Tajiri mpole
JF-Expert Member
- Apr 15, 2018
- 3,127
- 6,098
Kwahiyo Mzungu amedhulumiwa sindio?
Asante kwa taarifa mwanana mkuu.Kwa maoni yangu serikali ipige hesabu na imkabidhi Hermanus Steyn bili yake.Kwa haraka haraka mambo ya kuzingatia ni yafuatayo:-UKWELI KESI YA MZUNGU NA AIRBUS YETU.
Na Bashir Yakub.
+255 784 482 959.
KABLA YA KUKAMATWA KWA NDEGE.
Mwaka 1983 kupitia kifungu cha 3( 1 ) cha Sheria iliyoitwa Acquisition and Transfer Management Act,1983 makampuni sita ya mzungu STEYN ambayo ni Rift Valley Seed Ltd, Hashman Estate Ltd,Lente Estate Ltd,Loldebbis Ltd,Mayoka Estate Ltd na Tanganyika Air Ltd yalitaifishwa na serikali ya Tanzania.
Baadae mzungu Steyn alifungua malalamiko kwenye taasisi ya usuluhishi(arbitration) akiomba haki zake zote katika makampuni yote yaliyotaifishwa jambo ambalo alifanikiwa mbele ya Jaji R.V. Makaramba aliyeamua alipwe Dola za kimarekani 36,375,672.81(Dola milioni 36 na hizo nukta),imebidi niongeze sauti kwenye mabano.
Muda ukapita lakini baadae tarehe 3 / 5 / 2011 mzungu akaamua kuisajili hiyo hukumu ya taasisi ya usuluhishi katika mahakama kuu ya biashara ili iwe hukumu ya mahakama na hivyo iweze kutekelezeka.
Tarehe 17/7/ 2012 wakati akiwa katika mchakato wa kufuatilia utekelezaji, serikali na mzungu wakaingia makubaliano kuwa aachane na hiyo hukumu ili imlipe Dola 30,000,000 ( dola milioni 30) badala ya zile 36,375,672.81 zilizoamuliwa awali. Mzungu akakubali na makubaliano yakasainiwa, na makubaliano hayo yakasajiliwa na mahakama na hivyo yakasimama kama hukumu mpya ya mahakama.
Kufikia tarehe 3 / 3 / 2016 serikali ikawa tayari imemlipa mzungu Dola 20,099,155.12(dola milioni 20 na hizo nukta), bila shaka sauti inatosha.
Mwaka 2018 wakati malipo yanaendelea kidogo kidogo serikali ikasitisha malipo na kufungua maombi namba 168/2018 mahakama kuu ya biashara Tanzania. Ikawa inaiomba mahakama iifanyie marejeo hukumu ya taasisi ya usuluhishi iliyoamua mzungu kulipwa Dola 36,375,672.81 kwa hoja kuwa ilikuwa na mapungufu ya kisheria.
Tarehe 14 / 12 / 2018 Jaji B.K.Philip alitoa maamuzi kwa kukataa maombi ya serikali ya kuifanyia marejeo hukumu hiyo kwa hoja kuwa hukumu hiyo haipo na ilishakufa baada ya serikali na mzungu kuamua kuelewana na kuyasajili maelewano hayo mahakamani na hivyo kuyafanya maelewano hayo kuwa hukumu mpya.
Katika maombi hayo serikali iliwakilisha na Wakili Jackline Kinyasi wakati mzungu aliwakilishwa na Wakili Erick Ngmaryo.
Hoja kuu ya wakili Erick hapo mahakamani ilikuwa kwamba maamuzi ya taasisi ya usuluhishi(arbitration) yalishakufa na hayapo, na kuwa yaliuliwa na makubaliano kati ya mteja wake na serikali amapo makubaliano hayo nayo yalisajiliwa yakawa hukumu mpya ya mahakama, na hivyo serikali kuiomba mahakama iifanyie marejeo hukumu hiyo ya awali ni sawa na kuiomba irejee kitu ambacho kilishakufa na hakipo.
Mahakama ilikubali hoja hii ya Wakili Erick na kumpa ushindi kwa hoja hii. Kumbuka huyu Erick ndiye anayetajwa kuongoza mchakato wa kuzuiwa kwa Airbus South Africa.
KUKAMATWA KWA NDEGE.
