Ukweli mchungu: Magufuli atashinda tena 2020

Ukweli mchungu: Magufuli atashinda tena 2020

Kwa katiba iliyopo lazima ashinde
Haukuwa na haja ya kuandika uzi mrefu na kutumia nguvu nyingi
Wakati jibu ambalo ni fupi linajulikana!

Ova
 
Nadhani uko sahii kabisa mtoa uzi, personally nilishalijua hili kitambo. Upinzani unazidi kujikanyaga wenyewe hata haujui ushike lipi uache lipi. . . . .ukifika muda wa kunchagua mgombea wao wa urahisi ndio yatadhihirika haya maana wenye ambitions hizo ni wengi sana
 
Sipingi ulichoandika lakini badala ya kusema Magufuli atashinda tena ingefaaa usema "atatangazwa tena mshindi" . Hoja yangu ni kuwa kwa mfumo na tume iliyopo haitatokea vinginevyo.
 
Nadhani uko sahii kabisa mtoa uzi, personally nilishalijua hili kitambo. Upinzani unazidi kujikanyaga wenyewe hata haujui ushike lipi uache lipi. . . . .ukifika muda wa kunchagua mgombea wao wa urahisi ndio yatadhihirika haya maana wenye ambitions hizo ni wengi sana
unaamini jpmi Leo akigombea kupitia upinzani atashinda
 
unaamini jpmi Leo akigombea kupitia upinzani atashinda
JPM hawezi kugombea upinzani kwasababu he is the most hated person huko so hawawezi kumpokea. Ikitokea amehamia upinzania basi amini kwamba LISSU, MBOWE na miamba mingine mingi itakuwa radhi kuachana na shughuli za siasa kuliko kumuunga mkono. Na upinzani kumpa ticket JPM ya kugombea yatakuwa ni maajabu ya dunia na amini usiamini HATOSHINDA hata
 
muwe mnafikiria kabla ya kuandika! kwani kipindi katiba ya CCM inafanyiwa marekebisho juu ya uteuzi wa mgombea wa CCM katika kiti cha urais kupita moja kwa moja pasipo mchujo-ulikuwa wapi?
 
JPM hawezi kugombea upinzani kwasababu he is the most hated person huko so hawawezi kumpokea. Ikitokea amehamia upinzania basi amini kwamba LISSU, MBOWE na miamba mingine mingi itakuwa radhi kuachana na shughuli za siasa kuliko kumuunga mkono. Na upinzani kumpa ticket JPM ya kugombea yatakuwa ni maajabu ya dunia na amini usiamini HATOSHINDA hata
kwa hiyo upinzani hautakiwi whatever candidate?.
 
Naam, Magufuli anawafanyia udikteta Wapinzani lakini hata mkoloni alifanya hivyo kwa TANU lakini uhuru ukapatikana. In fact, huo udikteta wa Magufuli unavisaidia baadhi ya vyama kuficha udhaifu wake no wonder vimekuwa mahiri kudandia matukio badala ya kuwashawishi Watanzania kuwa vyama hivyo vinaweza kuwa mbadala wa CCM.
Mkuu andiko hili limeonyesha hujui kitu wewe ni mpiga domo tu! Mkoloni alitoa uhuru wa bendera kwa matakwa yake, hakuna cha TANU wala Nyerere walioweza kushindana na hao wakoloni. Jiulize ni kwanini mifumo mingi ya nchi hii bado ni ile ile ya wakoloni..?!
 
yani alichokiandika mtoa mada kinadhihilisha kabisa baadhi ya watanzani ni kama kondoo unakuta ni mwanachama wa kukubali kila kitu hajui hata chama chake kimetoka wapi,kilipo na kinaelekea wapi.huyu mtoa mada angekuwa najua asingethubuti kuongea utumbo kuwa JPM na kuteuliwa na CCM kupeperusha bendera tena.ninawashangaa hata hao wanaomkomalia membe kuwa anafanya siasa ili ateuliwe na chama 2020 si bure akili zao zitakuwa na matope huku wanajua fika kulifanyika mabadiliko ya katiba ya CCM juu ya hilo swala.

