Ukweli kuhusu kampuni ya Katani LTD

Huyo mke wa shamte nadhani aliwahi kuwa meneja masoko shirika la reli enzi zile,anyway huyo shamte nadhani hajaonewa kwa lolote hata yeye anafahamu hilo.
 
Asante Mkuu Maalim Mohammed Said kwa bandiko hili kutoka gazeti hilo. Na mimi ni muumini wa haki bin haki, ila katika hili la nyumba kwanza ni kweli nyumba za TSA ziliuzwa kihalali na PSRC.

Kuna watu walio zinunua kihalali, wakalipa fedha na kupewa stakabadhi za malipo. Nyumba hizo ni zao kihalali na hawajanyang'anywa.

Waliokuwa wafanyakazi wa Mkonge, nao wakaomba kuuziwa nyumba na kuahidi kuzilipia kwa mafao yao, na kwa vile ni kweli walikuwa wanasubiri mafao yao, ikakubalika mafao yao yatumike kama bond, wakakabidhiwa nyumba na kuzimiliki kihalali kusubiria mafao wazilipie.

Kwa vile TSA imebinafsishwa, wafanyakazi hao 87 wakiongozwa na Salum Shamte wakaunda umoja wao wa wafanyakazi na kusajili kampuni ya MIM, kwa share capital ya mafao yao.

Hapa ndio mchezo ulipoanza. Mafao yao tayari waliisha yatumia kama bond kununulia nyumba za TSA na nyumba wameisha kabidhiwa bado tuu kuzilipia, halafu wakaunda kampuni hiyo ya MIM na kutumia mafao hayo hayo ku subscribe as the share Capital ya hiyo kampuni yao.

Wafanyakazi hao kupitia mafao yao kwa pamoja waliweza subscribe 10% shares za Katani Ltd na kuzilipia hizo hisa za Katani Ltd kwa mafao yao yale yale ambayo ndio wameyatumia kulipia nyumba.

Hivyo mafao yamelipia nyumba na yakalipia hisa. Kwa vile hakuna figures za mafao yao yalikuwa kiasi gani, kama yalikuwa billions yanaweza kununu nyumba, yakanunua hisa na bado balance ikabaki wakapewa cash.

Kamati ilipochunguza ikakuta mafao yalilipia shares na stakabadhi za malipo zipo. Walipotafuta stakabadhi za malipo ya kulipia nyumba hazikuwepo!. Hivyo wameuziwa nyumba kihalali na kuzilipia kwa ahadi ya mafao, mafao yalipotoka, yakanunulia na kulipia hisa huku nyumba waliisha kabidhiwa!.

Kilichofanyika ni kuitisha kila aliyenunua nyumba kuonyesha stakabadhi, walio onyesha proof ya malipo, walibaki na nyumba zao, walionunua kwa ahadi bila kulipa chochote, walisainishwa surrender document na kuzirejesha hizo nyumba na zimerejeshwa serikalini.

Ila kwenye nyumba zilizoko kwenye mashamba kuna watu waliuziwa na kuzilipia kihalali na stakabadhi wanazo, ila wamelazimishwa kuzirejesha kwasababu nyumba hizo hazina hati, hawa wanapaswa wafidiwe kurejeshewa fedha zao. Mauziano yoyote ya jengo ni hati na sio jengo. Huwezi kuuziwa nyumba bila hati kama ambavyo huwezi kununua gari bila kadi.

P
Asante mkuu kwa uchambuzi
 
Safi Paskali hapa nimekuelewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngongo,
Mimi si niliyeandika makala hiyo.
Hii makala iko katika gazeti la Jamvi la Siasa.
Nimeelewa si wewe, ni vema umeleta nasi tujue kuna upotoshaji unaendelea.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga ametajwa kamanda huyu asiguswe kabisa. RC na Katani ugomvi ni kutolipa wakulima a hali anasema anatoa gawio. "wewe upate faida halafu hao wanaoitwa wakulima wadogo huwapi hela zao hadi miezi 8"
Halafu anasema alisema mkonge uliagizwa uuzwe kwa mchina, kweli hii?
au mnada umefanyika na mchina akashinda ambaye ndiyo hata Katani alikuwa anamuuzia?. yaani mnunuzi na 1 duniani kwa sasa!
mambo mengine ya Katani kuuza makorona hadi Kenya hayo hayajulikani. TSA ikiwa chini ya shamte na hao 80+ ndo walihujumu na kujiuzia. na mafao hayo walinunua hisa na baadaye wakazichukua baadhi yao.

kwa vile mmeleta huku watakuja wenyewe waseme yote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tujifunze jamani. Uongo unajitenga na kweli. Ni suala la muda tu. Haya magumashi hayana mtoto wa mjini wala wa porini. Yakifumuka yanaangusha wote.
Pole mzee wangu. Another day and another lesson. Tuache kushabikia mambo sababu ya dini
 
kilichonisikitisha ni jinsi pesa za wafanyakazi kupitia mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF zinavyopotea, zilipotea general tyre na bado kuna watu walitaka zitumike kuanzisha viwanda vikiwemo viwanda vya sukari.Kuna namna salama ya kuwekeza fedha za mifuko ya hifadhi ya jamii kama kununua dhamana za serikali lakini sio kujenga majumba ambayo wanaongeza thamani ya viwanja na gharama za ujenzi matokeo yake yanakosa hadi wapangaji au wanunuzi huku wafanyakazi wakizungushwa mafao yao
 
Sony,
Mimi si niliyeandika makala hiyo.
Hii makala iko katika gazeti la Jamvi la Siasa.
Pole sana mkuu. Umenikumbusha tulipokuwa watoto baba yangu alikunikuta nachezea vipande vya chupa vilivyopasuka akanikaripia na mimi nikajitea sina kosa kwani nimepewa na rafiki yangu tena aliyekuwa mdogo kiumri kwangu. Utoto bwana.
 
Uchambuzi wa pascal umeweka maswali fikilishi ya msingi. Huyo shamte ana matatizo ya kiupigaji inaonekana kampuni ni yake binafsi na kafanya janja janja ndio maana wazungu wanasepa ye yupo tuu kwa sababu alijua kutumia udhaifu wa watendaji wa awamu zilizopita.
 
Pole sana mkuu. Umenikumbusha tulipokuwa watoto baba yangu alikunikuta nachezea vipande vya chupa vilivyopasuka akanikaripia na mimi nikajitea sina kosa kwani nimepewa na rafiki yangu tena aliyekuwa mdogo kiumri kwangu. Utoto bwana.
Macho...
Wala mfano huo haufanani hata kwa mbali.

Sijapewa chochote labda taarifa kuwa soma gazeti la Jahazi la Siasa kuna taarifa ya Katani.

Nimeichukua na kuleta barzani kwa wana-barza na wao wastafidi.

Habari ndani ya gazeti hapewi mtu iko wazi kwa atakae kuisoma.

Anachopewa mtu ni kile hawezi kukipata hadi mwenyewe akitoe.

Fikiri kabla ya kuandika na kutoa pole.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mohamed Said ,

..nilitaka nikushambulie lakini nimeshindwa nianzie wapi.

..ila na wewe kwanini uka-post makala hii kwenye jukwaa la HISTORIA?

..kwanini hukuileta sebuleni / jukwaa la siasa ili ionekane na wanachama wengi?

Jokakuu,

Mada zake nyingi zinabeba wale tu anaoshare nao imani za kidini. Bahati mbaya wameanza kumuangusha. Unakumbuka ile ya Idd Simba. Mkapa pamoja na kumzika, aliandika alitolewa baraza la mawaziri kwa kwenda kinyume na maadili ya kazi zake.
Niliwahi kusoma huko nyuma juu ya kamanda Chico. Alikuwa Kilimanjaro. I hope hakumaanisha. Maana ni majanga tupu
 
Nashangaa hujamtaja Nyerere. Our reality as people with no credibility has started popping up. Najua kwako ina maanisha kitu kingine. Pole sana. Hawa watu wengine unaowapamba humu, hawastahili hizo heshima unazozipigania sababu tu ya dini
Ndahani,
Unashangaa sijamtaja Nyerere.

Hapa wewe ndiye umemtaja Nyerere si mie.

Sasa ndiyo utashangaa zaidi.

Leo wamekuja nyumbani kwangu TBC na Kumbukuzi ya Nyumba ya Mwalimu Nyerere kunihoji kuhusu Nyerere na uhusiano wake na Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes, Mshume Kiyate na Kasella Bantu.

Tumefanya mahojiano kwa ajili ya kipindi cha TV takriban zaidi ya saa moja.

Waulize wamiliki wa vyombo hivyo kwa nini mmekwenda kumuhoji Mohamed Said kuhusu Nyerere?

Sasa nani amshangae nani?

Picha hiyo hapo chini wakinitayarisha kabla ya mahojiano.
20200317_173351_001.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom