Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Status
Not open for further replies.
...................Mwalimu wangu Maalim Haruna akisema, "Kila binadamu umuonae katika mgongo wa ardhi jua ana kitu kinamtisha hata akiwa na nguvu kiasi gani. ...............
Ok thats.......the hypothesis.............now lets see unavyotaka kutuonyesha hypothesisi hiyo inavyothibitishwa......kama uelezapo hapa chini.

.........Mimi nilkuwa kwa muda mrefu natafuta kitu kinachomtia hofu Nyerere. Nikakipata. Kwanza hakuwa anapenda kunasibishwa na waasisi waliomtangulia katika kupigania uhuru wa Tanganyika. Pili alikuwa akiuhofia sana Uislam................

1.KUTOKUPENDA HAIMAANISHI KUTISHIKA/KUOGOPA
2. KUHESHIMU HAIMAANISHI KUTISHIKA/KUOGOPA
3. MWL JKN ALISHIRIKIANA NA WAISLAM VIZURI TU KAMA MZEE WAKO ALIWEKWA KIZUIZINI ISIWE NDI SABABU YAKO YA KUTAKA KUGOMBANISHA HISTORIA KWA KUINGIZA UDINI................na vile vile usituchanganye

Kw ahiyo unataka kutuaminisha kuwa MWL JKN alijenga Msikiti Butiama kwa hofu ya UISLAM?

Halafu ushahidi huo hauendani kabisa na hypothesis iliyotolewa na Mwl wako.......tofautisha HOFU na CHUKI/WIVU/CHOYO/UBINAFSI..........nilidhani wewe ni mswahili mwenzetu au?

.............Ushahidi nimetoa ukumbini jinsi alivyowapa Kivukoni kazi ya kuandika historia ya TANU na ikaandikwa kwa sampuli ya kumpendeza yeye..................

NI upotoshaji kutumia shahidi zisizo shabihihiana na hypothesis ya Mwl wako...................kama ni mpira wa miguu..........Mwl Haruna alikupiga tobo/dobo............

Nilipoandika ile makala katika Africa Events (March/April 1988) magazeti yakakusanywa na kuchomwa moto. Hapo ndipo nilipojua kinachomtisha na ndiyo nikatoa anuani hii kwa kitabu changu: The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Utold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika.
..........mangapi yalikusanywa na kuchomwa ndugu yangu...........mbona unataka kuwapumbaza watu na fikra zako ambazo tayari zimeathirika na background yako.............ndugu?..............wee unazungumzia kuchomwa magazeti/vitabu.............vipi wengine waliofichwa na waliporudi wakawa mabubu..............wote wale walikuwa Waislam?.................Hivi MWL JKN alisumbua biashara za akina Sykes?................
 
Mtu mzima kuwa muongo wala haipendezi. Unasema sikukujibu na hii hapo juu nilikuwa namjibu nan na ninii? Si nilikuuliza kama kweli wakina Mwakagile wamenukuu paper zako verbati basi wanachosema ni kweli hata kama waliupata ukweli huo kwa njia ya udanganyifu? Na kama ni kweli basi hayo maneno yao ( ambayo unasema ni ya kwako) yanapinga hoja yako kuwa ni waislamu peke yao wakiongozwa na wakina Sykes ndio waliokuwa vinara katika kugombea uhuru wa nchi yetu. Tofauti na unavyotaka tuamini, ni wewe unaekacha kujibu maswali!

Amandla......

Jibu lenyewe unalosema ni hili ulipokuwa ukimjibu Mohammed:

"Cha msingi hapa ni je anayosema ni uongo? Kuwa hao wote hawakuhusika katika jitihada za kugombea uhuru? Kama Mwakikagile amenakili kazi yako na yote alioyaandika yamo kwenye kitabu chako basi huu si ushahidi tosha kuwa hata wewe unajua kuwa walihusika wengi katika kudai uhuru na sio waislamu au wakina Sykes au wazee wako peke yako? Kama ukweli huu unaujua na umeuandika kwenye kitabu chako kwa nini basi kwenye mihadhara yako hausemi hivyo bali unashikilia kuwa ni waislamu PEKE YAO ndio waliohusika katika mpambano huo na wakristu walibebwa tu? Na kama Mwakikagile amenakili kazi yako bila kukutaja kwa nini basi usimpleke kwa Pilato maana plagiarism ni kosa kubwa sana!! Lakini kama amekunukuu na kukutaja, hiyo ni kawaida katika uandishi kama wewe mwenyewe jinsi ulivyonukuu kazi za wengine. Mimi nimekuambia tangu mwanzo kuwa maandishi yako yanakushitaki maana humo humo una-refute haya unayoyasema hadharani kwa wale ambao ni wavivu wa kufikiri."

