Ukweli ni upi : Alexander the Great akiwa INDIA

Mkuu zitto junior asante kwa kuniita kwenye huu uzi wako na mimi kama kawaida yangu nitachangia kwa msaada wa kitabu nikipendacho kuliko vyote "Biblia Takatifu". Alexander The Great alitabiriwa kwenye Biblia kwenye kitabu cha Danieli ingawa hakutajwa jina lake moja kwa moja lakini utawala wake kuanzia mwanzo wake mpaka kuanguka kwa ufalme wake vimeandikwa ndani ya kitabu hichi.

Nabii Danieli akiongozwa na MUNGU alitabiri kumuhusu Alexander The Great takribani miaka 250 kabla Alex hajawa Mfalme wa Macedonia ambayo ni Ugiriki. Danieli 8:5 inaelezea kuanza kwa utawala wa Alex na Danieli 8:8 inaelezea mwisho wa Alex yaani kifo chake. Sasa tunajua kuwa aliyekuwa akizungumziwa ni Alex hasa pale tunaposoma Danieli 8:22 ambapo anasema; "tena katika habari za pembe ile iliyovunjika ambayo badala yake zilisimama pembe nne, falme nne zitasimama kutoka katika taifa lile lakini si kwa nguvu kama zake(Alex)".

Ukiendelea kusoma kitabu cha Danieli 11:4 utaona anazielezea hizi falme nne ambazo zitagawanyika kutoka kwenye Ufalme wa Alexander. "Naye atakaposimama ufalme wake utavunjika na kugawanyika katika pepo nne za mbinguni, lakini hautakuwa wa uzao wake, wala hautakuwa kama mamlaka yake ambayo alitawala kwayo, kwa maana ufalme wake utang'olewa hata kwa ajili ya wengine zaidi ya hao"...... Na hakika hichi ndicho kilichofanyika hasa, maana baada ya Alexander kufa, Ufalme wake uligawanyika mara nne tena katika hizo falme nne hakukuwa na mrithi wa Alex wa damu.

Falme hizo nne ni Cassander, Lysimachus, Seleucus, na Ptolemy I. Falme zote hizi hakuna hata moja ambayo ni mrithi wa damu wa Alex. Hivyo utabiri wa Nabii Danieli ulitimia kama alivyotabiri na ndiyo maana mimi huwa nasema naipenda sana Biblia!

Tena kuna stori ambayo nilisoma nje ya Biblia inasema kuwa eti kisa Alexander hakuuharibu mji wa Jerusalem ni sababu alipofika Jerusalem alipokewa na Kuhani mkuu wa wakati ule ambaye alimpokea kwa heshima kubwa sana na kumpeleka moja kwa moja Hekaluni ambapo alimwonyesha Kitabu cha Danieli na kumsomea huo unabii na kumwambia kuwa unabii huo unamuhusu yeye Alexander. Kwa sababu Alex alikuwa anaijua lugha ya Kiebrania, alijosomea mwenyewe na akafurahi sana kuona Ufalme wake ulitabiriwa kwa uwezo wa MUNGU, hivyo akaona haitakuwa busara kuuharibu Jerusalem.

Kwa kuhitimisha hoja yako, mimi binafsi nakubali kuwa Wazungu wameipotosha historia ya Alexander ili wampatie sifa isiyomuhusu. Utabiri wa Danieli unasema wazi kabisa kuwa "pembe yake itavunjika", maana ya pembe kuvunjika ni kama Mfalme kufa kifo cha mapema na ufalme wake kuvunjika. Na hichi ndicho kilichotokea kwa Alex kwani alikufa akiwa na miaka 32 tu. Hivyo ni sahihi kabisa kuwa Alex alipoteza vita ya India na alipigwa vibaya sana na Mfalme Porus na kujeruhiwa na kupelekea mauti akiwa bado kijana.

NB
Utanisamehe mkuu kwa majibu marefu maana mimi huwa siandiki kwa kifupi.
hakika umechambua vizuri sana,, yani biblia ukiisoma ina stori za kusisimua sana.
 
I remember nimesoma soma kidogo History ya Alexander the Great, wanaodai kuwa alikuwa anashinda mapambano yote sio kweli. I remember kuwa Alexander alipata upinzani mkali sana katika ardhi ambayo leo ni Afghanistan ya leo, ujuzi wangu kiukweli kuhusu eastern campaign za Alexander the Great unaishia hapo. Wanahistoria wanasema upinzani mkali wa Afghanistan haukuanza kuonekana kwa Mmarekani
 
Hii story ipo kwenye kitabu cha daniel mkuu. But hakutajwa tu moja kwa moja.
najua,lakini unabii unatafsiriwa kulingana na matakwa au mtazamo wa watu fulani,kwa mfano wakatoliki na wasabato wanatofautiana katika kutafsiri unabii wa kwenye kitabu cha UFUNUO WA YOHANA
 
Mkuu zitto kama Alexander alikufa kwa kujeruhiwa baada ya kushindwa vita na kupata kipigo kikali basi hata mafundisho church hawako sahihi maana tusoma Alexander alikufa kwa homa kali na ulevi na ndipo majenerali wake akina cassander , Ptolemy n.k wakagawana falme mpk kuja wakati wa Roman empire
 
Mkuu zitto kama Alexander alikufa kwa kujeruhiwa baada ya kushindwa vita na kupata kipigo kikali basi hata mafundisho church hawako sahihi maana tusoma Alexander alikufa kwa homa kali na ulevi na ndipo majenerali wake akina cassander , Ptolemy n.k wakagawana falme mpk kuja wakati wa Roman empire
Mkuu mafundisho church bado wako sahihi maana kama ni homa kali huenda ilichangiwa na majeraha ya vitani ya muda mrefu !!!
 