Baada ya maombi ya serikali kutupwa kama tulivyoona hapo juu basi kumlipa mzungu kukakoma. Mzungu alikosa namna ya kukaza hukumu hapa Tanzania kwakuwa Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Serikali,1967 inakataza kukamata mali za serikali kama njia ya kukazia hukumu, lakini pia haitoi muda wa ukomo wa lini mtu aliyeishinda serikali awe amelipwa . Unasubiri mpaka iamue yenyewe kulipa na kwa muda inaotaka.
Baada ya kuyaona hayo mzungu akakimbilia South Africa mahakama ya Guateng na kufungua shauri namba 28994/2019 la kukazia hukumu akijua huko South mali za serikali ruksa kukamatwa katika kukazia hukumu.
Kumbuka kuna hukumu mbili. Ya kwanza ile iliyokufa ile ya taasisi ya usuluhishi, na ya pili ni hii iliyotokana na makubaliano kati ya mzungu na serikali ambayo iko hai.
Swali kwa mzungu na timu yake lilikuwa ni hukumu ipi ikaziwe hapo South kati ya hizi mbili.
Hii iliyotokana na makubaliano ambayo sasa ndo iko hai ilikuwa haiwezekani kukaziwa South Afrika kwakuwa mahakama ya south haitakuwa na mamlaka kutokana na kuwa tukio au makubaliano yalifanyika Tanzania na hivyo mahakama za Tanzania pekee ndizo zenye mamlaka.
Mzungu na timu yake kwa kulijua hilo wakaamua waachane na hiyo hukumu iliyo hai na kuamua kuomba kukazia hii iliyotokana na Taasisi ya usuluhishi ambayo mahakama ya South inaweza kuikazia kwakuwa ni ya kimataifa.
Lakini kumbuka hukumu hii sio hai tena kwakuwa iliuliwa na ile hukumu iliyotokana na makubaliano, na zaidi Wakili Erick na mzungu walishasema kuwa hukumu hiyo ilishakufa wakati wanapinga maombi ya serikali kama tulivyoona hapo juu na kwa hoja hiyohiyo wakashinda.
Kwahiyo wakaamua kuomba kukazia hukumu ambayo wanajua kabisa kuwa ilishakufa na hawakuthubutu kulisema hilo mahakamani ili wafanikiwe, na hakika walifanikiwa kwa kuizuia AIRBUS 5H-TCH.
KUACHILIWA KWA NDEGE.
Mawakili wa serikali walipoungana na wale wa South Africa waliwasilisha hoja nyingi lakini mojawapo ni hii kuwa ndege imekamatwa kwa kutumia hukumu iliyokwishakufa.
Kwa kuzingatia hoja hii na kwa ushahidi, Jaji TWALA M.L akaridhika na akaona haja ya kuiachia ndege kwakuwa ilikamatwa kimakosa kwa kutumia hukumu mfu/ambayo haipo.
MAMBO MAWILI MUHIMU.
KWANZA, je deni la mzungu limekufa . Jibu ni hapana deni bado lipo mpaka hapo serikali itakapoweza kufanikisha utaratibu wa kisheria wa kuliondoa, au kuamua kumlipa, au mzungu atumie taratibu za ndani kupata hela hiyo, au asamehe.
PILI, je serikali inaweza kupata chochote kwa mzungu. Jiu ni ndio,inaweza kupata chochote kama ifuatavyo;,
mosi, imeamriwa serikali ilipwe gharama zake zote za kuendeshea kesi,ikifuatilia italipwa.
Pili, inaweza kumfungulia mzungu mashtaka na kumdai fidia ya hasara zote alizosababisha ikiwamo kuiharibia hadhi na kuipotezea dira route ya Tanzania -South ambayo kwa ukweli itachukua mda kuirejesha na kuaminiwa kama ilivyokuwa.
Na hili linawezekana kwasababu mchakato mzima wa kuzuia ndege ulijawa na uongo/udanganyifu kwakuwa hawa walijua kabisa hukumu wanayokazia imekufa lakini kwa makusudi wakaendelea kufanya hivyo(abuse of court process).
Yote kwa yote hivyo ndivyo ilivyokua.
