Ukweli kuhusu maisha ya ughaibuni

Mkuu mbona umekatisha.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha.
Poa kaka kila la kheri.
Tuendelee kuwatia moyo wazamiaji ila kiukweli kama huna elimu ya kueleweka Canada utaenda kusota.
ataishia kifanya kazi za warehouse ambazi nyingi zinalipa $16 kwa saa ambapo kwa wiki kisheria utafanya masaa 20 tu. na hapa ndipo linapokuja suala la kuwa na multiple Jobs.
 
Sina neno mkuu...

Una experience yoyote nje ya nchi? Ulishaishi wapi mzee....
 
No. Marekani sio. Unajua nini? Wengi wanakimbilia Marekani. Huyu jamaa amecheza kwenda Canada. Na mpaka kuleta uzi hapa ujue mambo yake tayari yanenyoooka

Sent using Jamii Forums mobile app
Exactly my point kiongozi....sasa msikie huyu jamaa Papi Chulo anavyojidanganya... Kule kama ni mzamiaji na huna mwelekeo mzuri utaelewa maisha ni nini....kuna watu wanazurula daily kule newyork hopeless... Kodi tu room standard $2,600...bado chakula,usafir cjui starehe na ugumu wa kupata kazi huo....kule ukienda jipange...
At least Canada mchomoko upo...
 
Mkuu umesema kweli elimu ndio mkombozi....ukiwa na skill highly needed,wala usihangaike kuzamia...nenda ubalozini kaombe visa... Hili jambo nimelishuhudia sana....
 
HALAFU UJUE MAISHA NA MTAZAMO WA MAISHA TUMETOFAUTIANA SANA. Yupo mtu anasubiri hela za msimu,huyo anaweza kupata hata milioni 200,anahakikisha ameiteketeza yote kwanza ndio anatafuta kazi tena. Wakati huo huo yupo mwenye mtaji wa milioni 50 tu anaendesha maisha yake ya kila siku vizuri sana na anaonekana ni bora kimaisha kuliko yule anaepataga milioni 200,100 mara nyingi. Nakuhakikishia hao wanaolalamika maisha magumu marekani ni wale machinooh kama hao. Hata alipokuwa hapa hataki kazi. AMEFIKA KULE MAREKANI AMEUNGANA NA WENYEJI MAJOBLESS,AMEANZA MAMBO YA MADAWA YA KULEVYA,KUVUTA BANGI,ANATAKA AENDE DISCO,KSBB NDIVYO VIJIWE ALIVYOVIZOEA HATA ALIVYOKUWA HUKU,HAPO ANATEGEMEA/ANASUBIRI HELA YA MIUJIZA. NA HAO NDIO WENGI WANAOSEMA MAISHA MAGUMU MAREKANI NA HAO NDIO WENGI WALIOUAWA HATA SOUTH AFRICA KSBB HATA SEHEMU ZA KUWAKUTA NI RAHISI NI KWENYE MAJUMBA MABOVU WAKIVUTA BANGI,WAKISUBIRI HELA ZA MSIMU. Marekani pia kazi za mashopaz zipo,ila inategemeana wanampatia mtu wa aina gani?. Kama unaonekana umechoka choka,mlevi kila wakati kwa nini wakupe?. Muda mwingine hata hao hao wenyewe hawataki kuomba hizo kazi za mabox,wakiwaiga wenyeji kwamba ni kazi za chini. Uliwahi kuletwa uzi hapa,wapo baadhi ya WaTz wanaoishi au waliofika Marekani wakasema kabisa nani afanye kazi za kujidhalilisha hizo za kubeba mabox kwenye mashoprite?. Lakini ni kazi zenye ujira mkubwa sana UKIJITAMBUA NA UWE NA MALENGO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli mkuu..... Nidhamu ya maisha na kujipanga vyema ndo vitakufanya uishi vizuri popote pale.
 
Sina neno mkuu...

Una experience yoyote nje ya nchi? Ulishaishi wapi mzee....
USA (Boston), UK (London & Birmingham).
In the bucket List for the coming year.- France & Belgium Huku natakiwa nikawakilishe taifa kwenye uwanja wa 6X6 😁 😁

NB: Siendi kuzamia huko anytime nikitaka kwenda napeleka tu kitabu nagongewa tu mhuri.

Hizo nimekutajia nilizokaa mwezi na kundelea.
Zile ambazo nimekaa not more than a week kwa safari za kikazi ziko kibao.

