ukweli kuhusu hii kampuni ya kuuza magari ya japan TRADE CAR VIEW

wandugu mwenye kujua ukweli wa hii kampuni ya CA TRADE CAR VIEW ya japan inayohusika na kuuza used car kutoka japan naomba unipe uhakika wa hii kampuni isije ikawa ni matapeli wa nigeria wanatumia mtandao kutaka kutapeli pesa . nia yangu ni kuagiza gari kupitia kampuni yao. kama yupo aliyewahi kuitumia hii kampuni tafadhali naomba anipe uhakika

Ni kampuni nzuri ya kutangaza magari yanayouzwa kama yalivyo mengi na malipo hupitia kwao, na magari yao huuzwa "As Is." Kama gari ikifika utaona matatizo yanaanza kukusumbua kichwa hawahusiki maana biashra ukishalipa mnaachana we shughulia na tolori lako kulitengeneza kama hukufanya uhakiki kabla ya kununua.
Note:
Nilipotaka kununua gari kupitia kwao nilishangaa kuona kuna nyongeza ambazo awali hazikuainishwa kwenye bei ya kununulia na kusafirisha
Picha ya gari inapendeza lakini hakuna uhakika na ubora wa gari kwa vile mfanya biashara anachotaka ni gari yake iuzike apate chake.

Kuna gharama za kawaida ambazo ni shipping, inspection, bima, lakini kuna makampuni utashangaa yanakuongezea gharama zaidi ambazo hazikuainishwa awali katika matangazo yao.

Nilichofanya:
Kupata kampuni inayojitangaza huko Trade car view ambayo mtu atafanya uhakiki wa ubora wa gari ninayokusuda kuuza, kwa kuwa magari mengi ni used na yanauzwa as is.

Kwa bahari rafiki yangu mmoja anafanyia kazi moja ya makampuni hayo ni mtanzania, tumesoma pamoja na kuwa friends muda mrefu aliyeko huko huko Japan ndiye aliyenisaida kupata gari bora sana ambalo wengi walishangaa kwa bei niliyonunua na linavyoonekana moto wa kuotea mbali.

Watanzania wengi huangalia mradi kuwa na gari bila kuangalia ubora, ni jambo ambalo nawaangalisha wengi, maana mimi jasho langu huwa sipendi lipotee kwa uzembe, maana mtu kufikia kukusanya za kununua gari ujue amejifunga ukanda na kupangua yasiyo lazima ili kujaza kibaba.

Jambo la msingi bora uwe na mtu ambaye anafanya inspection kwa ajili ya kukuhakikishia ubora, maana kutumiwa gari tu kesho ukishatumia wiki moja matatizo mengi yanaanza kukumiza kichwa kama transmission nk. nini sababu ulitazama mvuto wa umbile na rangi bila kuangalia mambo ya ndani kama ina ubora huenda imechakachuliwa katika kutangaza biashara.

Wenye bahati wanabahatika kupata magari mazuri na wengine inakula kwao, na hata pengine kusihia pesa kuota mbawa kwani ninayo mifano ya uhakika katika hilo, hapa tusiongope tuwe wakweli, maana pesa kama umeitokea jasho unahitaji kupata chambo kitakachokusaidia muda wa kutosha vinginevyo litakuwa pambo nyumbani una gari usiloweza kutoka nalo hata mita moja.

Kama uko Tanzania, na kabisa jiji la Dar es Salaam, nenda Mikocheni pale Shoppers Center kuna kampuni tanzu ya LUCUS Japan ambao hutumia pia mtandao huo huo wa Trade Car View, watakusaidia kuchagua gari na mambo mengine na hata pesa utailipia pale kwao. Lakini wanataka uachie kitu wakati mwingine kama posho ya uagizaji. Ukitaka nikupe anayeweza kukufanyia ukaguzi wa kupata gari moja zuri ambaye anafanya kampuni hiyo hiyo aliyeko Japan, please PM me nitakuunganisha. Note mimi sifanyi biashara hiyo, itakuwa kukusaidia mdau wa JF.

Uwe mwangalifu, humu kuna wafanyabiashara wa magari, wanakuvutia lakini uwe makini na kuwa na jicho la ziada kusoma comments za watu.
 


Mkuu.., uko sawa kabisa hapo kwenye AUTOREC, Jamaa hawabatishi na Gari zao almost Brand New.!!!

Wanazo pia ofisi pale Jmall, juzi kati nilikuwa naye sales Manager wao, Mr.Mizuno yuichi pale Mlimani city..

na kunihakikishia wanayo stock nzuri kwa ajili ya Mazingira ya barabara za Tanzania, ila bei zao zimechangamka kidogo.!!!