UCHAMBUZI WA AMI

Hapa ni pale uliposhikwa kuhusu nakili yako ya mtu aliyenakili kitabu cha Muhammed Said ukitaka kutetea kuwa kuna wakristo waliopigania uhuru ambao Muhammed hakutaka kuwataja.
Hilo haliwezi kuwa jibu bali ni ubabaishaji,na wewe kurudia suala hili kujaribu kujitetea ni kujipaka matope zaidi.Waswahili twasema Muungwana akivuliwa nguo huchutama.
Jibu hasa lingelikuwa kwa wewe kuleta majina mengine ambayo wewe unayo au umeyapata kwengine sio kwa Mwakikagile kutetea hoja yako.
Nimeona wanaukumbi wapya wanaingia kukusaidieni Fundi na Lole ambao ndio ninaowaona ni viongozi upande unaompinga Mohammed, lakini wewe na majibu yako hamna hadhi tena kuendelea kubishana na Mohammed Said,kuhusiana na hizi njama za kanisa kujikweza dhidi ya uislamu.
Hakuna pahala Mohammed kasema hivi kama unavyosema wewe
"Na kama ni kweli basi hayo maneno yao ( ambayo unasema ni ya kwako) yanapinga hoja yako kuwa ni waislamu peke yao wakiongozwa na wakina Sykes ndio waliokuwa vinara katika kugombea uhuru wa nchi yetu".
Kwani kuna tatizo gani kuona kitu ambacho kiko wazi kuwa Nyerere na serikali yake walikula njama kuwatenga waislamu katika historia ya kupigania Uhuru wa Tanganyika?.Bila kuwa ni njama si rahisi kwa binadamu wa kawaida kuwasahau watu aliocheza nao kwa muda mrefu iwe ni utotoni au kwenye siasa.
Mimi nina dondoo ya kisaikolojia ambayo nimeipata katika kajiutafiti wangu kuwa . CHAKULA KITAMU NA KISICHOSAHAULIKA NI KILE KILIWACHO UTOTONI.
Vyakula alivyokula Nyerere katika utoto wa siasa haikuwa rahisi kuvisahau.Huyu mtu alikuwa mbaya, mchoyo na asiyejua kulipa fadhila kwa mema ya wenzake.

Wakati umefika wa Serikali kuomba radhi kuhusiana na historia iliyopotoshwa.Katika kufanya hivyo historia iliyoandikwa na Kivukoni ichomwe moto hadharani siku ya sherehe za uhuru,watu waone kwenye runinga,na historia mpya chini ya jopo ambalo Mohammed Said atakuwa mjumbe iandikwe upya.
 
La sivyo ?
 
Naona wewe hapa si mchambuzi tu bali pia liwali. Utatoaje hukumu wakati wewe na Mohammed mko upande mmoja?
 
Kulikuwa na viongozi katika kila jimbo (mikoa ilivyokuwa inaitwa nyakati zile), na katika kila wilaya, waliopigania uhuru wa nchi yetu. Sehemu za pwani, wengi walikuwa ni Waislamu. Sehemu za bara wengi walikuwa ni Wakristo. Hata Dar es Salaam kulikuwa na Wakristo, na bara kulikuwa na Waislamu lakini Wakristo walikuwa wengi sehemu zingine za Tanganyika na siyo kama za pwani.

Tunapowazungumzia viongozi wa Tanganyika miaka ile, tusisahau kazi aliyofanya Oscar Kambona kama secretary-general wa TANU kusaidia kuijenga na kuikuza TANU na kueneza ujumbe nchi nzima kutoka makao makuu ya chama hicho. Hakuwa Muislamu. Alikuwa Muanglikana.

Ukienda Mwanza, utawakuta watu wengi wanaowakumbuka viongozi sehemu hizo waliosaidia kuijenga TANU; miongoni mwao, Paul Bomani, mkristo, Seventh-day Adventist (SDA).

