Ukweli kesi ya mzungu na Airbus yetu

Ukweli kesi ya mzungu na Airbus yetu

Shangazi hodari wa kesi na mjuzi wa sheria bado anadai 1 billion kwa yulee..ua alishalipwa
Mkuu haya madini. Shangazi alileta uongo kule twitter mpaka sisi ma layman tukamuamini. Na alijigamba kabisa kumbe longolongo. Yeye alileta hadithi ati kesi ilikua kati ya huyu mzungu na aliyemkodisha na kwamba alishalipwa ila anataka kula huku na huku.

Leo nimeamini ndiyo maana shangazi hua hashindi kesi. Wenzetu wanadhani madini ni kuzungumuza kiingereza
 
Unajua fidia ya defamation kwa shirika kubwa kama hili ka Atcl ambalo ndio lilikwisha anza kutengeneza jina kisha kulibomoa?
Nakuuliza katika ku award damages kuna speficic damages na general damages specific damages lazima ziwe proved je unaweza prove vipi good will ya shirika kama hilo la ATCL kwamba linapata faida kiasi fulani ili uweze kukokotoa hasara..wakati ukaguzi wake wa mahesabu ni classified..?
 
Dhuruma ni mbaya mlipeni Mzungu wa watu..ni kazi ya mikono yake, acheni janja janja.
 
Sasa kwanini asilipwe ela yake???, dawa ya deni kulipa, ukiangalia hapo mkorofi ni serikali kwa kutokumlipa huyo mzungu deni la haki kabisa ,deni lililosajiliwa na mahakama yetu wenyewe, kwanini serikali haitaki kumlipa huyo mzungu???, huyo mzungu ni haki yake kupigania haki yake.

Hivi watanzania na serikali yetu hatuoni aibu kwa serikali yetu kutotii hukumu ya mahakama yetu katika shauri hilo???. Ni aibu.
Mahakama kipindi kile zilikua corrupt,walikua wanapitisha hukumu halafu wanazichukua kwa mlango wa nyuma kwa kushirikiana na mzungu,michezo hii imefanyika mingi sana kwa mawakili wa serikali kuzembea kwa makusudi ,kisha mahakama kumpa ushindi yule atakae wagawia .
Serikali ilipoteza kodi nyingi za wananchi kwa mtindo huu.
Magufuli alipoingia ndio maana akagoma kulipa ili.kesi ipitiwe upya tena ndpo kimbembe kilipoanzia
 
Nakuuliza katika ku award damages kuna speficic damages na general damages specific damages lazima ziwe proved je unaweza prove vipi good will ya shirika kama hilo la ATCL kwamba linapata faida kiasi fulani ili uweze kukokotoa hasara..wakati ukaguzi wake wa mahesabu ni classified..?
Mkuu subiri,yote yatajulikana,wote wamejipanga,kuonuyeshana umwamba,na uzuri kesi inatafanyikia nchini
 
UKWELI KESI YA MZUNGU NA AIRBUS YETU.

Na Bashir Yakub.
+255 784 482 959.

Yote kwa yote hivyo ndivyo ilivyokua.

Asante sana kwa ufafanuzi huu maana kulikuwa na hii gap ya kati ya yaliyotokea 1992 hadi hivi juzi. Nilikuwa najiuliza sana ni nini kilisababisha serikali iache kumlipa. Lakini hata sasa inaonekana kuacha kumlipa kulifanywa bila nguvu au utaratibu wowote wa kisheria. Kama tulikuwa tunamlipa na tukaona kuwa hatutaki kumlipa tulienda mahakamani na hoja ikafutuliwa mbali. Kumbe jukumu letu ni kama nilivyosema mahali pengine. Tukae chini na huyu bwana tuamue kumlipa a "lump sum" ya kiasi fulani tumalizane; sisi tutasamehe gharama zote za kesi Afrika ya Kusini na yeye atatupa punguzo nono la deni tumlipe yaishe. Tumpe ofa ambayo hawezi kuikataa.
 
Kesi hii toka 1983, zama za Mwalimu, huyu nasikia naye alikuwa mgumu kulipa hadi meli yetu ikakamatwa huko Holland kwa amri ya mahakama ikanadiwa na huyo Mzungu akalipwa sehemu ya madai yake, ikaja zama za mzee Ruksa, ikaja zama za Mkapa (uwazi na ukweli), ikaja zama za Mzee wa msoga huyu nasikia alilipa kidogo, sasa imekuja zama za Uncle Magu (hapa kazi tu hakuna kulipa !!?).

Sasa, kama meli yetu ilishikwa na kuuzwa ili mzungu alipwe kwanini leo Ndege isishikwe??!!.

