Ukweli kuhusu Mabilioni ya NIDA: Kulinganisha NEC na NIDA Kimantiki

Ukweli kuhusu Mabilioni ya NIDA: Kulinganisha NEC na NIDA Kimantiki

Uzuri wa Rais wetu akikurupuka huwa anajirudi fasta na kimya kimya. Hapa tunaongea Dr Feisal Issa alikuwa RAS Mwanza tayari yuko ofisini pale Tamisemi Dodoma anachapa kazi. John Wanga, mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela Mwanza aliyesimamishwa kwa mbwembwe naye amerudishwa kinyemela...
Heche Suguta wa NEMC naye amerudishwa kimya kimya!
 
Mkuu umetoa mchanganuo vizuri, sisi wengine tunasubiri uchunguzi umalizike tujue mbivu na mbichi, lakini tukae tukijua hakuna mchunguzi anayeweza kuwa na Guts za kum-prove Rais wrong, lazima jamaa watapatikana na hatia somewhere, haiwezekani wawe wasafi kwa 100% hata katika mchakato wa procument mahala ambapo tulio wengi ndipo tunapatia viada vya shule za watoto.

Nashauri na NEC pia wachunguzwe kwa matumizi yao yote ikiwemo uchapishaji wa vitambulisho vya mpiga kura.
Kwa uwezo mdogo nilio nao isije ikawa wao ndio wamewachonhea NIDA ili kuficha ubadhirifu wao uliokidhiri.
 
mtoa Mada naona umesahau kutuambia utajiri usiosemekana aliokuwa maimu, amehamisha watu mikocheni, amejenga mahekalu yasiyosemekana na ameanzisha na band, pili ilifika hatua NIDA wakashindwa mpaka kununua mafuta ya magari halafu , anayepinga hatua aliyoichukua magufuli dhidi ya maimu huyo haitakii mema nchi hii. fatilieni utajiribwa huyo jamaa
 
Exactly! Hii ndiyo point hebu mletamada kabla ya yoooooote tolea ufafanuzi wa haya. Hivi Tanzania imekuwaje kutetea WIZI mchana kweupe hebu achana kwanza na ooh technologia ooh what hebu fafanua kwanza haya. Je Ufisadi ulifanyika au haukufanmyika kwanini mjustify Ufuisadi???? This is not acceptabl;e. Tunajua mko wengi na mna nguvu ya pesa lakini wazalendo pia wapo na kwa sasa ndio wenye nguvu. Go Mh. Magufuli go tuko pamoja nawe!!!
Ukiwa mzalendo huku ukitegemea habari za upande mmoja tu badala ya kupokea zote na kuzichambua na kuchanganya na zako (kusoma na kutafiti), haina faida yoyote, sana sana utaendelea kuyumbishwa na huyo unayemtegemea kwani chochote atakachosema utafuata
 
Nimesoma Magazeti mbali mbali na kumsikiliza mhe.Rais, baadhi ya mitandao ya kijamii na utafiti wangu mwenyewe , ki mantiki NEC na NIDA ni mbingu na Ardhi.

Wakati NIDA ni taasisi mpya na zoezi linalofanyika halijawahi kufanyika nchini kwetu kwa maana ya kumtambua mtanzania, mazoezi mengine yalikuwa ni ya usajili tu kama NEC wanavo fanya.

Madhumuni ya NIDA ni kumtambua nani Raia, nani Mgeni mkaazi na nani mkimbizi. Hili zoezi sio rahisi maana nchi yetu inapakana na nchi nyingi na kuwatofautisha watu wake sio rahisi.

Zoezi la NEC ni la kisiasa wakati mfumo wa NIDA una manufaa kiuchumi, kijamii na kiusalama ndo maana kazi yao inafanywa kwa umakini sana kwa kuhusisha vyombo vingine Kama RITA, Uhamiaji, Tamisemi na vyombo vingine vya ulinzi.

NIDA vs NEC.

1. Card ya NEC ni ya plastic na ina expire in 3 yrs kulingana na material iliyo tumika wakati ya NIDA ni smart card na life span yake ni miaka 10. Hivo ununuzi wa card za NIDA utakuwa ni wa juu kuliko wa card za NEC.

2. Kwa kuwa card za NIDA ni smart Card, hata printers zake ni specialized ili kuweza kuingiza data kwenye chip (watu wa IT watanielewa) wakati NEC ni printer za kawaida unazo weza print popote. Hivo ununuzi wa printa za NIDA utakuwa ghali.

