Ukweli na Uwongo upi hudumisha ndoa? Au vyote?

Sio mfumo dume, sisi tuliokulia vijijini tulipewa mafunzo wakati wa jando kwamba si jambo jema kufunua chakula kilichoandaliwa na mwingine hata akiwa mkeo.

Bravo Hmaster.Avatar yako imetulia,mambo ya wapi hiyo?
 
kama wamjua mkeo ni mtu wa wivu bora umwambie uongo unaofanana na ukweli, kwa case yako hapo usingemwabia unampeleka mwanamke tegeta bora ungemdanganya kuna mzigo unaenda chukua/peleka tegeta, dar inaeleweka kwa foleni so angekuelewa. we mtu mzima unatunga uongo ambao ataelewa utakaokupeleka tegeta!
 
Lakini kumbuka wakati wa kula kiapo cha ndoa tuliahidi kuambiana ukweli wakati wote, ina maana sasa tunakiuka kufuata mafundisho ya ndoa na badala yake tunaridhishana tu? Hivi hawa akina rose'80, michelle, DE, AD, Lizy, mariarose na wengine wakiwa kama wanawake sijui au miavator tu wao wanasemaje? Mi nshachoka na sasa nataka kuwa mwongo wa kimataifa (IL). Au turudi tena kwa baba paroko sijui?
 
Juzi nilikuwa maeneo ya Ubungo ambapo nilikutana na dada furani akiwa na watoto wa2 na mizigo kadhaa na baada ya kusalimiana aliniomba nauli ya daladala ili aende Tegeta kwa dada yake kwani alikuwa ameibiwa pochi yake ambayo ilikuwa na pesa akiwa safarini kutokea Songea. Mimi kwa vile nilikuwa na gari na kwa namna alivyoonyesha huzuni niliona bora nimchukue tu kwenye gari yangu hadi Tegeta kisha nikarudi hadi Magomeni ninapoishi. Kwa sababu ya foleni nyingi na muda ulipita sana kabla ya kurudi home, hata hivyo my wife wangu nilimweleza kila kitu lakini badala ya kuona umuhimu wa mimi kumsaidia mwanamke mwenzake yeye alikwenda mbali zaidi na aliamua kukata simu na hakupatikana hadi nafika home. Baada ya kufika nikamkuta tayari yupo kitandani akiwa na nguo zake zote, eti ndo keshakasirika na kuamua kulala hiyo saa tatu na wakati huwa tunalala hata saa 5 kila siku. Nilipojaribu kumwamsha ili aniandalie chakula alinijibu niende kula kwa malaya niliyemsindikiza Tegeta. Nilijitahidi kumwelewesha lakini ilishindikana. Nikajiandalia chakula mwenyewe, nikaoga na kisha kulala kwa maana kwa hali hiyo hata kumchombeza sikuweza. Sasa swali ni je Ukweli na Uwongo upi hudumisha ndoa, au vyote? Wenye experince na mambo haya waweke hapa maana sasa najiandaa kuwa mwongo kwa vile ukweli umenitokea puani. Na kama wanawake humu jf watueleze wenyewe kipi wanataka kutoka kwetu kati ya hivyo vitatu ili wawe na amani. Nawasilisha!

Mkuu nimekupata..ushauri wangu sema ukweli..ingawa siku mbili tatu bibie atanuna lakini akiona umekazania ukweli wako atakubali..ila ukipanic na kubadili sentensi ataona umeongopa..Pia kikubwa kama amenuna usimfuate nawe ukanuna utakuwa umepoteza point zote…If you are innocent..you will be innocent forever..Najua hali kama hiyo ina-disturb sana..na yataka moyo lakini ndugu yangu epuka “nidhamu ya woga” ..
 
Hmaster hongera kwa kua na roho nzuri yenye huruma na pia kwa kua mkweli.

Wewe baki na ukweli wako..atakasirika kwa muda ila baadae atapotezea au atakuelewa.Ukianza kudanganya jua kabisa unaweza kudanganya kitu kidogo sana kisicho na maana kikaja kukuletea matatizo makubwa sana kwenye ndoa yako.Imagine ulivyomjulisha unaenda Tegeta kama ungemwambia unapeleka mzigo au unamfuata mtu alafu bahati mbaya ukapata ajali.Aje kugundua kwenye gari ulikua na mwanamke mwenye mtoto kwa jinsi anavyoonekana ana wivu angeshakusingizia huyo ni mwanamke wako na mtoto ni mwanao ndoa imekufa.Uongo hata siku moja haulipi....jitahidi tu kua unamweleza na kumwelewesha taratibu bila kua mkali!
 
