Ukweli ni kitu gani?

Ukweli ni kitu gani?

katika swala zima la ukweli ni umbo lenye pande Sita three dimension sasa hatuwezi kuwe sawa ingawa wote tutakua wakweli Aliyeona juu hatajua chini Kuna nn na aliuona chini hatajua mbele na vitu mfano Wa hivyo usishangae leo hii watu wanne walioshuhudia tukio moja kila mtu akija na stori yake na inawezekana wanabishana na ngumi zikapigwa
Ngumi Tena 😂😂😂🤣🤣🤣hapo sasa
 
Ukweli ni Kujua na kutambua hali halisi na kutoa utata wa sintofahamu. Knowing, casying the shadow of doubt, replacing belief with knowledge.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli kinyume cha Uwongo. Biblia imesema Mungu ni Kweli na Shetani ni Baba wa Uwongo. Yesu alisema yatupaswa kumuabudu Mungu kwa Njia ya Roho na Kweli. Kuijua kweli lazima tupate picha halisi ya Uwongo kwani kinyume chake cha Uwongo ndio Kweli. Kwa mfano nikikuuliza jee unajua rangi ya Kinyonga? Hakuna anaeijua Rangi halisi ya Kinyonga kwani inabadilika kila inapotokea hali ya mabadiliko ya mazingira yanayo mzunguka.

Kutokuwa halis, na kubadilika ndio tunaita hali ya uwongo. Haijalishi madailiko hayo ni ya muda mfupi au mrefu ilimradi kuna uwezekano wa kutokea mabadiliko ya aina yeyote ile au mabadiliko ya msimamo basi huo ni uwongo.

So long jiwe linaweza kubasilika na kuwa kokoto likilipuliwa na baruti basi nalo sio halisi ni uwongo, au chuma hakikuwa kilivyo kimebadilika kutoka Iron ore basi sio halisi ni uwongo, mbao ilikuwa mti, ambao ulikuwa kambegu kaliko jipanda aridhini na kuvyoza virutubisho udongo hivyo sio halisi ni uwongo.

Kwa utambuzi wetu twaona kuwa vitu vyingi vina hali ya kweli wakati sio. Mfano hali ya maji, maji yana hali ya kimiminika, lakimi ukiyaweka kwenue jokofu yanaganda na kuwa barafu, ukiyachemsha yanapata moto, na joto likipanda ya kuwa mvuke na kukauka. Kama rangi ya kinyonga maji hali ya maji hubadirika hivyo ni hali ya uwongo.

Ukweli ni ile hali kuwa bila mabadiliko ya aina yeyote katika hali yeyote, kwa jua, kwa mvua, au kwa muda, au mahali uliopo ni hali ya milele. Ukweli uko kama ulivyo sasa, kabla ya sasa, na baadae, Ukweli ni hali ya umilele.

Kweli ni Uhai na Uwongo na Maumbile yake.

Binadamu ana nafsi mbili, ananafsi ya kweli ambayi ni Roho na nafsi ya uwongo ambayo ni Mwili. Roho haina mwanzo wala mwisho, lakini mwili una mwazo na mwisho, unakua na kuzeeka, unazaliwa na kufa.

Ndio maana YESU anataka tumwabusu Mungu kwa Njia ya Kweli yaani Kwa Roho zetu kwa Mungu Roho.

Kila unachokiona, unachokitamani kukipata, kula, kunywa, kuzini au kufurahi nacho ni vyo uwongo. Hivyo vinakinaisha, havikidhi matarajio, haviridhishi.
 
Japo hiyo quotation yako kutoka Bible ni tata, haina uthibitisho kupitia kifungu, ila

Ukweli ni hali ya nafsi kujirizisha pasipo na shaka.
 
Ukweli ni uhalisia wa jambo jinsi lilivyo bila kuongeza wala kupunguza. Ni habari au taarifa ya kitu au jambo lilivyo tendeka.
Kila kitu au jambo uliloona, kusikia na hata kuadithiwa linaukwe halisi.
Ukweli halisi na ikiwa uhalisia wa jambo haupo, huo si ukweli ni uongo.
Kwa hali ya kusikitisha, wengi tunashindwa kuelewa tofauti kati ya UKWELI na IMANI.
UKWELI ni mambo ambayo tayari yamefanyika na kuthibitishwa.
IMANI ni mambo ambayo hutarajia kufanyika.
Lakini ikumbukwe kwamba Imani inajengwa na mambo ambayo tayari yamefanyika. Ni lazima mambo yaliyo fanyika na kuthibitishwa (UKWELI) yatangulie ili upate uhakika wa a mambo yajayo (IMANI).
 
