JINSI YA KUTUMIA JICHO LA TATU
Unajua mtu anaishi katika sehemu mbili Katika ulimwengu wa 3D na katika ulimwengu wa 4D.
D= Dimension.
Katika ulimwengu wa 3D ndio huu unaoniwezesha sasa naandika haya kwenye kompyuta na nikiangalia ninaona jua magari na tunaenda shule kusoma nk. Ni ulimwengu huu ambao umeuzoea siku zote tuna kula na kunywa. Katika ulimwengu huu tunatumia macho mawili na huku tunashangaa kwanini watu wengine wanafanya miujiza wakati sisi wengine hatuwezi? Au kwanini watu wengine wanatabiri wakati sisi hatuwezi?
Hawa watu wanaweza wakafanya hivyo kwa sababu wanaweza wakatumia jicho la tatu ambalo mtu akiwa mtoto mdogo au mchanga huwa lipo active. Na kadri anavyozidi kuwa mkubwa jicho hilo hufumbwa na kufanya asiweze kuona tena vitu vilivyo kwenye 4D.
Watu wanafanya mambo hayo ni kwa sababu wanauwezo wa kufumbua jicho la tatu na kuona vitu vilivyo kwenye 4D. Huo uwezo wa kufumbua hilo jicho ndio unaosababisha watu wanafanya miujiza wanatabiri na wanafanya vitu vingi ambavyo havionekani.
Kwa sababu mtu amefumba jicho hilo kwa mda mrefu huwa inamchukua mda kuwa na uwezo wa kulifumbua jicho hilo. La kini kwa maelekezo maalumu jicho hilo linaweza likafumbuka. Jicho la tatu linakufanya uone ulimwengu mwingine tunaoishi sisi ambao ni mzuri sana. Tafauti na huu ambao umeharibiwa na watu wachache. Mantiki ya sisi kuwepo ni kuufanya ulimwengu huu ufanane na ulimwengu ulio kwenye 4D. Uoga na kuogopeshwa kumewafanya watu wasiweze kabisa kuingia katika ulimwengu huo.
Nitajaribu kueleze jinsi ya kuingia katika ulimwengu huo hatua kwa hatua na ndipo sasa utaanza kujielwea wewe mtu ni wa namna gani je ni nguvu gani uliyo nayo ambayo umefungwa na watu wachache walioweka kanuni zao ili wewe upumbazike.