Ukweli kuhusu CHADEMA Iringa na uongo wa TUNTEMEKE

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,330
33,954
Kweli leo nimestushwa sana na habari kuhusu kile kinachoitwa uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mkoa wa Iringa. Ingawa habari yenyewe imeondolewa lakini madhara yake yatakuwa ni makubwa sana kama Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Iringa nikikaa kimya. Sijui kama huyo anayejiita TUNTEMEKE kama hata anajua ni kwa jinsi gani watu wanapambana kuuondoa mfumo mbovu uliopo.

Tangu mwaka 2010 CHADEMA Iringa tulikuwa hatuna Mwenyekiti wa MKoa kutokana na yule aliyekuwepo Benny Kapwani kujiuzulu Uenyekiti hapo tarehe 21/08/2010. Tangu wakati huo mpaka tulipofanya kikao cha baraza la Mashauriano Mkoa wa Iringa tarehe 25/02/2012 tulikuwa hatuna Mwenyekiti wa Mkoa.

Kwenye kikao hicho hatukuwa na uchaguzi kama inavyoelezwa bali wanachama walifanya uteuzi kwa mujibu wa Katiba kwani kikao hicho ndicho chenye mamlaka ya kuchagua viongozi wa ngazi ya mkoa. Wajumbe wa Baraza la mashauriano walipendekeza majina ya watu watatu kukaimu nafasi ya Mwenyekiti nao ni: Otmar .O. Haule, Chiku .A. Abwao na Thomas .S. Nyimbo.

Isingekuwa rahisi kwa wote watatu kukaimu nafasi hiyo kwa hiyo wajumbe walipiga kura si kuchagua mwenyekiti bali kuteua miongoni mwa hao watatu nani anafaa zaidi kukaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Mkoa kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi 2013 tutakapofanya uchaguzi wa nafasi hiyo kikatiba. Baada kura kupigwa Chiku Abwao alipata kura 59 na Thomas Nyimbo alipata kura 30 na Otmar Haule alijitoa kabla ya kura kupigwa.

Kwa hiyo hoja ya TUNTEMEKE kwamba kulikuwa na fomu za kugombea nafasi hiyo si za kweli kwani si Chiku Abwao wala Thomas Nyimbo walioingia kwenye kikao kile wakiwa ni wagombea wala wanachama hawakuja kwenye kikao wakijua kuwa Abwao na Nyimbo ni wagombea.

Na kikao kile cha Baraza la Mashauriano cha mkoa wa Iringa hakikufanyikia Makao Makuu ya Mkoa kama TUNTEMEKE anavyotaka tuamini bali kikao kile kilifanyikia Makambako kwenye Mkoa Mpya wa Njombe ambao kichama bado ni sehehmu ya Mkoa wa Iringa.

Uchaguzi ule niliusimamia mimi mwenyewe kutokana na sababu za kiufundi wala si kwa utashi wangu mimi binafsi, CHADEMA hatuna kamati tendaji ngazi ya Mkoa badala yake tuna Baraza la Uongozi la Mkoa ambalo wakati huo lilikuwa halina Mwenyekiti. Kwenye kikao cha Baraza hilo ambalo Chiku na Msigwa ni wajumbe na wote walihudhuria (24/02/2012) ilikubaliwa kwamba niendeshe mchakato wa kuteua kaimu Mwenyekiti wa Mkoa ili kikao kiendeshwe na Mwenyekiti anayekubalika na wajumbe wa Kikao badala ya Baraza la Uongozi kuteua Mwenyekiti wa kuongoza kikao hicho.

TUNTEMEKE ana chuki binafsi na DR. Slaa lakini ukweli utabaki kuwa hakukuwa na fomu za kugombea kwa hiyo kusema kwamba Dr. Slaa alimshawishi Chiku Abwao kuchukua fomu ni uongo uliopindukia na wala si kweli kwamba Peter Msigwa amewahi kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Iringa. Huu nao ni uzushi unaotakiwa kupuuzwa kwa nguvu zote. Labda TUNTEMEKE anaweza kutuambia ni lini Msigwa alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Iringa na kikao kilichomchagua kilifanyikia wapi na uchaguzi ulisimamiwa na nani?

Nawasilisha!!

Allen Kilewella
Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Iringa
 
Mkuu heshima mbele!!
Tunashukuru kwa ufafanuzi uliokamilika na kwa wakati, tunawahakikishia tu kwamba tuko macho na tunaelewa mchezo unaofanyika hapa..

Wengine kwenye post zao wamekiri kwamba 'watawaaminisha watu kuwa Slaa si yule watu wamdhaniaye'- Waberoya.

Huu upuuzi unaoletwa hapa sisi wenye macho tanauona, na hapa tunafahamu kuana watu wanajiita hawana chama ambao literally ni vuguvugu na sisi wengine tulishawatapika siku nyingi!!

Tunangoja taarifa rasm ya CC toka mamlaka husika!!
:yo:
 
asante kamanda wetu pande hizo kwa ufafanuzi mzuri na unaoeleweka! huyu Tumtemeke anatatufuta kila njia kukihujumu chama na kuwadhalilisha viongozi wetu ila tulishamtukia hana lolote ana uchu wa madaraka tu basi makamanda endeleeni kuchapa kazi kwa mujibu wa katiba yetu acheni tumtemeke aendelee kupiga kelele kama debe tupu!!
 
safi sana kamanda wetu,acha na huyu gamba ambae ata anufaiki na ufisadi wa magamba wenzie anabaki kuleta habari za uzushi tu! tunampa adhabu ya kumpuuza huyu gamba la mamba.
mtikisiko wa ubongo una muhusu
 
Tuntemeke again? Bado ni bifu la Bavicha?
Thanks kwa ufafanuzi, japo naona Tuntemeke hana mapenzi ya dhati na CDM, achukue tu uamizi mwepesi aende ccm.
 