Juzi nilikuwa maeneo ya Ubungo ambapo nilikutana na dada furani akiwa na watoto wa2 na mizigo kadhaa na baada ya kusalimiana aliniomba nauli ya daladala ili aende Tegeta kwa dada yake kwani alikuwa ameibiwa pochi yake ambayo ilikuwa na pesa akiwa safarini kutokea Songea. Mimi kwa vile nilikuwa na gari na kwa namna alivyoonyesha huzuni niliona bora nimchukue tu kwenye gari yangu hadi Tegeta kisha nikarudi hadi Magomeni ninapoishi. Kwa sababu ya foleni nyingi na muda ulipita sana kabla ya kurudi home, hata hivyo my wife wangu nilimweleza kila kitu lakini badala ya kuona umuhimu wa mimi kumsaidia mwanamke mwenzake yeye alikwenda mbali zaidi na aliamua kukata simu na hakupatikana hadi nafika home. Baada ya kufika nikamkuta tayari yupo kitandani akiwa na nguo zake zote, eti ndo keshakasirika na kuamua kulala hiyo saa tatu na wakati huwa tunalala hata saa 5 kila siku. Nilipojaribu kumwamsha ili aniandalie chakula alinijibu niende kula kwa malaya niliyemsindikiza Tegeta. Nilijitahidi kumwelewesha lakini ilishindikana. Nikajiandalia chakula mwenyewe, nikaoga na kisha kulala kwa maana kwa hali hiyo hata kumchombeza sikuweza. Sasa swali ni je Ukweli na Uwongo upi hudumisha ndoa, au vyote? Wenye experince na mambo haya waweke hapa maana sasa najiandaa kuwa mwongo kwa vile ukweli umenitokea puani. Na kama wanawake humu jf watueleze wenyewe kipi wanataka kutoka kwetu kati ya hivyo vitatu ili wawe na amani. Nawasilisha!
Heshima kwako Hmaster,kiongozi nadhani hapo kwako kuna tatizo labda uniambie hiyo ndoa yako ina week ya pili hivyo umjui vilivyo mkeo,mi nadhani majibu au sababu ambazo ulipaswa kumpa mwenza wako ni zile zinazojenga kutokana na unavyomuelewa mwenza wako huyo,kwa mfano kama unatambua ni mwenye wivu kupindukia juu yako ungejua njia mbadala ya kumwambia kilichojiri kuliko kumweleza ukweli ambao kwake ni uongo.Hivyo basi kusema ukweli au uongo katika maisha ya ndoa au ya mahusiano yote ni sawa iwapo lengo ni kujenga.Mfano mimi naweza kudanganya leo kwa lengo la kujitetea kama mwenza wangu hayupo kwenye mood,then baada ya siku kadhaa tukiwa wote tupo kwenye mood naweza kumwambia,"unajua dear last week ilibidi nikudanganye maanake ulikuwa umekasirika sana lakini ukweli ilikuwa hivi............" i mean umedanyanya then umeungama uwongo wako hivyo inakuweka huru tena....Mjue mwenza wako kiongozi japo kwa kiasi kidogo tu.
 
Hmaster hongera kwa kua na roho nzuri yenye huruma na pia kwa kua mkweli.

Wewe baki na ukweli wako..atakasirika kwa muda ila baadae atapotezea au atakuelewa.Ukianza kudanganya jua kabisa unaweza kudanganya kitu kidogo sana kisicho na maana kikaja kukuletea matatizo makubwa sana kwenye ndoa yako.Imagine ulivyomjulisha unaenda Tegeta kama ungemwambia unapeleka mzigo au unamfuata mtu alafu bahati mbaya ukapata ajali.Aje kugundua kwenye gari ulikua na mwanamke mwenye mtoto kwa jinsi anavyoonekana ana wivu angeshakusingizia huyo ni mwanamke wako na mtoto ni mwanao ndoa imekufa.Uongo hata siku moja haulipi....jitahidi tu kua unamweleza na kumwelewesha taratibu bila kua mkali!
Sister Lizzy,asilimia kubwa ya ndoa zenye amani na zinazodumu zimejaa uwongo kuliko ukweli,ingawa si maanishi uwongo wa "kujiiba "natumai unajua nachomaanisha kwenye bold hapo...kwa mfano ni mwezi wa tano nadaiwa 'Nadia' nina mambo mengine mengi yananizunguka mfuko hautoshelezi kwa yote at a time inabidi ilo la nadia nidanganye na mtu analidhika na furaha tele,Je nikimpa makavu si itakuwa hatari Sis? hivyo uwongo katika maisha ya mahusiano yenye amani haukwepeki kabisa.
 
