Ukweli ni kitu gani?

Kwa hiyo una maanisha hakika inazaliwa baada ya Ukweli?!..
Kwa maana hakika inatokana na instict ya mtu mwenyewe?!
Let me break it Down..
Well umesema ukweli una Asili,nambie ni nini kisicho na Asili lakini bado ni kweli??
Chochote kilicho na asili ndiyo ukweli kwasababu ndivyo kilivyo kwa jinsi yake. Hakuna kisicho na asili halafu kiwe ukweli!
 
katika swala zima la ukweli ni umbo lenye pande Sita three dimension sasa hatuwezi kuwe sawa ingawa wote tutakua wakweli Aliyeona juu hatajua chini Kuna nn na aliuona chini hatajua mbele na vitu mfano Wa hivyo usishangae leo hii watu wanne walioshuhudia tukio moja kila mtu akija na stori yake na inawezekana wanabishana na ngumi zikapigwa
 
Ukweli ni Kujua na kutambua hali halisi na kutoa utata wa sintofahamu. Knowing, casying the shadow of doubt, replacing belief with knowledge.
Habari wana JF

Wakati tunaelekea mwisho wa mwaka kwenye msimu wa sikukuu nimejaribu kutafakari peke yangu hili jambo tajwa hapo juu (ukweli ni kitu gani?) bila mafanikio. Msingi wa tafakari yangu unatokana na maandiko matakatifu (biblia agano jipya) ambapo Yesu aliulizwa na Pilato je ukweli ni kitu gani? Bahati mbaya muandishi hakueleza kama Yesu alijibu na jibu lake lilikua ni lipi? (kwa wale wenye uelewa zaidi ya huu watanijuza pia).

Kwa kutumia uwezo wangu nimejaribu kujiuliza hili swala muda mrefu sana nisipate jibu lake. Mara nyingine utaona watu wanabishana na kila mmoja ana amini anachosema ni cha ukweli, sasa hapo shida ndipo inapoanza ukweli ni upi sasa?

Tafsiri ya kwanza inaweza ikawa, ukweli unaweza ukawa ni maneno au jambo analolisema mtu amabalo analoliamini na yuko tayari kulishuhudia lakini linaweza likawa sahihi au siyo sahihi. Ni nini basi kinachoamua usahiii wa jambo? mara nyingi ni imani (dini au mila), mapokeo, maono (jinsi lilivyoonwa) na mazoea. Hali kadhalika imani, mapokeo, maono na mazoea yanaweza yakawa na tafsiri tofauti kati ya waumini wa imani moja na nyingine, au jamii moja na nyingine au mtazamaji mmoja na mwingine.

Kwa maana hiyo basi jambo moja linaweza likawa na tafsiri zaidi ya moja kulingana na imani, maono, mapokeo na mazoea. Kwa mustakabali huo basi, ukweli ni kitu gani? je kuna ukweli mmoja (universal truth) au kuna various versions of truths? Naomba kujuzwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitu chochote ambacho kina chanzo chake kinaitwa ukweli lkn kama jambo au taarofa ambyo haina chanzo chke hyo ni maoni au utashi ama mtazamo bnfsi wa mtu
Ukweli una mambo mawili chanzo pamoja na jinsi utakamvyomuathili mpokeaji wa taarifa hyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kile kilichoko ndani ya moyo ndiyo kinaitwa ukweli
Yani unaweza kuwaambia watu jambo ambalo ni lakweli lakini wengine wasikuamini na wengine wakaamini
Pia unaweza kudanganya watu wakaamini na wengine wasiamini
Ila ukweli unakuwa nao wewe moyoni mwako
Mfano kuna watu wana share stories zao hapa na bado watu wanaziita chai ila ukweli anakuwa nao mwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wana JF

Wakati tunaelekea mwisho wa mwaka kwenye msimu wa sikukuu nimejaribu kutafakari peke yangu hili jambo tajwa hapo juu (ukweli ni kitu gani?) bila mafanikio. Msingi wa tafakari yangu unatokana na maandiko matakatifu (biblia agano jipya) ambapo Yesu aliulizwa na Pilato je ukweli ni kitu gani? Bahati mbaya muandishi hakueleza kama Yesu alijibu na jibu lake lilikua ni lipi? (kwa wale wenye uelewa zaidi ya huu watanijuza pia).

Kwa kutumia uwezo wangu nimejaribu kujiuliza hili swala muda mrefu sana nisipate jibu lake. Mara nyingine utaona watu wanabishana na kila mmoja ana amini anachosema ni cha ukweli, sasa hapo shida ndipo inapoanza ukweli ni upi sasa?

Tafsiri ya kwanza inaweza ikawa, ukweli unaweza ukawa ni maneno au jambo analolisema mtu amabalo analoliamini na yuko tayari kulishuhudia lakini linaweza likawa sahihi au siyo sahihi. Ni nini basi kinachoamua usahiii wa jambo? mara nyingi ni imani (dini au mila), mapokeo, maono (jinsi lilivyoonwa) na mazoea. Hali kadhalika imani, mapokeo, maono na mazoea yanaweza yakawa na tafsiri tofauti kati ya waumini wa imani moja na nyingine, au jamii moja na nyingine au mtazamaji mmoja na mwingine.

Kwa maana hiyo basi jambo moja linaweza likawa na tafsiri zaidi ya moja kulingana na imani, maono, mapokeo na mazoea. Kwa mustakabali huo basi, ukweli ni kitu gani? je kuna ukweli mmoja (universal truth) au kuna various versions of truths? Naomba kujuzwa.
Ukweli ni kile unachoamini wewe kama wewe bila kumlazimisha mtu mwingine kuamini!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli ni very complex concept, na ni moja kati ya mada pana sana hususan kwenye mambo ya falsafa (phylosophy) na theolojia(theology), ila in simple words it means 'being in accord with fact or reality, or fidelity to an original or standard.'

the Legend☆
 
Back
Top Bottom