Ukutiiiiii ukutiiii......

Mtazamaji

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
5,937
1,437
jamani ehee tukumbushane enzi zile ile zile za chekechea darasa la kwnaza la pili mpaka tatu.

Ile michezo ya
  • Ukuuuuuti ukutiiiiiiiiiiii wa mnaziiiiii wa mnaziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii........ nimesahu hapo sijuie uliendeleaje
  • Kile kitabu cha Juma na Rosa unakumbuka hadithi gani
  • Au kile kitabu Neema Musa baraka Mr and Mrs Daudi.
  • mchezo mwingine wa kombolela au kibaba baba na kimama mamam.........
  • Siku ya kufunga shule kuna mchezo wa chamuagano

Unaumbuka nini wakati wa umri wa miaka 5 - 8 ?
 
Kioo kiooo..alikivunja naaaani?!
Simjui simjui wa mwisho akamatwe atiwe hatiaaaani!!


Watoto wangu ehhhh...
EHHHHHHH
Mimi baba yenu...sina nguvu tena za kuua simba.Simba ni mkali...alia mama...akaua kaka...akau mjomba.
Watoto wangu njoooooooni!
 
Kioo kiooo..alikivunja naaaani?!
Simjui simjui wa mwisho akamatwe atiwe hatiaaaani!!


Watoto wangu ehhhh...
EHHHHHHH
Mimi baba yenu...sina nguvu tena za kuua simba.Simba ni mkali...alia mama...akaua kaka...akau mjomba.
Watoto wangu njoooooooni!


Nimekukubali Lizzy kiooo kiooo si ndo ule watu wawili wanshikana mikono alafu wengine mnapita mmoja moja kati kati yule mabye wimbo unaishia kiwa kati kati inakuwaje ....... Miwshoni minavutanaaaaau nimekosea


Hiyo ya watoto wangu eheeeeeeee
sie tulikiwa tunase hivi
watoto wangu eheeeeeeeeee
mimi baba yenu
sina nguvu tena
ya kuuuua simba
Simba ni mkali
aliua mama akaua kaka
aya kimbieni....
 
Nimekukubali Lizzy kiooo kiooo si ndo ule watu wawili wanshikana mikono alafu wengine mnapita mmoja moja kati kati yule mabye wimbo unaishia kiwa kati kati inakuwaje ....... Miwshoni minavutanaaaaau nimekoseaHiyo ya watoto wangu eheeeeeeeesie tulikiwa tunase hiviwatoto wangu eheeeeeeeeee mimi baba yenu sina nguvu tena ya kuuuua simbaSimba ni mkalialiua mama akaua kaka aya kimbieni....
Mtazamaji inawezekana mimi ndo nimepotosha mwisho wa “simba ni mkali“.....it‘s been a while!!Ehheh alafu kuna huu nlikua naimbiwa na mimi nachangia bila kujua naimbwa mimi!! Desh desh na Devi wanameremeta *4Ohh wanameremeta!!Then nakumbuka tulioteshaga karanga zetu pembeni ya mfereji mimi na msichana wa jirani...waaaay older than me.Nadhani ndipo nilipojenga mazoea ya siku zote kua kwenye kampani ya watu wakubwa kuliko mimi kiumri.Tulikua tunapika kwenye vikopo fulani hivi sijui vilikuaga vya kitu gani....kichoma mahindi nje....kwenda shule na mahindi ya kukaanga....kunywa uji wa chumvi na limao sikuwahi kupenda wa sukari....maparachichi na makande au ugali wa maharage shuleni...chakula la walimu kwa wale tuliokua matawi kidogo....kushika namba asubuhi...kuagizwa kuni,vifagio na vidumu vya kumwagilia...kufinywa ukikosea MWANDIKO....kuhesabu kwa kutumia vifuniko vya soda aka VISODA...kutoroka shule...Dah...lots of memories.Ngoja niwatafute wenzangu tukumbushane vituko vyetu vya enzi zile!
 
