Kinacho wafelisha Ughaibuni Part 2

Kinacho wafelisha Ughaibuni Part 2

nzalendo

Platinum Member
Joined
May 26, 2009
Posts
12,884
Reaction score
14,578
Sehemu hii ya pili pia ni mfano hai,
Angalizo
Haya maandiko ni sehemu ya kupata Elimu kwa wanao,walio na watakao.

Katika sehemu ya kwanza tuliona mfano mmoja lakini takwimu zaonyesha ni maelfu ya watu hukumbwa na mikasa inayofanana na mfano ule.

Kimsingi si waTanzania pekee,bali ni Afrika kwa ujumla kwani maisha yetu, hulka zetu na mifumo yetu inafanana,

Yaliyomkuta yule MTZ katika part 1 pia yamewakuta wa West Afrika,Wa Kenya wa Congo (ambao wengi wapo magharibi ya mbali kama wakimbizi).

Katika sehemu hii ya pili ni mtu na familia yake wametoka Tanzania kwa Green Card baba ni msomi na mama ni msomi na watoto watatu bado wapo shule za msingi,

Wakafika magharibi ya mbali kwa mbwembwe na bashasha na shamra shamra na hoi hoi na vifijo.

Wanadamu ni viumbe hatari sana wakawapokea wageni sherehe siku hadi siku lakini hawawafahamishi hawa wenyeji kwamba nchi hii ya magharibi ya mbali ipo chini ya mifumo ya kishetani.

Basi ikawa usiku ikawa mchana wasomi wakapata kazi za maana, mama ana kazi baba ana kazi,,,,ghafla wakajikuta wapo katika madeni,,,kumbe magharibi ya mbali kuna tu mitego ambapo kuitambua labda umpate muungwana mwenye hofu ya Mungu akustue au Roho wa Mungu akupe akili ya utambuzi,

Baba kachukua mkopo wa gari..bonge la gari...kapiga picha gari karusha kwenye mitandao kapata likes na comments za kutosha,,,mama nae akakopa boooonge la gari nae akapost.

Halafu wakakopa boonge la jumba,,,jumba ,,,jumba kwelie kweli,,,nalo wakapost,,wenye husda wakaliona nk nk

Kukopa harusi kulipa matanga.

Huku bongo maswali yanazidi kukosa majibu...wenzetu tunawaona mitandaoni maisha mazuri...lakini mbona hata kirisimasi hawaji????

Halafu mbona hata nyumba ya baba yao wanashindwa angalau kupaka rangi???
KUMBE
Kiuhalisia watu wanapiga shift usiku na mchana kulipa bills. mogeji na madeni kibaao.

>>>bado stori zitaendelea>>>>>>>
 
Hii itahusu wale waosha mavi...au wachambaji...katika vijumba vya kutunza wazee...na wengi wamekuja nchi za magharibi ya mbali wakiwa na familia nyumbani Afriquer
 
Back
Top Bottom