samahani kwa kuwarudisha nyuma, hivi hapa swala ni dini mtu aliorithi, anayoamini au ni utendaji wake?
manake kama anafanya kazi ya ovyo, lazima awajibishwe, bila kujali dini yake, na ndio JF inaposimamia, tusipotezane,
Swala la anasali wapi, tumuachie yeye na mungu au shtani wake.
Kama Mkapa yuko kama kivuli, na yeye ndie bosi, awajibishwe ka kutega kazi. na kushindwa kuperform.
Vita hii ya udini inatupeleka kubaya, manake hakuna mshindi, hata sijui mnaipendea nini. Manake wote hapa tuna marafiki, ndugu na jamaa mchanganyiko, ina maana tunawapenda hadi wapi?
Nilisema hivyo tangu zamani kwenye vita ya ufisadi, tusifuate personalities kwa chuki binafsi, tutafute hela zetu zilizopotea na kuwashitaki waliozipoteza, basi. hata akiwa ndugu yako.
Sio tu kumchukia mtu na kumpaka matope kwa utajiri wake au udini wake au kabila lake.
Lazima utaishia kuchafua hewa tu na bila kupata unachotaka.
Ufisadi, wizi wa mali ya umma, upendeleo kazi, leta hoja, ushahidi, hakuna hata haja ya jina wala dini wala kabila, taja tu ofisi na majukumu yake inatosha. watu watajua kama una point au la.
Inasikitisha siku hizi JF imeingiliwa na wasiopenda HAKi ya ukweli, pamekuwa mahali pa kuchafuana na kusafishana, this is so low!!!!
Inatupa ugumu wa kuchuja mada za kusoma au kuignore.
Please jitahidini kidogo,
zile comments za lete ushahidi, ziko wapi? ukiuliza lete ushahidi unashambuliwa weeeee