ukweli ni uwazi na uthibithisho wa jambo,kauli isio na shaka ndani yake,inayo zungumzia uhakika wa jambo au wa kitu, je utaijuaje kua kauli hii haina pingamizi na ni sahihi!! jibu ,ufasaa na ushahidi halali ima kupitia vigezo au kwa kukileta kitu mbele ya mtaka ushahidi na kukihakikishaa!!!
#23
 
Kwangu naona Yesu sio jibu kwani ni mchongo uliochongwa tu na Wayahudi wenye akili kuuhadaa ulimwengu. Na wamefanikiwa kwani hiyo imani imeenea sehemu kubwa ulimwenguni hasa dunia ya tatu yenye masikini wengi. Wanafalsafa wa zamani Socrates, Plato na Aristotle walishindwa kujua ukweli. Labda siku ya kufa roho itajua ukweli ni nini.
 
Kwa jini nilivyo ipitia michango ya hii thread na thread yenyewe I declare ukweli it's just an complicated things it depends na Imani ya watu Mila desturi na mazingira ya watu hao husika

Mfano kula kitimoto Kwa cristian ni halali na kwao huo ni ukweli to them you can't change that fact

But to Muslim ni Haram and to them you can't change that fact

So ukweli ni complicated things
 
Ukweli ni uhalisia wa jambo jinsi lilivyo bila kuongeza wala kupunguza. Ni habari au taarifa ya kitu au jambo lilivyo tendeka.
Kila kitu au jambo uliloona, kusikia na hata kuadithiwa linaukwe halisi.
Ukweli halisi na ikiwa uhalisia wa jambo haupo, huo si ukweli ni uongo.
Kwa hali ya kusikitisha, wengi tunashindwa kuelewa tofauti kati ya UKWELI na IMANI.
UKWELI ni mambo ambayo tayari yamefanyika na kuthibitishwa.
IMANI ni mambo ambayo hutarajia kufanyika.
Lakini ikumbukwe kwamba Imani inajengwa na mambo ambayo tayari yamefanyika. Ni lazima mambo yaliyo fanyika na kuthibitishwa (UKWELI) yatangulie ili upate uhakika wa a mambo yajayo (IMANI).
Nimeperuzi uzi wote angalau wewe umefafanua vizuri sana mkuu

Watu wanachanganya sana UKWELI na IMANI

UKWELI ni HALISI ya jambo/kitu kilivyo
 
Kwa jini nilivyo ipitia michango ya hii thread na thread yenyewe I declare ukweli it's just an complicated things it depends na Imani ya watu Mila desturi na mazingira ya watu hao husika

Mfano kula kitimoto Kwa cristian ni halali na kwao huo ni ukweli to them you can't change that fact

But to Muslim ni Haram and to them you can't change that fact

So ukweli ni complicated things
Mkuu unachanganya IMANI na UKWELI

Ukweli huwa ni mmoja tu kwa jambo mmoja

Imani ni kukubali jambo kuwa ni kweli bila uthibitisho……. Ndio maana kila imani inaamini kivyake vyake tofauti na imani nyingine kwa jambo hilo hilo moja

Futi moja ni futi moja dunia nzima lakini kitimoto ni halali au haramu itategemea na wewe umeamua kukubali kuamini lipi
 
Ukweli ni fiction shauri yako ,

Unaweza ukaamini kwamba huyo unaye mfahamu kuwa ni baba Yako kuwa ndiye baba Yako halisi na katika huo uliopo kwako ndio ukweli ukweli wenyewe

Lakini kumbe kiuhalisia sio baba Yako , so hauoni kwamba Hadi hapo ukweli ni issue ambayo ni complicated
 
Umeandika vizuri sana “unaweza ukaamini”

Jamii imekubali kwamba “kitanda hakizai haramu” ndio maana imeamua kukubali kuamini kwamba baba akikubali mtoto ni wake basi ni wake(kulea inatosha)…….. Lakini ukitaka kujua UKWELI HALISI basi una check na DNA mkuu
 
Kuna vitu viwili, 'ukweli' na 'uhalisia'.

Ukweli ni kile ambacho mtu anaamini/ amaaminishwa. Kwa mfano ukimwambia muislamu au mkristu dininipi ni ya kweli Kila mtu atataja dini yake (kwa sababu anaamini au ameaminishwa).

Uhalisia ni jinsi kitu kilivyo hata kama kikisemwa au kuchuliwa vinginevyo.
 
Back
Top Bottom