MABADILIKO ya Katiba ya CCM yamempa ulaji Mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais wa nchi, John Magufuli, kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho 2020 bila kupingwa na mwanachama mwingine ndani ya chama.

Kutokana na mabadiliko hayo, Mwenyekiti wa CCM amepewa ruhusa ya kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho kwa kipindi cha pili bila kupingwa na mwanachama yeyote ndani ya chama isipokuwa atashindana na wagombea wa vyama vya upinzani.

Hivyo, kama kulikuwa na mwanachama yeyote mwenye nia au ndoto za kuomba au kuwania nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu ujao wa 2020, asubiri baada ya mwenyekiti wa sasa kumaliza kipindi cha pili, labda asubiri 2025.

Mabadiliko hayo yaliyopitishwa na Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM uliofanyika Machi 12, mwaka huu, kwenye Ukumbi wa Kikwete mjini Dodoma yaliridhiwa kwa kauli moja na wajumbe wote wa mkutano huo.

Katiba itakayotolewa baada ya marekebisho haya itakuwa toleo la 13 katika mabadiliko ambayo wakuu wa chama hicho tawala wamesema yamelenga muundo, mfumo, uongozi na utendaji wa viongozi wa chama tangu ngazi ya shina hadi Taifa.

Kabla ya mabadiliko hayo ya karibuni, CCM ilikuwa inaruhusu mwanachama wake yeyote kujitokeza kuwania urais hata wakati wa muhula wa kwanza wa urais unapomalizika kwa rais aliyeko madarakani, ambaye kwa miaka yote tangu Uhuru ametokana na chama hicho kikongwe nchini.

Aidha, katika mkutano wa Machi 12, ulioongozwa na Mwenyekiti wake, Dk Magufuli uliridhia kwamba kura za maoni za wabunge zipigwe na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jimbo badala ya utaratibu wa zamani wa kupiga wanachama wote.

Vile vile kura za maoni za madiwani zitapigwa na Mkutano Mkuu wa Kata na sio wanachama wote kama ilivyokuwa katika Katiba ya CCM ya 1977 Toleo la 2012.

Marekebisho ya upigaji kura yanalenga kudhibiti taratibu za kura za maoni majimboni, kuepusha migawanyiko, kuziba mianya ya rushwa na kuepusha wapigakura mamluki.

Mabadiliko ambayo yaliyosomwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kabla ya Mwenyekiti Magufuli kuuliza wajumbe wa mkutano kuyaridhia, alisema yanalenga kupunguza vikao vya uamuzi kutokana na gharama kubwa za kuviendesha.

Pamoja na kupunguza vikao vya uamuzi, pia yanalenga kupunguza wajumbe mikutano katika ngazi mbalimbali ukiwamo Mkutano Mkuu wa CCM kutoka wajumbe 2,422 hadi 1,706 ambapo wajumbe waliobaki ni sawa na asilimia 70.4.

Aidha, wajumbe wa Halmashauri Kuu wamepunguzwa kutoka 388 hadi 163 ambao wamebaki wajumbe asilimia 40.01, pungufu ya nusu ya wajumbe wote.

Wakati wajumbe wa Kamati Kuu (CC) wemepungua kutoka 34 hadi 24 ambao ni sawa na wajumbe asilimia 70.6 waliobaki na kufanya idadi ya wajumbe waliondolewa kwenye vikao vitatu vya uamuzi kufikia theluthi moja ya wajumbe sawa na asilimia 33.43.

Kinana alisema, chama kimepunguza wajumbe katika ngazi za juu, ili kukirudisha chama kwa wananchi, au kwenye ngazi za chini ambako kuna wapiga kura.

