Ukweli kuhusu maisha ya ughaibuni

Ukweli kuhusu maisha ya ughaibuni

Wale hawaombagi tu hela waga wanatenda ile dhambi mbaya pia.... Yaani wamexico,wazanzibari,wamarekani,wasomali wakuache hivihivi...
Baadhi ya watu wana akili mbovu sana.Wewe ni mmoja wao wakati ile ni biashara haramu ya watu wanachohitaji ni pesa tu sio lingine.Na Wamexico ndio waliokuwa na wanaovusha watu wengi kutokea kwao Mexico kuingia Marekani.Halafu usichokijua ni kwamba Canada na Marekani hakuna Ukuta au uzio wowote sehemu kubwa ipo wazi unaweza hata kuvuka bila kukamatwa,Utakamatwa ukishavuka ukawa upo Canada.Ila Mexico na Marekani kuna Ukuta Mkubwa sana huwezi kuvuka kirahisi lakini still Wamexico ukiwapa pesa Wana njia zao wanakuvusha kutokea Mexico kuingia Marekani ila border Patrol ni kubwa sana Upande wa Marekani.Nimejifunza mengi hapa Canada nimekutana na Wazanzibari kibao na Wasomali kibao nao wamevushwa kutokea Mexico mpaka Canada

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku nakanyaga Marekani, aisee watanirudisha bongo labda nikiwa nime-dead..!

Niache kuonana na akina toni braxton,akina jhene aiko..nirudi bongo kufanya nini!
Sasa unamtangazia nani....au unatafuta huruma ya mtoa mada....
 
Habari za humu wa wadau wa JF,

Nichukue nafasi hii kumshukuru mwenyezi mungu kwa neema na baraka nyingi ambazo ametupa na kikubwa zaidi ni afya njema na maarifa mazuri aliyoturuzuku. Lakini pia nitakuwa mchoyo wa fadhila iwapo sitawashukuru Great thinkers wote wa JF ambao walitoa mawazo yao juu ya Mpango wangu wa kuzamia Nchini Marekani mara baada ya kupata Visa ya nchi hiyo.

Nafahamu wapo watu ambao walitamani sana kujua nini kilichojiri baada ya mimi kufika USA na kilichoendelea baada ya kuzamia huku Ughaibuni. Niwakumbushe tu kidogo kuwa nilisafiri tarehe 15 August mwaka huu 2019 kwaajili ya kuhudhuria mkutano ambao ulifanyika na nilihudhuria Nchini Marekani katika mji wa Washington DC ambapo ilinichukua siku 3 kukamilisha kile nilichotumwa na ofisi yangu kukikamilisha.

Nakumbuka watu wengi wa JF walinipa ushauri baada ya kumaliza mkutano nirudi Bongo kwa sababu sina pa kuanzia Marekani ila kwangu mimi hiyo haikuwa sababu ya kunizuia nisizamie Marekani.Kiukweli Marekani ni kuzuri mno japokuwa sijawahi kwenda nchi yeyote hiyo ndio Mara yangu ya kwanza tangu nizaliwe ila sidhani kama kuna nchi nzuri kuliko Marekani hapa duniani,Ni kuzuri nashindwa hata kuelezea kwa kweli.

Mara baada ya kutuma ile Post hapa jukwaani kuna jamaa alinitafuta Private kabla ya kuruka akanipa mchongo akaniambia hapo Marekani hapafai akasema atanipa njia niende Canada ila nikifika nijiripue kama mkimbizi wa Kisomali ndivyo Wazanzibari wengi hufanya hivyo na alinitumia Makaratasi ya Somalia niyasome ili niijue vizuri Somalia kuna maeneo Somalia wanaongea kiswahili.

Nilipomtumia picha yangu akasema nafanana sana na Msomali hivyo nikifika Marekani nimtafute ataniunganisha na mtu nitakayemlipa anivushe upande wa pili yaani Nchini CANADA. Kwa kweli nilikuwa naogopa sana na niliogopa isije ikawa anataka kunipoteza ila nilikuwa na moyo wa ujasiri na nilishachunguza kuwa watu wengi wanatoka Marekani na kuingia Canada kupitia Illegal borders.hivyo nilijipa moyo na kusema ntaweza.

Hivyo nilipomaliza mkutano nikawasiliana na jamaa mvushaji akasema niende New York atakuja kunipokea Airport,kwasababu nilikuwa na Pocket money ya kutosha nilijiamini sana.Baada ya kufika akanipeleka hoteli fulani akasema atakuja kesho asubuhi, Ilipofika majira ya saa 4 asubuhi akafika akiwa yeye na mwenzake ambae alikuwa ni Mmexico na huyo alienipokea alikuwa ni Mzanzibari.