Ukienda nyanda za juu kusini, kulikuwa na akina Mwakangale, Mwambenja na wenzao. Sijawahi kumsoma Mwambenja mara nyingi kama Mwakangale na Mwanjisi ingawa yeye pia alikuwa ni kiongozi mkubwa wa TANU katika wilaya ya Rungwe na sehemu za Mbeya mara tu baada ya TANU kuanzishwa. Alikuwa ni mwenyekti wa TANU katika wilaya ya Rungwe lakini pia alifanya kazi kubwa kusaidia kuijenga TANU sehemu za Mbeya. Pia Mwakangale alikuwa mmoja wa viongozi wa PAFMECA. Iringa kulikuwa na Julius Mwasanyagi na wengineo.

Hao wote hawakuwa Waislamu. Na ni mara chache nyakati hizi unasikia jina la Oscar Kambona linatajwa kati ya viongozi waliokuwa mbele kugombea uhuru. Na hata linapotajwa, Ukristo wake siyo moja ya sifa zake.
 
Kuna watu wanaoamini kwamba Waislamu walikandamizwa na Nyerere na kanisa la Kikatoliki na wanaendelea kukandamizwa na Wakristo. Wanaamini pia kwamba ni Waislamu waliokuwa mbele katika ukombozi wa nchi yetu kutoka kwa wakoloni. Hata majina ya Wakristo yanayojulikana nchi nzima na kuthibitisha kwamba Wakristo pia walikuwa miongoni wa viongozi waliokuwa mbele katika ukombozi wa nchi yetu hayatoshi na hayateweza kuwaridhisha ndugu zetu wanao amini kwamba ni Waislamu waliokuwa viongozi katika ukombozi wa Tanganyika.

Wataendelea kuamini hivyo. Ushahidi unao onyesha kwamba huo siyo ukweli, hata unapotoka kwa Waislamu wenzao, hauwezi kubadili mawazo yao.
 
Nane: Hizo takwimu za Waislam Bungeni sijaziona tafadhali nitumie tena

Mimi ndio maana naona hata uvivu kujadiliana na wewe. Kama mtu unaweza kudai kuwa katika bunge ambalo asilimia 24.4 ni waislamu basi katika hiyo asilimia 75.6 iliyobaki ni asilima 0.6 tu ni walutheri, waanglikana, mamethodist, wa-african inland church, wa-seventh day adventist, mashahidi wa jehova, wa-baptist, wa-bahai n.k. basi iko kazi! Sasa ukiwaingiza wazanzibari basi uongo wako unatisha zaidi. Kutokana na hizi takwimu zako, kuna wabunge 55 kutoka zanzibar ambayo ni asilimia 32.73. Ukiwajumlisha hawa na waislamu wa bara ( umekiri mwenyewe kuwa karibu kama sio wote ni waislamu), basi bunge hilo lina waislamu 96 ambayo ni asilimia 57.13 ! Hii kwa hesabu zozote zile ni majority, hata kama utaunganisha madhehebu yote ya kikristu chini ya banner ya ukristu! Sasa bado katika bunge ambalo zaidi ya nusu ni waislamu wewe bado unadiriki kudai kuwa si tu linahodiwa na wakristu bali linahodhiwa na WAKATOLIKI!

Ulishindwa nini kuitafuta mwenyewe kama wengine tunavyofanya? Pamoja na kuwa nimekuwekea hapa , kwangu mimi ni ishara ya arrogance yako maana inaonyesha kuwa hausomi kikamilifu tunapokujibu.

Amandla........
 
Waasisi wa TANU walikuwa watanganyika. Watu waliopiga uhuru wa Tanganyika walikuwa watanganyika. Kilichowaunganisha katika harakati zao ni utanganyika wao na nia yao ya dhati ya kutaka nchi yao iwe huru. Kamwe si dini. Hakuna dini iliyopigania uhuru wa Tanganyika, hakuna dini yenye haki ya kudai 'credit' kuhusu uhuru wetu. Kwa maana hiyo, muktadha wa 'Muslim struggle' katika kuleta uhuru kama anavyotaka Mohamed Said tuuchukulie hivyo ni upotoshaji wa dhahiri. Ile ilikuwa 'struggle' ya watanganyika, si ya waislam.
 
Jasusi: Labda unifahamishe kwa hiyo TAWA na katiba kuweka hapa kwa kuwa unahisi ni kitu kikubwa? Kama ni hivyo jibu ni kuwa Kleist Sykes kaasisi African Association 1929 akiwa katibu na alikuwa kijana wa miaka 25. African Association ndiyo hii iliyokuja kuzaa TAA na TANU. Hivi unataka kuita TAWA harakati? Au unataka kufananisha TAWA na TAA? Labda nikuulize hiyo TAWA ilifanya nini? Sidhani kama unahitaji mimi nieleze yale yaliyofanywa na AA na TAA. Najua yote umeshasoma katika kitabu changu. La kama utapenda niyaweke ukumbini kwa ajili ya faida ya wanaukumbi ahlan wasahlan.