“Uzito mkubwa umewekwa katika kuimarisha chama katika ngazi ya shina, eneo ambalo wapo wapigakura, kwa kufanya hivyo, chama kitakuwa karibu na watu, watakiona ni chama chao,” alisema Kinana.

Wajumbe wa mkutano huo maalumu waliridhia kwamba, wajumbe wa NEC watakuwa wanatokana na mikoa si wilaya kama ilivyokuwa awali, hivyo kila mkoa utakuwa na M-NEC mmoja, ikimaanisha kwamba hakuna tena MNEC wa wilaya.

Marekebisho hayo katika Ibara ya 61(d) yanaonesha kwamba wajumbe waliokuwa wanaingia katika mikutano hiyo kama makatibu wa fedha na uchumi kuanzia ngazi ya tawi hadi mkoa wamefutwa sambamba na makatibu wasaidizi wa mikoa na wilaya.

Katika futafuta hiyo, Kinana alitangaza kwamba wajumbe wawili wa kuchaguliwa kwenye kamati za siasa za mikoa na wilaya wamefutwa.

Mabadiliko hayo pia yamelikumba shirikisho la vyuo vikuu au mkoa wa vyuo vikuu wa CCM, ambayo ilikuwa taasisi inayojitegemea, sasa itakuwa Idara ya UVCCM na itawajibika chini ya jumuiya hiyo ya chama.

Lengo la mabadiliko hayo, kwa mujibu wa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole ni kukirudisha chama kwa wananchi, lakini pia ni kuongeza ufanisi na utendaji wa viongozi wake.

Pia ni kuzima tabia ya viongozi wachache kujilimbikizia nafasi nyingi za uongozi zenye kazi ya muda wote, ambao hushusha ufanisi na kupunguza tija.
 
kwa hiyo upinzani hautakiwi whatever candidate?.
Upinzani unatakiwa sana, bila upinzania chama kilichopo madarakani kitabweteka tu. Ni vile tu wapinzani wameishiwa strategies na focus. Wameishiwa mikakati
 
Hii si taarifa, ni kitu kilicho wazi. Safari hii atafikisha zaidi ya asilimia 70% believe me.
Mwaka 2015, alipata 58% pekee kutokana na ubovu wa watangulizi wake. Kipimo cha mafanikio yake subirini hata Uchaguzi wa Serikali za Mitaa tu wa 2019. Wapinzani wamenyang'anywa majimbo na kata kiulaini halafu hao ndio wampe shida Rais 2020?
Dreamliner tumeiona.
Ma-Airbus mengine yanatua soon.
2019 tayari mchuma wa SGR tunaanza kuupanda.

Kila kitu kinaenda sawa isipokuwa vilaza wachache wa mitandaoni wanaodhani mkulima kijijini anafikiria wabavyofikiria wao. Wapinzani wakati wa Kampeni watakuwa wanailalamikia Serikali kwa wananchi huko vijijini - eti oooohh, Serikali
  • imeminya demokrasia,
  • inawakamata Wapinzani kwa uonevu,
  • imefungia Bunge live,
  • imekataa mchakato wa Katiba mpya,
  • tumetengwa na mataifa ya nje. Na blah blah ...
Serikali inakuja na kuwaeleza wakulima vijijini kuwa imetoa:
  • Elimu bure,
  • Imesambaza umeme vijinini,
  • Imesambaza maji kwa kasi kubwa,
  • Imeboresha huduma za afya kwa kujenga hospitali na vituo vya afya,
  • Imeboresha miundombinu ya barabara vijijini (TARURA)
  • Imeboresha mazingira ya kibiashara ya wanyonge (machinga).
  • Imekuza usafirishaji kwa kuleta ndege, meli mpya, treni mpya, bandari kupanuliwa,
  • Imeboresha customer care maofisini, etc, etc, etc.
Jiulize hapo mkulima atampaje Mpinzani kura?

