Ukweli kuhusu vibanda vilivyochomwa moto z'bar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukweli kuhusu vibanda vilivyochomwa moto z'bar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GHIBUU, May 12, 2011.

 1. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #1
  May 12, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Ukweli kuhusu vibanda vilivyojengwa vya wafanyabiashara ya vinyago eneo la Pwani Mchangani, Kaskazini Unguja ni kama hivi: Ukweli ambao SMZ-GNU hautaki kuusema kwa faida yao na matakwa yao zaidi ya kisiasa. Soma maelezo sahihi na uchambuzi wa kina:
  - Vibanda hivi vimejengwa bila kibali cha aina yeyote ile au ya umiliki wa ardhi. Na kama kipo tunaomba tuonyeshwe. Balozi Seif Ali Iddi anajua hilo, lakini amekurupuka na kuzungumza siasa zaidi ya kutaka kukamilisha agenda yake ya Tanganyika. Nina challenge balozi Seif Ali Iddi atuonyeshe hati miliki ya hao wamachinga wa hapo. Jamani, tuzungumze sheria, na haki, sio hamasa wala siasa au chuki.
  - baada ya kuvamia, wamejenga kanisa, jambo lililowakera wananchi wazawa wa hapo. Balozi Seif Ali Iddi anisute kama sio kweli.
  - wanakijiji/wazawa, walilalamika kwa serikali, za wilaya, mkoa na serikali kuu kuhusu kadhia hiyo, hakuna lililochukuliwa, smz imepuuza madai ya wananchi wake. Leo, yametokea mengine, wanajaribu kugeuza kibao kwa wenyeji. Uonevu gani huu, ndani ya nchi yetu. Madai ya wananchi yapo hai, tena kwa maandishi na kesi ipo, files zipo. Madai yao yapo halali kabisa, lakini walipuuzwa kwa sababu wao ni wenyeji, na wamekuzwa watu wageni wasiokuwa na hata saa moja ya kuishi Zanzibar. Sasa, OK, tujaalie SMZ iamue kuwalipa watoto wa wafalme, wataanzia wapi; any document ya kuhalilisha malipo au uhalali wa umiliki wao hapo, kisheria; tusiende kisiasa.
  * Jamani, tunataka kuambiwa nini na Balozi Seif Ali Iddi, Charlie Chaplin. Nilisema awali kuwa huyu Seif NO.2 siye/hatufai. Na kadhalika Seif NO.1; pia ni mzigo kwetu kwa maslahi ya Zanzibar.
  Hiyo ni SET NO .1
  SET NO.2 ya mazungumzo yetu:
  - hoteliers pia wamelalamika sana na watu hawa – NO action. Kamisheni ya utalii pia wamekereka na watu hawa – no action: kwa sababu wanaiharibu sekta yote ya utalii Zanzibar.Hoteli nyingi ama zinakosa biashara kwa kuwepo vibanda vile pale. How? wageni wao wanaibiwa, wanakuwa harrased na hotels zinakosa ‘positve image/good image’ kwa kuzungukwa na vibanda hivyo. Hoteli ya fur star worth over 20m dollars, imezungukwa na kibanda cha shilingi elfu kumi. Uoza mtupu. Sekta ya utalii inakufa kutokana na wauza ugali na vinyago hawa. Hii ni serious, na naomba SMZ na nyie wote muitazame huko, kama angle ya biashara zaidi /sio siasa zaidi.
  SET NO.3 ya amzungumzo yetu:
  - biashara gani walikuwa wanafanya hawa watoto wa wafalme?
  1. Kuuza Vinyago
  2.Kuuza pombe/madawa ya kulevya
  3.Uhalifu wa kupindukia.
  4.Ukahba.
  Katika uhalifu, iliwahi kukamatwa hata silaha katika mabanda hayo, ingawa polisi imebana kimya. Haya na mengine , mstahiki balozi seif ali iddi hataki kuyasema wala hatoyasema maisha.
  Angalia ufedhuli wa watu hawa, jana wanasoma risala mbele ya Seif Ali Iddi na kusema kuwa kama serikali haitochukua hatua, wao watachukua hatua mikononi mwao. Huyu eti ni VP 2 wa nchi, na watu wanamwambia watavunja sheria, yeye na timu yake, wanacheka. Watu wanafikiria kulipiza kisasi, au kuuwa, au kufanya hujma, yeye mwenzetu anaona rahaaa, na anacheka kwa kuraha. Keli tumepata vingozi au tumepatikana.
  Lakini yote hayo ya nini? Hayo ni mambo yamepanga na system. Inawezekana waliochoma moto ni serikali au hata hoteliers, au hata wengine xxxx! ili kukamilisha agenda yao. Mnaijua?
  Jawabu: katiba mpya. Kwa vile mmeikataa, sasa wanabuni tension, ili kukamilisha agenda hiyo.
  Bottomline: lazima katiba mpa iwe by 2014, kama alivyosema au anavyotaka JK.
  Sasa Zanzibar kuanzia siku mliyoikataa mswada wa katiba mpya, mpaka 2014 – mtaona mambo mengi ya ajabu ajabu – popobawa atarudi, wale ramba ramba watarudi, vitisho, na visa, na mikasa mingi tu mtaiona. Ushindi lazima, na lazima katiba mpya ipite, na lazima Zanzibar tuifute katika ramani ya dunia…kwa utaalamu na kisayansi.
  Tusisahau kuwa katika kuchomwa moto vibanda hivi upo mkono wa kanisa.
  Unajua huko nyuma sana, nilisema kwa sauti kubwa kuwa Seif NO.1 na NO.2 hawatufai, na ni lame duck – niliambiwa sijui niko CUF, wengine wakasema mimi CCM. Ahhhh…jamani: mimi atayesema ni CUF – basi mimi ni CUF aliyekata kamba zizini; na atayesema mimi CCM; basi mimi ni CCM mfu – sina mbele, sina nyuma. GNU, narudia tena haitufai; inazidi kutuletea matatizo.
  - Na Maalim seif mwenyewe (menyewe….baba dogo veve, amekiri juzi jamat khan) kuwa hawawezi kutatua matatizo ya wananchi, na ametoa visingizio miteni kidogo. Mwisho hana la kusema anasingizia eti pirates wa Somalia, ndio wamesababisha kupanda kwa bei ya vyakula. Balahau bora sasa ukae na uandike vitabu vya comedy. Maalim Seif bora aungane na akina Chimbeni Kheri au Mr.Bean, watupatie tales za vichekesho.
  Mwisho,nimesitikitika zaidi kuona waandishi kama Salma Said, naye amejaa tele katika hamasa na kuandika lugha mbovu kabisa, iweje yeye aandike neno ‘vibanda vya wabara’. si aseme tu, vibanda vya wafanya biashara……yaani wazanzibari wote tumetekwa akili zetu na watu hawa.
  Inasikitisha sana.
   