Basi mkuu ngoja tuone wazee wa mapingamizi wanaweza kushinda vipi hii kesi..Mkuu Lyamber, fifa nafikiri ni zaidi ya mambo hayo mawili. Kumbuka ATC wamekuwa wakusafirisha abiria kupitia reprotection arrangement na wataendelea kufanya hivyo mpaka narudi katika soko hilo kutokana na forward booking walizonazo. Nafikiri ATCL wakiwa na team nzuri ya mawakili kuna michuzi ya kutosha maana madai ni lukuki.
Nakubaliana na wewe.Asante sana kwa ufafanuzi huu maana kulikuwa na hii gap ya kati ya yaliyotokea 1992 hadi hivi juzi. Nilikuwa najiuliza sana ni nini kilisababisha serikali iache kumlipa. Lakini hata sasa inaonekana kuacha kumlipa kulifanywa bila nguvu au utaratibu wowote wa kisheria. Kama tulikuwa tunamlipa na tukaona kuwa hatutaki kumlipa tulienda mahakamani na hoja ikafutuliwa mbali. Kumbe jukumu letu ni kama nilivyosema mahali pengine. Tukae chini na huyu bwana tuamue kumlipa a "lump sum" ya kiasi fulani tumalizane; sisi tutasamehe gharama zote za kesi Afrika ya Kusini na yeye atatupa punguzo nono la deni tumlipe yaishe. Tumpe ofa ambayo hawezi kuikataa.
Mi ya kwangu imechakaa kwa kweli, bora zije mpya.Kwahiyo akitupa fidia kila mtanzania naweza kupata noah moja kama ile ya accacia?
Kwa kawaida mahakamani ni vielelezo. Mathalani kama ATCL wataweza kuwakilisha mapato yao kabla ya hiyo ndege kushikiliwa VS baada ya ndege kushikiliwa, na ikathibitika pasipo shaka kuwa walikuwa na mapato mazuri kabla ya kadhia hii na baada ya kadhia mapato yamepungua sana, watakuwa na haki ya kuomba fidia ya uharibifu wa jina katika biashara.Unajua fidia ya defamation kwa shirika kubwa kama hili ka Atcl ambalo ndio lilikwisha anza kutengeneza jina kisha kulibomoa?
kumbe kuwa mpiga "polishi na kuchoma mishikaki" kuna kupa uwezo wa kutafsiri Judge atakavyo amua na pia wakili wa mleta madai atakavyo leta madai yake.1. Gharama za mawakili hazitazidi $200,000
2.Parking charges hazifiki hata $20,000
3.Hao abiria walishafaulishwa kwenye ndege zingine zinazokuja Tanzania i.e Malawi Airlines na South African Airlines pia kwa siku husika labda walilzwa kwenye 3-5 star hotel swali ni je walikua wangapi na karatasi za malipo ziko wapi hio gharama haiwezi zidi $300,000
4. Hukumu ya kuharibu reputation ipo kwenye general damages maana huwezi ku prove hiki kitu unaweza pingwa kwamba hili shirika halina reputation nzuri maana lina cancellation nyingi na delays, hivyo ni swala ni la jaji husika kuamua
5. Hizo gharama za serikali kufatilia ndege haziwezi kufika $400,000
Kwaio mkuu kama unavyoona hizo gharama gazifiki hata $3,000,000
Kuna kitabu kimoja nlisoma kinaitwa "historia ya watu wa bara la afrika toka mwaka 1888" kama sijakosea, hawa watu weupe si wakutetea hata kidogo!!!Sasa kwanini asilipwe ela yake???, dawa ya deni kulipa, ukiangalia hapo mkorofi ni serikali kwa kutokumlipa huyo mzungu deni la haki kabisa ,deni lililosajiliwa na mahakama yetu wenyewe, kwanini serikali haitaki kumlipa huyo mzungu???, huyo mzungu ni haki yake kupigania haki yake.
Hivi watanzania na serikali yetu hatuoni aibu kwa serikali yetu kutotii hukumu ya mahakama yetu katika shauri hilo???. Ni aibu.
watakuwa bado wapo njiani, unajua SA na Bongo mbali hasa ikiwa ndege zote hazitaki kukuchukua, na yule "mkulima muhuni " naye kuja bongo itakuwa shida, sijui atakuja na shirika lipila ndege?Ndege yetu imerudi, wake mawakili wa kitsnzania waliomsaidia mzungu kukamata ndege wamerudi pia?
Kuna kitabu kimoja nlisoma kinaitwa "historia ya watu wa bara la afrika toka mwaka 1888" kama sijakosea, hawa watu weupe si wakutetea hata kidogo!!!
