Ukweli kuhusu kifo cha mfanyakazi mgodi wa Barrick North Mara

Jamal Akbar

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
413
471
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya, Geofrey Sarakikya, amesema mfanyakazi wa mgodi wa Barrick North Mara Emmanuel Chacha, aliyefariki dunia Machi 11, mwaka huu hakupigwa risasi.

Aliyasema hayomkoani Mara, wakati akitoa ufafanuzi kuhusu kifo cha Chacha, ambapo alisema alifariki dunia baada ya kujirusha katika shimo lenye urefu wa mita 20.

"Hiyo ni kwa mujibu wa maelezo ya watu waliokuwepo eneo la tukio na majibu ya matokeo ya uchunguzi wa mwili wa marehemu uliofanywa na daktari wa Hospitali ya Rufaa Bugando Mwanza, zimebainisha kifo chake kimetokana na majeraha yaliyotokana na kujirusha kwenye shimo lenye urefu wa mita 20,"alisema.

Kamanda Sarakikya alisema kabla ya kujirusha katika shimo hilo, kikosi kazi kilimkuta mfanyakazi huyo akiiba mawe yanayodhaniwa kuwa na dhahabu ndani ya mgodi huo.

Alisema kikosi kazi kilijumuisha ofisa madini wa mkoa, maofisa kutoka Jeshi la Polisi, kitengo cha ulinzi cha mgodi na kampuni ya ulinzi ya Nguvu Moja.

Aidha, Kamanda Sarakikya alisema taarifa zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii zikidai aliuawa kwa kupigwa risasi hazina ukweli.

"Kwa hali hiyo ni vyema ifahamike taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa kifo cha Emmanuel Chacha kilitokana na kupigwa risasi, siyo za kweli," alisema Kamanda Sarakikya

Kamanda Sarakikya alitoa ufafanuzi huo kutimiza ahadi aliyoitoa Machi 12, mwaka huu ambapo aliahidi angetoa taarifa kamili ya kifo hicho baada ya kupata majibu ya daktari kuhusu uchunguzi wa mwili wa marehemu.

Katika taarifa yake ya awali, alisema kifo hicho kilitokea Machi 11, mwaka huu katika eneo la Gokona ndani ya mgodi wa Barrick North Mara.
 
Kwan kama ameuwawa , au kujirusha.

Siuchunguzi ufanyike?.

Teknolojia yote hiiii ya Leo bado tunaishia Kwa maneno Maneno

Hata kama wamemzika, anafukuliwa, Uchunguzi unafanyika.


Easy !!.
 
Kwan kama ameuwawa , au kujirusha.

Siuchunguzi ufanyike?.

Teknolojia yote hiiii ya Leo bado tunaishia Kwa maneno Maneno

Hata kama wamemzika, anafukuliwa, Uchunguzi unafanyika.


Easy !!.
Kama aliuawa hata kwa risasi selasini wakiamua kuufunika ukweli hakuna uchunguzi hapo kwani dr, askari sijui na mahakama watakuwa na Lao moja?
 
Hapo tarime nliwahi shuhudia ndugu wakilia binti yao alipigwa na mumewe akafa vile tu upande wa mauaji walikuwa na pesa postmortem ilifanyika wakasema ilikuwa ectopic ila kiuhalisia hakuwa na mimba wala nini, Dr na maaskari walikula pesa haki ya mtu ikaishia hapo.....nliujua ukweli wa hayo na mimi nlikuwa na mishe yangu yule afande alikuwa na jalada la kesi yangu ndo alikuwa pia na jalada la hiyo kesi afu ni shost sasa alooh.....huyo kijana rumours zina ukweli sana
 
Kwa mujibu wa kamanda uchunguzi umefanyika Bugando Hospitali
Uchunguzi uliofanyika ,ulifanyika kama Forensic Autopsy Yaan polisi wenyewe ndio waliotaka Uchunguzi ufanyike Kwa mujibu wa SHERIA kwakua ni tukio la mauaji ?.....( Hiii shooo inasimamiwa na polisi mwanzo mwisho hivo ni rahisi mchezo mchafu kufanyia).

Au Hospital Autopsy? Ndugu wenyewe ndio walioomba ?.( Hapa angalau Ndugu wa marehem anakua na kauli).


Sema nn, Watanzania tunaumizwa na Ujinga wa kutokujua mambo mengi.
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Back
Top Bottom