UWAZI,UMAKINI,NI JAMBO ZURI KWA VIONGOZI WETU TUNAKUSHUKURU KATIBU KWA UFAFANUZI MZURI NA UMAKINI WA KUJIBU HOJA KWA WAKATI UNAOTAKIWA BIG UP KUBWA CHADEMA NGUVU YA UMMA

Thanks
 
Tuntemeke ni jina la hovyo sana, ndio maana hata yule mwingine aliporudi toka ughaibuni akampa shida sana Mwl. Nyerere maana alikuwa hataki cheo chochote zaidi ya uraisi na mwishowe akapigwa detention. Ni jina la kipuuzi sana nadhani huyu ni wakufukuza tu hakuna haja ya kuhangaika nae yeyd ni nani kwani, fukuza huyo.
 
Huyu TUNTEMEKE na wenzake ni boya ambayo mawimbi ni yao na upepo ni wao na si siri kundi lao linayumba. Wanafikiri kwa shutuma nyepesi namna hii wanaweza wakaurudisha nyuma umma wa watanzania walioamua kwa dhati kusonga mbele kwa mtazamo wa kuleta mabadiliko. Huyu ni mfa maji na ushahidi wa kamanda hapa unamfanya apwaye humu ndani na kuzidi kuzama kwenye kundi la wazushi na mmojawapo wa watu wenye hoja nyepesi na fake.
 
huyu tuntemeke ni one of the vibaraka wa ccm asiyejua hata anachofanya au ametumwa afanye nini, hayo mambo kama alikuwa anataka kusema angeenda kwenye sehemu husika za CDM akaseme, kuja hapa kwenye JF na kutoa alichotumwa ni upuuzi, ujinga na ununda umemjaa kama ulivyowajaa wenzake huko alikotumwa
 
Tutemeke tena,

Mgogoro huu hautadumu kitambo,kwa mkoa wa Iringa mpaka Juni mwaka huu utakuwa umejigawa na kuwa mikoa miwili.Iringa na Njombe.

Pia Katibu si uko kwenye baraza kuu naomba uyaongee huko.
Uzushi na Uongo huu ulisemwa humu na ni lazima ukanushwe humu humu JF. Juzi kulikuwa na Uzushi mwingine tena. hawa watu wasiposhghulikiwa watajijengea mazoe ya kuzua mambo na kuharibu taswira ya chama kwa wananchi.
 
TUNTEMEKE .. Mhasibu garasha.. Hajamalizia Ujenzi wa kibanda Chake akashtukiwa kwa wizi ndani ya chama Na kiondolewa kwenye idara ya fedha.. Hata Kama una urafiki na Chair ila Maslahi ya Nchi ni Muhimu zaidi meku.

Dr Slaa nimewahi kumsikia Mtu mmoja hapa Cheki ambaye alifanya kazi kwenye halmashauri ya wilaya ya Karatu time Dr. Akiwa mbunge pale. Alinambia Dr kwenye kusimamia Matumizi Na uhalali wa mapato Hana mjadala Wala undugu. Pole tunte.. Omba kazi ya Uhasibu Magambaz
 
Aje hapa huyo dada muimba taarabu kwa jina la TUNTEMEKE aliyetumwa na anatumika,ndo maana kwenye post yake nimdesema amechanganyikiwa yule,hela za masharti za kwa Mwakipande zmeisha naona sasa anawekwa mjini na wanaomtumia kuimba nymbo kama hzo,waje na mwenzie ritz na Judi wa kishua,na mwaka huu watakonda sana na MUZIKI WA M4C, VIVA CHADEMA
 
Tutemeke tena,

Mgogoro huu hautadumu kitambo, kwa mkoa wa Iringa mpaka Juni mwaka huu utakuwa umejigawa na kuwa mikoa miwili. Iringa na Njombe.

Pia Katibu si uko kwenye baraza kuu naomba uyaongee huko.
Haya sasa kama si kujichanganya ni nini? Katibu amefafanua vizuri sana huyu Josephine anakuja na kusema mgogoro huu hautadumu kitambo. Kwani katibu kasema kuna mgogoro? Jamani mbona mnatuchanganya? Mtu akisema mnasema mnafiki. Hilo nalo hapo hamlioni?
 
Haya sasa kama si kujichanganya ni nini? Katibu amefafanua vizuri sana huyu Josephine anakuja na kusema mgogoro huu hautadumu kitambo. Kwani katibu kasema kuna mgogoro? Jamani mbona mnatuchanganya? Mtu akisema mnasema mnafiki. Hilo nalo hapo hamlioni?
Kimbunga CHADEMA ni taasisi kwa hiyo kuwa na migogoro ni kawaida. Nadhani hoja hapa ni hizi tuhuma kwamba yaliyotokea yametokea kwa sababu kuna mkono wa Dr. Slaa, jambo ambalo si la kweli!!
 
Last edited by a moderator:
Haya sasa kama si kujichanganya ni nini? Katibu amefafanua vizuri sana huyu Josephine anakuja na kusema mgogoro huu hautadumu kitambo. Kwani katibu kasema kuna mgogoro? Jamani mbona mnatuchanganya? Mtu akisema mnasema mnafiki. Hilo nalo hapo hamlioni?

Wewe si mwanachama wa CDM wala CCM kinachokuchanganya nini??

Punguza kwanza ushabiki na unafiki hutachanganyikiwa!!
 
Back
Top Bottom