Ukweli gani mgumu umekubaliana nao baada ya kuwa mtu mzima?

Binti wa zamani

Platinum Member
Joined
Nov 19, 2011
Posts
11,763
Reaction score
27,149
adult (1) copy.png

Acha nianze:

  1. Maisha hayana huruma - unaweza kufanya kila kitu kwa ubora na kama inavyotakiwa na bado ukafeli.

  2. Ukimya ni jibu - jifunze kunyamaza na kucontrol hisia zako, itakupunguzia matatizo mengi ambayo si ya lazima.

  3. Watu watakuja na kuondoka kwenye maisha yako, ni mzunguko wa asili. Usije kufanya kosa la kung’ang’ania mtu ambaye muda wake kwenye maisha yako umekwisha.

  4. Vifo vya watu unaowapenda, vitakuumiza kwa muda mrefu kuliko utakavyorajia.

  5. Pesa haitakupa furaha ila itakuheshimisha na kukurahisishia maisha.

  6. Ukiwa mtoto wa kwanza kwenye familia kubwa, maisha yako hayatokua na mapumziko, utategemewa na kila mtu anayekuzunguka mpaka kifo chako.

  7. Familia ambazo wazazi wetu wanatokea (wajomba, mababa wakubwa, mama wadogo, mashangazi etc.) ni watu wa kuishi nao kwa busara sana au kukaa nao mbali.

Endelea ....................
 
Kwa wasichana / wanawake - Mtu yoyote anayekuja kwenye maisha yako na kuyafanya yawe magumu badala ya kukupa afadhali, achana naye.

View attachment 3559757
Cc: Seran , Mallerina
Hapo tu ndio ninapokupendea dada ake😍

Kwakweli sikufichi, mtu wa kuniongezea ugumu kwenye maisha yangu sitaki kabisa anisogelee! Magumu niliyonayo yananitosha sana🤝🏽
 
1. Dunia Haina huruma kwa mwanamke asiyekuwa na kipato chake
2. Kosea pote usikosee kuoa/kuolewa haijalishi ni Muslim/Christian
3. Kuna watu watakuja na wataondoka na hutakuwa na uwezo wa kuwauzia (marafiki, business partners)
4. Kukaa kimya ni Bora zaidi kuliko kujieleza ( ukija ukasema 1+1 = 200 natakiwa kukuunga mkono ili maisha yaendelee)
 
View attachment 3559754

Acha nianze:

  1. Maisha hayana huruma - unaweza kufanya kila kitu kwa ubora na kama inavyotakiwa na bado ukafeli.

  2. Ukimya ni jibu - jifunze kunyamaza na kucontrol hisia zako, itakupunguzia matatizo mengi ambayo si ya lazima.

  3. Watu watakuja na kuondoka kwenye maisha yako, ni mzunguko wa asili. Usije kufanya kosa la kung’ang’ania mtu ambaye muda wake kwenye maisha yako umekwisha.

  4. Vifo vya watu unaowapenda, vitakuumiza kwa muda mrefu kuliko utakavyorajia.

  5. Pesa haikutokupa furaha ila itakuheshimisha na kukurahisishia maisha.

  6. Ukiwa mtoto wa kwanza wa familia kubwa, maisha yako hayana mapumziko, utategemewa na kila mtu anayekuzunguka mpaka kifo chako.

  7. Familia ambazo wazazi wetu wanatokea (wajomba, mababa wakubwa, mama wadogo, mashangazi etc.) ni watu wa kuishi nao kwa busara sana au kukaa nao mbali.

Endelea ....................
Upwiru is not an issue...kupata mwanamke ni kitu rahisi sana kuliko nilivyofikiri awali.
 
No. 05
Nimegundua watu wanakuja kwenye maisha yako kwa sababu fulani, na sio wote watabaki haijalishi kuna sababu au hakuna! Kuna watu mtaclick vizuri tu lakini wataondoka na wengine watabaki! Nimejifunza kuelewa hii hali na wala hainisumbui!

I choose to let things flow on own, no hard feelings 🤞🏾
 
1. Dunia Haina huruma kwa mwanamke asiyekuwa na kipato chake
2. Kosea pote usikosee kuoa/kuolewa haijalishi ni Muslim/Christian
3. Kuna watu watakuja na wataondoka na hutakuwa na uwezo wa kuwauzia (marafiki, business partners)
4. Kukaa kimya ni Bora zaidi kuliko kujieleza ( ukija ukasema 1+1 = 200 natakiwa kukuunga mkono ili maisha yaendelee)
Ahsante
 
No. 05
Nimegundua watu wanakuja kwenye maisha yako kwa sababu fulani, na sio wote watabaki haijalishi kuna sababu au hakuna! Kuna watu mtaclick vizuri tu lakini wataondoka na wengine watabaki! Nimejifunza kuelewa hii hali na wala hainisumbui!

I choose to let things flow on own, no hard feelings 🤞🏾
Good
 
Back
Top Bottom