Ukweli na Uwongo upi hudumisha ndoa? Au vyote? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukweli na Uwongo upi hudumisha ndoa? Au vyote?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Hmaster, Jun 20, 2011.

 1. Hmaster

  Hmaster JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 347
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Juzi nilikuwa maeneo ya Ubungo ambapo nilikutana na dada furani akiwa na watoto wa2 na mizigo kadhaa na baada ya kusalimiana aliniomba nauli ya daladala ili aende Tegeta kwa dada yake kwani alikuwa ameibiwa pochi yake ambayo ilikuwa na pesa akiwa safarini kutokea Songea. Mimi kwa vile nilikuwa na gari na kwa namna alivyoonyesha huzuni niliona bora nimchukue tu kwenye gari yangu hadi Tegeta kisha nikarudi hadi Magomeni ninapoishi. Kwa sababu ya foleni nyingi na muda ulipita sana kabla ya kurudi home, hata hivyo my wife wangu nilimweleza kila kitu lakini badala ya kuona umuhimu wa mimi kumsaidia mwanamke mwenzake yeye alikwenda mbali zaidi na aliamua kukata simu na hakupatikana hadi nafika home. Baada ya kufika nikamkuta tayari yupo kitandani akiwa na nguo zake zote, eti ndo keshakasirika na kuamua kulala hiyo saa tatu na wakati huwa tunalala hata saa 5 kila siku. Nilipojaribu kumwamsha ili aniandalie chakula alinijibu niende kula kwa malaya niliyemsindikiza Tegeta. Nilijitahidi kumwelewesha lakini ilishindikana. Nikajiandalia chakula mwenyewe, nikaoga na kisha kulala kwa maana kwa hali hiyo hata kumchombeza sikuweza. Sasa swali ni je Ukweli na Uwongo upi hudumisha ndoa, au vyote? Wenye experince na mambo haya waweke hapa maana sasa najiandaa kuwa mwongo kwa vile ukweli umenitokea puani. Na kama wanawake humu jf watueleze wenyewe kipi wanataka kutoka kwetu kati ya hivyo vitatu ili wawe na amani. Nawasilisha!
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,818
  Trophy Points: 280
  Mhhh! pole sana Mkuu kwa kesi yako hii labda ungesema uongo kwa mfano gari lilikuharibikia usingeweza kujibiwa majibu hayo ambayo yangeweza kabisa kuongeza purukushani ndani ya nyumba. Hongera sana kwa moyo wako wa huruma.
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Hapa i see nimekosa la kusema...heri nikae kimya
   
 4. CPU

  CPU JF Gold Member

  #4
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Wewe kama mdada mwenye uzoefu wa ndoa miaka mi4 sasa tunahitaji sana mchango wako hapa ili na sisi ambao hatujaoa tujue tuseme nini likitutokea ili mtuelewe akina dada. Tafadhali FL1, usifiche hekima zako hapa, tunawapenda sana na tunataka tuwaelewe vizuri
   
 5. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #5
  Jun 20, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  sema tu usiogope.........
  ni kweli kwamba kila sekunde,kila dakika tuseme ukweli,
  je kwa kusema uongo japo kiduchu tu pale inapobidi, si unaweza jikuta umesalimisha mambo mengi ya hatari?

  ....ila UWONGO hata mungu hapendi ...lol...
   
 6. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #6
  Jun 20, 2011
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Inawezekana umezoea kutumia staili hiyo hiyo kumdanganya kiasi kwamba hata unaposema ukweli anakuwa hakuamini. Vinginevyo Hongera kwa moyo wa huruma uliuonyesha
   
 7. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #7
  Jun 20, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,087
  Trophy Points: 280
  Siku hizi uongo ndo ukweli na ukweli ndo uongo kwa hiyo kwenye ukweli unareplace uongo na penye uongo unareplace ukweli
   
 8. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #8
  Jun 20, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,017
  Likes Received: 3,198
  Trophy Points: 280

  Kumbe unaweza, ila bado unamfumo dume.

  Kani kabla ya kuoa nani alikua anakufanyia hayo yote?
   
 9. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #9
  Jun 20, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Ukweli daima utakuweka huru! Pamoja na gharama zake kama hizo ulizoingia wewe....lakini gharama za kudanganya huwa ni kubwa zaidi. ukidanganya mara moja unaweza kujikuta unaingia gharama ya kudanganya tena na tena...ili kulinda uongo uliofanya awali (kwa mfano)...and you will never be free! Sema ukweli na simama kwenye ukweli....hata Mungu anakuona. Labda cha kujifunza ni namna na wakati wa kusema unachotaka kusema hata kama ni ukweli.
   