Well kama uongo kwako unasaidia mi ni nani hata nikwambie uache?!Endelea tu ila jua kwamba mtu mzima hadanganyiki kila siku...na kama ukweli tu anakua mgumu kuukubali na kurlewa imagine siku atakapogundua unamdanganya tena akiwa na uhakika....ndo utazushiwa mpaka yasiyo zushika.Alafu kama hutojali mimi kuuliza unalazimika vipi kumdanganya mkeo mambo yahusuyo pesa?!Kwani yeye hajua hali yenu ilivyo?!Hamna mambo ambayo mmeyawekea kipaumbele kwa pamoja?!Nauliza tu maana kitu kama hicho inabidi nacho umdanganye wakati na yeye yupondani ya hiyo ndoa ni KAAZI KWELI KWELI.Samahani kama ntakua nimekukwaza!
 
Mkeo hawezi kukusifu kwa ushujaa wako kumpeleka huyo mama tegeta, wanawake wanajuana, Just danganya hatakama ilikuwa jambo jema they don't wan't you as a hero kwa wa dada wengine! and they don't trust us at all
 
Kuna ya kusema na ya kutokusema bora ukae kimya tu, kama hapo ungenyamaza labda mkeo anakujua kabisa wewe sio mtu wa kutoa misaada ya aina hiyo, ghafla umempeleka mwanamke huyo tegeta, hata mimi pangechimbika tu, kwa nini usingempeleka stand ukampa alf kumi akasepa zake
 
We bora ulimwambia ukweli,huo ni wivu tu ulikuwa unamsumbua hamna lolote,unajua hawa watu bwana wako complex sana.Hapo angeranza kukuambia yani huyo ndio umemwona muhimu kuliko mimi etc but wanaume huwa na moyo wa huruma siku zote.Ungemdanganya then upate ajali mwenge na wewe ulimwambia uko posta unafikiri ingekuwaje?
 
Well kama uongo kwako unasaidia mi ni nani hata nikwambie uache?!Endelea tu ila jua kwamba mtu mzima hadanganyiki kila siku...na kama ukweli tu anakua mgumu kuukubali na kurlewa imagine siku atakapogundua unamdanganya tena akiwa na uhakika....ndo utazushiwa mpaka yasiyo zushika.Alafu kama hutojali mimi kuuliza unalazimika vipi kumdanganya mkeo mambo yahusuyo pesa?!Kwani yeye hajua hali yenu ilivyo?!Hamna mambo ambayo mmeyawekea kipaumbele kwa pamoja?!Nauliza tu maana kitu kama hicho inabidi nacho umdanganye wakati na yeye yupondani ya hiyo ndoa ni KAAZI KWELI KWELI.Samahani kama ntakua nimekukwaza!
Asante,ujanikwaza hayo ni maoni yangu na hayo ni ya kwako,na hapo nimejaribu kutoa mfano ambao unaweza kunikuta na nikajaribu kutumia uwongo kuweka mambo sawa ingawa hauna uhalisia...Pia sidhani kama mnaweza kukubaliana kila kitu katika maisha ya mahusiano labda kama mmoja wapo anaburuzwa,hivyo hata katika mambo ambayo mnaweza kuyapa kipaumbele mnaweza kushindana pia,itakuwaje kama yeye kumiliki kwanza usafiri ndilo liwe la kwanza then mengine yafatie? Maisha ya mahusiano ni sanaa na waigizaji ni wale ambao wako katika hayo mahusiano kwa mtazamo wangu.
 
