Ukweli kuhusu ndege za Serikali

Lissu biashara hajui ila kakalia kishabiki shabiki tu

kuna biashara unaweza tumia Mil.50 kuifungua ila faida ikaja robo au hata robo isifike kwa mwezi m1

Biashara imegharimu 50mil ila faida per day 100k ukipiga kwa mwaka unapata 36,000,000M

Unaweza ukaona ndani ya mwaka mzima Hata hela ya biashara(mtaji haijarudi) ila huwezi sema hii biashara MBAYA

au HAILIPI
BADO safari inaendelea kwenye biashara kuna miaka inaendelea kwenda Faida itaonekana TU

Tatizo la watu waliozoea mishahara ya mwisho wa mwezi ni 1 tu wao UVUMILIVU kwao ni ZERO.

Yani lissu anataka anza leta siasa kwenye Biashara (huyu mtu huyu aseeee) yani iko hivi bwana Lissu

Hizo ndege hata zikifanya kazi kwa miaka 20 hazijrudisha hiyo hela Bado siwezi sema eti Tulifanya makosa zinunua

Ila tu hizo ndege ningekuona wamaana kama ungesema zimetengeneza HASARA kiasi fulani au zimetengeneza MADENI

kiasi fulani Ndio tungepima Mizani sasa HASARA vs FAIDA ila usitupimie biashara kwa kipimo chako cha CAPITAL vs FAIDA

Faida zipo indirect way na Direct way

Lissu usitake jitoa ufahamu hujui ni watalii wangapi wameshaletwa nchini na kuacha pesa tofauti na Hela(faida) walizosema ATCL

ki ufupi bwana Lissu TUACHE KIDOGO.
 
Siyo kila anayekuja JF lazima achangie hoja. Wengine muwe mnasoma na kujifunza tu. Yaani kwa akili yako unaamini kweli matumizi ya Serikali yamepungua kwa sababu safari za watumishi wa umma zimepungua?

Na unaamini ndiyo zilizonunua ndege? Pole sana, Serikali hii ndiyo ina matumizi makubwa ya kutisha kuliko zote. Kama una elimu ya kawaida tu nenda kasome CAG Report, ukielewa ndiyo urudi hapa
 
Kwenye suala hili Dotto anaingiaje?
Tujikite kwenye maada maana ndugu zangu nyingi mkitoa hoja na kujibiwa kwa hoja badala ya kuendelea na mjadala mna tabia ya ku-diverge issue yenyewe na hivyo kupoteza maana.
Dotto kama kitaalamu alipaswa mwambie mjomba wake namna taratibu za fedha zinavyotaka kwa kuwa yeye ndiye mtaalamu.
 
Hebu tupige hesabu....... Mapato Bil 30 - Uwekezaji 1.7 Trilion ( Bil 1700 )

% Interest after 3 years = 30//1700 times 100 = 1.76 Billion. (Hii si Faida bali ni Gross)

Ukifanya kwa kila mwaka inakuwa 1.76 divice by 3 = 589 milion. (Hii nayo ni Gross).

Kifupi unawekeza 1.7 Trillion then unapata Gross income ya 589 mil kwa mwaka.

au ni sawa na kusema unakusanya Tshs Million moja kama Gross kwa uwekezaji wa Billion 2.9
 
Pole sana wewe unayeumia roho. Ulizoea kula vya bure kama nzi awamu iliyopita. Fanya kazi.
 
Wapinzani mnapokosa mambo ya msingi ya kujadili mnakuwa vituko sana. kwa hiyo unalinganisha makampuni ya Bakhresa ambayo yanatafuta faida kubwa na taasisi za serikali ambazo ni kwa ajili ya kutoa huduma?
Heeeee!!! Mkuu yaani hizo ndege ni kwa ajili ya kutoa huduma? Ipi hiyo vitu vingine sio lazima kuchangia,
 
Dotto kama kitaalamu alipaswa mwambie mjomba wake namna taratibu za fedha zinavyotaka kwa kuwa yeye ndiye mtaalamu.
Inaelekea wewe hufahamu serikali inavyofanya kazi. Hivyo basi wazaramo wanasema 'karaga baho'
 
Naiunga mkono hoja yako kwa 100%
 
Wananunuzi wa Ndege wao wanataka 10% yao kwenye ununuzi na pia kwenye matengenezo service zake, wao wanaangalia matumbo yao kwanza mengineyo ni mbele kwa mbele huko
Tuna tabia ya kuzungumzia mambo ambayo hatuna weledi nazo . Na hizo tunazikuza kiasi kwamba hata ukweli unapotolewa kwa vile haupendezi basi ni wachache tu wanaweza ku-appreciate hayo.
 
CHADEMA mnajidhalilisha sana kwenye Ilani yenu ya uchaguzi 2015 mliandika kuhusu ndege ukurasa wa 53 hivi mnadhani watu hatusomi au hatukumbuki mliyokuwa mkiyanadi sasa yamefanywa na CCM mnaona mabay au mnadhani watanzania ni wote mazuzu.

Hapo kwenye huo ukurasa walisema watanunua ndege kwa cash bila hata bunge kushirikishwa?
 

Faida ni nyingi mno;
Aione TL kwenye Jalada
 
Inaelekea wewe hufahamu serikali inavyofanya kazi. Hivyo basi wazaramo wanasema 'karaga baho'
Kati ya mimi na wewe nani anajuwa Serikali? Wewe ni mshabiki tu wa huu utawala mbovu mimi ni muumini wa Good Governance and rule of law.
 
Wapinzani mnapokosa mambo ya msingi ya kujadili mnakuwa vituko sana. kwa hiyo unalinganisha makampuni ya Bakhresa ambayo yanatafuta faida kubwa na taasisi za serikali ambazo ni kwa ajili ya kutoa huduma?
Sijui kama unajua vipau mbele vya taifa, na sidhani kama utavijua kama hutakaa uwaze vyema na kufikiri kwa kutumia akili ya kichwani.
 

Mzalendo ananajisi box la kura au mimi ndio sijui maana ya uzalendo? Sasa hivi ni ngumu kutofautisha uzalendo na ujinga.
 
Kupanga ni kuchagua ndege ni muhimu pia,lkn tungeanza na vigusavo wengi mfano miradi igusayo watu ili kukuza ajira na kuongeza idadi ya walipa kodi,kisha ziada ndo tukimbilie kwenye miradi hii mikubwa bila kuwasomesha watu namba kwa kuathiri shughuli zao. Hicho kilichokusanywa ni kidogo sana kulinganisha na thamani za ndege hizo kama tungewekeza kwenye miradi mingine ya kukuza ajira za vijana nchini.
 
Mzalendo ananajisi box la kura au mimi ndio sijui maana ya uzalendo? Sasa hivi ni ngumu kutofautisha uzalendo na ujinga.
Neno Uzalendo limebadili maana siyo ile tunayoijua. Kwa mfano hapa Tanzania hakuna mtu amepigania haki za madini kutoka kwa wawekezaji kushinda Tundu Lissu. Halafu Meko anasema Tundu Lissu siyo mzalendo auliwe. Ridiculous!!

Wanaijiita wazalendo ndiyo akina Bashite, Meko na Ole Sabaya wakati kazi yao ni kujitajirisha kwa fedha za unyang'anyi wa wazi wazi.
 
Hata kama wanapiga dili si watazitapika ukiingia awamu nyingine maana madaraka ni sawa na koti la kuazima.Maana huwezi ficha Mali au pesa zitataifishwa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…