View attachment 814513
Habari za jioni wakuu bila kupoteza muda niende moja kwa moja kwenye mada

Natumaini wote tumeshasikia mengi sana kuhusu alexander the great ila kuna mambo machache yananitatiza na tusaidiane kujuzana kuhusu mtawala huyu.

ALEXANDER NI NANI
View attachment 814519

Alexander III wa Macedonia alizaliwa 20/21 July 356 BC na kufariki 10/11 June 323 BC (Miaka 33) maarufu kama Alexander the Great aliyekuwa mfalme wa nchi ya makedonia iliyokuwa ndani ya ufalme wa kigiriki na alitumia muda wake mwingi wa maisha kupigana vita za kuteka miji mbalimbali ili kuongeza ufalme wake

UMAARUFU WAKE
View attachment 814517

Umaarufu wake ulikuja baada ya kuwa mwanajeshi asiyewahi kushindwa vitani na kufikia umri wa miaka 30 alikwisha angusha falme zote kubwa zilizokuwa tishio kati ulimwengu wa kale akitandika mataifa makubwa kuanzia ulaya,Afrika hadi Asia hivyo anatazamiwa kuwa commander bora zaidi wa kijeshi katika historia.

ALEXANDER AKIWA INDIA
baada ya kupata picha kidogo ya nani anazungumziwa twende moja kwa moja kwenye swali langu JE NINI KILITOKEA KWA ALEXANDER INDIA
View attachment 814512


Alexander baada ya kuvamia ufalme wa uajemi na kuutandika alielekea India akiwa na ndoto za kuifikia china hivo kutawala Asia nzima. Lakini kuna vita ilipiganwa kati yake na mfalme Puru/porus iliyozaa utata mkubwa.

1. Kwa upande wa wazungu wanadai Alexander alimpiga mfalme Porus na kwamba aliposhinda alimuona Porus ni mzuri vitani sababu alimpa ushindani hivyo akaamua kumrudishia ufalme wake wa hilo eneo aliloteka na alexander akaamua tu kugeuza kurudi uajemi baada ya wanajeshi wake kuweka mgomo kuwa wamechoka!alitoa upinzani kwa tembo 100 tu hivyo akaogopa sana na kuamua yaishe na arudi alipotoka maana wanadai kama alexander alishinda kwanni ageuze?? Kwanni ampige Puru alafu asimuue wala kumpora utawala wake??
View attachment 814518

Maswali ya kujiuliza GT
1. Alexander the Great anafahamika kwa ukatili wake awamo kwenye uwanja wa vita ssa iwaje hapa aliguswa na huruma ilihali alichomwa mkuki ambao ungeweza muua ila bado akamsamehe Porus na kumuachia eneo hilo alitawale????!!!

2. Kingine kabla ya vita hyo alexander alikwisha ingia ubia na mfalme Ambhi wa taxila ambaye aliahidiwa kama atamsaidia kumpiga mfalme porus watagawana utawala na mfalme Ambhi sasa najiuliza kama walishinda vita kivipi huyu Ambhi hakupewa huo ufalme alioahidiwa ila huyo huyo aliyepigwa yaani Porus ndio aliambiwa aendelee kutawala?? Na wala hakuna ushahidi wa kishitoria unaoonyesha mfalme ambhi akilalamika kunyimwa ahadi na alexander je kama kweli alexander alishinda kivp nchi hakupewa Ambhi.

3. Hoja nyingine ni kwamba wanadai jeshi la alexander liliamua tu baada ya kushinda kugeuza nyumbani eti kisa wamechoka?? Swali langu ni hili maeneo yote ambayo wanajeshi wake waligoma walinyongwa na pia jeshi lilikuwa na utaratibu wa kubadilisha wanajeshi ambapo waliokaa muda mrefu walirudishwa na vijana fresh wabichi kabisa walichukuliwa kuongeza nguvu sasa waliochoka ni wakina nani?? Pia kabla ya hapo ukimgomea alexander unachinjwa sasa ni muujiza gani walitumia hao askari kumpinga alexander na hakuwachinja??

HITIMISHO
Baada ya vita hii alexander alijeruhiwa vibaya sana na alifia akiwa huko babeli alipokuwa anarudi kutoka India na hata farasi wake alifia kwenye vita hiyo ya India!! Na baada ya hapo utawala wake ulimeguka baada ya wanajeshi wake kugombea madaraka hivyo jeshi kugawanyika na utawala kuporomoka na mpaka anakufa wazungu wanadai alexander hakuwahi kupigwa na hata kuna muda ulifika akaanza kulia sababu amekosa wapinzani wa kupigana nao hapa dunia!!! Je Great thinker unafkiri kuna historia inapotoshwa kuhusu mtawala huyu E]

Kuhusu India in kweli alishinda vita ila kuna romance kuhusu kupigwa kwake na. Queen of punt maana siamini baada ya kuichukua kemet hakutakata kushuka puntland,ila vita nayoamini pia hakushinda kiurahisi ni ile ya Iran maana walikuwa na mafunzo ya kutumia tembo toka enzi za Cyrus the great(role model of Alexander)
 
Back
Top Bottom