Ukuti ukuti

Wamnazi wamnazi

Gunia gunia

La chumvi la chumvi

Mwenzetu kapondwa

Na nini, na gari

Tukampleke hospitali, atakaeanguka shauri yake, asije kusema, kwa mama yake, yamle yamle yamle waaaahhh
 
.....Tulikua tunapika kwenye vikopo fulani hivi sijui vilikuaga vya kitu gani....kichoma mahindi nje....kwenda shule na mahindi ya kukaanga....kunywa uji wa chumvi na limao sikuwahi kupenda wa sukari....maparachichi na makande au ugali wa maharage shuleni...chakula la walimu kwa wale tuliokua matawi kidogo....kushika namba asubuhi...kuagizwa kuni,vifagio na vidumu vya kumwagilia...kufinywa ukikosea MWANDIKO....kuhesabu kwa kutumia vifuniko vya soda aka VISODA...kutoroka shule...Dah...lots of memories.Ngoja niwatafute wenzangu tukumbushane vituko vyetu vya enzi zile!

Hiyo ya kuipikilisha always nilikuwa nakuwa mtoto siku moja nikagoma kuwa lazima niwe baba. nikaambiwa eti mdogo... . teh teh teh.

Then siku moja moja nilikuwa nacheza na wadada ile inaitwa Ready shake kama sikosei na ule mchezo mwingine wa kuruka ruka vyumba square vilivyochorwa chini sijui unaitwaje

Ukuti ukuti

Wamnazi wamnazi

Gunia gunia

La chumvi la chumvi

Mwenzetu kapondwa

Na nini, na gari

Tukampleke hospitali, atakaeanguka shauri yake, asije kusema, kwa mama yake, yamle yamle yamle waaaahhh

Hahahahhaa and waht about
  • kombolelaaaaaaaaaaa
  • Tayariiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii badooooooooooooooooooooooo?
 
Abunwasi na mkewe eliza, eliza
walikwenda na safari
ktk ya safari .......................

karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
wakataka na kauli, iwafae maishaini,

kitabu cha wagagagigigogo
 
Aisee minakumbuka hii salamu kwa walimu na wagen.....

CCM inaamin ya kwamba, kila binadamu ni sawa, na kila mtu anastahili heshima, shikamoooooo mwalimuan je unahali una hali gani?????

Hiyo ni mwalimu akiingia darasan....
 
Abunwasi na mkewe eliza, eliza
walikwenda na safari
ktk ya safari .......................

karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
wakataka na kauli, iwafae maishaini,

kitabu cha wagagagigigogo

Hili shairi kama sikosei ni std six tujifunze lugha yetu. Au siooo. hapo mwalimu ndio mn afundishwa vina na mizani.

Lakini kabla ya darasa la sita kuna lile shairi la darasa la tatu la sungura

hadithi inayokuja ni ya sungura sikia
hadithi uliyongoja leo ninakuleatea
Alitoka siku moa njaaa aliposikia
Njaaa aliposikia sungura nakuambia

Siku ile akaeeeeda porini kutembeleaaaa
akayaona matunda mtini yameeeneaaaa
Sungura akayapenda mtini akasogea,
Mtini akasogea sungura nakuambia
..................................

anayeumbuka amalizie . Wish i could rewind my age


Aisee minakumbuka hii salamu kwa walimu na wagen.....

CCM inaamin ya kwamba, kila binadamu ni sawa, na kila mtu anastahili heshima, shikamoooooo mwalimuan je unahali una hali gani?????

