Ukweli Kuhusu UDOM huu hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukweli Kuhusu UDOM huu hapa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MaMkwe, Sep 30, 2009.

 1. M

  MaMkwe JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2009
  Joined: Sep 5, 2007
  Messages: 284
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Siku za hivi karibuni imewahi kuandikwa juu ya madai ya udini, ukabila, ukanda, ubabe katika Chuo Kikuu cha Dodoma. Mimi kama Mtanzania mwenye uchungu na taifa langu niliamua kuzifanyia kazi tuhuma hizo nzito. Niliamua kufanya hivyo kwa kuwa natambua athari za udini, ukabila, na ubaguzi wa aina nyingine katika jamii. Nchi nyingi zimejikuta katika mapambano ya kumwaga damu kutokana na aina mbalimbali za ubaguzi. Katika kuzifanyia kazi tuhuma hizo nilifanya uchunguzi na kubaini yafuatayo:-

  Udini Uongozi wa UDOM

  Chancellor: H. E. Benjamin W. Mkapa (catholic)
  Vice Chancellor: Prof. Idris Kikula (Muslim)
  Chairman of Council: Hon. Dr. M. G. Bilal (Muslim)
  Deputy Vice Chancellor (Academic): Prof. L. Kinabo (catholic)
  Deputy Vice Chancellor ( Administration) Prof. S. Mlacha ( Muslim)

  Viongozi wengine wa ngazi za juu UDOM

  Principal - College of Education: Prof. K.M. Osaki (catholic)
  2 Deans of Schools in the College are all Christians

  Principal - College of Humanities: Prof. C. M. Rubagumya (Christian)
  2 Deans of Schools in the College are all Christians

  Principal- College of Informatics: Prof. N. Mvungi (Christian - Protestant)
  2 Deans of Schools in the College are all Christians

  Dean of Student (Christian)

  Dean, School of Natural Science (Christian)
  Dean, School of Medicine (Christian)
  Dean, School of Nursing ( Christian)

  Source: (UDOM Prospectus and Website)

  Wafanyakazi - Wanataaluma - Christians 96%
  - Muslim 4%

  Wafanyakazi Waendeshaji - Christians 86%
  - Muslim 14%

  Wanafunzi - Christians 92%
  - Muslim 8%

  (Source UDOM Website, newpapers, announcements of student admission)

  Inashangaza sana kuona mtu mzima mwenye akili zake timamu kuzusha kwamba UDOM ni Chuo cha Waislam kwa kuwa kuna viongozi watatu Waislam bila kuyafanyia kazi madai yake. Bila shaka watu hao na wapambe wao hawalitakii mema Taifa letu.

  Waungwana, kutokana na uchungu nilionao juu ya jambo hili bado nitaendelea kufanya utafiti kuhusu muundo wa uongozi katika vyuo na taasisi nyingine za umma na kumwaga data hapa uwanjani kwa madhumuni ya kuwasuta wote wasiotaka mwananchi wa dini au kabila fulani apewe madaraka hata kama ana uwezo. Ukweli ni kwamba viongozi wa UDOM hawakuteuliwa kwa sababu ya dini zao bali uwezo wao ambao kwa kiasi kikubwa unajidhihirisha kwa jinsi ulivyofaulu kubadilisha mandhari ya vilima vya Chimwaga na vitongoji vyake, pamoja na ramani ya nchi yetu katika dunia ya elimu ya juu. Ujenzi wa UDOM umesaidia sana kuinua kiwango cha elimu kwa vijana wanaomaliza kidato cha sita. Vijana wa wakulima na masikini wengine wa Tanzania ambao sasa wanasoma UDOM wangeishia kuwa wapiga debe kwenye vituo vya daladala kwa kukosa sehemu za kujiendeleza. Wanaobeza na wabeze, lakini mimi naifagilia nchi yangu na serikali yake kwa ujenzi wa UDOM bila kujali itikadi za Chama. Wanaosoma UDOM ni Watanzania haijalishi ni wanachama wa CHADEMA, CUF, TLP, CCM, NCCR, au ANR.

  Watanzania tuamke, tuache kutumiwa kwa madai ya udini, ukabila, jinsia, kanda nk. Tusipokuwa makini tutajikuta kama majirani zetu.

  Naamini JF ni kijiwe cha watu wenye busara, ni vizuri kikatumika kutoa taarifa zilizofanyiwa kazi. Nitasikitika sana endapo JF itageuzwa kuwa kijiwe cha majungu
   
 2. K

  Kyaruzi Member

  #2
  Sep 30, 2009
  Joined: Mar 23, 2007
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haya mambo ya dini sasa yamekuwa too much hapa JF kila siku kutafutana uchawi. Nadhani umefika wakati sasa post zote zenye mirengo ya kidini zikapelekwa kwenye forum maalum ya mambo haya, na hapa tuachieni tuchape siasa kwa kwenda mbele.

  Mshindwe wadini wote!
   
 3. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli tunaenda mbali sasa! Tanzania huru yenye amani niliyokuwa naijua mm inakufa vibaya.


  Is like wen one great philosopher of FRANCE said during FRANCE REVOLUTION before his death; I CARRY WITH ME THE LAST RAG OF THE MONARCHY... And he died after...

  Baba wa Taifa kaondoka na Tanzania Huru, waliobaki ni TULE TWENDE...
   
 4. J

  Jews4ever Member

  #4
  Sep 30, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mleta hoja umejaa vioja!
  Upo chuo cha MUM?

  Mlalamikaji alisema mishahara inatolewa kwamisingi ya udini?
  Huyo msilamu aliye na cheo cha kugawa fedha za mishahara anatumia rungu lake vibaya,anawapendelea wajahedina kuliko wagalatia.

  Top brass yote hapo UDOM ni urafiki kati yao na JK, MKAPA yupo kama kivuli tuu, hicho cheo hakihitaji,wala hakimnyimi kula,Top hapo ni Pr.Kikula

  Angalia posts anazoshika kikulla ndio utajua nini kipo kati yake na JK.

  I hate majahudina.
   
 5. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wewe data hizi umezitoa wapi??
   
 6. Geeque

  Geeque JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2009
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 848
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Tatizo linakuja hata pale mambo ya kawaida ya Siasa yanapozungumzwa hapa bodini, kuna baadhi ya watu humu ndani ni wadini wakubwa na lazima waingize falsafa zao za kibaguzi wa kidini. Kuna baadi ya watu na heshima zao humu ndani zikishaingizwa habari zitakazohusishwa na dini, wanageuka wapayukaji na kuongea vitu visivyo na maana na kuonyesha rangi zao za ukweli za kibaguzi wa kidini.

  Nakumbuka ile habari ya uongozi wa University of Dodoma, mletaji habari alisema wazi kuwa uongozi wa chuo umejaa waislamu na wanatumia udini kupeana mishahara mikubwa. Na ilitokea baadhi ya watu wakaunga mkono ile habari bila ya kuwa na ushahidi wowote na kukurupuka kutoa shutuma mbalimbali.

  Badilikeni nyinyi wadini mnatia kinyaa na kunuka kimawazo kama mashimo ya vyoo.
   
 7. O

  Omumura JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sidhani kama ni busara sana kubishana na mtu mwenye hoja dhaifu na nyepesi kama unyoya wa ndege.Haya mambo ya udini yakiachwa yaendelee, walah tutagawana mapori ya nchi hii na hatapatikana mshindi, Mungu aepushie mbali!
   
 8. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #8
  Oct 1, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mamkwe,
  Umetbibitisha tu kuwa ni kweli kile chuo cha UDOM kimeshikwa na Waislaam. Huyu Mchaga Kinabo (kama sikosei) kapewa cheo cha Academic. Huko yeye anadeal na wanafunzi, waalimu, masomo, nk wakati huyu anayeshukiwa kuwa MDINI yaani Pro. S. Mlacha na Kikula, ndiyo Maboss wenyewe na ndiyo wameshika MPINI. Hapo ongeza Bilal ambaye ubabe wake ulionekana wakati Mkapa ni Waziri wa Sayari na Elimu ya Juu na yeye ni Katibu Mkuu. Akipata tatizo badala ya kwenda kwa Mkuu wake Mkapa, alikuwa anaenda moja kwa moja Ofisi ya Jirani yaani IKULU.

