ukweli kuhusu hii kampuni ya kuuza magari ya japan TRADE CAR VIEW

kupe

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
1,035
326
wandugu mwenye kujua ukweli wa hii kampuni ya CA TRADE CAR VIEW ya japan inayohusika na kuuza used car kutoka japan naomba unipe uhakika wa hii kampuni isije ikawa ni matapeli wa nigeria wanatumia mtandao kutaka kutapeli pesa . nia yangu ni kuagiza gari kupitia kampuni yao. kama yupo aliyewahi kuitumia hii kampuni tafadhali naomba anipe uhakika
 
Tradecarview ni ubao wa matangazo, au ni sehemu ya kutagazia biashara ya magari, hawahusiki moja kwa moja na kuuza magari, wao ni sehemu ya kuwajuza watu wanaohitaji kununua magari au kuuza magari. Ndani ya tradecarview kuna makampuni mengi ya kuuza magari. Jaribu kusoma terms conditions (masharti yao) ili kuelewa zaidi. Lakini kwa msaada zaidi kuna kampuni kama TRUST (japanesevehicles.com) hii kampuni inajihusisha moja kwa moja kuuza magari pia wana ofisi hada Dar eneo la Kurasini lakini bei zao ziko juu kidogo.
 
Yeah, umesema vizuri kuhusu trade car view. Wao ni sehemu ya kuwajuza watu wanaohitaji kununua magari au kuuza magari. Tradecarvie huwa wanadeal na wauzaji wa magari walio waaminifu. Ukipata tatizo lolote kutoka kwa muuzaji waliye na mkataba naye, wanakusaidia kushughulikia tatizo lako. Mimi nimeshafanya biashara na wauzaji tofauti tofauti wanaojitangaza kwenye site ya tradecarview na kila kitu kimeenda vizuri kabisa!
 
achana nao wana ghalama kubwa,mwanzo utona kama wana bei ndogo lkn ukkwani kuna ishafikia muafaka ndio baadae utakuja kugundua kuna ghalama za kamishina zinaongezeka mimnakushauli tumia enhance auto ukigoogle utaona picha yenye bendera ya tz ambayo mi mwenyewe nimepiga na gari ya blue toyota ist.
 
Japan Car Trade View ni moja ya makampuni yaliyowaliza watu mob mwaka juzi watanzania walilizwa zaidi ya 96,000Usd, unaweza kuchagua gari then ukatumiwa kanyaboyaa, Hiyo Mzee hiyo ni website mtu yeyote anayeuza gari anapost, Uhakika tumia autorec japan uhakikahao jamaa magari yao uhakika na wanaofisi Dar, au Beforward Japan
 
Tradecarview wana paytrade ni uhakika sana sana...pesa yako haiwezi potea,wao wanakaa na pesa yako hadi ukihakikisha gari imefika nchini kwako...ndio wana release fund to dealer!!Pia befoward wako safi sana wanakupa hata tracking of docs and your car likiwa kwenye meli...
 
Nimetoa juzi tu kwa kuwatumia carview ni wazuri sana na uhakika mkubwa tena wapo safi sana kila kitu kipo wazi sema utatakiwa kulipa paytrade charges minimum ni USD 150 vinginevyo ni 3.7 or 3.9 percent of your car price (kama sijakosea) plus USD 50.
 
mkuu unaweza pia tumia SBT JAPAN,wana ofisi hapa akiba, hapo mi nimepitishia magari kibao
 
Tradeacarview hawauzi magari ...ile ni website tu ambayo madealer ndo wana nadi magari yao..sasa hapo ndio uangalie na kampuni ambazo uta deal nao ..coz zingine ni ndogo sana hata wakashindwa kukuletea Gari lako kwa wakati...sababu kuna kampuni ishawah chelewesha Gari for 2months
 
Japan Car Trade View ni moja ya makampuni yaliyowaliza watu mob mwaka juzi watanzania walilizwa zaidi ya 96,000Usd, unaweza kuchagua gari then ukatumiwa kanyaboyaa, Hiyo Mzee hiyo ni website mtu yeyote anayeuza gari anapost, Uhakika tumia autorec japan uhakikahao jamaa magari yao uhakika na wanaofisi Dar, au Beforward Japan

Mkuu.., uko sawa kabisa hapo kwenye AUTOREC, Jamaa hawabatishi na Gari zao almost Brand New.!!!

Wanazo pia ofisi pale Jmall, juzi kati nilikuwa naye sales Manager wao, Mr.Mizuno yuichi pale Mlimani city..

na kunihakikishia wanayo stock nzuri kwa ajili ya Mazingira ya barabara za Tanzania, ila bei zao zimechangamka kidogo.!!!

hakikisha unatumia mfumo wao wa malipo PAYTRADE ingia kwene web yao chek maelezo kwa kina
 
nawatumia sana,kama una shida ninaweza kukusaidia
wandugu mwenye kujua ukweli wa hii kampuni ya CA TRADE CAR VIEW ya japan inayohusika na kuuza used car kutoka japan naomba unipe uhakika wa hii kampuni isije ikawa ni matapeli wa nigeria wanatumia mtandao kutaka kutapeli pesa . nia yangu ni kuagiza gari kupitia kampuni yao. kama yupo aliyewahi kuitumia hii kampuni tafadhali naomba anipe uhakika
 
kama alivyosema KBM,tradecarview ni ubao wa matangazo ambao unatakiwa kuulipia,mnunuzi na muuzaji,

Kuna matapeli wengi ndani yake,Nafkiri ni vizuri kama unahitaji gari Japan ukapitia ubalozini kupata taarifa za makampuni ya watanzania wanaoishi kule ambao ni waaminifu pia,tuwe wazalendo na tujenge kuaminiana,mi nawatumia hao na napata magari mazuri tu.
 
[Beforward japan ndio mpango mzima]

Nakubaliana na wewe kaka, mambo yote Beforward, nina mwezi wa tatu sasa nimevuta Duet yangu kwa bei poa kabisa.
 
Ni kweli bei zao zimechamka ila ni uhakika, nimeshanunua magari mengi kwao na hakuna Longo longo, Tena Mizuno amewahi kunipa zawadi ya radio ya gari, maana ukiona hujaridhika na radio ya kwenye gari unapaswa kulipia 200Usd ili wakubadilishie Radio nyingine, mi nilipewa Radio bure ya Mizuno,

Back
Top Bottom