 2. w

  wimbi la mbele JF-Expert Member

  #2
  May 12, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 647
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Sasa subiri utasikia watoto wa Kijamaa watakavyokujia juu kuwa hutaki kumuenzi mfu!
   
 3. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #3
  May 12, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  only seif sharif hamad have the answers.
   
 4. w

  wimbi la mbele JF-Expert Member

  #4
  May 12, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 647
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  haooo watoto wa Kijamaa washaanza kuja

  bado nasubiri wale wenye kuongozwa na mfu!
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  May 12, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,519
  Likes Received: 19,944
  Trophy Points: 280
  viongozi wenu wa zanzibar ndio wanataka huu muungano uendelee kuwepo amkeni
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  May 12, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,519
  Likes Received: 19,944
  Trophy Points: 280
  mbona sijakuelewa unamaanisha nini?hi nayo ni hoja au ni jazba !
   
 7. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #7
  May 12, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Kwa nini wazawa walikerwa na kujenga kanisa? Ni dini gani haina uvumilivu kwa dini nyingine? Mbona sijasikia msikiti umechomwa?
   
 8. w

  wimbi la mbele JF-Expert Member

  #8
  May 12, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 647
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  sasa mbona spidi ya wa watoto wa KIJAMAAA imekuwa ndogo?
   
 9. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #9
  May 12, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Mmmmmmh! Hii mijitu ya Zenj mibaguzi sana! Yenyewe imeajiriwa kwenye Idara ambazo hata si za Muungano, inafanya biashara huku Bara kwa raha mstarehe!
   
 10. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #10
  May 12, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  ghibuu,majambo na malaria sugu mna matatizo ya akili,your not great thinker.To be a great thinker you have to be impartial and rational.Nyie ni wabaguzi mnaona wabara hawana uhalali wa kuishi zenj mbona huku bara wazanzibar hadi wanagombea Ubunge wanapewa si tumenyamaza tu.Namnukuu pinda vunjeni basi muungano tuone nani atakaye athirika.Mnapenda sana kuomba omba eti serikali ya muungano imezuia misaada.Wanachokifanya wazenj hawajui madhara yake,wabara wakiamua kulipiza jiulizeni wazenj wangapi wapo bara na wabara wangapi wapo zenj? tUMIENI AKILI BANA
   
 11. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #11
  May 12, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Hata tusingelikuwa na muungano kama sheria inaruhusu mgeni kufanya biashara basi wangekuja kufanya,wachina wako,wakenya na wahindi,kila kona tena wachina wauza mpaka mwili au hujui wewe ?
  Wabongo kibao sasa wanazaa na wachina humo majiani hujui hilo ? Au pia muna muungano na china na wahindi na wakenya ?