Asante kwa kutoa ufafanuzi, limeelekweka. Lakini kuna matatu ambayo nimeyaona;UKWELI KESI YA MZUNGU NA AIRBUS YETU.
Na Bashir Yakub.
+255 784 482 959.
KABLA YA KUKAMATWA KWA NDEGE.
Mwaka 1983 kupitia kifungu cha 3( 1 ) cha Sheria iliyoitwa Acquisition and Transfer Management Act,1983 makampuni sita ya mzungu STEYN ambayo ni Rift Valley Seed Ltd, Hashman Estate Ltd,Lente Estate Ltd,Loldebbis Ltd,Mayoka Estate Ltd na Tanganyika Air Ltd yalitaifishwa na serikali ya Tanzania.
Baadae mzungu Steyn alifungua malalamiko kwenye taasisi ya usuluhishi(arbitration) akiomba haki zake zote katika makampuni yote yaliyotaifishwa jambo ambalo alifanikiwa mbele ya Jaji R.V. Makaramba aliyeamua alipwe Dola za kimarekani 36,375,672.81(Dola milioni 36 na hizo nukta),imebidi niongeze sauti kwenye mabano.
Muda ukapita lakini baadae tarehe 3 / 5 / 2011 mzungu akaamua kuisajili hiyo hukumu ya taasisi ya usuluhishi katika mahakama kuu ya biashara ili iwe hukumu ya mahakama na hivyo iweze kutekelezeka.
Tarehe 17/7/ 2012 wakati akiwa katika mchakato wa kufuatilia utekelezaji, serikali na mzungu wakaingia makubaliano kuwa aachane na hiyo hukumu ili imlipe Dola 30,000,000 ( dola milioni 30) badala ya zile 36,375,672.81 zilizoamuliwa awali. Mzungu akakubali na makubaliano yakasainiwa, na makubaliano hayo yakasajiliwa na mahakama na hivyo yakasimama kama hukumu mpya ya mahakama.
Kufikia tarehe 3 / 3 / 2016 serikali ikawa tayari imemlipa mzungu Dola 20,099,155.12(dola milioni 20 na hizo nukta), bila shaka sauti inatosha.
Mwaka 2018 wakati malipo yanaendelea kidogo kidogo serikali ikasitisha malipo na kufungua maombi namba 168/2018 mahakama kuu ya biashara Tanzania. Ikawa inaiomba mahakama iifanyie marejeo hukumu ya taasisi ya usuluhishi iliyoamua mzungu kulipwa Dola 36,375,672.81 kwa hoja kuwa ilikuwa na mapungufu ya kisheria.
Tarehe 14 / 12 / 2018 Jaji B.K.Philip alitoa maamuzi kwa kukataa maombi ya serikali ya kuifanyia marejeo hukumu hiyo kwa hoja kuwa hukumu hiyo haipo na ilishakufa baada ya serikali na mzungu kuamua kuelewana na kuyasajili maelewano hayo mahakamani na hivyo kuyafanya maelewano hayo kuwa hukumu mpya.
Katika maombi hayo serikali iliwakilisha na Wakili Jackline Kinyasi wakati mzungu aliwakilishwa na Wakili Erick Ngmaryo.
Hoja kuu ya wakili Erick hapo mahakamani ilikuwa kwamba maamuzi ya taasisi ya usuluhishi(arbitration) yalishakufa na hayapo, na kuwa yaliuliwa na makubaliano kati ya mteja wake na serikali amapo makubaliano hayo nayo yalisajiliwa yakawa hukumu mpya ya mahakama, na hivyo serikali kuiomba mahakama iifanyie marejeo hukumu hiyo ya awali ni sawa na kuiomba irejee kitu ambacho kilishakufa na hakipo.
Mahakama ilikubali hoja hii ya Wakili Erick na kumpa ushindi kwa hoja hii. Kumbuka huyu Erick ndiye anayetajwa kuongoza mchakato wa kuzuiwa kwa Airbus South Africa.
KUKAMATWA KWA NDEGE.
Baada ya maombi ya serikali kutupwa kama tulivyoona hapo juu basi kumlipa mzungu kukakoma. Mzungu alikosa namna ya kukaza hukumu hapa Tanzania kwakuwa Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Serikali,1967 inakataza kukamata mali za serikali kama njia ya kukazia hukumu, lakini pia haitoi muda wa ukomo wa lini mtu aliyeishinda serikali awe amelipwa . Unasubiri mpaka iamue yenyewe kulipa na kwa muda inaotaka.