Mkuu itakua ni kwenye ile ishu ya Tanzania Autofest 2012,,Autorec wako poa sana sema gharama zao ziko juu kidogo
 
Usihangaike kuagiza mbali mi nna mchuma upo bomba Isuzu Wizard mwaka 2000 imetembea km 140,000 silver colour nzuri tu.Nimeishaitumia tangu 2010,naiuza si kwamba ina tatizo ila nataka kubadili gari. Kwa yeyote anayehitaji tuwasiliane kupitia namba 0784-733529 nipo DAR
 
wandugu mwenye kujua ukweli wa hii kampuni ya CA TRADE CAR VIEW ya japan inayohusika na kuuza used car kutoka japan naomba unipe uhakika wa hii kampuni isije ikawa ni matapeli wa nigeria wanatumia mtandao kutaka kutapeli pesa . nia yangu ni kuagiza gari kupitia kampuni yao. kama yupo aliyewahi kuitumia hii kampuni tafadhali naomba anipe uhakika


Nimeagiza magari zaidi ya saba kupitia Tradecarview. Inawezekana nina bahati sana, vinginevyo naweza kusema ni sehemu isiyokuwa na ubabaishaji. Cha muhimu ni kuwasiliana na muuzaji kupitia Tradecarview website na sio muuzaji moja kwa moja. Muuzaji anayetaka uwasiliane naye moja kwa moja anataka kukutapeli. Pia tumia Paytrade ambapo hela yako inashikiliwa na Tradecarview mpaka muuzaji akutumie gari.

Kuhusu ubora wa gari kila kitu kinaonyeshwa kwenye page ya gari husika na kama lina kasoro yoyote basi watakwambia ili uamue mwenyewe kama utalinunua hivyo hivyo au la. Pia tukumbuke kuwa kuna inspection na wenzetu wako very strict, gari ambalo halijafikia viwango litazuiwa. Nakumbuka niliagiza Toyota Spacio ikazuiwa kwenye inspection kwani ilikuwa na matatizo kwenye engine ikabidi muuzaji anitafutie nyingine.

Ni kweli kuna wahuni wako mle ndio maana Tradecarview wanasisitiza uwasiliane na muuzaji kupitia website yao na si vinginevyo. Kampuni yoyote ya kibabaishaji huwa inakuwa blacklisted na orodha ya makampuni hayo ya kitapeli utaikuta humo katika website yao. Good luck!
 
Kama walivyotangulia wachangiaji wa mwanzo tradecarview ni ubao tu wa matangazo,kuna kampuni kibao za uuzaji wa magari zimo humo,wako vizuri wana kupa chaguo pana na si matapeli nasema hivyo kwasababu nina gari 2 nimeziagiza toka kwao na zimefika salama na zikiwa na hali nzuri.Cha kuzingatia unapochagua gari angalia profile ya kampuni inayouza hilo gari ina mtaji kiasi gani,magari mangapi na uzoefu wao.Mwisho hakikisha unachagua gari lenye paytrade system.Paytrade ni mfumo wa bima flani kati yako na carview,itakuhakikishia kuwa hela uliyotuma inakua reliased kwa muuzaji wa gari pale tu gari lako linapothibitika limepakiwa kwenye meli.

Kila raheli.
 
Trade carview ni mtandao unaounganisha wauzaji wengi wa magari na ni wa uhakika. Ila kuwa makini uchague pay trade system. Ukitumia pay trade system jamaa wa trade car view wana hold pesa yako mpaka gari ikufikie. Ukiona muuzaji anakwambia muwasiliane naye moja kwa moja kataa kabisa mawasiliano yote yapitie trade carview na huwa wanamonitor mawasiliano yanayopitia kwao. Na wana ku alert kabisa ukifanya mawasiliano na muuzaji bila kupitia kwao ikitokea chochote imekula kwako. Niliagiza gari april mwaka jana ilifika within a month baada ya kulipia na mpaka leo ipo bomba mbaya yaani namwaga tu oil kila baada ya 3,000 km matengenezo mengine ni madogo madogo kutokana na barabara ninapoishi kuwa mbovu. Kuhusu inspection usihofu japan wapo vizuri na hata trade carview hawaruhusu gari mbovu ziuzwe kwenye website yao.
 
Waweza pia kuwatumia Japan Trade Car (Jina la kampuni ni Trade Haus Logistics (THL)) ni waaminifu na mimi binafsi nimenunua gari kutoka kwao na nikalipata bila usumbufu wowote.
 
Mh!!!...Hivi hizi biashara za matoroli kila mmoja yumo...kwa kweli inaumiza kichwa inapofika wakati wa kujitafutia ka-transport....Mi siku hizi napita pita kule kitumbini na mitaa ya kati e.g mtaa wa India na kwingineko kwa wadosi mle nanunua magari. Nakagua mtambo tunaimbishana mpaka biashara inafanyika...Hivyo kwenye mitandao bhana roho juu tu!!
 
[Beforward japan ndio mpango mzima]

Nakubaliana na wewe kaka, mambo yote Beforward, nina mwezi wa tatu sasa nimevuta Duet yangu kwa bei poa kabisa.

Mbona huwa nikichungulia gari zao kwenye website naona kama zimechoka sana?
 
Back
Top Bottom