Ukweli kuhusu maisha ya ughaibuni

Ukweli kuhusu maisha ya ughaibuni

Habari za humu wa wadau wa JF,

Nichukue nafasi hii kumshukuru mwenyezi mungu kwa neema na baraka nyingi ambazo ametupa na kikubwa zaidi ni afya njema na maarifa mazuri aliyoturuzuku. Lakini pia nitakuwa mchoyo wa fadhila iwapo sitawashukuru Great thinkers wote wa JF ambao walitoa mawazo yao juu ya Mpango wangu wa kuzamia Nchini Marekani mara baada ya kupata Visa ya nchi hiyo.

Nafahamu wapo watu ambao walitamani sana kujua nini kilichojiri baada ya mimi kufika USA na kilichoendelea baada ya kuzamia huku Ughaibuni. Niwakumbushe tu kidogo kuwa nilisafiri tarehe 15 August mwaka huu 2019 kwaajili ya kuhudhuria mkutano ambao ulifanyika na nilihudhuria Nchini Marekani katika mji wa Washington DC ambapo ilinichukua siku 3 kukamilisha kile nilichotumwa na ofisi yangu kukikamilisha.

Nakumbuka watu wengi wa JF walinipa ushauri baada ya kumaliza mkutano nirudi Bongo kwa sababu sina pa kuanzia Marekani ila kwangu mimi hiyo haikuwa sababu ya kunizuia nisizamie Marekani.Kiukweli Marekani ni kuzuri mno japokuwa sijawahi kwenda nchi yeyote hiyo ndio Mara yangu ya kwanza tangu nizaliwe ila sidhani kama kuna nchi nzuri kuliko Marekani hapa duniani,Ni kuzuri nashindwa hata kuelezea kwa kweli.

Mara baada ya kutuma ile Post hapa jukwaani kuna jamaa alinitafuta Private kabla ya kuruka akanipa mchongo akaniambia hapo Marekani hapafai akasema atanipa njia niende Canada ila nikifika nijiripue kama mkimbizi wa Kisomali ndivyo Wazanzibari wengi hufanya hivyo na alinitumia Makaratasi ya Somalia niyasome ili niijue vizuri Somalia kuna maeneo Somalia wanaongea kiswahili.

Nilipomtumia picha yangu akasema nafanana sana na Msomali hivyo nikifika Marekani nimtafute ataniunganisha na mtu nitakayemlipa anivushe upande wa pili yaani Nchini CANADA. Kwa kweli nilikuwa naogopa sana na niliogopa isije ikawa anataka kunipoteza ila nilikuwa na moyo wa ujasiri na nilishachunguza kuwa watu wengi wanatoka Marekani na kuingia Canada kupitia Illegal borders.hivyo nilijipa moyo na kusema ntaweza.

Hivyo nilipomaliza mkutano nikawasiliana na jamaa mvushaji akasema niende New York atakuja kunipokea Airport,kwasababu nilikuwa na Pocket money ya kutosha nilijiamini sana.Baada ya kufika akanipeleka hoteli fulani akasema atakuja kesho asubuhi, Ilipofika majira ya saa 4 asubuhi akafika akiwa yeye na mwenzake ambae alikuwa ni Mmexico na huyo alienipokea alikuwa ni Mzanzibari.

Kwa hiyo tukapanda bus mpaka sehemu ambapo tulishuka na tukachukua Taxi tukawa tunaenda nikaona msitu tu nilipouliza akaniambia kuwa huku sasa ndio tunaelekea CANADA nikashangaa sana tuliposimama sehemu tukashuka na kukutana na watu watano na wale wawili wakawa saba wakaniambia niwape hela tuliyokubaliana yaani Dollar 3000 ikabidi niwape then tukaendelea na safari nikiwa nahofia kuwa nisije nikawa naenda kuchinjwa na kutolewa viungo vya mwili wangu maana hakuna ninaemjua pale na hata huyo Connector wangu nilikuwa simjui ila ilikuwa balaa la hofu limetanda naona sifiki.

Hatimaye nilifika sehemu nikaoneshwa bendera ya Canada na kuambiwa nenda pale na waeleze kuwa wewe ni mkimbizi kutoka Somalia utasaidiwa.Nikaenda na nikavuka mpaka nilipofika nikapigwa pingu palepale kwa kosa la kuvuka kinyume na utaratibu.

Itaendelea...

Nitawaeleza siku nyingine baada ya Pale ila kwasasa nipo Canada.

Sent using Jamii Forums mobile app
inabana
 
Back
Top Bottom