Ukweli kesi ya mzungu na Airbus yetu

Ukweli kesi ya mzungu na Airbus yetu

Hauwezi kufanya kitu kama hicho maana kwa vyovyote vile gharama za kuipaki ndege SA kwa siku zote haiwezekani wala gharama za hao mawakili wa huko SA haiwezi kufika $10,000,000 tangu siku ndege imeshikiliwa hadi inaruhusiwa..sheria ni tamu sana kama unaijua..
Mkuu kuwa mambo mengi ya kuangalia hapo,
1.Gharama za mawakili
2.parking charges
3.disturbance allowance kwa abiria wa S.A, na wengine wote waliokuwa wanaisubiria ndege kwenye route yake
4.Hili ndio kubwa zaidi, kuondoa uaminifu kwa wateja wa ATCL na kutengeneza image mbaya ya ATCL kwenye biashara.
5.Gharama za serikali kuifuatilia ndege.
 
Hauwezi kufanya kitu kama hicho maana kwa vyovyote vile gharama za kuipaki ndege SA kwa siku zote haiwezekani wala gharama za hao mawakili wa huko SA haiwezi kufika $10,000,000 tangu siku ndege imeshikiliwa hadi inaruhusiwa..sheria ni tamu sana kama unaijua..
Sidhani kama garama ni hizo mbili tu, ukiunganisha na hasara iliyopata ATCL ya nauli na huduma kwa abiria walioshushwa siku hiyo, hasara ya kusimamisha biashara ya shirika kwz siku zaidi ya saba, ongeza na kushushiwa uaminifu kibiashara inaweza ongeza tudolali kidogo.
 
UKWELI KESI YA MZUNGU NA AIRBUS YETU.

Na Bashir Yakub.
+255 784 482 959.

KABLA YA KUKAMATWA KWA NDEGE.

Mwaka 1983 kupitia kifungu cha 3( 1 ) cha Sheria iliyoitwa Acquisition and Transfer Management Act,1983 makampuni sita ya mzungu STEYN ambayo ni Rift Valley Seed Ltd, Hashman Estate Ltd,Lente Estate Ltd,Loldebbis Ltd,Mayoka Estate Ltd na Tanganyika Air Ltd yalitaifishwa na serikali ya Tanzania.

Baadae mzungu Steyn alifungua malalamiko kwenye taasisi ya usuluhishi(arbitration) akiomba haki zake zote katika makampuni yote yaliyotaifishwa jambo ambalo alifanikiwa mbele ya Jaji R.V. Makaramba aliyeamua alipwe Dola za kimarekani 36,375,672.81(Dola milioni 36 na hizo nukta),imebidi niongeze sauti kwenye mabano.

Muda ukapita lakini baadae tarehe 3 / 5 / 2011 mzungu akaamua kuisajili hiyo hukumu ya taasisi ya usuluhishi katika mahakama kuu ya biashara ili iwe hukumu ya mahakama na hivyo iweze kutekelezeka.

Tarehe 17/7/ 2012 wakati akiwa katika mchakato wa kufuatilia utekelezaji, serikali na mzungu wakaingia makubaliano kuwa aachane na hiyo hukumu ili imlipe Dola 30,000,000 ( dola milioni 30) badala ya zile 36,375,672.81 zilizoamuliwa awali. Mzungu akakubali na makubaliano yakasainiwa, na makubaliano hayo yakasajiliwa na mahakama na hivyo yakasimama kama hukumu mpya ya mahakama.

Kufikia tarehe 3 / 3 / 2016 serikali ikawa tayari imemlipa mzungu Dola 20,099,155.12(dola milioni 20 na hizo nukta), bila shaka sauti inatosha.

Mwaka 2018 wakati malipo yanaendelea kidogo kidogo serikali ikasitisha malipo na kufungua maombi namba 168/2018 mahakama kuu ya biashara Tanzania. Ikawa inaiomba mahakama iifanyie marejeo hukumu ya taasisi ya usuluhishi iliyoamua mzungu kulipwa Dola 36,375,672.81 kwa hoja kuwa ilikuwa na mapungufu ya kisheria.

Tarehe 14 / 12 / 2018 Jaji B.K.Philip alitoa maamuzi kwa kukataa maombi ya serikali ya kuifanyia marejeo hukumu hiyo kwa hoja kuwa hukumu hiyo haipo na ilishakufa baada ya serikali na mzungu kuamua kuelewana na kuyasajili maelewano hayo mahakamani na hivyo kuyafanya maelewano hayo kuwa hukumu mpya.