Baada ya kuyaona hayo mzungu akakimbilia South Africa mahakama ya Guateng na kufungua shauri namba 28994/2019 la kukazia hukumu akijua huko South mali za serikali ruksa kukamatwa katika kukazia hukumu.
Kumbuka kuna hukumu mbili. Ya kwanza ile iliyokufa ile ya taasisi ya usuluhishi, na ya pili ni hii iliyotokana na makubaliano kati ya mzungu na serikali ambayo iko hai.
Swali kwa mzungu na timu yake lilikuwa ni hukumu ipi ikaziwe hapo South kati ya hizi mbili.
Hii iliyotokana na makubaliano ambayo sasa ndo iko hai ilikuwa haiwezekani kukaziwa South Afrika kwakuwa mahakama ya south haitakuwa na mamlaka kutokana na kuwa tukio au makubaliano yalifanyika Tanzania na hivyo mahakama za Tanzania pekee ndizo zenye mamlaka.
Mzungu na timu yake kwa kulijua hilo wakaamua waachane na hiyo hukumu iliyo hai na kuamua kuomba kukazia hii iliyotokana na Taasisi ya usuluhishi ambayo mahakama ya South inaweza kuikazia kwakuwa ni ya kimataifa.
Lakini kumbuka hukumu hii sio hai tena kwakuwa iliuliwa na ile hukumu iliyotokana na makubaliano, na zaidi Wakili Erick na mzungu walishasema kuwa hukumu hiyo ilishakufa wakati wanapinga maombi ya serikali kama tulivyoona hapo juu na kwa hoja hiyohiyo wakashinda.
Kwahiyo wakaamua kuomba kukazia hukumu ambayo wanajua kabisa kuwa ilishakufa na hawakuthubutu kulisema hilo mahakamani ili wafanikiwe, na hakika walifanikiwa kwa kuizuia AIRBUS 5H-TCH.
KUACHILIWA KWA NDEGE.
Mawakili wa serikali walipoungana na wale wa South Africa waliwasilisha hoja nyingi lakini mojawapo ni hii kuwa ndege imekamatwa kwa kutumia hukumu iliyokwishakufa.
Kwa kuzingatia hoja hii na kwa ushahidi, Jaji TWALA M.L akaridhika na akaona haja ya kuiachia ndege kwakuwa ilikamatwa kimakosa kwa kutumia hukumu mfu/ambayo haipo.
MAMBO MAWILI MUHIMU.
KWANZA, je deni la mzungu limekufa . Jibu ni hapana deni bado lipo mpaka hapo serikali itakapoweza kufanikisha utaratibu wa kisheria wa kuliondoa, au kuamua kumlipa, au mzungu atumie taratibu za ndani kupata hela hiyo, au asamehe.
PILI, je serikali inaweza kupata chochote kwa mzungu. Jiu ni ndio,inaweza kupata chochote kama ifuatavyo;,
mosi, imeamriwa serikali ilipwe gharama zake zote za kuendeshea kesi,ikifuatilia italipwa.
Pili, inaweza kumfungulia mzungu mashtaka na kumdai fidia ya hasara zote alizosababisha ikiwamo kuiharibia hadhi na kuipotezea dira route ya Tanzania -South ambayo kwa ukweli itachukua mda kuirejesha na kuaminiwa kama ilivyokuwa.
Na hili linawezekana kwasababu mchakato mzima wa kuzuia ndege ulijawa na uongo/udanganyifu kwakuwa hawa walijua kabisa hukumu wanayokazia imekufa lakini kwa makusudi wakaendelea kufanya hivyo(abuse of court process).
Yote kwa yote hivyo ndivyo ilivyokua.
potelea mbali atulipe fidia tuHauwezi kufanya kitu kama hicho maana kwa vyovyote vile gharama za kuipaki ndege SA kwa siku zote haiwezekani wala gharama za hao mawakili wa huko SA haiwezi kufika $10,000,000 tangu siku ndege imeshikiliwa hadi inaruhusiwa..sheria ni tamu sana kama unaijua..
Baridi tu..mkuu ngoja tuone wazee wa mapingamizi watafika wapipotelea mbali atulipe fidia tu