Kwa hiyo tukapanda bus mpaka sehemu ambapo tulishuka na tukachukua Taxi tukawa tunaenda nikaona msitu tu nilipouliza akaniambia kuwa huku sasa ndio tunaelekea CANADA nikashangaa sana tuliposimama sehemu tukashuka na kukutana na watu watano na wale wawili wakawa saba wakaniambia niwape hela tuliyokubaliana yaani Dollar 3000 ikabidi niwape then tukaendelea na safari nikiwa nahofia kuwa nisije nikawa naenda kuchinjwa na kutolewa viungo vya mwili wangu maana hakuna ninaemjua pale na hata huyo Connector wangu nilikuwa simjui ila ilikuwa balaa la hofu limetanda naona sifiki.

Hatimaye nilifika sehemu nikaoneshwa bendera ya Canada na kuambiwa nenda pale na waeleze kuwa wewe ni mkimbizi kutoka Somalia utasaidiwa.Nikaenda na nikavuka mpaka nilipofika nikapigwa pingu palepale kwa kosa la kuvuka kinyume na utaratibu.

Itaendelea...

Nitawaeleza siku nyingine baada ya Pale ila kwasasa nipo Canada.

Sent using Jamii Forums mobile app
Fuucckkk... Thread.. No supporting docs..
Atleat some pics..the adventurous..strange scenes..

Fk
 
Kwani hata kupiga picha hilo wingu la nje shng ngapi!?!??

Just snap that Ass hole fucker Sky
 
Karibu Canada...
Screenshot_20191228-033308.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha hope zisizo na mashiko...angetoboa wapi?

Wangapi wanapata hizo milioni 6 halafu hawatoboi.
Nimempenda huyo jamaa..waeza kua hata na 20m bongo..ukashindwa izalisha na ikaisha.. sababu kubwa ni kukosa exposure..
Nimempenda sana jamaa aliejilipua, naezasema ame-take maximum risk... big up mzee. Kwa wale risk takers tunamuelewa.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimempenda huyo jamaa..waeza kua hata na 20m bongo..ukashindwa izalisha na ikaisha.. sababu kubwa ni kukosa exposure..
Nimempenda sana jamaa aliejilipua, naezasema ame-take maximum risk... big up mzee. Kwa wale risk takers tunamuelewa.


Sent using Jamii Forums mobile app
Lililopo ni kwamba hakuna guarantee ya moja kwa moja kama angebaki akaizungusha hiyo pesa angefanikiwa.

Na pia sio kwamba mbele nako kurahisi kivileee. Ila mimi mtu akiniambia bongo maisha ya utafutaji marahisi kuliko Canada nitabisha maana tumezaliwa Bongo tunaijua vizuri...
 
Lililopo ni kwamba hakuna guarantee ya moja kwa moja kama angebaki akaizungusha hiyo pesa angefanikiwa.

Na pia sio kwamba mbele nako kurahisi kivileee. Ila mimi mtu akiniambia bongo maisha ya utafutaji marahisi kuliko Canada nitabisha maana tumezaliwa Bongo tunaijua vizuri...
Ni kweli mkuu, yawezakua hakuna guarantee, muhimu hapo ni exposure kaka... tunahitaji sana hii kitu ili tufanye maajabu kwetu na jamii kwa ujumla. Jamaa amechagua njia hiyo kupata exposure..
Amini kitu kimoja mtembea bure sio sawa na mkaa bure..
Ukiniuliza mimi nitakuambia Hapa bongo kuna fursa nyingi sana kuliko Canada .. Ndio zipo..! ila huezi kuziona kama umekaa tu sehemu moja..hata humuhumu ndani ya bongo hutembei!!
Muhimu ni kutoka , pata exposure then rudi home wekeza nina uhakika ukiwa na shauku ya kufanikiwa..lazima kieleweke.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh Boss
watu wengi huwa wanatoka huko Canada kwenda USA kutafuta maisha
ILA
wewe umetoka USA Kwenda Canada kutafuta maisha?

watu Kama:
Drake Graham -Rapper
Celine Dion
Marley Brinx
Sunny Leone
Justin Bieber
Jim Carrey
Keanu Reeves
Shania Twain

Yaani wapo wengi mno waliotoka Canada
na USA ndipo wametoboa!
KILA LA KHERI RAFIKI
na
Next year mwezi wa April nakuja USA
Maryland (MD) panapo majariwa tukutane huko!
Unachosema ni kweli kabisa ila wabongo ni watu wa fuata upepo,USA in cheap kuishi kuliko Canada kodi kibao
 
We jamaa mbona una kimbelembele sana,una-quote kila mtu angalia usiwe ka demu,posti nyingine unazipotezea tu
Acha jazba za kindezi....unafikir marekani ina huruma na watu ka nyie....wenzio wanatafuta njia waingie Canada kutoka US....hujiulizi..
 
Acha jazba za kindezi....unafikir marekani ina huruma na watu ka nyie....wenzio wanatafuta njia waingie Canada kutoka US....hujiulizi..
Kila mtu na mtazamo wake wengine wanatoka canada wanaingia Marekani,hujiulizi!

Eti marekani ina huruma,we inaonekana ni muoga sana,watu wanaingia Marekani kila leo
 
Back
Top Bottom