Katika maombi hayo serikali iliwakilisha na Wakili Jackline Kinyasi wakati mzungu aliwakilishwa na Wakili Erick Ngmaryo.

Hoja kuu ya wakili Erick hapo mahakamani ilikuwa kwamba maamuzi ya taasisi ya usuluhishi(arbitration) yalishakufa na hayapo, na kuwa yaliuliwa na makubaliano kati ya mteja wake na serikali amapo makubaliano hayo nayo yalisajiliwa yakawa hukumu mpya ya mahakama, na hivyo serikali kuiomba mahakama iifanyie marejeo hukumu hiyo ya awali ni sawa na kuiomba irejee kitu ambacho kilishakufa na hakipo.

Mahakama ilikubali hoja hii ya Wakili Erick na kumpa ushindi kwa hoja hii. Kumbuka huyu Erick ndiye anayetajwa kuongoza mchakato wa kuzuiwa kwa Airbus South Africa.

KUKAMATWA KWA NDEGE.

Baada ya maombi ya serikali kutupwa kama tulivyoona hapo juu basi kumlipa mzungu kukakoma. Mzungu alikosa namna ya kukaza hukumu hapa Tanzania kwakuwa Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Serikali,1967 inakataza kukamata mali za serikali kama njia ya kukazia hukumu, lakini pia haitoi muda wa ukomo wa lini mtu aliyeishinda serikali awe amelipwa . Unasubiri mpaka iamue yenyewe kulipa na kwa muda inaotaka.

Baada ya kuyaona hayo mzungu akakimbilia South Africa mahakama ya Guateng na kufungua shauri namba 28994/2019 la kukazia hukumu akijua huko South mali za serikali ruksa kukamatwa katika kukazia hukumu.

Kumbuka kuna hukumu mbili. Ya kwanza ile iliyokufa ile ya taasisi ya usuluhishi, na ya pili ni hii iliyotokana na makubaliano kati ya mzungu na serikali ambayo iko hai.

Swali kwa mzungu na timu yake lilikuwa ni hukumu ipi ikaziwe hapo South kati ya hizi mbili.

Hii iliyotokana na makubaliano ambayo sasa ndo iko hai ilikuwa haiwezekani kukaziwa South Afrika kwakuwa mahakama ya south haitakuwa na mamlaka kutokana na kuwa tukio au makubaliano yalifanyika Tanzania na hivyo mahakama za Tanzania pekee ndizo zenye mamlaka.

Mzungu na timu yake kwa kulijua hilo wakaamua waachane na hiyo hukumu iliyo hai na kuamua kuomba kukazia hii iliyotokana na Taasisi ya usuluhishi ambayo mahakama ya South inaweza kuikazia kwakuwa ni ya kimataifa.

Lakini kumbuka hukumu hii sio hai tena kwakuwa iliuliwa na ile hukumu iliyotokana na makubaliano, na zaidi Wakili Erick na mzungu walishasema kuwa hukumu hiyo ilishakufa wakati wanapinga maombi ya serikali kama tulivyoona hapo juu na kwa hoja hiyohiyo wakashinda.

Kwahiyo wakaamua kuomba kukazia hukumu ambayo wanajua kabisa kuwa ilishakufa na hawakuthubutu kulisema hilo mahakamani ili wafanikiwe, na hakika walifanikiwa kwa kuizuia AIRBUS 5H-TCH.

KUACHILIWA KWA NDEGE.

Mawakili wa serikali walipoungana na wale wa South Africa waliwasilisha hoja nyingi lakini mojawapo ni hii kuwa ndege imekamatwa kwa kutumia hukumu iliyokwishakufa.

Kwa kuzingatia hoja hii na kwa ushahidi, Jaji TWALA M.L akaridhika na akaona haja ya kuiachia ndege kwakuwa ilikamatwa kimakosa kwa kutumia hukumu mfu/ambayo haipo.

MAMBO MAWILI MUHIMU.

KWANZA
, je deni la mzungu limekufa . Jibu ni hapana deni bado lipo mpaka hapo serikali itakapoweza kufanikisha utaratibu wa kisheria wa kuliondoa, au kuamua kumlipa, au mzungu atumie taratibu za ndani kupata hela hiyo, au asamehe.