One of them wrote back saying that there existed an organisation
in Tanganyika which would be excellent for my purposes, the Tanganyika African Association. It had quite a past, Sir Donald
Cameron having founded it t
o provide Africans in towns with a sounding board and a place where they could discuss their views.
It had the further advantage, he said, of having branches in all sizable towns. Cameron had not intended it as a political organisation
although he had not forbidden political discussion."

Huyu Donald Cameron ndie Kleist Sykes? Kwa nini haumtaji kuwa yeye ndie muasisi na mwanzishaji wa AA na wakina Kleist Sykes walitumiwa tu? Au una ushahidi kuwa anachodai Jasusi kuwa kiliandikwa kwenye hicho kitabu ni uongo?

Amandla........
 
K: Labda nikuulize kama umesoma kitabu changu. Ndani utakuta mengi ya kulijibu swali lako. La hujasoma nitaweka vitu hapa ukumbini kulidhihirisha hilo. Katika hilo nakuapia mimi sina wasiwasi. Uhuru ulipiganiwa na Watanganyika wote lakini ni Waislam ndiyo walioongoza mapambano. Muulize yeyote yule anaeijua historia ya TANU utaelezwa ni hiyo ndiyo ikawa sababu ya kufutwa historia hiyo. Kwani hujapata kuona picha za TANU za miaka ya 1950?
 
FM: Mimi sitatoa jibu la hilo. "Soma Kleist Sykes the Townsman" by Daisy Buruku (binti yake Abdu Sykes) katika "Modern Tanzanians" Ed. John Illife. Hiyo "The Townsman..." inatoka katika mswada aloandika mwenyewe Kleist Sykes kwa mkono wake kabla hajafa 1949. Ikiwa umeshindwa kupata kitabu nifahamishe nitakuwekea vitu hapa ili upate kujua African Association ilianzishwaje. La kama kuna mwanaukumbi atapenda kupata habari hizo aseme nitaweka taarifa kwa ukamilifu wake.

Sheikh Muhammad Ayubu (Mungu katuusia) katuusia kuwa ilm ni amana wenyewe wakiitaka huna budi kuwapa. Kwa "wenyewe" akikusudia kila atakae kujua jambo na wewe una ujuzi nalo basi mfikishie.
 
FM: Hizo takwimu ni zangu sasa unanambia nisome kitu nilichokuwekea wewe? Kumbe tazizo ni Wakatoliki? Hebu changanua kati ya Wakatoliki na makanisa mengine wengi ni nani?
 
K: Labda nikuulize kama umesoma kitabu changu. Ndani utakuta mengi ya kulijibu swali lako. La hujasoma nitaweka vitu hapa ukumbini kulidhihirisha hilo. Katika hilo nakuapia mimi sina wasiwasi. Uhuru ulipiganiwa na Watanganyika wote lakini ni Waislam ndiyo walioongoza mapambano. Muulize yeyote yule anaeijua historia ya TANU utaelezwa ni hiyo ndiyo ikawa sababu ya kufutwa historia hiyo. Kwani hujapata kuona picha za TANU za miaka ya 1950?

Sikubaliani nawe. Kwa nini hujasema ni wanaume walioongoza mapambano? Au kwa nini hujasema makabila yao? Au kwa nini hujasema umri wao? Hoja yangu ni kuwa kwa nini unaweka msisitizo katika ubaguzi, kuwagawa watu? Hata hao walioongoza mapambano walifanya kama watanganyika, na si kama waislamu, kwa hiyo kinachowapa sifa kwa juhudi zao hizo ni uzalendo wao kwa Tanganyika, si uislamu.
 
