Fursa Pesa
JF-Expert Member
- May 30, 2012
- 4,437
- 3,260
Ukiwa muongo,ugopa kusahau.Asante Mkuu Maalim Mohammed Said kwa bandiko hili kutoka gazeti hilo. Na mimi ni muumini wa haki bin haki, ila katika hili la nyumba kwanza ni kweli nyumba za TSA ziliuzwa kihalali na PSRC.
Kuna watu walio zinunua kihalali, wakalipa fedha na kupewa stakabadhi za malipo. Nyumba hizo ni zao kihalali na hawajanyang'anywa.
Waliokuwa wafanyakazi wa Mkonge, nao wakaomba kuuziwa nyumba na kuahidi kuzilipia kwa mafao yao, na kwa vile ni kweli walikuwa wanasubiri mafao yao, ikakubalika mafao yao yatumike kama bond, wakakabidhiwa nyumba na kuzimiliki kihalali kusubiria mafao wazilipie.
Kwa vile TSA imebinafsishwa, wafanyakazi hao 87 wakiongozwa na Salum Shamte wakaunda umoja wao wa wafanyakazi na kusajili kampuni ya MIM, kwa share capital ya mafao yao.
Hapa ndio mchezo ulipoanza kwa baadhi mafao yao tayari waliisha yatumia kama bond kununulia nyumba za TSA na nyumba wameisha kabidhiwa bado tuu kuzilipia, halafu wakaunda kampuni hiyo ya MIM na kutumia mafao hayo hayo ku subscribe as the share Capital ya hiyo kampuni yao.
Wafanyakazi hao kupitia mafao yao kwa pamoja waliweza subscribe 10% shares za Katani Ltd na kuzilipia hizo hisa za Katani Ltd kwa mafao yao yale yale ambayo ndio wameyatumia kulipia nyumba.
Hivyo mafao yamelipia nyumba na yakalipia hisa. Kwa vile hakuna figures za mafao yao yalikuwa kiasi gani, kama yalikuwa billions yanaweza kununu nyumba, yakanunua hisa na bado balance ikabaki wakapewa cash.
Kamati ilipochunguza ikakuta mafao yalilipia shares na stakabadhi za malipo zipo. Walipotafuta stakabadhi za malipo ya kulipia nyumba hazikuwepo!. Hivyo wameuziwa nyumba kihalali na kuzilipia kwa ahadi ya mafao, mafao yalipotoka, yakanunulia na kulipia hisa huku nyumba waliisha kabidhiwa!.
Kilichofanyika ni kuitisha kila aliyenunua nyumba kuonyesha stakabadhi, walio onyesha proof ya malipo, walibaki na nyumba zao, walionunua kwa ahadi bila kulipa chochote, walisainishwa surrender document na kuzirejesha hizo nyumba na zimerejeshwa serikalini.
Ila kwenye nyumba zilizoko kwenye mashamba kuna watu waliuziwa na kuzilipia kihalali na stakabadhi wanazo, ila wamelazimishwa kuzirejesha kwasababu nyumba hizo hazina hati, hawa wanapaswa wafidiwe kurejeshewa fedha zao. Mauziano yoyote ya jengo ni hati na sio jengo. Huwezi kuuziwa nyumba bila hati kama ambavyo huwezi kununua gari bila kadi.
P