  Hao Waalimu na viongozi Waislaam wanaweza kuwa wachache ila unyanyasaji wao ukawa wa kutisha. Mbona Rwanda na Burundi Watusi walikuwa 10% ila ubabe wao ulikuwa wa kutisha. Wageruman walikuwa wachache tu ila wakatutawala.
  Kama jamaa wanapata UBABE kutoka kwa Kikwete basi itakuwa ni too bad. Nasema kama wanatumia huo UISLAAM kujifanyia mambo kienyeji, itakuja kuwa mbaya sana kwao huko miaka ya baadaye. Hii aliifanya Prof. Kigoma Malima wakati akiwa Waziri wa Fedha. Alikuwa akitoa misamaha ya kodi kwa Waislaam kama kawa. Upuuzi huo akaja kuufanya Mkapa na genge lake na matokeo yake akina Mramba tunawaona Kisutu.

  JIPANGE na uje hapa UPYA.
   
 9. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #9
  Oct 1, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,582
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280

  Mkuu naweza kuamhua sasa hivi nikazusha jambo la kidini, kama ni uongo si kaa kimya?? utapingana na vingapi dunia hii, ndio nyie hata ubalozi wa nyumba nne nne hamuwezi!!!

  xxx (Islam)
  www (catholic)
  wwwww(pagan)
  fffff(mlokole)
  JJJ(hindu


  xxxxx(islam-sunni)
  wwhyy)islam-shia)
  wwww(catholic old)
  eeeeee(catholic-wakarisma)
  ee........

  ggggg(walokole(kakobe, kulola, list goes on)  Kaka utaendelea weee mwisho wake utajikuta uko wewe na mkeo ndani, kama mnatoka kabila moja, vizuri lakini hamtoki familia moja

  Ukienda Bukoba wao wanashindana koo, koo hii wajinga,, koo hii wana akili,..


  Kuzungumzia au kuwa sensitive na dini, ukabila Tanzania ni uwendawazimu, wewe kutuma post kama hii unaongeza tatizo , hausaidii watu waliokuwa wala hawawazii hii ishu.

  Mimi nimekua nchi hii sijui wala kuuwazia udini, leo mijitu kama nyie....


  Si siri kuwa waislam wengi wana inferiority complex ambao ndio mzizi wa matatizo mengi, ukikuta mkristo anayewagwaya waislam , basi aidha mzembe, hana kazi, hana elimu, hajui anafanya nini katika maisha yake ya kila siku!!!!!

  DWA YA WAKRISTO AU WAISLAM WANAOENDEKEZA UDINI, NI KUTOWASIKILIZA KAMA WAKIPOST THREAD HAPA WALA HAICHANGIWI!


  MOD; muanzisha thread amegusia swala la kuwa waangalifu, hizi ishu zifuteni kabisa zikija humu, AIBU JAMANI kuzungumzia udini na ukabila!!!!
   
 10. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #10
  Oct 1, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,582
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280

  Mkuu naweza kuamhua sasa hivi nikazusha jambo la kidini, kama ni uongo si kaa kimya?? utapingana na vingapi dunia hii, ndio nyie hata ubalozi wa nyumba nne nne hamuwezi!!!

  xxx (Islam)
  www (catholic)
  wwwww(pagan)
  fffff(mlokole)
  JJJ(hindu


  xxxxx(islam-sunni)
  wwhyy)islam-shia)
  wwww(catholic old)
  eeeeee(catholic-wakarisma)
  ee........

  ggggg(walokole(kakobe, kulola, list goes on)  Kaka utaendelea weee mwisho wake utajikuta uko wewe na mkeo ndani, kama mnatoka kabila moja, vizuri lakini hamtoki familia moja

  Ukienda Bukoba wao wanashindana koo, koo hii wajinga,, koo hii wana akili,..