Pole sana bwana Utingo.
Inaonekana wee ni miongoni mwa wale wasiopenda kuijua historia ya kweli ya Tanganyika. Nakushauri bwana na wengine kama wewe muitafute na kuisoma historia ya kweli kuhusu tanganyika kuliko kukaa na kulaumu.
Wataalam wanatueleza kuwa NI VIZURI UKAIJADIRI HIJA KULIKO KULIKO KUMJADIRI MTOA HOJA, kwani inawezekana hata mwendawazimu akatoa wazo zuri.
 
kwanini asiwataje kama waislam?jee wewe kianchokuumiza kwamba kwanini watajwe kama waislam? lkkn mbona hili ni rahisi tu.
leo hii jk kama angaliweka mawaziri wote wenye majina ya kiislam wakiristo wangalikaa kimya?makanisa yangalikaa kimya? kjee hawa sio watz mbona magazeti mabli mbali waliita gov ya jk ni ya kidini eti kwa kuwa waislam wamejitokeza kwenye baraza la mawaziri?

Huu ndio ubaguzi ninaouzungumzia. Na mbaguzi mwenyewe ni huyu Mohamed Said. Wazee wa watu wameshiriki harakati za kudai uhuru kwa uzalendo wao, leo huyu anadai ni uislamu ili awatenge na wenye imani tofauti. Mwalimu Nyerere katofautiana na wengi tu wakati wa utawala wake na kuwasweka kizuizini, kwa sababu za kisiasa. Leo Mohamed Said anataka kutuamiaminisha kuwa wale waislamu miongoni mwao walioingia katika mkumbo huo yaliwapata hayo kwa sababu ya uislamu wao, ili tu atuchonganishe! Hasemi na wale wa dini tofauti waliofanyiwa ubaya nao ni dini ipi iliwaponza. Hatuambii hali kadhalika kuwa wale waislamu waliofaidika na utawala wa Nyerere nao dini yao waliiweka wapi wakati huo, au Nyerere hakujua kuwa ni waislamu?

Narudia kumtaka bwana Mohamed Said akatafute sababu halisi iliyowafanya hao wazee wake kutendewa hivyo, kwani hakika ni wazi kabisa dini yao haikuchangia chochote katika hatia yao kama wanayo hatia hata ya kusingiziwa.
 
Kulikuwa na viongozi katika kila jimbo (mikoa ilivyokuwa inaitwa nyakati zile), na katika kila wilaya, waliopigania uhuru wa nchi yetu. Sehemu za pwani, wengi walikuwa ni Waislamu. Sehemu za bara wengi walikuwa ni Wakristo. Hata Dar es Salaam kulikuwa na Wakristo, na bara kulikuwa na Waislamu lakini Wakristo walikuwa wengi sehemu zingine za Tanganyika na siyo kama za pwani.

Tunapowazungumzia viongozi wa Tanganyika miaka ile, tusisahau kazi aliyofanya Oscar Kambona kama secretary-general wa TANU kusaidia kuijenga na kuikuza TANU na kueneza ujumbe nchi nzima kutoka makao makuu ya chama hicho. Hakuwa Muislamu. Alikuwa Muanglikana.

Ukienda Mwanza, utawakuta watu wengi wanaowakumbuka viongozi sehemu hizo waliosaidia kuijenga TANU; miongoni mwao, Paul Bomani, mkristo, Seventh-day Adventist (SDA).

Ukienda nyanda za juu kusini, kulikuwa na akina Mwakangale, Mwambenja na wenzao. Sijawahi kumsoma Mwambenja mara nyingi kama Mwakangale na Mwanjisi ingawa yeye pia alikuwa ni kiongozi mkubwa wa TANU katika wilaya ya Rungwe na sehemu za Mbeya mara tu baada ya TANU kuanzishwa. Alikuwa ni mwenyekti wa TANU katika wilaya ya Rungwe lakini pia alifanya kazi kubwa kusaidia kuijenga TANU sehemu za Mbeya. Pia Mwakangale alikuwa mmoja wa viongozi wa PAFMECA. Iringa kulikuwa na Julius Mwasanyagi na wengineo.

Hao wote hawakuwa Waislamu. Na ni mara chache nyakati hizi unasikia jina la Oscar Kambona linatajwa kati ya viongozi waliokuwa mbele kugombea uhuru. Na hata linapotajwa, Ukristo wake siyo moja ya sifa zake.

Asante, Mkuu kwa kuweka wazi hili. Nasikia Kambano alifanya kazi pasipo mshahara wa uhakika maana TANU ilikuwa hoi bin taaban kifedha wakati ule. Wakina MS hawataki kukubali kuwa bila watu wa bara kuunga mkono TANU huo uhuru wala usingepatikana. Na TANU ingekuwa identified kama ya waswahili basi watu wa bara wangeisusia. Ni jitihada kubwa na uzalendo wa hali ya juu wa viongozi wa wakati ule ndio uliofanya watanganyika waweke pembeni masuala ya ukabila na dini na kuungana WOTE kudai uhuru ambao leo tunajivunia. Kwangu mimi ni matusi makubwa kujaribu kuugeuza uzalendo wao na kuufanya udini.

