Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,574
- 34,531
Kweli leo nimestushwa sana na habari kuhusu kile kinachoitwa uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mkoa wa Iringa. Ingawa habari yenyewe imeondolewa lakini madhara yake yatakuwa ni makubwa sana kama Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Iringa nikikaa kimya. Sijui kama huyo anayejiita TUNTEMEKE kama hata anajua ni kwa jinsi gani watu wanapambana kuuondoa mfumo mbovu uliopo.
Tangu mwaka 2010 CHADEMA Iringa tulikuwa hatuna Mwenyekiti wa MKoa kutokana na yule aliyekuwepo Benny Kapwani kujiuzulu Uenyekiti hapo tarehe 21/08/2010. Tangu wakati huo mpaka tulipofanya kikao cha baraza la Mashauriano Mkoa wa Iringa tarehe 25/02/2012 tulikuwa hatuna Mwenyekiti wa Mkoa.
Kwenye kikao hicho hatukuwa na uchaguzi kama inavyoelezwa bali wanachama walifanya uteuzi kwa mujibu wa Katiba kwani kikao hicho ndicho chenye mamlaka ya kuchagua viongozi wa ngazi ya mkoa. Wajumbe wa Baraza la mashauriano walipendekeza majina ya watu watatu kukaimu nafasi ya Mwenyekiti nao ni: Otmar .O. Haule, Chiku .A. Abwao na Thomas .S. Nyimbo.
Isingekuwa rahisi kwa wote watatu kukaimu nafasi hiyo kwa hiyo wajumbe walipiga kura si kuchagua mwenyekiti bali kuteua miongoni mwa hao watatu nani anafaa zaidi kukaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Mkoa kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi 2013 tutakapofanya uchaguzi wa nafasi hiyo kikatiba. Baada kura kupigwa Chiku Abwao alipata kura 59 na Thomas Nyimbo alipata kura 30 na Otmar Haule alijitoa kabla ya kura kupigwa.
Kwa hiyo hoja ya TUNTEMEKE kwamba kulikuwa na fomu za kugombea nafasi hiyo si za kweli kwani si Chiku Abwao wala Thomas Nyimbo walioingia kwenye kikao kile wakiwa ni wagombea wala wanachama hawakuja kwenye kikao wakijua kuwa Abwao na Nyimbo ni wagombea.
Na kikao kile cha Baraza la Mashauriano cha mkoa wa Iringa hakikufanyikia Makao Makuu ya Mkoa kama TUNTEMEKE anavyotaka tuamini bali kikao kile kilifanyikia Makambako kwenye Mkoa Mpya wa Njombe ambao kichama bado ni sehehmu ya Mkoa wa Iringa.
Uchaguzi ule niliusimamia mimi mwenyewe kutokana na sababu za kiufundi wala si kwa utashi wangu mimi binafsi, CHADEMA hatuna kamati tendaji ngazi ya Mkoa badala yake tuna Baraza la Uongozi la Mkoa ambalo wakati huo lilikuwa halina Mwenyekiti. Kwenye kikao cha Baraza hilo ambalo Chiku na Msigwa ni wajumbe na wote walihudhuria (24/02/2012) ilikubaliwa kwamba niendeshe mchakato wa kuteua kaimu Mwenyekiti wa Mkoa ili kikao kiendeshwe na Mwenyekiti anayekubalika na wajumbe wa Kikao badala ya Baraza la Uongozi kuteua Mwenyekiti wa kuongoza kikao hicho.
TUNTEMEKE ana chuki binafsi na DR. Slaa lakini ukweli utabaki kuwa hakukuwa na fomu za kugombea kwa hiyo kusema kwamba Dr. Slaa alimshawishi Chiku Abwao kuchukua fomu ni uongo uliopindukia na wala si kweli kwamba Peter Msigwa amewahi kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Iringa. Huu nao ni uzushi unaotakiwa kupuuzwa kwa nguvu zote. Labda TUNTEMEKE anaweza kutuambia ni lini Msigwa alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Iringa na kikao kilichomchagua kilifanyikia wapi na uchaguzi ulisimamiwa na nani?
Nawasilisha!!
Allen Kilewella
Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Iringa