3. Teknolojia ya NIDA ni ya kisasa na
ndo inayo tumika kwa sasa ulimwenguni na ni takwa la E. Africa comunity.

4. Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania la leo tarehe 08.02.2016, ukurasa wa 4 , mwandishi amegawanya pesa za usajili za NEC (70b) kwa idadi ya vitambulisho (23m) na kupata kila
kimoja ni sh. 3,010 na kwa NIDA kachukua 179.6b kagawa kwa vitambulisho 2m. Kimsingi 70b ya NEC ni ya usajili tu bila kuweka gharama za BVR. Kama sikosei wakati wa zoezi la usajili wa NEC magazeti yaliwahi kureport gharama ya BVR moja kuwa ni kama $ 6,800 na walinunua BVR 8,000 hivo basi NEC walitumia kama $54,400,000 sawa na karibu 120b bila gharama za usafiri (logistics), karatasi nk hivo si kweli NEC walitumia 70b tu. Wakati gharama za NIDA sh179.6b ni pamoja na gharama za kujenga mfumo wa kielectronic, kumlipa mkandarasi, kununua mashine za usajili na consultant aliye andikwa gazeti la Mtanzania la leo, magari, ofisi zao kila wilaya, na jukumu kubwa la utambuzi linalohusisha vyombo mbalimbali ambalo NEC hawalifanyi (nilivo vitaja hapo juu) na kama mnavyojua uanzishwajiwa ofisi ni pamoja na ununuzi wa samani etc.

5. Wakati NEC hizi pesa walipewa ndani ya mwaka mmoja, na kwa sababu ya uchaguzi NEC walikuwa na cut off time, NIDA pesa hizi
wamepewa tangu mradi uanze mwaka 2011.

6. Kama expiration ya card za NEC ni 3 yrs na NIDA ni 10 yrs hivo cost of investment ya NEC ni mara 3 ya NIDA.

7. Kuhusu sahihi (signature) kuto kuwa kwenye kitambulisho ni suala la kiteknolojia na kiusalama zaidi.Vitambulisho vingi vya kisasa na hata vya nchi nyingi tu havina signature on the face ya kitambulisho maana data zimo ndani ya kitambulisho na zinasomeka kielectronic. Vitambulisho vya Nigeria, Malaysia, Philippines etc havina signature . Data za mhusika husomwa na kitu kinaitwa Card reader. Ni kwa sababu za kiusalama tu maana signature inaweza kugushiwa lakini finger prints haziwezi. Nimeona kwenye magazeti mengi NIDA wamepata award (tuzo) mbili za kimataifa kuhusiana na teknolojia yao lakini hapa kwetu hatuvithamini, mi naona kuna shida.

Mpaka sasa hivi, kwa utafiti wangu, toka 2011 NIDA ilipo anza, NIDA imepata 20% ya pesa zilizo idhinishwa na bunge kwa miaka yote hiyo na sababu hii ya ukata ndo maana zoezi linasuasua na hawajaweza malizia usajili na wameshindwa toa elimu kwa Umma sababu ya Ukata.

Sio nia yangu kutetea ufisadi na ndo maana najiita "Tanzania Njema Yaja". Naiona Tanzania ikielekea kwenye nuru lakini hatutafika kilele cha uzuri huo kama ukweli hautaelezwa... ni vema Watanzania wakauelewa ukweli kabla ya kuhukumu. Mh. Raisi alisema, "msema kweli ni mpenzi wa Mungu" nami naona nimetimiza usemi huo. Na ninaamini baada ya uchunguzi ambao mh. Raisi ameelekeza ufanyike, ukweli utafahamika na haki itatendeka.

Long live Tanzania. Ukweli utatuweka huru.......
This is cheating..... Utafiti umeuanza lini? Umetumia methodology gani? Kama na we ni mojawapo wa jipu kweny hil suala la nida ni vema a utulie usizid kuongeza utetez wako upeleke huko kwenye tume iliyoundwa huku upotoshaj unaotuletea huku hautakusaidia chochote
 