  Musichukulie sababu chache za watu binafsi mukataka kuimaliza zanzibar kiuchumi,hawa watu walochoma hiviyo vibanda hawana kosa wala sio vizuri vile vile wa kulaumiwa serikali kwa nini hawakuchukua hatua za makusudi hawa watu ikiwa wanafanya biashara kimakosa,? Hawana vibali vya kufanya biashara,pia wamevamia ameneo ya wanakijiji ya makazi yao ,,,

  Mimi sioungi mkono ila pia siwalaumu wananchi kwa jazba,kwani serikali ndio kawaida yao kuyafumbia macho makosa,hapa zanzbar hazuiwi mtu kufanya biashara ila tunataka miashara mabzo zinafuata sheria,na utamaduni wa zanzibari,musitumie jazba kuvuruga na kuweka chuki bana yetu ni bora muende huko zanzbar kutembelea eneo hilo na kuwauliza wananchi.

  Pia kujifunza mila na utamaduni wa zanzbar,kila nchi ina tamaduni zake,japokuwa munachukulia yote tanzania ila kuna zanzbar kuna tamaduni zake.

  Hakuna aneutaka muungano,kwani wazanzbari ushawatoka katika nyoyo zao.
   
 12. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #12
  May 12, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Inaonekana hujui nini maana ya muungano na hwezi kutofautisha katia ya mbunge na muakilizi wa zanzbar,mbunge anaweza kugombania mtu yoyote katika jimbo alimuradi kuwa umekubalika kwa sababu bunge ni la muungano baina ya pande zote mbili,pia hata raisi pia anaweza kutoka pande zote mbili,ikiwa rais katoka bara makamo wa rais anakuwa rais wa zanzbar na ndio makubaliano ya article of union.

  Makubaliano ya ARTICLE OF UNION inasema hivi,mtu yoyote kutokaba zanzbar anapewa haki ya kumiliki ardhi ndani ya tanganyika,na mtu yoyote kutoka tanganyika hana haki ya kumiliki ardhi ndani ya zanzbar,,,,jiulize kwanini ? Sababu ni kwamba ardhi za zanzbar ni ndogo,na ndivyo walivyo kubaliana waasisi wetu.

  Suala la biashara hazuiwi mtu kufanya popte pale alimuradi awe amefuata masharti ya nchi,kwa mfano kandoro aliondoa mabanda na nyumba kibao barabarani kwa nini ? Hiyo ni sheria ambayo iliwekwa na seriali ya jamuhuri ya muungno na yaondoshe,mbona wapemba wali athirika pia hatukusema kitu ?

  Kuliwahi kutoka kuvunjwa kwa macontena masaki pale kama 10 ya wapemba kipindi hicho Makamo ni OMAR juma Marehemu mungu amlaze mahali pema,walichofanya masaki walivunja makontena yote likabakishwa moja tu,tena lilikuwa la mtu fulani ambaye anatambulika kiserikali,kesi ilipelekwa mahakamani walishinda wapemba na kulipwa,lakini hatukuchukulia kiubaguzi wala hatukusema kitu.

  Haya waliyotokea hapa zanzbar kuchomwa kwa vibanda hawa watu hawakutimiza masharti ya nchi na kufuata mila na utamaduni wa zanzbar,vibanda hvi vikitumiaka kuuza vinyago,bangi humo humo na ukahaba,kama munabisha njooni muwaulize wananchi,na wanakijiji walilalamikia serikali lakini hawazichukulia hatua malalamiko hayo.

  Wananchi wamepanda jazba na kuvamia eneo na ku destroy it,sasa tumlaumu nani ? Hapa zanzbar asilimia 99ni waislamu,sasa wee uje uvamie eneo la wakazi ufanye unavyotaka ikisha mujenge na kanisa katika eneo la mtu nani atakubali ? Umepewa na nani haki ya kujenga wewe ? Umepewa na nani leseni ya duka ? Katiba ipi inayokulinda wewe uweze kumiliki eneo ?

  Lazima tufahamu kuwa kila sehemu kuna mila na desturi zake na heshima yake.
   
 13. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #13
  May 13, 2011
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,607
  Likes Received: 6,774
  Trophy Points: 280
  Wewe wacha uwongo, Serikali ya wilaya imetamka wazi kwamba hao watu wapo kisheria, na wamefuata kanuni zote za kufanya biashara hapo.

  Na kitu kingine ni kwamba, kama hao watu wamekosea si ni mamlaka ya serikali ndiyo kusimamia sheria?, kwa mujibu wa katiba ya zanzibar na sheria za Zanzibar ni nani ana mamlaka ya kutunga, na kutekeleza sheria?.