Amandla......
 
FM: Hizo takwimu ni zangu sasa unanambia nisome kitu nilichokuwekea wewe? Kumbe tazizo ni Wakatoliki? Hebu changanua kati ya Wakatoliki na makanisa mengine wengi ni nani?

Takwimu zako hazielezi unachodai ( hata ingekuwa wakristu wote ni wakatoliki, wasingefikia 75% ya bunge maana takwimu zako zinaonyesha 57% ya bunge ni waislamu!). Na ni hiki ndicho nilichokionyesha( soma jibu langu). Sasa kama ulifanya hivyo makusudi ( kutoa takwimu feki ili kujenga chuki) basi kwa nini nisikuite muongo? Ni kile kile kiburi kinachokuzuia kusoma alichoandika mwenzako ali mradi ametofautiana na wewe.

Amandla........
 
FM: Mimi sitatoa jibu la hilo. "Soma Kleist Sykes the Townsman" by Daisy Buruku (binti yake Abdu Sykes) katika "Modern Tanzanians" Ed. John Illife. Hiyo "The Townsman..." inatoka katika mswada aloandika mwenyewe Kleist Sykes kwa mkono wake kabla hajafa 1949. Ikiwa umeshindwa kupata kitabu nifahamisha nitakuwekea vitu hapa ili upate kujua African Association ilianzishwaje. La kama kuna mwanaukumbi atapenda kupata habari hizo aseme nitaweka taarifa kwa ukamilifu wake.

Sheikh Muhammad Ayubu (Mungu katuusia) katuusia kuwa ilm ni amana wenyewe wakiitaka huna budi kuwapa. Kwa "wenyewe" akikusudia kila atakae kujua jambo na wewe una ujuzi nalo basi mfikishie.

Unataka kutuambia kuwa Kleist Sykes alidai kuwa ni yeye ndiye aliyeanzisha A.A.? Huyo Cameron hakuwepo? Haya si yale yale unayodai kuwa Nyerere aliyafanya, kujikusanyia sifa mwenyewe na kudharau mchango wa wengine.

Amandla.......
 
Sheikh mohammed said. kwa faida yangu na wana ukumbi jee nasikia kwamba waislam wakifanya siasa zao za kupigania uhuru ndani ya misikiti.unaweza kunitajia baadhi ya miskiti maarufu iliokuwa kitovu cha mapambano hayo?
jee wakiristo nawao wakitumia makanisa harakati za kumngoa mkoloni?

Kama kuna waliotumia misikiti, hizo ndio siasa za utengano waziwazi maana asiyekwenda huko msikitini atajikuta ametengwa. Na kwa demographic structure ya Tanganyika, huwezi kufanya siasa za namna hiyo ukafanikiwa maana walioko nje ya msikiti ni wengi kuliko walioko ndani. Wazee wetu walilitambua hilo, ndio maana wakajitahidi kueneza harakati zao nchi nzima, na zikafanyika katika mazingira ya kuhusisha wote, wanaoswali na wasioswali maana wote Tanganyika ni yao.

Kama wakristo hawakutumia makanisa katika mapambano hayo, naona walifanya vema maana wangetumia makanisa wangewatenga walioko nje ya makanisa ambao pia ni wengi kuliko walioko ndani. Nawasifu sana wazee kwa kuanzisha TANU maana kilikuwa chombo rasmi cha kudai uhuru bila kutumia dini, kilikuwa chama cha siasa siyo cha kidini, hakuna dini yenye haki ya kudai credit kwa kazi iliyofanywa na TANU maana hiki kilikuwa chama cha wazalendo wa Tanganyika, si cha dini yoyote ile.

Nasema tuwape wazee wetu heshima wanayostahili. Walipigania uhuru wa nchi hii kwa uzalendo wao, na si kwa dini zao. Wamejitahidi kutujengea nchi yenye watu wa imani tofauti wanaofanya kazi za kujenga nchi kwa kuheshimiana bila kubaguana kidini. Wazee wetu walishika dini zao, lakini hawakubagua wa dini tofauti. Hayo ndiyo tunayowaenzi nayo wazee wetu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom