Nikupateje , nimeona mantiki yako katika suala hili.
Je kwa kutumia mantiki yako, tunayo haki pia ya kuwauliza wale wanaodai ziwa lote ni lao ilikuwaje wanaruhu mapaka leo hii watanzania wanafanya shughuli za uvuvi kwenye "ziwa lao" - utakumbuka sisi tulivyofanya kwenye lile sakata la "samaki wa Magufuli"!.
Je ilikuwaje wakaruhusu(wakaachia) watanzania kuingiza ferry (MV Songea nk) ndani ya mipaka yao na kufanya shughuli za usafirishaji wa watu? Kwa nini wasiwazuie/kuwakamata wavuvi na hata hizo ferry zinazoingia kwenye "territory yao" bila kufuata taratibu? Kama wanaamini ziwa lote ni lao kama "mikataba" inavyosema, je ni wazi kuwa wamalawi wameshindwa kulinda mipaka yao?
Hivi ni kweli kuwa "Malawi" (wajerumani, waingereza) ilikuwepo kabla ya wamanda, wakisi, wangoni, wapangwa na wengineo wanaoishi kando ya ziwa nyasa/malawi?