  Kuzungumzia au kuwa sensitive na dini, ukabila Tanzania ni uwendawazimu, wewe kutuma post kama hii unaongeza tatizo , hausaidii watu waliokuwa wala hawawazii hii ishu.

  Mimi nimekua nchi hii sijui wala kuuwazia udini, leo mijitu kama nyie....


  Si siri kuwa waislam wengi wana inferiority complex ambao ndio mzizi wa matatizo mengi, ukikuta mkristo anayewagwaya waislam , basi aidha mzembe, hana kazi, hana elimu, hajui anafanya nini katika maisha yake ya kila siku!!!!!

  DAWA YA WAKRISTO AU WAISLAM WANAOENDEKEZA UDINI, NI KUTOWASIKILIZA POPOTE PALE; NA KAMA WAKIPOST THREAD HAPA WALA HAICHANGIWI!


  MOD; muanzisha thread amegusia swala la kuwa waangalifu, hizi ishu zifuteni kabisa zikija humu, AIBU JAMANI kuzungumzia udini na ukabila!!!!
   
 11. m

  muzunje New Member

  #11
  Oct 1, 2009
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  maneno ya sikonge inathibitisha wazi kwamba yeye ni mdiniwa wazi..huo uongozi wa juu una watu wa3,kwa namna yeyote ile lazima dini1 ingekuwa na watu2 na nyingine iwe na mtu1...tatizolinakuja kwa wagalatia hawataki kuona idadi ya waislamu inazidi wagala ktk jambololote lile la kimaendeleo,, misingi hii wamejengewa na baba yao nyerere...hebu leteni ripoti ya vyuo vingine na taasisi zingine za elimu tuone dini gani ina watu wengi...wakristo hasa wakatoliki wanabagua waislamu,,pia wanabagua wakristo wenzao wa madhehebu mengine,, jambo hililinahitaji suluhishokwani hukombelehatutofika,, lazimakuwe na equality..we are all tanzanians, we should enjoy every singleoportunity 2gether...god bless tanzania,
   
 12. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #12
  Oct 1, 2009
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  jamani mbona haya mambo tulisha ya jadili, kuwa na viongozi wengi wa dini mmoja c lazima kuwe na udini..kwanza mtu kama kikula sio muislam wa msimamo mkali kama mnavyodhania pili mambo ya mishahara ya waalim vyuo vikuu...JAMANI INALIPWANA HAZINA NA SI KIONGOZI WA CHUO, NA INAJULIKANA JAMANI EHHH watanzania hapa kabisa inaonekana jinsi gani tulivyo nyuma kielim mambo madogo kama haya hatuwezi kuyaelewa..mmh inatia shaka sana utendaji kazi wetu
   
 13. Mukuru

  Mukuru Member

  #13
  Oct 1, 2009
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii no hoja dhaifu mno. Hivi mtoa mada unatarajia kuwa kila sekta idadi ya waislamu na wakristo kuwa sawa? Ni kitu ambacho hakiwezekani kwani nafasi za kazi hazijazwi kuzingatia dini ya mhusika bali sifa za kitaaluma na ujuzi. Serikali inaweza kwa makusudi kabisa kujaribu kuoanisha uwiano huo lakini itakuwa si jambo la busara kujaza nafasi kwa kigezo cha dini kwani matokeo yake ni kuweka watu kwenye nafasi wasizoweza kuzimudu. Tunapobandika mada tutafakari kama tunachobandika kina mantiki isiwe ni suala tu la vidole kuweza kukandamiza 'keyboard".
   
 14. Geeque

  Geeque JF-Expert Member

  #14
  Oct 1, 2009
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 848
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Mukuru nadhani hujamuelewa mwandishi wa hii hoja, alichokuwa anafanya ni kujaribu kujibu madai ya mtoa mada mwingine ambayo inapatikana hapa https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-elimu-education-forum/39165-udini-wa-kutisha-udom.html
   
 15. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #15
  Oct 1, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  MIMI NAONA MADA HII IKAE HAPA ILI UKWELI UJULIKANE.WAKATI UDOM INAANZA ILICHUKUWA WANAFUNZI ELFU TANO NA WAISLAM WALIKUWA 110. KAMA UONGOZI WA UDOM NI WA KIISLAM VIPI IDADI YAO IWE NDOGO KIASI HICHO? UONGOZI WA WANAFUNZI WOTE UMESHIKWA NA WAKRISTU.