Elimu bure je imekidhi viwango?? Taaluma ya sasa ni bora kuliko ya miaka 10 nyuma?
Ndege sawa je zimekuza kipato cha taifa?, zimeongeza ajira?
SGR 2019 uongo Ila CCM watatumia kama point.
Kuhusu machinga wanamaeneo wala hawana kero zao za awali lakini mauzo yakoje??
Watabrag madawa, usimamizi mzuri lakini kuna vingi vya kucrush ukitoa upinzani na demokrasia .
Lakini watashinda uchaguzi kwa hata asilimia 90 yanaweza kua kama maigizo na si campaign tena nahisi hakuna atakayejaza watu katika mikutano yake
Maisha ya mkulima ni mabaya saizi kuliko jana yaani kama mtu mwaminifu mwenye kipato cha kati kapigika atakua kapuku aliyekua akiungishwa na wapiga dili??
 
Ukweli una sifa moja muhimu: kuuchukia ukweli hakuufanyi kuwa uongo. Na kuuchukia ukweli hakuuzuwii kutokea.

Kwa wanaojali mahesabu, imebaki miezi 22 tu kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. Tunajua bayana kuwa tayari mgombea wa CCM ni Magufuli. Naam, ukweli ndo huo maana kwa wanaoijua CCM wanafahamu fika kuwa hakuna nafasi ya kujitokeza Mwana-CCM wa kum-challenge.

Hapana, sio kwamba sheria inakataza bali ni muhimu kutambua kuwa CCM sio chama tu bali ni mfumo wa maisha. What I mean here ni kwamba, yeyote atakayeamua kuwa "Liwalo Na liwe" na kuamua kupambana na Magufuli kuwania kuteuliwa na CCM mwaka 2020 atakuwa anaweka rehani maisha yake ya kisiasa na kibinafsi. Jambo hili la ovyo kabisa linakera na kuchukiza lakini unfortunately ndio hali halisi hiyo.

Kitu pekee ndani ya CCM kinachoweza kumzuwia Magufuli ni yeye mwenyewe. Aidha aamue kuwa hatogombea au sijui aboronge kiasi gani. Lakini kutegemea sijui Membe, sijui Mwandosya, sijui nani ni kujaribu tu kujipa matumaini hewa.

Na ukweli mwingine mchungu ni kwamba njia pekee ya kumzuwia Magufuli mwaka 2020 ni ndani ya CCM. Lakini hilo nimeshaongelea hapo juu.

Kwanini ndani ya CCM na sio kwa Upinzani? Kwa sababu miezi 22 kabla ya uchaguzi, wapinzani wapo bize kumshangilia Membe badala ya kukaa kitako na kupanga mikakati ya ushindi 2020.

Naam, Magufuli anawafanyia udikteta Wapinzani lakini hata mkoloni alifanya hivyo kwa TANU lakini uhuru ukapatikana. In fact, huo udikteta wa Magufuli unavisaidia baadhi ya vyama kuficha udhaifu wake no wonder vimekuwa mahiri kudandia matukio badala ya kuwashawishi Watanzania kuwa vyama hivyo vinaweza kuwa mbadala wa CCM.

Chama kikuu cha upinzani Chadema bado kinakabiliwa na ombwe la ajenda. Ikumbukwe kuwa moja ya sababu zilizopelekea Chadema kukubalika kwa Watanzania wengi ni ajenda yake ya vita dhidi ya ufisadi.

Unfortunately, chama hicho kililazimika kutelekeza ajenda hiyo baada ya kumpokea Lowassa, mwanasiasa ambaye chama hicho kilimwandama kwa miaka tisa mfululizo kikimtaja kuwa "baba la ufisadi." It's neither rocket science nor brain surgery kwamba huwezi kumchafua mtu kwa miaka tisa kisha ukataka kumsafisha kwa miezi mitatu. Hiyo ni historia kwa sasa.