Naomba usiwe tomaso tafadhali
 
Mkuu umesema kweli elimu ndio mkombozi....ukiwa na skill highly needed,wala usihangaike kuzamia...nenda ubalozini kaombe visa... Hili jambo nimelishuhudia sana....
Tatizo ndugu zetu humu watabisha sana kwa hili. wanaona kama wanakatishwa tamaa.
 
Then kuna sehemu unapwaya.

Kwa experience yako nilidhani utajua maisha yetu hayalingani kabisa hasa kiuchumi achilia mbali kifikra.

Unafikiri utamwambia mtoto wa Mo ajilipue Ulaya? Haya chukua graduate aliyesomeshwa kwa shida hana mtaji anayekosa hata ajira za viwandani na kesho yake haijui umwambia nakupa fursa ya Norway.

Ataikataa? Tomaso ni nini?
 

Sawa kabisa umedadavua vizuri mkuu tatizo wengi humu ujuaji wakati hawajui kitu kuongezea Canada bad inahitaji wahamiaji na sio ngumu sana kama USA changamoto ni baridi
 
Habari za leo Wana JF,Natumai mko poa sana na wale ambao hawako vizuri kwa namna moja au nyingine namuomba mwenyezimungu awaondoe katika hali hiyo na awapeleke katika hali nzuri zaidi ili waweze kuendelea na mapambano ya maisha ya kila siku.Nichukue nafasi hii kipekee kabisa kuweza kumshukuru mwenyezimungu,Mwenyezimungu ambae anatupenda sana sisi Wanaadamu na ametuumba umbile zuri kuliko kiumbe mwingine yeyote yule na ametufanya kuwa na akili ya kufikiria na kuamua na kuchagua kile ambacho tunakitaka hivyo hatuna budi kumshukuru.Ntakuwa mchoyo wa Fadhila kama sitawashukuru wana JF ambao wamesoma na kucoment hadithi yangu ya ukweli na sio ya kutunga hivyo nawashukuru sana.

Inaendelea...........

Baada ya kuvuka ile border ya USA na Canada nilikutana na polisi na bila ya kunihoji walinipiga Pingu jambo ambalo lilinishitua sana na moyo wangu ukaanza kwenda mbio nikaona sasa nimejiingiza kwenye matatizo maana sikuambiwa kuwa ntapigwa Pingu niliambiwa ntasaidiwa tu.Nikasachiwa mwili mzima then nikapelekwa kwenye kituo cha polisi,Nilipofika mule ndani nikafunguliwa pingu kisha kikafunguliwa chumba kidogo sana ambacho kilikuwa na Choo chake nikaingizwa ndani kisha nikaambiwa na Polisi wawili wa CANADA nivue nguo zangu zote hivyo kubaki uchi kama nilivyozaliwa kisha wakanifungia mlango wakaondoka.Walipoondoka nikaanza kukiangalia kile chumba huku nikiwa na wasiwasi mkubwa na mawazo nikaona heater na Camera nne nikawasha heater maana kulikuwa na baridi kiukweli nilikuwa katika wakati mgumu sana nilikumbuka nyumbani hasa mama yangu,Watoto wangu,mke wangu na ndugu zangu nikaanza kutokwa na machozi nikikumbuka nilivyosoma kwa shida na kupata kazi na nikawa namudu maisha yangu na kusaidia ndugu zangu nikajiona katika watu wapumbavu mimi ni mpumbavu kwelikweli.Chumba hakikuwa hata na kigodoro hivyo sikuweza kulala Usiku mzima.
Ilipofika asubuhi majira ya saa tatu mlango ukafunguliwa na Polisi wawili wakafungua mlango kisha wakaingia ndani ya chumba changu wakanipa nguo zangu na kisha wakaniambia niwafuate.Tukaingia chumba kingine mulemule ndani nikakutana na Afisa mwengine wa Polisi akaniuliza kwa ukali "Why did you cross the border Illegally?" Nikamwambia kuwa mimi ni mkimbizi kutoka Somalia nimeletwa na Agent Marekani na amenipokea mtu ambae amenileta mpaka hapa akaniambia nivuke ntasaidiwa hivyo wakaniuliza tangu naianza hii Safari nimetokea wapi na nimepita wapi mpaka nimefika hapa,Waliniuliza maswali mengi sana ambayo sitaweza kuyaandika yote humu Pia waliniuliza kwanini nisiombe Asylum USA nikawaambia kuwa nimeambiwa USA hawapokei wakimbizi na uzuri nilishapangwa cha kusema hivyo nilikuwa naigiza vilevile nilivyofundishwa kujibu na wakati wananiuliza walikuwa wanaandika kwenye computer walipomaliza tu wakatoa Karatasi ambayo ilikuwa inaonesha maswali niliyoulizwa na nilichojibu kisha nikaambiwa nitie Signature yangu.