Dawa ya deni ni kulipa, kama Mahakama ni corrupt sasa hiyo ni juu yetu, kinachoangaliwa ni hukumu iliyosajiliwa na mahakama zetu, siyo mahakama za kigeni. Upo hapo??!!🤪🤣🤣
 
Sasa kwanini asilipwe ela yake???, dawa ya deni kulipa, ukiangalia hapo mkorofi ni serikali kwa kutokumlipa huyo mzungu deni la haki kabisa ,deni lililosajiliwa na mahakama yetu wenyewe, kwanini serikali haitaki kumlipa huyo mzungu???, huyo mzungu ni haki yake kupigania haki yake.

Hivi watanzania na serikali yetu hatuoni aibu kwa serikali yetu kutotii hukumu ya mahakama yetu katika shauri hilo???. Ni aibu.
Hapa ndipo walakini wa sheria ulipo. Kwamba unapeleka madai dhidi ya serikali mahakamani. Unaishinda serikali kesi. Kisha hiyo Serikali ndiyo inaamua ukulipe inavyotaka yenyewe!!!?
Hapa kuna hitilafu mahali. Yawezekana sheria imeiachia serikali Uhuru mpana katika suala la malipo ya madai kwa sababu za kibajeti. Kwamba mdai anaweza kuwa anaidai serikali fedha inayoizidi bajeti ya seikali kwa Mwaka au miaka kadhaa, lakini vyovyoye iwavyo ni muhimu sheria iweke ukomo wa utekelezaji wa hukumu ya aina hii ya Bwana Steyn.
Mwisho ipo haja ya sheria kuwakinga wadai dhidi ya serikali wasiathiriwe na maamuzi ya watawala wenye hila na roho ya kudhulumu Mali za wengine kwa kutumia fimbo ya madaraka.
Naisema hii ya mwisho kwa sababu za tetesi kuwa Mkulima alitishwa na hivyo kukimbia kwa hofu ya kutaka kutangazwa: 'persona non grata' na serikali.
 
Sasa kwanini asilipwe ela yake???, dawa ya deni kulipa, ukiangalia hapo mkorofi ni serikali kwa kutokumlipa huyo mzungu deni la haki kabisa ,deni lililosajiliwa na mahakama yetu wenyewe, kwanini serikali haitaki kumlipa huyo mzungu???, huyo mzungu ni haki yake kupigania haki yake.

Hivi watanzania na serikali yetu hatuoni aibu kwa serikali yetu kutotii hukumu ya mahakama yetu katika shauri hilo???. Ni aibu.
Hapa ndipo walakini wa sheria ulipo. Kwamba unapeleka madai dhidi ya serikali mahakamani. Unaishinda serikali kesi. Kisha hiyo Serikali ndiyo inaamua ukulipe inavyotaka yenyewe!!!?
Hapa kuna hitilafu mahali. Yawezekana sheria imeiachia serikali Uhuru mpana katika suala la malipo ya madai kwa sababu za kibajeti. Kwamba mdai anaweza kuwa anaidai serikali fedha inayoizidi bajeti ya seikali kwa Mwaka au miaka kadhaa, lakini vyovyoye iwavyo ni muhimu sheria iweke ukomo wa utekelezaji wa hukumu ya aina hii ya Bwana Steyn.
Mwisho ipo haja ya sheria kuwakinga wadai dhidi ya serikali wasiathiriwe na maamuzi ya watawala wenye hila na roho ya kudhulumu Mali za wengine kwa kutumia fimbo ya madaraka.
Naisema hii ya mwisho kwa sababu za tetesi kuwa Mkulima alitishwa na hivyo kukimbia kwa hofu ya kutaka kutangazwa: 'persona non grata' na serikali.
 
Mahakama kipindi kile zilikua corrupt,walikua wanapitisha hukumu halafu wanazichukua kwa mlango wa nyuma kwa kushirikiana na mzungu,michezo hii imefanyika mingi sana kwa mawakili wa serikali kuzembea kwa makusudi ,kisha mahakama kumpa ushindi yule atakae wagawia .
Serikali ilipoteza kodi nyingi za wananchi kwa mtindo huu.
Magufuli alipoingia ndio maana akagoma kulipa ili.kesi ipitiwe upya tena ndpo kimbembe kilipoanzia
Ugoro huo umeandika
 
UKWELI KESI YA MZUNGU NA AIRBUS YETU.

Na Bashir Yakub.
+255 784 482 959.

KABLA YA KUKAMATWA KWA NDEGE.