PILI, je serikali inaweza kupata chochote kwa mzungu. Jiu ni ndio,inaweza kupata chochote kama ifuatavyo;,

mosi, imeamriwa serikali ilipwe gharama zake zote za kuendeshea kesi,ikifuatilia italipwa.
Pili, inaweza kumfungulia mzungu mashtaka na kumdai fidia ya hasara zote alizosababisha ikiwamo kuiharibia hadhi na kuipotezea dira route ya Tanzania -South ambayo kwa ukweli itachukua mda kuirejesha na kuaminiwa kama ilivyokuwa.

Na hili linawezekana kwasababu mchakato mzima wa kuzuia ndege ulijawa na uongo/udanganyifu kwakuwa hawa walijua kabisa hukumu wanayokazia imekufa lakini kwa makusudi wakaendelea kufanya hivyo(abuse of court process).

Yote kwa yote hivyo ndivyo ilivyokua.

Asante sana....Ndiyo maana wakati mwingi huwa naipenda Jamii forums
 
Mkuu ghrarama za kesi zinainclude parking fee ya ndege pale O R. Kwenye kuharibu reputation ya ATCL labda ndo hela inaweza kupatikana.
Hauwezi kufanya kitu kama hicho maana kwa vyovyote vile gharama za kuipaki ndege SA kwa siku zote haiwezekani wala gharama za hao mawakili wa huko SA haiwezi kufika $10,000,000 tangu siku ndege imeshikiliwa hadi inaruhusiwa..sheria ni tamu sana kama unaijua..
 
Nakuuliza katika ku award damages kuna speficic damages na general damages specific damages lazima ziwe proved je unaweza prove vipi good will ya shirika kama hilo la ATCL kwamba linapata faida kiasi fulani ili uweze kukokotoa hasara..wakati ukaguzi wake wa mahesabu ni classified..?
Mkuu, umenitafakarisha khs specific damages na general damages.
 
Hauwezi kufanya kitu kama hicho maana kwa vyovyote vile gharama za kuipaki ndege SA kwa siku zote haiwezekani wala gharama za hao mawakili wa huko SA haiwezi kufika $10,000,000 tangu siku ndege imeshikiliwa hadi inaruhusiwa..sheria ni tamu sana kama unaijua..
Mkuu 10 million ni ndogo sana kwenye biashara kama hiyo na tukio zima. Kama kuna watu binafsi tu wanadai 1 Billion Tshs kwa kutukanwa na Msiba, I believe Serikali kupitia ATCL wanaweza kabisa kuwa na madai ya kufikia hicho kiasi .... Tatizo ni kuwa kama hawatafanikiwa wanaweza kututia hasra zaidi. Bora walipe hicho kidogo!!
 
Hivi wale jamaa walokuwa wanashangilia wako wapi

Wanaugulia maumivu....wengine wamekwenda kwenye bomba la mafuta...wengine wanapita humuhumu kimyakimya...kejeli dhidi ya wanaasheria wetu hazipo tena...Ni sawa na uzi wa kesi moja iliyomhusu aliyekuwa mbunge mmoja ..wakati kesi ikiendelea mahakamani kukawa na updates nyingi ...binafsi nikawa nafuatilia kwa umakini...updates zenyewe zilikuwa zina mwelekeo wa upande mmoja ..updates kuhusu walichosemma mawakili wa upande wa serikali zikawa zinasuasua na mara zikagota..baadhi wakawa wanauliza humu jamani kuna nini na maamuzi yakoje?? ikawa kimya, wengine tukajua kuna kitu hapo...mara mmoja miongoni mwetu 'akaropoka' humu na kusema mkiona kimya mjue upande fulani mambo siyo sawasawa......wengine tukacheka kimyakimya...
 
hiyo fidia watalipwa "saccos" na "mzalendo" maana waondio wenye kuamini mali zote za Tanzania ni zao.
 
hiyo fidia watalipwa "saccos" na "mzalendo mpiganaji" maana wao ndio wenye kuamini mali zote za Tanzania ni zao.
 
Kwenye uzalendo hakuna upande wa pili kwani uzalendo ni uzalendo tuu.
 
Je haki itaonekana ikitendeka,?
Haki itaonekana imetendeka kwa sababu hawa wazungu wamezulumu ardhi ya mababu zetu 'ancestral land' kiujanjaujanja kama alivotaka kufanyaya kwenye kesi hii. JPM ni kiboko yao, peleka hii wakili uchwara kama muhujumu uchumi. 'ukifanya dhambi malipo hapahapa'.
 
