Ukweli kuhusu ndege za Serikali

Chapa Kazi JPM wasiotaka kwenda na kasi hii wahame nchi sivyo minyororor ipo tutawaburuza tu. Hapa Kazi tu.
 
Yaani 1.2 T. Kwa ajili ya kutoa huduma!!!?
Ni maji hayo!!!??
Ni umeme huo!!!?
Ni vituo vya afya hivyo!!!?
Ni barabara na madaraja!!!?
Ni posho ya vijana wetu waliomtaani wasio na kazi!!??
Ni pembejeo za kilimo au ruzuku!!?
Ni malimbikzo ya madeni ya watumishi wetu!!!?
Nimelipa zaidi ya 400,000 kwenda na kurudi Dar kutoka Mbeya,je hii huduma mama yangu anayelima mpunga pale Kyela,analipewa na nani!!?
Wapinzani mnapokosa mambo ya msingi ya kujadili mnakuwa vituko sana. kwa hiyo unalinganisha makampuni ya Bakhresa ambayo yanatafuta faida kubwa na taasisi za serikali ambazo ni kwa ajili ya kutoa huduma?
 
Kuna watu wezi kweli duniani, kila siku ndege ndege, mpaka watu wanakushtukia una maslahi yako binafsi.
 
Endelea kuwa na mawazo ya fisi ukisubiri mkono uanguke.
 
Muafrika siku zote anachojua ni kukosoa tu. Ukimwambia aje na wazo mbadala ni vichekesho vitupu utakavyovisikia.
 
Endelea kuwa na mawazo ya fisi ukisubiri mkono uanguke.

Muda si mrefu akili ikiwarudia mtaanza kutafuta visingizio vya sababu kwanini uwekezaji wenu umebuma; lakini wakati huo wananchi maskini watakuwa wameisha umia sana!!
 
Hapa ndipo mnapodhihira kuwa wapinzani hamna akili sawa sawa... Mkuu umeshawahi kwenda AirPort ukaona lile Dreamliner linavyoshusha watu? Kwani lazima kila kitu mpinge?
Leta mahesabu bana. Kushusha watu haimaanishi mnapata faida. By the way, kwa nini hamtaki CAG akague mahesabu ya ATCL?
 
Leta mahesabu bana. Kushusha watu haimaanishi mnapata faida. By the way, kwa nini hamtaki CAG akague mahesabu ya ATCL?
Watu wamepanda burr kwahyo🤣🤣🤣🤣... Na wewe lete ushahidi kuwa hawataki CAG akague, na tafadhali usilete screenshots za tweets za kina sarungi na zitto maana ndio madereva wenu 😂😂😂😂
 
Uko sawa kichwani ?
Wapinzani mnapokosa mambo ya msingi ya kujadili mnakuwa vituko sana. kwa hiyo unalinganisha makampuni ya Bakhresa ambayo yanatafuta faida kubwa na taasisi za serikali ambazo ni kwa ajili ya kutoa huduma?
 
Dah kweli wapinzani mmeishiwa, hivi nani kazuia CAG asifanye kazi?
Nimetafuta audited accounts online sijaziona. Mimi sio mpinzani for the sake of upinzani na kwa kweli maneno "vyama vya upinzani" si sahihi kwani hawapingi kila kitu. Wangeitwa vyama mbadala au litafutwe neno muafaka. Chama kinachopinga kila kitu hakifai kuwepo.
 
Ndege ni lazima zinunuliwe, tupende, tusipende. Ni kawaida uchaguzi mmoja unapoisha unafuata mwingine baada ya miaka 5. Na hela lazima itafutwe. Fisadi zote kubwa katika nchi zisizo na democracy huwa na mkono wa dola ukilenga kupata pesa kukikomboa chama tawala.
 
Muda si mrefu akili ikiwarudia mtaanza kutafuta visingizio vya sababu kwanini uwekezaji wenu umebuma; lakini wakati huo wananchi maskini watakuwa wameisha umia sana!!
Bado unaendekeza akili za fisi. Kuna uwekezaji wa aina nyingi ukibuma wa aina moja watu wanawekeza kwingine.

Unasubiri kuona kutofanikiwa yaani mambo yale yale ya kutegemea mtu kushindwa.
 
Marekani
Kwahiyo unataka nchi iendeshwe kama kiwanda cha mtu binafsi? Nitajie Nchi moja iliyo uchumi wa kati ambayo haina shirika la ndege.

Ati hawa ndio wapinzani!
 
Kuna uwekezaji wa aina nyingi ukibuma wa aina moja watu wanawekeza kwingine.

Hiyo hasara ya huo uwekezaji uliobuma kwanini wananchi wabebeshwe wakati ujeuri wa watawala ndio chanzo cha hasara hizo? Hasara ya korosho ni mfano dhahiri ambapo wananchi wanaumia kwasababu ya upuuzi wa mtu mmoja.
 
Una uhakika korosho imeleta hasara? Au ni maongezi ya mtu wa Dar akiongelea masuala ya mikoa ya kusini?.

Unafurahia kuona mkulima wa korosho akitumia gharama zaidi ya tshs 2000 halafu mnunuzi anakuja na tshs 1800?. Epuka porojo za mitandaoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…