Ukweli kuhusu wimbo wa Malaika

Ukweli kuhusu wimbo wa Malaika

Huu wimbo ni wa mfalme kichaa GK (King Crazy GK)
 
Bado nafikiri jina la kumpa wa kiume ila lazima liwe la kiswahili, so far nina Amani au Heri naendelea kufikiri mengine.

Malaika ni jina nililonalo kichwani toka miaka mingi. Vp wewe mkuu?
Ila kina Angel wanakuwaga vicheche hao! Jiandae.
 
Maana wanajionaga kama malaika kweli sasa hapo ndio shida huanzia hapo mjomba utapiga mpaka utaua jiandae babu.
 
Mimi ninachofahamu ila sina uhakika nacho kwa asili mia mia moja ni kuwa wimbo huo uliimbwa/ulitungwa na jamaa mmoja mchaga alikuwa anapiga muziki kutumia gitaa la galatoni anaitwa Frank. walijulikana kama Frank na dada zake baada ya hapo ndipo Fadhili William akauiga.
 
Wimbo ulitungwa na mtanzania aliyekuwa anapiga kwenye bend moja uko nairobi ila alirudi tanzania kabla ajaimba kwenye bend yake, ile bend wakaupiga wimbo huo, na maria makeba aliusikia wimbo akiwa kenya akauliza wimbo katunga nani, akambiwa mtunzi ni mtanzania alirudi kwao tanzania, ndo akawaomba kurudia wimbo na akasema wimbo ni kutoka tanzania.
Hii habari nilimsikia mtunzi wa wimbo huu akiojiwa, alikuwa anaishi dubai sijui kama bado yupo hai?
 
Huu wimbo kwa mara ya kwanza ulitungiwa Kigoma Ujiji eneo moja linaitwa Buzebazeba, aliutunga kijana mmoja wa Kiswahili mwenye asili ya Kikongomani lakini alikuwa na asili ya Zanzibar kwa kuwa mama alikuwa Mzanzibari na baba alikuwa Mkongomani,aliuimba akiwa anamuimbia dada mmoja ambae baba yake alikuwa mfanyabiashara maarufu wa Kinyakyusa ambae mpaka sasa anavuma bado na biashara mzee Mwakalindile.
Wimbo huu ni maarufu Kigoma kuliko sehemu nyingine yeyote Tanzania kwa kuwa ndiko chimbuko la wimbo huu
 
habarini wadau,

leo nimekumbuka hili na kuona sii vibaya tukashare:

Wimbo wa "malaika" ni wimbo unaofahamika sanaaa sio afrika tu bali hata katika mabara mengine,nakumbuka mwaka 2011 nikiwa chuoni walikuja wanafunzi kutoka asia na waliusikia huo wimbo kwenye laptop ya mtu na mmojawapo (mkorea) aliweza kuuimba nusu na kuonesha kuupenda sana.

Mwaka huo huo mwishoni nikiwa nasikiliza kipindi cha miziki ya zamani na historia zake nilisikia kuwa wimbo wa malaika ulitungwa na kuimbwa kwa mara ya kwanza kabisa mkoani arusha(eneo la kaloleni ya leo) kabla kabisa ya uhuru,nilitafituli zaidi kwa kuwauliza baadhi ya wazee wapenda miziki nikaambiwa huu wimbo uliimbwa na kijana aliyekuwa akichunga mbuzi karibu na maghorofa ya wahindi kipindi hicho kumwimbia binti mmoja mwenye asili ya asia,na kurekodiwa na binti huyo kwenye redio yake ndogo.

Baada ya hapo binti yule alikuwa na uhusiano na kijana yule ila uhusiano wao ulikatishwa na wazazi pamoja na ndugu wa binti.binti yule alihifadhi ile rekodi ya wimbo na kuja kuirudisha kwa muimbaji naye akawapa baadhi ya watu,

baada ya hapo studio za kwanza kabisa arusha kama radio habari maalum(rhm) zikaanza kuupiga wimbo huo pamoja na kwaya za mwanzoni na kukubalika sana.

Leo hii wimbo huu bado ni maarufu sana na ulirudiwa kuimbwa na mwimbaji maarufu miriam makeba (mama afrika) na wengine. Binafsi naupenda huu wimbo.
majengo mkoani kilimanjaro
na kwa mara ya kwanz aulirekodiwa kenya
 
Ila kina Angel wanakuwaga vicheche hao! Jiandae.

Mkuu ni Malaika sio Angel. Musa ni Musa tu hata aende Ulaya haitwi Moses.

Nitakua mkali kwa wote wataojifanya wazungu na kumuita Angel, ni mwiko mwanangu kuwa na jina la kizungu
 
Back
Top Bottom