.

Tafuteni movie hii iendayo kwa jina la PORUS. Kumedadavuliwa kila kitu. Na mzigo umeenda shule sana
Nitaitafuta hii Nazani YouTube itakuwepo
 
Back
Top Bottom