mtoa Mada naona umesahau kutuambia utajiri usiosemekana aliokuwa maimu, amehamisha watu mikocheni, amejenga mahekalu yasiyosemekana na ameanzisha na band, pili ilifika hatua NIDA wakashindwa mpaka kununua mafuta ya magari halafu , anayepinga hatua aliyoichukua magufuli dhidi ya maimu huyo haitakii mema nchi hii. fatilieni utajiribwa huyo jamaa
Mkuu mi nimeongelea nnacho kijua.. . Suala la Maimu na mali zake silijui... ila kuanzisha band ni ghali sana kwel? Je umefika kule uchochoroni watu wanako kupublish ni mtaa mzima? Nasema tena ..... jambo usilo lijua ni siku wa giza..... ukisikia nyuma ya shoperz plaza watu wanahamaki lakini kuna uswahilini kule na yeye ndo aliko wekeza .... tuwaachie wachunguzi hili, ila narudia.... usihukumu mtu kwa kusikia maneno ya mtaani tu..... ningefurahi kama hata ungeweka picha hapa au kuja na tathimini....
 
mkuu mi nimefanya utafiti na kuja na data... kama una data tofauti na hizi basi zieleze..... hatutafanikiwa kama tutawakatisha tamaa watendaji wanao pigana kufanikisha jambo eti kwa sababu umesikia 179 bi zilizo tolewa kwa zaidi ya miaka 5... ulizia nchi jirani kenya na Uganda kwenye mchakato wao wameisha tumia sh ngapi....
mtoa mada unafikiri serikali ni wajinga kimsimisha jamaa, unafikiri hawakufanyabutafiti juu ya maimu? huyu jamaa anastahili adhabu kubwa sana ni fisadi anapaswa ashughulikiwe vizuri, dada yangu alifanya kazi nida alinisimulia adha wanazopata huku wamerundikiwa fedha lukuki, lakini tukumbuke kuwa state organ zimefanya kazi yao.
 
Tatizo la NIDA ni financing period...... mengine kwa mtizamo wangu ni majungu...
 
Huyo sijui Tanzania njema nae yupo huko huko NIDA anahusika directly or indirectly kwa hio kakimbilia JF kupata mawazo ya GT but all in all NIDA mmefanya ufisadi na dawa yenu iko jikoni ingekua China ilikua ni kitanzi tuu hamna mjadala..pesa ilotumika haiendani na idadi ya watu..msiwafanye watz wajinga.Na kwa taarifa yako mm siko bongo lakini huo wizi na then mnakuja na mahesabu kuhalalisha nilshaufanya sana Enzi hizo za mzee Rukhsa..Kwahio wewe na Mwaimu na genge lenu la wezi la wezi Tingatinga liwatoe mavi, huyo ni ngosha chapa ng'ombe haogopi kitu, kunyea debe kunawahusu sana mkipenya hapo ni mwisho wa dunia..fyuuuuu.
 
Ha haaa haaaa....

We huna hoja..... kakojoe ulale.... unaleta mambo ya mzee ruksa hapa .... ndo data hizo? Utakuwa umabeba maboksi ya nanii wewe hk uliko....
 
Exactly! Hii ndiyo point hebu mletamada kabla ya yoooooote tolea ufafanuzi wa haya. Hivi Tanzania imekuwaje kutetea WIZI mchana kweupe hebu achana kwanza na ooh technologia ooh what hebu fafanua kwanza haya. Je Ufisadi ulifanyika au haukufanmyika kwanini mjustify Ufuisadi???? This is not acceptabl;e. Tunajua mko wengi na mna nguvu ya pesa lakini wazalendo pia wapo na kwa sasa ndio wenye nguvu. Go Mh. Magufuli go tuko pamoja nawe!!!
Umeisoma yote hiyo mada!
 
Mkuu mi nimeongelea nnacho kijua.. . Suala la Maimu na mali zake silijui... ila kuanzisha band ni ghali sana kwel? Je umefika kule uchochoroni watu wanako kupublish ni mtaa mzima? Nasema tena ..... jambo usilo lijua ni siku wa giza..... ukisikia nyuma ya shoperz plaza watu wanahamaki lakini kuna uswahilini kule na yeye ndo aliko wekeza .... tuwaachie wachunguzi hili, ila narudia.... usihukumu mtu kwa kusikia maneno ya mtaani tu..... ningefurahi kama hata ungeweka picha hapa au kuja na tathimini....

Mkuu, pamoja na kushindwa kwako kujibu maswali yangu mawili ya msingi huko juu,naamini kabisa hatua ya kumsimaisha mtu kazi kama kuna ubadhilifu ni hatua sahihi kabisa.