master, ukweli utakuweka huru daima. kumbuka njia ya mwongo ni fupi na ukitaka kuwa muongo usiwe msahaulifu ili uweze kkuendelea kudanganya kila mara ili kuulinda uongo wa kwanza lazima ukumbuke vema kuhusu uongo wa kwanza,je huoni kama kusema uongo kutakugharimu zaidi kuliko kuwa mkweli? lakini yote hayo pia yanategemea sana na aina ya mwenzi ulienae, uwezo wake wa kufikiri na kuchanganua mambo, kiwango chake cha uelewa wa mambo, maisha yake/yenu ya nyuma n.k. nina maana kama upeo wake wa kutafakari mambo ni mdogo basi huyo akidanganywa anaridhika zaidi kuliko kuambiwa ukweli, au kama ni mwenye wivu wa ajabu ajabu basi huyo huridhika kuambiwa mambo mazuri tu hata kama ni ya uongo, lakini kwa mwanamke aliyepevuka akili hupenda kujua ukweli. na kama una historia ya kuwa mkweli basi mkeo atakuelewa tu kuwa hiyo ndio tabia yako na wala hawezi kukushuku kwa lolote baya, ila kama una historia ya kutokuwa mwaminifu hapo usimlaumu sana huyo mkeo kwani alishaumwa na nyoka!
 
Kuna ya kusema na ya kutokusema bora ukae kimya tu, kama hapo ungenyamaza labda mkeo anakujua kabisa wewe sio mtu wa kutoa misaada ya aina hiyo, ghafla umempeleka mwanamke huyo tegeta, hata mimi pangechimbika tu, kwa nini usingempeleka stand ukampa alf kumi akasepa zake

Undhani hilo la kumpa buku 10 huyo mdada ndio lingemlidhisha wife, au ulitaka baadaye niuchune tu bila kumpa mkasa huo?
 
Msemakweli ni mpenzi wa mungu. Mie na kusifu kwa ukweli wako.
Kudanganya: Fikiria kama ungedanganya alafu unapata ajari, unakutwa wewe na mwanamke na watoto ndani ya gari mumeumia, je unafkiri mkeo angekufikiriaje? Angekuona muongo na sio muaminifu. Bora ulivo muambia ukweli maana baadae atagundua kama angekuwa mpenzi wako husinge muambia, ungeficha. Ni wivu tu unamuangaisha sio lengine.

Jiulize hata ingekuwa wewe mwenyewe kama mkeo angetoa msaada kama uwo kwa mwanaume na kuchelewa kurudi home ungejiskiaje? Sababu msaada hata wanaume wanaitaji pia. Nazani hata wewe ungekasilika pia, ungeona wivu na ungefikiria vingine.

Mwanaume wengine akili zenu fupi bana, munafanya vitu bila kuzingatia. Mtu alie kuwa ktk ndoa hatakiwi kufanya vitu kama hivyo bila kumshirikisha mwenzawake. Kama ungelikuwa na akili nzuri ungempa nauli huyo dada ukawai home kwa mkeo mda unao takiwa.
Au ungempigia sim mkeo na kumuliza je umpe nauli au umuendeshe huyo dada. Munayataka wenyewe sababu hamtumii akili.
 
Kuna ukweli mwingine ni noma hausemeki
 
Kaka pole sana, sio kila siku lazima useme ukweli hata uongo unasaidia sana kujenga ndoa, kwa hili suala lako ungemdanaganya tu mama asikngekuwa vile ulivyomkuta kwa mfano ungesema nilikutana na rafiki yangu (wa kiume) pale Ubungo akaniomba nimpeleke Tegeta hivyo nimechelewa kurudi kwa sababu ya msongamano wa magari, hapo ungekuwa salama kwamba ni kweli Tegeta umeenda, hata kama kuna mtu aliona gari lako angeshuhudia hivyo hivyo ungebaki salama.

Unapoishi na mkeo jaribu kuishi kwa akili kwa sababu unaishi na kiumbe dhaifu (sio maneno yangu jamani, ni biblia imesema, akina dada msinishambulie tafadhali).
 
Kuna ukweli mwingine ni noma hausemeki

Well, kwaiyo umekubali kudanganywa kuliko kuambiwa ukweli? hakuna ukweli husiosemeka, hata mtu alie ua akisema ukweli kama ameua anasameheka, kuliko alie ua na akakataa. Ukweli unajitokeza wenyewe hata kama ikachukua miaka 10, hapo uenda ukaonekana mshenzi, husie aminika, na ukaonekana umefanya mengi yasio ridhisha na kufanya siri, jamii ikakuzodoa.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom