Bufa
JF-Expert Member
- Mar 31, 2012
- 13,644
- 28,801
Atakuwa na mbawa huyo atakusumbua sana:flypig:
Hahah itakua poa tu.
Atakuwa na mbawa huyo atakusumbua sana:flypig:
Kwa kufuatilia mabishano kama haya utajua kuwa waafrika na watu weusi kwa ujumla tuna tatizo moja kubwa sana ambalo mababu zetu walilifanya na litatugharimu mpaka kesho. Tatizo hilo ni lack of documentation. Kila kitu kilikuwa ni kuhadithiana kwa mdomo tuu bila maandishi au vitu kuwa rasmi. Hakuna aliyehangaika kuweka vitu kimaandishi kabisa. Tatizo kama hili limepelekea mpaka leo wamarekani weusi hawajui exactly asili yao kwa Afrika ni sehemu gani hasa. Wengine watakuambia Ethiopia, Senegal, Nigeria n.k yaani kila mtu anavyojisikia. Ukiangalia vizazi ambavyo vimepita tangu wapelekwe utumwa ni vichache sana kupoteza kumbukumbu kubwa kama ya wametokea wapi Afrika! Tatizo hili pia lipo upande wa Afrika hakuna kumbukumbu au hesabu ya waliochukuliwa utumwa upande huu na walipelekwa wapi na akina nani?
Nadhani utakua ni huu wa Manu Dibango - Ayé Africa utafute.
Nadhani utakua ni huu wa Manu Dibango - Ayé Africa utafute.
Naomba mnisaidie kujua jina la wimbo wa aei afrika u naopigwa radio DW wanapokuwa wanasoma Habari za Africa...naupenda sana ila sijui muimbaji...
Mtunzi na muimbaji na Franklin Boukaka, ni muimbaji na alikua ni mwanaharakati wa kupigiwa mfano ambae aliuawa wakati wa jaribio liloshindwa huko Congo ya Brazzavile
Aliuawa mwaka 1972 Akiwa na umri wa miaka32.
natamani sana kuijua historia halisi ya huu wimbo. comments za humu zimenichanganya tuHabarini wadau,
Leo nimekumbuka hili na kuona sii vibaya tukashare:
Wimbo wa "Malaika" ni wimbo unaofahamika sanaaa sio Afrika tu bali hata katika mabara mengine,nakumbuka mwaka 2011 nikiwa chuoni walikuja wanafunzi kutoka Asia na waliusikia huo wimbo kwenye laptop ya mtu na mmojawapo (mkorea) aliweza kuuimba nusu na kuonesha kuupenda sana.
Mwaka huo huo mwishoni nikiwa nasikiliza kipindi cha miziki ya zamani na historia zake nilisikia kuwa wimbo wa malaika ulitungwa na kuimbwa kwa mara ya kwanza kabisa mkoani Arusha(eneo la kaloleni ya leo) kabla kabisa ya uhuru,nilitafituli zaidi kwa kuwauliza baadhi ya wazee wapenda miziki nikaambiwa huu wimbo uliimbwa na kijana aliyekuwa akichunga mbuzi karibu na maghorofa ya wahindi kipindi hicho kumwimbia binti mmoja mwenye asili ya Asia,na kurekodiwa na binti huyo kwenye redio yake ndogo.
Baada ya hapo binti yule alikuwa na uhusiano na kijana yule Ila uhusiano wao ulikatishwa na wazazi pamoja na ndugu wa binti.Binti yule alihifadhi ile rekodi ya wimbo na kuja kuirudisha kwa muimbaji naye akawapa baadhi ya watu,
Baada ya hapo studio za kwanza kabisa Arusha kama Radio Habari Maalum(RHM) zikaanza kuupiga wimbo huo pamoja na kwaya za mwanzoni na kukubalika sana.
Leo hii wimbo huu bado ni maarufu sana na ulirudiwa kuimbwa na mwimbaji maarufu Miriam Makeba (Mama Afrika) na wengine. Binafsi naupenda huu wimbo.
Kweli mtunzi original ni Mzee ADAM Salim Mallya mkibosho, alimtungia Halima Maruwa msichana aliyempenda ila wazazi wa msichana wakamwozesha tajiri chitora baada ya kuona Adam hakuwa njema saaana, ndipo Adam katika udhuni na kunung'unika yake akatoka na wimbo "wimbo wa malaika' kibaya zaidi akusajili/ hakuomba hati miliki. Hii ilifanya fadhili William mkenya Kwa namna yake Kwa vile alikuwa tajiri na mmiliki studio akajimilikisha na kuwa na hati miliki yeye, na amefaidika kweli kweli huyu fadhili Kwa kulipwa na waliorudia rudia wimbo hapa Dunia huku Mzee ADAM Salim akiachwa bila kitu. Watu au makundi maarufu waliorudia wimbo malaika' kama BONEY M amemwa acknowledge MZEE ADAM SALIM KAMA MTUNZI WA KWANZA.Mtumzi ni Adam Salim alikuwa ni Mtanzania aileishi Nairobi, na alikuwa ni mechanics wa magari alimuimbia Halima mnamo mwaka 1945-46
Wakenya kwa haya ni kawaidaKweli mtunzi original ni Mzee ADAM Salim Mallya mkibosho, alimtungia Halima Maruwa msichana aliyempenda ila wazazi wa msichana wakamwozesha tajiri chitora baada ya kuona Adam hakuwa njema saaana, ndipo Adam katika udhuni na kunung'unika yake akatoka na wimbo "wimbo wa malaika' kibaya zaidi akusajili/ hakuomba hati miliki. Hii ilifanya fadhili William mkenya Kwa namna yake Kwa vile alikuwa tajiri na mmiliki studio akajimilikisha na kuwa na hati miliki yeye, na amefaidika kweli kweli huyu fadhili Kwa kulipwa na waliorudia rudia wimbo hapa Dunia huku Mzee ADAM Salim akiachwa bila kitu. Watu au makundi maarufu waliorudia wimbo malaika' kama BONEY M amemwa acknowledge MZEE ADAM SALIM KAMA MTUNZI WA KWANZA.
Mzee ADAM ni marehemu alifariki mwaka 90 au 80 mwishoni.
Kweli kabisa na wakenya kwa kuiba na kusema ni vyao kawaida sanaKweli mtunzi original ni Mzee ADAM Salim Mallya mkibosho, alimtungia Halima Maruwa msichana aliyempenda ila wazazi wa msichana wakamwozesha tajiri chitora baada ya kuona Adam hakuwa njema saaana, ndipo Adam katika udhuni na kunung'unika yake akatoka na wimbo "wimbo wa malaika' kibaya zaidi akusajili/ hakuomba hati miliki. Hii ilifanya fadhili William mkenya Kwa namna yake Kwa vile alikuwa tajiri na mmiliki studio akajimilikisha na kuwa na hati miliki yeye, na amefaidika kweli kweli huyu fadhili Kwa kulipwa na waliorudia rudia wimbo hapa Dunia huku Mzee ADAM Salim akiachwa bila kitu. Watu au makundi maarufu waliorudia wimbo malaika' kama BONEY M amemwa acknowledge MZEE ADAM SALIM KAMA MTUNZI WA KWANZA.
Mzee ADAM ni marehemu alifariki mwaka 90 au 80 mwishoni.