  Halafu usichanganye na operesheni ya Kandoro huko dar-es-salaam, ile ni operesheni imeendesha na vyombo halali vya kusimamia kanuni nsa sheria, Umemuona "Kichogo, ndolanga, wamrima,mtwana,mkoloni mweusi,mnyamwezi", yeyote akijichukulia sheria mkononi kuvunja hizo mali za Wapemba?.

  Wewe Usijaribu kutetea kisichoteteeka, Usijaribu kuingiza habari za dini wakati unajua Zanzibar siyo nchi ya Malaika, mambo yanayotendeka duniani kote hata Zanzibar yanatendeka, Usituletee mambo ya "I am Hollier than thou".

  Nyinyi Wazanzibari, mna njia tele za kujitoa katika Muungano, Zifuateni basi mchukue nchi yenu, wala msidhani Watanganyika watatumia nguvu kuwazuia, Naona mnamuandikia barua raisi wa Tanzania kuhusu kuvunja muungano, Muandikieni pia na raisi wenu Shein, Wajumbe wa baraza la wawakilishi, Wabunge wenu.
  Tanganyika haina namna ila kuvunja muungano na Zanzibar ili mradi Wazanzibari wengi wawe hawataki Muungano.
  ACHENI KUNUN'GUNIKA, FUTAENI TARATIBU, VUNJENI MUUNGANO, MCHUKUE NCHI YENU.
   
 14. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #14
  May 13, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Siasa hujui, sheria hujui, historia hujui, mantiki huna, kujenga point huwezi, unaitwa 'Ghibuu' alafu unajiita great thinker! Computer hujui, kiingereza hujui, alafu unajitutumua kuvitumia!
   
 15. King Zenji

  King Zenji Senior Member

  #15
  May 13, 2011
  Joined: Feb 18, 2008
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33

  ,,,,Ghadhabu kali kuliko hali halisi,,,,walifikiria kuwa GNU ndo ingewasaidia,matokeo yake tunakamuliwa kwa kila kitu,hizo ni jazba tu kwenda kuwapa adhabu ndugu zetu kwa visingizio vya kitoto kabisa,eti utamaduni????,,hivi hizi tamaduni za kushabikia mambo ya kutoka WEST mbona hatuzipingi kwa nguvu??,mfano mtu aliepewa jukumu la kutokomeza madawa ya KULEVYA ktk GNU ni Maalim SEIF,,lakini wapiii bana,siku hizi ndo kila mtaa NYOKA wanazidi kuongezeka,,hamtaki kufanya ya maana mnaenda kuwapa adhabu watu wanaogombea angalau kujipatia mkate wao halali,,acheni UBAGUZI wa kijinga namna hii,hautufikishi popote.
   
 16. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #16
  May 13, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hivi hii thread ina mantiki gani??? Ina dhumuni gani?? Mkuu hueleweki!
   
 17. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #17
  May 13, 2011
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Kumbe Zanzibar hakuna mkristu!

  Amandla........
   
 18. Shenkalwa

  Shenkalwa JF-Expert Member

  #18
  May 13, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kinachowasumbua ndugu zetu wazanzibari ni udini na ubaguzi. Wazanzibari wamejazana huku tanganyika kiasi kwamba kila kona wapo na wamejenga, wamejineemesha na kusahabu hata kwao lakini watanganyika wachache tu walioko unguja wanapata shida sana kuwaona. Hivyo vibanda ukifuatilia sana utakuta havikuwa na shida sana kiasi cha kutoa maamuzi ya kuvichoma moto. Kilichowakera sana hapo ni "kanisa" kwa sababu ya udini walio nao kwa sababu hata makanisa machache ya zamani yamekuwa yakitishiwa kila mara kuchomwa. Wazanzibari badilikeni, semeni wazi kuwa hamtaki watu wa imani zingine huko zanzibari, wekeni iwe ni sheria kwamba imani zingine mbali na uislamu haitakiwi zanzibari na watu watawaelewa. Ishawishini serikali yenu iweke sheria hiyo. Vinginevyo kama hilo hamuwezi basi muwe wavumilivu kwa sababu kama kuna watu wa imani tofauti ya kidini na ile ya kwenu lazima nao wapate mahali pa kuabudia. Hamna lolote zaidi ya udini na ubaguzi nyie:behindsofa:
   
 19. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #19
  May 15, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wazanzibari wapo kila pembe ya dunia usitutishe kijana.

  Kama "muungano" huu ni kero, tena mbona kila baada ya miaka mitano mnakuja na zana za kijeshi kuulinda?

  Mnajua kuwa Zanzibar ikiondoka CCM hakuna huu muungano feki na huku ndio shamba lenu la bibi.

  Na uvunjike leo hii muadhirike, nchi tajiri, wananchi wake maskini.

  Zanzibar for Zanzibaris, Tanganyika mtajua wenyewe mlioiua.
   
Loading...