Mwaka 1983 kupitia kifungu cha 3( 1 ) cha Sheria iliyoitwa Acquisition and Transfer Management Act,1983 makampuni sita ya mzungu STEYN ambayo ni Rift Valley Seed Ltd, Hashman Estate Ltd,Lente Estate Ltd,Loldebbis Ltd,Mayoka Estate Ltd na Tanganyika Air Ltd yalitaifishwa na serikali ya Tanzania.

Baadae mzungu Steyn alifungua malalamiko kwenye taasisi ya usuluhishi(arbitration) akiomba haki zake zote katika makampuni yote yaliyotaifishwa jambo ambalo alifanikiwa mbele ya Jaji R.V. Makaramba aliyeamua alipwe Dola za kimarekani 36,375,672.81(Dola milioni 36 na hizo nukta),imebidi niongeze sauti kwenye mabano.

Muda ukapita lakini baadae tarehe 3 / 5 / 2011 mzungu akaamua kuisajili hiyo hukumu ya taasisi ya usuluhishi katika mahakama kuu ya biashara ili iwe hukumu ya mahakama na hivyo iweze kutekelezeka.

Tarehe 17/7/ 2012 wakati akiwa katika mchakato wa kufuatilia utekelezaji, serikali na mzungu wakaingia makubaliano kuwa aachane na hiyo hukumu ili imlipe Dola 30,000,000 ( dola milioni 30) badala ya zile 36,375,672.81 zilizoamuliwa awali. Mzungu akakubali na makubaliano yakasainiwa, na makubaliano hayo yakasajiliwa na mahakama na hivyo yakasimama kama hukumu mpya ya mahakama.

Kufikia tarehe 3 / 3 / 2016 serikali ikawa tayari imemlipa mzungu Dola 20,099,155.12(dola milioni 20 na hizo nukta), bila shaka sauti inatosha.

Mwaka 2018 wakati malipo yanaendelea kidogo kidogo serikali ikasitisha malipo na kufungua maombi namba 168/2018 mahakama kuu ya biashara Tanzania. Ikawa inaiomba mahakama iifanyie marejeo hukumu ya taasisi ya usuluhishi iliyoamua mzungu kulipwa Dola 36,375,672.81 kwa hoja kuwa ilikuwa na mapungufu ya kisheria.

Tarehe 14 / 12 / 2018 Jaji B.K.Philip alitoa maamuzi kwa kukataa maombi ya serikali ya kuifanyia marejeo hukumu hiyo kwa hoja kuwa hukumu hiyo haipo na ilishakufa baada ya serikali na mzungu kuamua kuelewana na kuyasajili maelewano hayo mahakamani na hivyo kuyafanya maelewano hayo kuwa hukumu mpya.

Katika maombi hayo serikali iliwakilisha na Wakili Jackline Kinyasi wakati mzungu aliwakilishwa na Wakili Erick Ngmaryo.

Hoja kuu ya wakili Erick hapo mahakamani ilikuwa kwamba maamuzi ya taasisi ya usuluhishi(arbitration) yalishakufa na hayapo, na kuwa yaliuliwa na makubaliano kati ya mteja wake na serikali amapo makubaliano hayo nayo yalisajiliwa yakawa hukumu mpya ya mahakama, na hivyo serikali kuiomba mahakama iifanyie marejeo hukumu hiyo ya awali ni sawa na kuiomba irejee kitu ambacho kilishakufa na hakipo.

Mahakama ilikubali hoja hii ya Wakili Erick na kumpa ushindi kwa hoja hii. Kumbuka huyu Erick ndiye anayetajwa kuongoza mchakato wa kuzuiwa kwa Airbus South Africa.

KUKAMATWA KWA NDEGE.

Baada ya maombi ya serikali kutupwa kama tulivyoona hapo juu basi kumlipa mzungu kukakoma. Mzungu alikosa namna ya kukaza hukumu hapa Tanzania kwakuwa Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Serikali,1967 inakataza kukamata mali za serikali kama njia ya kukazia hukumu, lakini pia haitoi muda wa ukomo wa lini mtu aliyeishinda serikali awe amelipwa . Unasubiri mpaka iamue yenyewe kulipa na kwa muda inaotaka.

Baada ya kuyaona hayo mzungu akakimbilia South Africa mahakama ya Guateng na kufungua shauri namba 28994/2019 la kukazia hukumu akijua huko South mali za serikali ruksa kukamatwa katika kukazia hukumu.

Kumbuka kuna hukumu mbili. Ya kwanza ile iliyokufa ile ya taasisi ya usuluhishi, na ya pili ni hii iliyotokana na makubaliano kati ya mzungu na serikali ambayo iko hai.

