Ukweli kuhusu tunaoishi nje ya Tanzania

HTML:
Nimeishi nchi kumi na moja za kiafrica pekee, sijawahi kutoka nje ya Africa

Hizo nchi 11 zinapatikana S Africa?


angola,zambia,congo drc,malawi,zimbabwe,namibia,swaziland,lesotho,mozambiq,sa,nk
 

kuna ukweli mkubwa mno kwenye hili,naona tatizo kubwa la nchi yetu maskiniwengi sana,halafu watu wana njaa sana sasa sijui utasaidia wangapi
mimi shida moja nayopata nikija home nimsaidie nani??unakuta una hela za kugawa mfukoni,sijui tuwekeje mambo hapo
 

ni kweli 90% ya watanzania wanaoishi hapa wanauza unga,lakini cha kushangaza kila siku utawaona vilevile,hamna mabadiliko
 
Maisha Tanzania kwa ujumla wake ni mazuri sana kama mtu ukijipanga vizuri, kwa kuwa kuna kila aina ya vianzio vya maisha kama ardhi nk, na ni rahisi kuanzisha biashara hata ndogondogo kuliko hizi nchi za nje ambazo ni vigumu sana kujikwamua.
 
"........iyo kupata kazi inakuwa Tabu sana matokeo yake wanakuwa ni wezi,majambazi, Wauza unga, kuna watu wengine wanalal nje kwa sababu hawana pesa za kulipa kodi ya nyumba na kodi ya nyumba kwa mwezi ni dola 300 au Dola 500 kwa mwezi ,na mengineyo mengi tu.

Jamani mimi nimeishi nchi nyingi sana na kutembelea baadhi,ninachojiuliza hawa wanaoshindwa yote wakati wamefika kwenye nchi yenye neema zaidi kidogo ya nchi uliyotoka,yaani unashindwa hata kuoa,kuolewa au kufanya chochote ukawa na maisha yaliyo bora kuliko uliyokuwa nayo TZ?Mimi nimeishi Sweden,Finland,UK, Japan,Poland, US kote huko ukitangaza kuolewa na mama Kibonge yaani ni mara moja au kama ukitangaza kumuoa bibi kizee ni mara moja,ukivumilia 10 years huwezi kurudi mtupu,nimeuliza Pretoria kuna mtu anaunganisha watu ingawa bahati mbaya ni kina bibi wa ki Israel wakikuooa inabidi ufanye kazi sana on the bed na yeye kazi ya kupika,kuosha mbwa nk ni juu yako lakini mvumilivu hula mbivu,lakini kwa wali soma nina imani kazi sio shida ila kazi ya kulipwa kiasi gani ndio shida-njooni huku Iceland,ukiingia ni pm,niliolewa 7 yrs lakini sasa mambo yangu si haba na nimerudi nikamuoa mswahili na mambo si mabaya. Ugali na maharage ndio vilivyonifanya nikapata akili-nyumbani pazuri lakini kwa mwenye kujua akiamka anaelekea wapi na ni bora kibaka wa SA au dunia nyingine kuliko wa TZ ukishikwa hata jela hufiki jamaa wameisha kuchoma moto.Mimi popote ninapoweza kuishi bila kubaguliwa au kubaguliwa kwa %ndogo naishi tu kuliko kujidai uzawa ukaenda kufa na njaa.
 
Karibuni Poland and Romania....huku mambo shwari


nikitoka hapo vacation zanguni mitaa ya Kosovo na Albania:happy:
 
Fuateni nasaha za Riz1 - tunaishi kimjinimjini na mtu anaweza kuishi hivyo po pote duniani!
 
 



mzee napongeza hiyo idea uliyotoa hapo,lakini kwa south africa ni ngumu sana swala la kuoa,
hata mie nilijaribu kuoa lakini did not work out,kilichonisaidia ni kufikiri na kutenda kilichonileta hapa
nafikiri ulaya ni rahisi kuoa na ku win but not sout africa.
unless ufanye kama wanavyofanya wanigeria kuoa kwa ajili ya kumbebesha unga mwanamke
 

You missed the point, hulipendi swali hilo kwa sababu una complex fulani, neno la kwamba "I am proudly African" ni neno lina sema una complex, kwanini uwaze kuwa uko proud na uafrika?
Mtu yeyote anayeonekana ni tofauti ktk mazingira fulani kuna uwezekano kabisa mkubwa wa kuwauliza unatoka wapi? mbona sie wazungu huwa tunawauliza kila siku wanatoka wapi na nchi gani na huwa wanaonekana kujivunia kutaja nchi zao, kwanini sisi tukwazike kutaja nchi zetu?
 

Kwahiyo huko uliko mambo safi kuliko TZ, sasa mbona unawabaia wasije huko ili baadae usiwagawie pesa?
 

Kuna wabongo wanapeta kwa sana tu nje ya nchi kwa kazi za maana na mishahara minono lakini kuna baadhi wana dhana kwamba kwa vile hawasikiki basi Watanzania wote wanaoishi nchi za nje ni wabeba box tu. Tena hao wenye kazi za maana wamejenga jina zuri sana kwa nchi yetu kwamba ni wachapa kazi hodari na si walalamishi, lakini kwa kuwa hawasikiki basi wote wa nje ni wabeba box tu!
 
Mkuu uko wapi hapo amerika? Watu wanazungumzia South africa wewe unazungumzia mambo ya Amerika?Kwani huko amerika hakuna Watu wanaoishi nje kulala lala ovyo mitaani? mbona unasema maneno ya uongo mkuu?
 
Mkuu wengi wao ni wabeba Mabox ukienda Uingereza utawakuta Wengi Watanzania Wanafanya ya kubeba Mabox kubeba Zege Mkuu wewe kwani upo wapi? unayajuwa maisha ya south africa? kwa kisomo cha Darasa la Saba au Form 4 Ya Tanzania huwezi kupata kazi nzuri south Africa au hata Uingereza lazima Ubebe Mabox tu mkuu upo na mimi? Wengi wasafiri hawana kisomo ndio maana wanakimbilia nje ya nchi mkuu unajuwa hiyo?
 
Reactions: BAK

Hata UK mimi nawafahamu wengi wanaofanya kazi zinazohitaji elimu ya nguvu, wengi wa hao unaowasema ni wale wakimbizi waliodai kukimbia manyanyaso baada ya uchaguzi wa 1995 na waliingia UK kama wakimbizi toka Bongo na wengi hawakuwa na elimu ya maana.
 

Mkuu kuna siku niko kwenye subway tumejazana......nikaona wazungu wanasoma magazeti, halafu kucheki gazeti ambalo mmoja anasoma....nikaona picha ya binti albino mikono yake imekatwa.......halafu kuangalia vizuri....nikaona tukio hilo lilitokea Tanzania......nakumbuka moyo ulinipiga pa....kijasho chembamba kwa mbaali kikaanza kunitoka.....hapo nikafikiria moyoni kuwa nikiulizwa tu kuwa unatoka TZ.......nahisi ningeukana utanzania kwa mara ya kwanza....lakini uzuri swali hilo halikuulizwa kama ilivyo kawaida ya watu hawa kutoongea kwenye public transport........

Jamani licha ya kuwa nyumbani ni nyumbani kuna matukio mengi sana ambayo yanavunja moyo yanataarifiwa......

But bado naamini home is Best....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…