Kwa watu kama mimi ambae nimeishi kwenye nchi zilizoendelea na zinazofuata na kuheshimu utawala wa sheria, nachukulia kwamba hzii ni jitihada sahihi za serikali katika kuweka uwajibikaji wa watendaji wake na wale wa idara zake.

Hivyo anachojaribu mheshimiwa raisi ni kutukumbusha sote mimi na wewe kwamba kuna utawala unaofuata sheria na kwa bahati mbaya kuna watu hawakuwa wameuzoea kwa miaka zaidi ya 30 sasa.

Hakuna mtu alietarajia Seph Blatter na Michael Platini na wenzao kama wangekuja kugundulika wanafanya vitendo vya rushwa, UFISADI na ubadhilifu ndani ya FIFA. Hio ni kwa sababu wamesahau kwamba wanatumia pia mfumo wa baadhi ya mabenki ambao uko controlled na American Federal Resevrve hivyo huwezi kuacha alama za vidole na miguu halafu vikafutika.

Hakuna nchi ambayo ipo asilimia 100 mambo yake safi, kwani hata Ulaya na Marekani nilikoishi kuna wauza unga wakubwa tu, wakwepa kodi (inaitwa cash in hand), na juzi tu Google imegundulika ilikuwa inakwepa kulipa kodi nchini Uingereza kwa miaka zaidi ya 10 mengine tu.

Pia nchini Marekani waligundua kwamba magari ya VW yale yanayotumia Diesel walikuwa waliweka chombo cha kudanganya kuhusu kiasi cha moshi unaotokana na matumizi ya mafuta ya Diesel.

Hivyo magari mengi yalikuwa na kasoro ya kutoa kiasi kikubwa cha moshi lakini waliweka chombo hicho na kudanganya matokeo ya emission test.

Kilichofuata kilikuwa ni bosi wa VW alieko Ujerumani kujiuzuru mwenyewe na baadhi ya wahandisi walio chini yake kupisha uchunguzi. Baadae mkurugenzi wa mashitaka akasema kulikuwa na makosa ya jinai na huo ni uhalifu.

Sasa unafahamu hasara ambayo VW imekula kwa kurudisha magari yote ya Diesel duniani yachunguzwe emission yake?

Kuna mifano mingi tu lakini hio ni michache hivyo si tatizo letu peke yetu kama nchi.

Hivyo imegundulika fedha kiasi cha bilioni 180 zimetumiwa kwa njia ambazo haieleweki na unafanyika uchunguzi, ila uchunguzi hauwezi kufanywa mpaka kwanza wahusika wasimamishwe kazi,huo ndio utaratibu.
 
Siwezi kutoa ufafanuzi wa matumizi ya Bilion 179
Naomba na mimi niseme ninavyofahamu
Vitambulisho vya Nida ni smart card na kuna taarifa za mwombaji ndani yake zote.
Niliwahi kuuliza why ina expire date wakanijibu kuwa si kitambulisho kina expire bali ni taarifa za mhusika zinabadilika kulingana na wakati mfano marital status,Age,Economic,Employment,Resident and permanent resident n.k hivyo hiyo expire date within 10yrs mtu anatakiwa aende ofisi ya Nida iliyo Karibu akaupdate taarifa zake
Kwa kweli content ya NIDA kitambulisho imeshiba.,Tatizo imeingiliwa na Siasa!
 
Mtoa mada kaleta data,wapinga mada wanaleta maneno halafu wanataka washinde.wengine eti ooh serikali sio wajinga,kwani maamuzi mangapi ya ajabu yamefanyika,iliyolazimisha mchakato wa katiba sio serikali?waelezeni watumie busara za kupata majibu kabla ya kuita makamera
 
Tanzania njema , kitanzi kinakuja hiko jiandae mbwaa wewe mlifikiri mtaiba milele na wenye nchi wanyamaze tu. Kiama chaja uchunguzi ushafanyika na mahakamani hamtoki nyie nyambaaf zenu wezi wakubwa eti shoppers plaza uswahilini unajua bei za nyumba mitaa hio wewe?? huyo bwana yako kwa mshahara gani kaweza kununua hapo???Eti kuanzisha band rahisi???kawadanganye watoto wadogo wewe hapa JF the home of GT!!! fyuuuu.
 
Mkuu, pamoja na kushindwa kwako kujibu maswali yangu mawili ya msingi huko juu,naamini kabisa hatua ya kumsimaisha mtu kazi kama kuna ubadhilifu ni hatua sahihi kabisa.