Swali kwa mzungu na timu yake lilikuwa ni hukumu ipi ikaziwe hapo South kati ya hizi mbili.

Hii iliyotokana na makubaliano ambayo sasa ndo iko hai ilikuwa haiwezekani kukaziwa South Afrika kwakuwa mahakama ya south haitakuwa na mamlaka kutokana na kuwa tukio au makubaliano yalifanyika Tanzania na hivyo mahakama za Tanzania pekee ndizo zenye mamlaka.

Mzungu na timu yake kwa kulijua hilo wakaamua waachane na hiyo hukumu iliyo hai na kuamua kuomba kukazia hii iliyotokana na Taasisi ya usuluhishi ambayo mahakama ya South inaweza kuikazia kwakuwa ni ya kimataifa.

Lakini kumbuka hukumu hii sio hai tena kwakuwa iliuliwa na ile hukumu iliyotokana na makubaliano, na zaidi Wakili Erick na mzungu walishasema kuwa hukumu hiyo ilishakufa wakati wanapinga maombi ya serikali kama tulivyoona hapo juu na kwa hoja hiyohiyo wakashinda.

Kwahiyo wakaamua kuomba kukazia hukumu ambayo wanajua kabisa kuwa ilishakufa na hawakuthubutu kulisema hilo mahakamani ili wafanikiwe, na hakika walifanikiwa kwa kuizuia AIRBUS 5H-TCH.

KUACHILIWA KWA NDEGE.

Mawakili wa serikali walipoungana na wale wa South Africa waliwasilisha hoja nyingi lakini mojawapo ni hii kuwa ndege imekamatwa kwa kutumia hukumu iliyokwishakufa.

Kwa kuzingatia hoja hii na kwa ushahidi, Jaji TWALA M.L akaridhika na akaona haja ya kuiachia ndege kwakuwa ilikamatwa kimakosa kwa kutumia hukumu mfu/ambayo haipo.

MAMBO MAWILI MUHIMU.

KWANZA
, je deni la mzungu limekufa . Jibu ni hapana deni bado lipo mpaka hapo serikali itakapoweza kufanikisha utaratibu wa kisheria wa kuliondoa, au kuamua kumlipa, au mzungu atumie taratibu za ndani kupata hela hiyo, au asamehe.

PILI, je serikali inaweza kupata chochote kwa mzungu. Jiu ni ndio,inaweza kupata chochote kama ifuatavyo;,

mosi, imeamriwa serikali ilipwe gharama zake zote za kuendeshea kesi,ikifuatilia italipwa.
Pili, inaweza kumfungulia mzungu mashtaka na kumdai fidia ya hasara zote alizosababisha ikiwamo kuiharibia hadhi na kuipotezea dira route ya Tanzania -South ambayo kwa ukweli itachukua mda kuirejesha na kuaminiwa kama ilivyokuwa.

Na hili linawezekana kwasababu mchakato mzima wa kuzuia ndege ulijawa na uongo/udanganyifu kwakuwa hawa walijua kabisa hukumu wanayokazia imekufa lakini kwa makusudi wakaendelea kufanya hivyo(abuse of court process).

Yote kwa yote hivyo ndivyo ilivyokua.
Lakini serikali haiwezi kujivunia dhulama kwa ujanja was kisheria, hili litaiondolea serikali credibility, haitaaminika kimataifa na kwa wawekezaji
 
Asante sana kwa ufafanuzi huu maana kulikuwa na hii gap ya kati ya yaliyotokea 1992 hadi hivi juzi. Nilikuwa najiuliza sana ni nini kilisababisha serikali iache kumlipa. Lakini hata sasa inaonekana kuacha kumlipa kulifanywa bila nguvu au utaratibu wowote wa kisheria. Kama tulikuwa tunamlipa na tukaona kuwa hatutaki kumlipa tulienda mahakamani na hoja ikafutuliwa mbali. Kumbe jukumu letu ni kama nilivyosema mahali pengine. Tukae chini na huyu bwana tuamue kumlipa a "lump sum" ya kiasi fulani tumalizane; sisi tutasamehe gharama zote za kesi Afrika ya Kusini na yeye atatupa punguzo nono la deni tumlipe yaishe. Tumpe ofa ambayo hawezi kuikataa.
Ha! Ha! Mwanakijiji, kwa kiburi hiki cha watawala hawa!!!? Wakae na beberu na kumalizana naye!!? Tusubiri!!!
 
Huu ukweli wako ungeuandika kabla ya Tz kushinda kesi ungeeleweka sana, lakini sio unasubiri kesi imeisha ndo unaleta habari yako hapa.
 
Back
Top Bottom