  NAOMBA KAMA SISI TUNA HURUMA NA MOYO WA MSHIKAMANO KWA TAIFA LETU TUPITIE NA VYUO KAMA UNIVERSITY OF DSM NA MZUMBE.

  NILIWAHI KUSOMA UTAFITI FULANI NA KUAMBIWA KUWA ASILIMIA 96 YA WAHADHIRI WA UDSM NI WAKRISTU NA KATI YAO ASILIMIA 60 WAMETOKA SEMINARY ZA KIKRISTU.WEBSITE YA UDSM NI WWW,UDSM.AC.TZ

  LAKINI MIMI NAOMBA LEO TUKITIZAME CHUO CHA MZUMBE.WWW.MZUMBE,AC.TZ TIZAMA SEHEMU YA SELECTED CANDIDATES WA UNDERGRADUATE NA POSTGRADUATE WATU WA DINI GANI WAMECHAGULIWA?. UKIMALIZA HAPO NENDA KWENYE STAFFS DIRECTORY.

  LABDA NIWEKE WATENDAJI WAKUU WA CHUO KIKUU MZUMBE.

  SENIOR OFFICERS=CHANCELLOR-JAJI SAMATTA-MKRISTU.

  VC PROFESSOR JOSEPH KUZILWA-MKRISTU.

  DEPUTY VICE CHANCELLOR (ACADEMIC) NI PROFESSOR MAGISHI MGASSA-MKRISTU.

  DEPUTY VC (ADMINSTRATION AND FINANCE) PROF-FAUSTINE KAMUZORA-MKRISTU.

  SECRETARY TO THE COUNCIL DR.RAPHAEL J.HABI -MKRISTU.

  HALAFU KUNA DEANS AND DIRECTORS.

  DEAN-SOCIAL SCIENCIES-PROF-EULALIA TEMBA.
  DEAN-FACULTY OF COMMERCE DR.JOSEPH KIMEME.
  DEAN-SCIENCE AND TECHNOLOGY-PROF PHILBERT NDUGURU.
  DEAN FACULTY OF LAW-ELEUTER MUSHI.
  DEAN FACULTY OF MANAGEMENT-PROF JOSEPHAT IFIKA.

  DIRECTORS KAMA WAFUATAVYO
  ALLOYCE P.MAZIKU,EMMANUEL MATIKU,MAKOMBE,DR.AGGREY KIHOMBO,MRS.MATILDA KUZILWA,DR.ANDREW H.MBWAMBO,MR.ROSS KINEMO.

  HALAFU KUNA ASSOCIATE DEANS.

  DR.JEREMIAH KIRWAY-SOCIAL SCIENCIES.

  MR.DAVIS J.MEELA =COMMERCE.

  MR.HILLARY LUBENGO-LAW-MKRISTU.

  MR.SIMON NJOVU -SCIENCE.

  DR.RICHARCH GELLEJAH-MANAGEMENT.

  DR.LETISIA WARIOBA -PUBLIC ADMIN.MKE WA VC ALIYEKUWA NA phD FEKI MZUMBE.

  MR.ADOLFH MAKAUKI -DEVELOPMENT STUDIES.

  HALAFU KUNA ASSOCIATE DIRECTORS MR.GABRIEL KOMBA-GRADUATE STUDIES.
  MR.GEORGE BEA-LIBRARY.

  OFFICE OF VC KUNA WATENDAJI WAFUATAO.
  MR.PETER A.MBUGHUNI-HEAD-INTERNAL AUDIT.
  MR.FOCUS J.MMARI -HEAD-PUBLIC RELATION.

  HALAFU KUNA ASSISTANT OFFICERS OF DEPUTY VC.
  MR.DIDALE BAASHA HEAD OF PERSONAL.
  MR.JOHN TLEGARY HEAD OF FINANCE.
  MR.GOLTFRIEND MWAMANGA-HEAD OF PLANNING.