 10. s

  shoshte Senior Member

  #10
  Jun 20, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi kwanza nakupa pole na hongera pia kwa kuwa na moyo wa huruma kiasi hicho mkuuu mi naona ni vyema uilesama ukweli wanasema TELL THE TRUTH AND THE TRUTH WILL SET YOU FREE sawa hakukuelewa ila baadae atakuelewa kama huna mazoea ya kuwa na mambo ya kazi za nje siunajua tena.Ndoa zinzdumishwa na ukweli kwani hutadanganya kila siku ipo siku utakamatwa tuu km ulimpeleka huyo dada Tegeta labda kuna watu walikuona uje kumwambie wife wako kuwa gari ilipata shida afu wale watu waliokuona wamwambie wife wako hapo napo vipi.ALWAYS TELL THE TRUTH...
   
 11. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #11
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Kama unaona ukweli unaweze kuvunja ndoa yako au kumpa karaha au kumuumiza mwenzako utakuwa punguani kusema ukweli... sababu utakuwa haujengi bali unabomoa... Honesty is the Best Policy............ (Well not Always.........)
   
 12. evelyne

  evelyne Member

  #12
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Inategemea wewe ukoje kama ni mtu wa kumfix tu unategemea nini .................binadamu wamebadilika ................mtu ukishang'atwa sijui kugongwa ukiguswa na unyasi tu unashtuka
   
 13. A

  Aine JF-Expert Member

  #13
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mimi kwa kweli siku zote napenda mume wangu aniambie ukweli, uongo kwangu mwiko. Sasa kwa kesi yako inategemea, kama siku zote wewe ni muongo ndiyo maana hakuamini, au inawezekana kuna tabia zako flani ambazo yeye anaziwekea mashaka ndiyo maana ulipomuambia hiyo habari pamoja na kumtaarifu toka mwanzo, alinuna.

  Ila take time uongee naye esp siku akiwa amefurahi, umwambie kilichotokea siku hiyo na yeye anachokifikiria ni vitu viwili tofauti. Na kwa upande wake, unatakiwa umsome mkeo, kama ni mtu wa wivu sana basi jitahidi ku-avoid mazingira yatakayomfanya ahisi vinginevyo. Wivu ni sehemu ya mapenzi usimlaumu sana, she loves you, ila wivu ukipiliza ni kero kwa kweli
   
 14. Hmaster

  Hmaster JF-Expert Member

  #14
  Jun 20, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 347
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sio mfumo dume, sisi tuliokulia vijijini tulipewa mafunzo wakati wa jando kwamba si jambo jema kufunua chakula kilichoandaliwa na mwingine hata akiwa mkeo.
   
 15. CPU

  CPU JF Gold Member

  #15
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kaka hiyo ni topic nyingine
  Huwezi jua walikubaliana vp kuhusu kupika
  Turudi tu kwenye mada kuu . . . . kudanganywa
   
 16. Hmaster

  Hmaster JF-Expert Member

  #16
  Jun 20, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 347
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Upo sahihi na hasa kiroho, lakini ndoa inayumba sana kupitia kusema ukweli ingawa yeye (mungu) ndo anavyotaka. Hakutakuwa na mwisho mbaya?
   
 17. A

  Aine JF-Expert Member

  #17
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  KJ hapo napingana na wewe kabisa, ni kawaida ya mwanamke kumuandalia mume wake chakula. Inapotokea mume kaamua kujiandalia mwenyewe chakula sio mbaya kwani ni makubaliano ya mume na mke, lakini si kuambiwa kaniandalie chakula halafu akatae. Mwanamke anatakiwa hata awe amechukia namna gani kumuandalia mume wake chakula ni wajibu wake, ugomvi anatakiwa auweke pembeni wakamalizane huko chumbani siyo mezani na watoto wakiwa wanashuhudia eti mama kakasirika leo baba anajiandalia mwenyewe chakula no thank you!!
   
 18. Hmaster

  Hmaster JF-Expert Member

  #18
  Jun 20, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 347
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lakini mheshimiwa kudanganya nako kuna madhala yake. Kwa kesi kama hii yangu: kumbuka gari ina namba na kwamba wife anaweza kukupigia simu baada ya kukuona umepita ili akutege, alafu wewe ndo unamdanganya eti gari limeharibika barabarani, si utachochea moto hapo?
   
 19. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #19
  Jun 20, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Kama tukizungumzia hii kadhia yako specifically, hicho unachokishuhudia (kununiwa) hasa sio tatizo bali dalili ya tatizo lililopo kwenye mahusiano yenu. Katika hali ya kawaida mwenza kumsaidia binaadamu mwingine hata kama ni wa jinsia tofauti haipaswi kuleta manung'uniko asilani! Ukweli kwamba mkeo anabnung'unika kwa kitendo ulichokifanya kinaashiria matatizo katika mawasiliano yenu....kwa nini hakuamini?
   
 20. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #20
  Jun 20, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  nadhani hujamwelewa vizuri VoR,
  Hebu msome tena,
  sidhani kama alimaanisha uwongo wa style hiyo....................
   
Loading...