Kwa watu kama mimi ambae nimeishi kwenye nchi zilizoendelea na zinazofuata na kuheshimu utawala wa sheria, nachukulia kwamba hzii ni jitihada sahihi za serikali katika kuweka uwajibikaji wa watendaji wake na wale wa idara zake.

Hivyo anachojaribu mheshimiwa raisi ni kutukumbusha sote mimi na wewe kwamba kuna utawala unaofuata sheria na kwa bahati mbaya kuna watu hawakuwa wameuzoea kwa miaka zaidi ya 30 sasa.

Hakuna mtu alietarajia Seph Blatter na Michael Platini na wenzao kama wangekuja kugundulika wanafanya vitendo vya rushwa, UFISADI na ubadhilifu ndani ya FIFA. Hio ni kwa sababu wamesahau kwamba wanatumia mfumo wa benki ambao uko controlled na American Federal Resevrve hivyo huwezi kuacha alama za vidole na miguu halafu vikafutika.

Hakuna nchi ambayo ipo asilimia 100 mambo yake safi, kwani hata Ulaya na Marekani nilikoishi kuna wauza unga wakubwa tu, wakwepa kodi (inaitwa cash in hand), na juzi tu Google imegundulika ilikuwa inakwepa kulipa kodi nchini Uingereza kwa miaka zaidi ya 10 mengine tu.

Pia nchini Marekani waligundua kwamba magari ya VW yale yanayotumia Diesel walikuwa waliweka chombo cha kudanganya kuhusu kiasi cha moshi unaotokana na matumizi ya mafuta ya Diesel.

Hivyo magari mengi yalikuwa na kasoro ya kutoa kiasi kikubwa cha moshi lakini waliweka chombo hicho na kudanganya matokeo ya emission test.

Kilichofuata kilikuwa ni bosi wa VW alieko Ujerumani kujiuzuru mwenyewe na baadhi ya wahandisi walio chini yake kupisha uchunguzi. Baadae mkurugenzi wa mashitaka akasema kulikuwa na makosa ya jinai na huo ni uhalifu.

Kuna mifano mingi tu lakini hio ni michache hivyo si tatizo letu peke yetu kama nchi.

Hivyo imegundulika fedha kiasi cha bilioni 180 zimetumiwa kwa njia ambazo haieleweki na unafanyika uchunguzi, ila uchunguzi hauwezi kufanywa mpaka kwanza wahusika wasimamishwe kazi,huo ndio utaratibu.
Bandiko lako la sasa limejaa hekima mkuu.... ya mwanzo kwa kweli niliyadharau na kuyaacha makusudi maana niliona yamejaa mihenuko.... kwa hili nakubaliana na wewe vizuri tu na hata uzi wangu uko kwenye mwelekeo huo.... hapa nilitaka kuweka ukweli nnao ujua mkuu na nikitaka tunapo linganisha NEC na NIDA tuwalinganishe kwenye mizania sawa.... yaani an aple to an aple.... ahsante.
 
Rais anasema havina sahihi!mkuu tuweke sawa hapo
Nnavo elewa mimi... sahihi ipo kwenye system na inasomwa kwa card reader na ni kwa sababu za kiusalama tu.... nilieleza kidogo kwenye main thread.....

Kumtambua mtu biometrically yaani kwa alama ya kidole ni salama na uhakika zaidi kuliko utambuzi wa sahihi/ signature ambayo mtu anaweza kuikana au kuigushi....
 
Bandiko lako la sasa limejaa hekima mkuu.... ya mwanzo kwa kweli niliyadharau na kuyaacha makusudi maana niliona yamejaa mihenuko.... kwa hili nakubaliana na wewe vizuri tu na hata uzi wangu uko kwenye mwelekeo huo.... hapa nilitaka kuweka ukweli nnao ujua mkuu na nikitaka tunapo linganisha NEC na NIDA tuwalinganishe kwenye mizania sawa.... yaani an aple to an aple.... ahsante.

Ukumbuke wakati mwingine unapoleta mada sensitive kama hii nawe unatakiwa uwe umejiandaa maana hapa tupo watu wa kila aina.

Mimi hujaribu kuwa very diplomat katika majadiliano lakini nipo firm na fair katika hoja zangu.
 
Lazima utakuwa gasho si bure..... maana sioni mantiki ya matusi hapa.... naweza kukutukana tu hata wewe mbeba maboksi.....

Back
Top Bottom