  MRS MARIAM M.NGOWI-HEAD OF STUDENTS WELFARE.
  DR.BUNINI MANYILIZU HEAD-HEALTH SERVICES.
  STEPHEN MPAPASINGO-HEAD -BUILDINGS AND ESTATES.

  HALAFU KUNA ASSISTANT OFFICERS OF DEPUTY VICE CHANCELLOR-(ACADEMIC).

  MR.NOEL MROPE SECRETARY TO SENATE.
  MR.MICHAEL MTILA-EXAMINATION OFFICER.
  MR.GEORGE IGULU-ADMISSIONS OFFICER.
  DR.SESABO MTILA-QUALITY ASSURANCE UNIT.

  NAOMBA WAISLAM WAKO WAPI HAPA MZUMBE? MMEFUMBA MACHO NA KUKAAA KIMYA. HADI MALECTURER FEKI NI WAKRISTU WAMEJIPENYEZA NA KUWA VC WA MZUMBE.
  HAPO SIJAWEKA WAHADHIRI WA MZUMBE AMBAO NI HAO HAO WAKRISTU.
   
 16. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #16
  Oct 1, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Nyie wabongo, Kutumia dini kama kigezo cha kutoa mshahara mzuri kwa mtu mwenye sifa sawa na mtu wa dini yako haikubaliki wether you are christian or Muslim.

  Hoja iliyoletwa hapa kubwa ilikuwa ni kutumia CHEO au madaraka aliyonayo mtuhumiwa.

  Ila nyie mlioenda "shule saana" mmeshaanza kulete UDINI hapa. Tofautisheni kuwa Mdini na kutumia DINI kama kigezo, I know there is a thin line between the two, but surely there is a line.

  Endeleeni kujadili DINI. Hebu tuleteeeni na Chuo cha Makumira Arusha kisha cha Tumaini kisha cha CBE. It is Obvious that you will find more Christians than Muslims.

  Sababu kubwa ni kuwa wakati Christians wanaenda shule ya kimagharibi, Muslims (wengi wao); walikuwa wanaenda Madrassa.

  Hii vilevile ni sawa na kukuta Wachaga au Wanyakyusa au Wasukuma ni wengi sehemu flani ya kazi. Ukweli unabaki kuwa waliwahi kwenda shule na ni wengi kikabila.

  Acheni udini tujadilini mambo ya maana.
   
 17. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #17
  Oct 1, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145

  No wonder kila kwenye vita (sehemu nyingi) ni kwasababu ya watu kama nyie... Somalia, Boko haram(Nigeria), Afghanistan, Iraq, Sudan....

  Mnaboa sana na analysis zenu hizi za kidini bila kufikiria nje ya BOX kwanini inakuwa hivyo.
   
 18. N

  Nangetwa Senior Member

  #18
  Oct 1, 2009
  Joined: Feb 9, 2009
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  I hate this discussion
   
 19. K

  Kikwebo JF-Expert Member

  #19
  Oct 1, 2009
  Joined: Aug 25, 2006
  Messages: 352
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Ukisikia kumkoma nyani giladi ndio huku.
  Kudos kanda2.

  Yaani umefunika, umeweka sawa kila kitu. Analysis yako imekuwa very extensive. Duh! kumbe jamaa zetu ndivyo walivo. Nafasi zote wamehodhi wao.

  The point ambayo watu wanaikosa humu ni moja tu. Waislamu hawapaswi kuonekana kwenye sehemu zozote za maendeleo na elimu. Wao wameshatengewa kazi zao ambazo ni upishi, usafi na udereva.

  Hii inchi sasa inaelekea kubaya na wenyewe wameshasema kama HAWADANGANYIKI. Unajuwa facts kama hizi wakizipata wale jamaa zangu pale Mtambani, Kichangani au Kwa Mtoro bdio watazdi kuchanganyikiwa, si unauwa Jazbii walivyo.
   
 20. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #20
  Oct 1, 2009
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Hivi mnatumia methodology gani kujua dini ya mtu?
  unamwangalia usoni? au unaangalia jina lake au mnafanyaje wandugu?
   
Loading...