Ukweli hausemwi. Kilimo cha Parachichi ni kigumu sana na pesa yake ni ndogo

mwanyaluke

JF-Expert Member
Jan 22, 2015
473
1,448
Nimefanya kilimo cha parachichi kwa miaka nane sasa, nilichokiona ni haya;

1. Kilimo kina mzunguko wake ni mdogo parachichi huzaa kidogo kidogo kadri miaka inavyoenda, unatumia million 10 unapata million mbili.
2. Bei hazijadiliki anayeamua ni mnunuzi unless uwe na mtaji mkubwa ambayo unakuruhusu ku export mwenyewe, na uwe na uwezo wa kuwa na cold room Ili zikikomaa uchume uzihifadhi kama bei hueilewi kwa kipindi hicho (hii mitaji watanzania wengi hatuna). 3. Management ya parachichi ni ngumu sana linahitaji maji kidogo (hapa unaweza manage kumwagilia) linahitaji mbolea za chumvi na mbolea za majani, sumu. Kila nk kwa kiasi kidogo, linahitaji muda Kwa wingi, upatikanaji wa Samadi ni mtihani sana (wengi wamejikuta parachichi zimedumaa na wengine wanazalisha reject kwa wingi) kisa tu wameshindwa kuwa na Samadi, udhibiti wa nyasi (ukweli ni kuwa Ili miti iwe Bora unahitaji kulima badala ya kufyeka nyasi)

Nimefanya observation shambani kwangu panapolimwa pana matokeo kuliko panapofyekwa, distance kati ya mti na mti inamua sana miti iliyokaribu inasumbua sana na mingi huwa haizai vizuri. Hizi issue zimefanya watu tukimbie mashamba yetu, hata kiwango cha pesa kinachotajwa wengi hawapati ni figure za uwongo Ili kujifariji, njoo na hoja zako kupinga zangu hapo juu, zangu ni hizo.

Nashauri kama una pesa zako kidogo lima mazao ya chakula tu viazi, mpunga, mahindi nk hivi vinalipa. Huku pesa ipo na kama location ulipo ni nzuri lima mazao yanayohifadhika like kahawa, miaka miwili inazaa, management yake rahisi. Nalima kahawa makete pia ni mwaka wa tatu tayari nimeanza kuvuna.

NB: Mazao ya chakula ndio kila kitu hizi nyingine tabu umezitafuta.
 
Nadhani ni mwaka juzi, wilaya ya Rungwe walipatapata kidogo kilo ilikua bei.

Ila mwaka huu ni kulia na kisaga meno, unaambiwa parachichi linauzwa kwa viroba na sio kilo tena.

Parachichi sio kilimo cha kukimbilia saivi, wengi walifyeka mapori walime parachichi ila ndo ivo wamepigwa za uso.
 
na semaje nasema hivi kitu kinapokuwa amplified kuna watu wanataka kupigwa kwa kuuziwa mbegu au mashamba..ila ukweli umejificha hakuna mtu atakupa siri ya bishara au mradi wake ili mfanikiwe pamoja...kuna husle ambazo atataka na wewe uingie uone ambazo huwa hazisemwi...mpunga niliwahi kulima nikatubu(kazi kweli kweli kama huna rasilimali watu na nyenzo)Mahindi hayapigiwi debe lakini ndio kitu ukilima una uhakika wa kuuza japo bei huwa chini ila ukiweza kusindika au kuhifadhi kwa muda sahihi wa kuuza unatoboa....kilimo cha miti ,katani ni fusra kubwa sana lakini huwekuta watu wanahamasishana kulima hizo mambo oxfarm walileta kilimo hicho kishapuu shy baada ya kuona ukame unazidi na zao ambalo litaweza kumkomboa mwanakijiji...waliokomaa nacho wanavuna hela vizuri tu ..ila mwanakijiji kumwambia heka yake moja aache kubet mazao ya chakula aweke katani ni ngumu labda wangekuwa wanapewa ruzuku ya chakula...Vinavyolipa havisemwi hovyo
 
Katika Mazao yote Ya Matunda yanayolimwa Tanzania, Wakulima wa Machungwa wanapiga hela kama Mkulima atakua Mtulivu, kilimo hiki Hakina siasa, Mtu mwenye heka Moja ya michungwa aina ya Valencia imbayo imechanganya kuzaa, kupata kuanzia milioni 6 ni mambo la kawaida, tunachoomba Mungu siasa isije ikaingia huku ,Tukaanza kuundiwa bodi,
Watu wanauza mpaka Tsh 100 kwa chungwa Moja bei ya Shamba kama unakua na Uvumilivu na unauza huku unaringa
 
Ukitumia akili kwenye jambo lolote unalofanya utakwepa mishale kama hii. Nimesoma na kufuatilia sana parachichi kwa China na nimekubali ni biashara ngumu sana.
1. Soko lake kubwa hasa hizo Hass ni China ambapo wao soko lao linapanda na kushuka kutokana na supply wanayopata kutoka Mexico, Kenya, Australia na zaidi ya nusu kutoka Peru. Ikitokea ni msimu wa Peru huko kwingineko bei inashuka sana, muda wa kupiga hela ni pale nchi nyingine zinapokuwa sio msimu.
China iko busy kujitosheleza kwenye parachichi kwahiyo soko litazidi kupungua, na uzuri wa China ni nchi kubwa yenye usawa wa bahari tofauti sana kila eneo hivyo kila upande unaweza zalisha kwa msimu wake na zikawa sokoni mwaka mzima.

2. Teknolojia hatuna. Unavuna parachichi unapakia kwenye fuso utamuuzia nani uko nje? Hamna cold rooms, hamna grading, hakuna refrigerated trucks, hamna kupima quality, water content, protein, texture, ile nyama ya ndani, mbolea haipimwi, ardhi wanatifua tu hata hawajui ardhi gani ina nini na inakosa nini. Tunaenda kienyeji.

3. Serikali inasubiri kutoza ushuru na kodi, yenyewe hata haijui hiyo biashara na kilimo chake inafanyikaje. Hakuna support kabisa sababu parachichi zikiachwa nchi haitokufa njaa.

4. Ni zao lenye usumbufu na linataka mtaji mkubwa. Wakati huo haliuziki ndani, ukikosa soko la nje ukauza ndani unakula hasara kutokana na gharama kubwa za uendeshaji.

5. Ni zao gumu sana kuuzwa, yani hawa walanguzi wetu wakienda nje uko wanapigwa za uso kirahisi sana. Unatafuta certifications za ubora na kila kitu unapeleka msimu huu, msimu ujao unaweka mtaji wote then Wachina wanapima wanakuta water content kubwa kisa mvua zilizidi uko Niombe. Zinamwagwa, huyo mfanyabiashara atarudi?
Mwaka juzi Wakenya walizuiwa na TFDA ya China kwamba kuna mlipuko wa fruit flies parachichi zao zinaenda na mayai yake. Wakaambiwa ukitaka kuuza menya uuze ile nyama ya ndani. Sasa process ya kumenya na kuuza nyama ya ndani alafu hiyo nyama isiwe nyeusi hata kidogo sio kazi ya kitoto.

Haya yote nimeyajua nikiwa sina mpango wa kulima, ningetaka kulima ningejua mengi zaidi. Sasa mkulima yeye akisikia kwenye redio anaamka na kufyeka eneo atengeneze shamba. Content creators ile ndio kazi yao, kuongea. Usikubali kushikwa masikio
 
Back
Top Bottom