Mkuu 10 million ni ndogo sana kwenye biashara kama hiyo na tukio zima. Kama kuna watu binafsi tu wanadai 1 Billion Tshs kwa kutukanwa na Msiba, I believe Serikali kupitia ATCL wanaweza kabisa kuwa na madai ya kufikia hicho kiasi .... Tatizo ni kuwa kama hawatafanikiwa wanaweza kututia hasra zaidi. Bora walipe hicho kidogo!!
Kisheria hua kuna specific damages na general damages...specific damages inabidi u prove ni kwa kiasi gani umepata hio hasara lazima uwe na documentation tukija kwenye general damages hizi zinatolewa kutokana na discretion ya judge husika hivyo si kweli kwamba kuna justification ya kuweza kufikisha $10,000,000 kwa kuzuia hio ndege kwa siku husika...
 
UKWELI KESI YA MZUNGU NA AIRBUS YETU.

Na Bashir Yakub.
+255 784 482 959.

KABLA YA KUKAMATWA KWA NDEGE.

Mwaka 1983 kupitia kifungu cha 3( 1 ) cha Sheria iliyoitwa Acquisition and Transfer Management Act,1983 makampuni sita ya mzungu STEYN ambayo ni Rift Valley Seed Ltd, Hashman Estate Ltd,Lente Estate Ltd,Loldebbis Ltd,Mayoka Estate Ltd na Tanganyika Air Ltd yalitaifishwa na serikali ya Tanzania.

Baadae mzungu Steyn alifungua malalamiko kwenye taasisi ya usuluhishi(arbitration) akiomba haki zake zote katika makampuni yote yaliyotaifishwa jambo ambalo alifanikiwa mbele ya Jaji R.V. Makaramba aliyeamua alipwe Dola za kimarekani 36,375,672.81(Dola milioni 36 na hizo nukta),imebidi niongeze sauti kwenye mabano.

Muda ukapita lakini baadae tarehe 3 / 5 / 2011 mzungu akaamua kuisajili hiyo hukumu ya taasisi ya usuluhishi katika mahakama kuu ya biashara ili iwe hukumu ya mahakama na hivyo iweze kutekelezeka.

Tarehe 17/7/ 2012 wakati akiwa katika mchakato wa kufuatilia utekelezaji, serikali na mzungu wakaingia makubaliano kuwa aachane na hiyo hukumu ili imlipe Dola 30,000,000 ( dola milioni 30) badala ya zile 36,375,672.81 zilizoamuliwa awali. Mzungu akakubali na makubaliano yakasainiwa, na makubaliano hayo yakasajiliwa na mahakama na hivyo yakasimama kama hukumu mpya ya mahakama.

Kufikia tarehe 3 / 3 / 2016 serikali ikawa tayari imemlipa mzungu Dola 20,099,155.12(dola milioni 20 na hizo nukta), bila shaka sauti inatosha.

Mwaka 2018 wakati malipo yanaendelea kidogo kidogo serikali ikasitisha malipo na kufungua maombi namba 168/2018 mahakama kuu ya biashara Tanzania. Ikawa inaiomba mahakama iifanyie marejeo hukumu ya taasisi ya usuluhishi iliyoamua mzungu kulipwa Dola 36,375,672.81 kwa hoja kuwa ilikuwa na mapungufu ya kisheria.

Tarehe 14 / 12 / 2018 Jaji B.K.Philip alitoa maamuzi kwa kukataa maombi ya serikali ya kuifanyia marejeo hukumu hiyo kwa hoja kuwa hukumu hiyo haipo na ilishakufa baada ya serikali na mzungu kuamua kuelewana na kuyasajili maelewano hayo mahakamani na hivyo kuyafanya maelewano hayo kuwa hukumu mpya.

Katika maombi hayo serikali iliwakilisha na Wakili Jackline Kinyasi wakati mzungu aliwakilishwa na Wakili Erick Ngmaryo.

Hoja kuu ya wakili Erick hapo mahakamani ilikuwa kwamba maamuzi ya taasisi ya usuluhishi(arbitration) yalishakufa na hayapo, na kuwa yaliuliwa na makubaliano kati ya mteja wake na serikali amapo makubaliano hayo nayo yalisajiliwa yakawa hukumu mpya ya mahakama, na hivyo serikali kuiomba mahakama iifanyie marejeo hukumu hiyo ya awali ni sawa na kuiomba irejee kitu ambacho kilishakufa na hakipo.