Ukijiuliza kitu gani kinaitambulisha Chadema kwa wananchi muda huu sidhani kama utapata jibu la kueleweka. We knew walikuwa mstari wa mbele dhidi ya ufisadi kabla ya ujio wa Lowassa. Kwahiyo ajenda yao kuu ilikuwa vita dhidi ya ufisadi. Je kwa sasa ajenda yao ni ipi?

CUF is too fragmented to mount any upinzani wa maana. Na CUF has always been chama cha Zanzibar. Lakini pia mtihani mkubwa kwa CUF 2020 ni suala la "mgombea wa kudumu wa kiti cha urais" yaani Maalim Seif. Tayari kuna vuguvugu la kutaka mgombea mwingine baada ya Maalim Seif kushindwa mfululizo.

Na hilo la mgombea ni headache nyingine kwa Chadema. Lowassa alishatamka kuwa atagombea 2020. Haihitaji ufahamu mzuri wa siasa za Tanzania kujua kuwa mwanasiasa huyo amesha-expire kisiasa. Vipi kuhusu ambitions za both Sumaye na Nyalandu? Na vipi kuhusu chaguo la wengi ndani ya Chadema Tundu Lissu? Lakini kwa kuzingatia kilichojiri 2015, what about MAKAPI kutoka CCM? Membe may be?

Let's hope busara ita-prevail na chama hicho kitapata mgombea sahihi. Tatizo ni kwamba, muda hauko upande wao. Mwaka 2020 ni kesho kutwa tu na so far maandalizi ni as good as nonexistent.

ACT ya Zitto imeshindwa kujipanua na imeendelea kuwa "chama cha mtu mmoja" ambacho licha ya kuwa kinachofanya vema sana kuliko chama kingine chochote kile cha siasa katika ufuatiliaji wa Bajeti, ripoti ya CAG, nk, kimebaki kuwa kikundi cha harakati zaidi kuliko chama cha siasa.

Idea ya Zitto kuwaunganisha wanasiasa na wanaharakati kuunda democratic front ni nzuri lakini sana sana itaishia kukirahisishia kazi kitengo kuhujumu Umoja kusudiwa. Huwezi kukusanya kila Tom, Dick and Harry kwa vile tu "lengo lenu ni moja" na kutarajia kuking'oa madarakani chama ambacho kinafahamu fika nini kitawakumba viongozi wake kikitoka madarakani.

Yes, CCM kama taasisi ya kihalifu inafahamu fika kuwa ikipigwa chini, watajazana jela. And they are not that stupid kuruhusu hilo litokee kirahisi.

Which brings me back to kichwa cha habari kuwa unless kuna miujiza itakayotokea kati ya sasa na 2020, Magufuli atashinda tena katika uchaguzi mkuu ujao. Kirahisi tu.

Jiskie huru kutafsiri vyovyote vile andiko hili lakini naomba kukumbushia tena kwamba "kuuchukia ukweli hakuufanyi kuwe uongo."

Na jingine la mwisho ni kwamba wishful thinking haiwezi kuleta mabadiliko yoyote yale.

I stand to be corrected.
Naona ichaguzi umekaribia unatafuta pesa zongine tena kama ilivyokuwa 2015 ukalipwa mamilioni yako. Hapa wanafiki wote kama nyie tutawaona mnavyobadilika badilika ghafla kujaribu kumpleaz jambazi mwenzenu.

Haya endelea tena kaka Tenda inakija tena ujipigie milioni zako 100 za kampeni mitandaoni.
 
Hicho kikundi sijui taasisi ndani ya CCM nacho kimeshamchoka huyo jamaa yenu wanajuta kumpa kijiti na kwa sasa wanatamani kumnyang'anya hicho kijiti walichompa kwa bahati mbaya.
UTAWALA WA JPM UNAKOSEA KWENYE HII HALI NGUMU YA KIMAISHA KINCHI NA KIJAMII
 
Back
Top Bottom