Baada ya hapo nikaambiwa niwafuate Polisi wale wawili walionitoa mule chumbani kisha tukatoka nje nikaambiwa nipande gari hivyo nikaingia kwenye gari ikiwa na Polisi wengine wapya watatu .Gari ikaanza mwendo ambapo nakumbuka ilituchukua masaa matatu mpaka Kufika mji mkubwa kidogo nakumbuka unaitwa Québec ambapo mji huo wanazungumza Sana Lugha ya Kifaransa.Nilipofika Quebec nikapelekwa sehemu kwenye mjengo mkubwa Sana ulivyo kama Hotel nikakabidhiwa kwa Ofisa mmoja mwanamke na akapewa karatasi zangu huku akiaambiwa kwa Kifaransa kisha wakaniaga wale walionileta wakaniambia wananitakia kila la kheri
Mwanamke huyo akaniuliza Je nkilichoandikwa kwenye zile karatasi ni kweli au uongo nikajibu ni kweli,Akatoka akaniletea kitambulisho kinachoonesha kuwa mimi Mkimbizi kutoka Somalia kisha ikapigwa simu kwa Security wakanipeleka sehemu humohumo ndani nikapewa Lotions,Sabuni za kuogea,Shuka na Blanket kisha nikapelekwa kwenye chumba ambacho kilikuwa na watu wawili tu ila kilikuwa ni chumba kidogo ambacho kilikuwa na vitanda vya Double decker viwili yaani kitanda kimoja mmoja analala juu na mwingine chini kwahiyo chumba kimoja hulala watu wanne japo nilikuta watu wawili tu ila ikiwa mtu na mkewe wanapewa chumba kimoja peke yao na kitanda kikubwa.Nilikaa pale mwezi mmoja huku nikapata breakfast na lunch na dinner kwenye Kantini kubwa iliyokuwa na watu wengi Sana ikiwa wengi wao ni Waarabu wa Syria,Yemen na Afghanistan pia kulikuwa na Wasomali wengi na Watanzania ambao wengi walikuwa Wazanzibari na Kutoka Dar ilikuwa nipo peke yangu ila hawakunibagua.
Niliiishi pale kwa miezi miwili huku nikiutembea mji maana tulipewa ticket za bure kwa mwezi mzima na ikiisha muda unapewa nyingine na tulikuwa tunalipwa kwa mwezi pesa kidogo bila ya kufanya kazi.Kwa kweli nilipata marafiki wengi wa Kizanzibar pale kambini na kupeana hope kuwa tutashinda kesi na kupata Papers za kuishi na kukubalika kisheria.Na tulipeana Technic nyingi za kushinda case maana kuna Wazanzibari walijiripua kuwa ni Wasomali na walipoulizwa kwenye Interview ya kesi zao walisema kuwa Walitoa rushwa ili wapate Passport za Tanzania na wengine walisema wao ni mashoga kwahiyo jamii zao zimewatenga na wanataka kuuliwa maana jambo hilo halikubaliki kisheria kwetu na wengine walisema wao ni Wanasiasa hivyo Serikali inawaua na kuwapoteza na wengine walisema kuwa ni Waandishi wa habari na vyeti feki wametengeneza vya Uandishi wa habari kwa kweli Wazanzibari uzamiaji upo kwenye Damu.
Baada ya mwezi mmoja niliitwa kwenye Interview yangu ya kwanza ya kuhojiwa kilichonikimbiza Somalia na nikienda nikahojiwa kwa muda wa masaa 6 na maswali niliyoulizwa ni mengi sana..........
ITAENDELEA................
Ntataja maswali yote niliyoulizwa kwasababu dhamira yangu sio kuwafundisha watu kuzamia ila wayajue maisha halisi ya kuzamia ili mtu akiamua kuja ajue nini kitakachotokea hivyo Kujiandaa kisaikolojia mapema

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…