Mahakama ilikubali hoja hii ya Wakili Erick na kumpa ushindi kwa hoja hii. Kumbuka huyu Erick ndiye anayetajwa kuongoza mchakato wa kuzuiwa kwa Airbus South Africa.

KUKAMATWA KWA NDEGE.

Baada ya maombi ya serikali kutupwa kama tulivyoona hapo juu basi kumlipa mzungu kukakoma. Mzungu alikosa namna ya kukaza hukumu hapa Tanzania kwakuwa Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Serikali,1967 inakataza kukamata mali za serikali kama njia ya kukazia hukumu, lakini pia haitoi muda wa ukomo wa lini mtu aliyeishinda serikali awe amelipwa . Unasubiri mpaka iamue yenyewe kulipa na kwa muda inaotaka.

Baada ya kuyaona hayo mzungu akakimbilia South Africa mahakama ya Guateng na kufungua shauri namba 28994/2019 la kukazia hukumu akijua huko South mali za serikali ruksa kukamatwa katika kukazia hukumu.

Kumbuka kuna hukumu mbili. Ya kwanza ile iliyokufa ile ya taasisi ya usuluhishi, na ya pili ni hii iliyotokana na makubaliano kati ya mzungu na serikali ambayo iko hai.

Swali kwa mzungu na timu yake lilikuwa ni hukumu ipi ikaziwe hapo South kati ya hizi mbili.

Hii iliyotokana na makubaliano ambayo sasa ndo iko hai ilikuwa haiwezekani kukaziwa South Afrika kwakuwa mahakama ya south haitakuwa na mamlaka kutokana na kuwa tukio au makubaliano yalifanyika Tanzania na hivyo mahakama za Tanzania pekee ndizo zenye mamlaka.

Mzungu na timu yake kwa kulijua hilo wakaamua waachane na hiyo hukumu iliyo hai na kuamua kuomba kukazia hii iliyotokana na Taasisi ya usuluhishi ambayo mahakama ya South inaweza kuikazia kwakuwa ni ya kimataifa.

Lakini kumbuka hukumu hii sio hai tena kwakuwa iliuliwa na ile hukumu iliyotokana na makubaliano, na zaidi Wakili Erick na mzungu walishasema kuwa hukumu hiyo ilishakufa wakati wanapinga maombi ya serikali kama tulivyoona hapo juu na kwa hoja hiyohiyo wakashinda.

Kwahiyo wakaamua kuomba kukazia hukumu ambayo wanajua kabisa kuwa ilishakufa na hawakuthubutu kulisema hilo mahakamani ili wafanikiwe, na hakika walifanikiwa kwa kuizuia AIRBUS 5H-TCH.

KUACHILIWA KWA NDEGE.

Mawakili wa serikali walipoungana na wale wa South Africa waliwasilisha hoja nyingi lakini mojawapo ni hii kuwa ndege imekamatwa kwa kutumia hukumu iliyokwishakufa.

Kwa kuzingatia hoja hii na kwa ushahidi, Jaji TWALA M.L akaridhika na akaona haja ya kuiachia ndege kwakuwa ilikamatwa kimakosa kwa kutumia hukumu mfu/ambayo haipo.

MAMBO MAWILI MUHIMU.

KWANZA
, je deni la mzungu limekufa . Jibu ni hapana deni bado lipo mpaka hapo serikali itakapoweza kufanikisha utaratibu wa kisheria wa kuliondoa, au kuamua kumlipa, au mzungu atumie taratibu za ndani kupata hela hiyo, au asamehe.

PILI, je serikali inaweza kupata chochote kwa mzungu. Jiu ni ndio,inaweza kupata chochote kama ifuatavyo;,

mosi, imeamriwa serikali ilipwe gharama zake zote za kuendeshea kesi,ikifuatilia italipwa.
Pili, inaweza kumfungulia mzungu mashtaka na kumdai fidia ya hasara zote alizosababisha ikiwamo kuiharibia hadhi na kuipotezea dira route ya Tanzania -South ambayo kwa ukweli itachukua mda kuirejesha na kuaminiwa kama ilivyokuwa.

Na hili linawezekana kwasababu mchakato mzima wa kuzuia ndege ulijawa na uongo/udanganyifu kwakuwa hawa walijua kabisa hukumu wanayokazia imekufa lakini kwa makusudi wakaendelea kufanya hivyo(abuse of court process).

Yote kwa yote hivyo ndivyo ilivyokua.
Ahsante sana,sasa nimeelewa!
 
Back
Top Bottom