Hiyo ni mwalimu akiingia darasan....

hahahhaha Aluuuuu umenikubusha Sisi katika kikwabgizo nadhani kuna shemu tulikuwa tunasema " elimuuuuu ni msingi wa maendeleo Shikamoooooo mwalimuuuuu"

Kuna Yale madftar yakujifunzia mwandiko yenye mistari mkubwa na mdogo uliyatumia wewe Udaa?
 
hahah mnanikumbusha wailes nyie jaman....
ukut ukut ndani ya get la mamamwera...
kibaba baba..jaman dahh..usiposema ahhh..siiiiiiiiiiii tamu basi aukui baba na mimi..ndo ivo anakulalia juu na nguo zake zote na wewe na ligauni lako lakin lazima asemee ehh ahhhh tamuuu ndo mchezo unaendelea asiposema kesho akubaliki kuwa bab et ajakua bado
 
Mtazamaji inawezekana mimi ndo nimepotosha mwisho wa "simba ni mkali".....it‘s been a while!!Ehheh alafu kuna huu nlikua naimbiwa na mimi nachangia bila kujua naimbwa mimi!! Desh desh na Devi wanameremeta *4Ohh wanameremeta!!Then nakumbuka tulioteshaga karanga zetu pembeni ya mfereji mimi na msichana wa jirani...waaaay older than me.Nadhani ndipo nilipojenga mazoea ya siku zote kua kwenye kampani ya watu wakubwa kuliko mimi kiumri.Tulikua tunapika kwenye vikopo fulani hivi sijui vilikuaga vya kitu gani....kichoma mahindi nje....kwenda shule na mahindi ya kukaanga....kunywa uji wa chumvi na limao sikuwahi kupenda wa sukari....maparachichi na makande au ugali wa maharage shuleni...chakula la walimu kwa wale tuliokua matawi kidogo....kushika namba asubuhi...kuagizwa kuni,vifagio na vidumu vya kumwagilia...kufinywa ukikosea MWANDIKO....kuhesabu kwa kutumia vifuniko vya soda aka VISODA...kutoroka shule...Dah...lots of memories.Ngoja niwatafute wenzangu tukumbushane vituko vyetu vya enzi zile!

mweeee umenikumbusha mbali weeeee. tulikua na zam za kuwapikia walimu basi siku ukiwa jikoni we ni muhimu sana, kama hakuna mwalimu wa kuwasimamia kwa saaana hahahhaha msosi unapitia dirishani.....na kuanzia asubuhi ukijua uko zam hata hom hunywi chai......

kwa wale wa kazi za UK... kubebe mchanga, kuchuma kahawa, kulima vibustani vya waalimu loooh.... kwa wale waliokua wa kwanza kujiliza na deko kibao wanabaki skuli kudeki madarasa yote...

na kombolelaaaaaaaa.... duuu watoto wa siku hizi sijui kama haya mambo yako tena. utasikia mambo ya kina ben 10, super mario na vikatuni kibaaaao na game kibao hata ngoma hakuna tena......

eeehe na somo la sanaa na uchoraji.... kuchonga miiko ( ukiwa mzuri unabaki jikoni au mwalimu anaupeleka kwake), na kutengeneza magari kwa mabua.... ubunifu ule atiii. siku hizi
 
Ooh! Wakati umekwenda wapi...jamani loh!! Nakumbuka enzi zile za Shule ya msingi. Mwenge ukiwa unapita ktk Tarafa yenu basi shule zote ndani ya Tarafa mnaenda kushangilia mwenge. Kutwa mnapigwa na njaa, kiu, jua kali na vumbi. Jioni wakati mnarudi kwenu mashamba yaliyo kando ya njia yanaipata kisawa! Mihogo na vingine vinavyofaa kupoza njaa vinakuwa halali yenu. Kesho yake malalamiko lukuki yanaletwa na wenye mashamba. Kinachofuatwa ni adhabu ya kucharazwa viboko kati ya vitatu hadi vitano kulingana na uharibifu wenyewe. Kesi imekwisha maisha yanaendelea mbele. Masomo matamu kama Jiografia, Historia, Siasa, Sayansi Kimu, Sanaa nk. Ikifika kipindi cha English angalia watu wanavyokuwa wagonjwa ghafla au ruhusa za kwenda msalani kibao, kisa... English bwana we! Raha kweli wajameni.
 
Ikiwa kiongozi fulani wa nchi anatembelea wilayani kwenu,mnakwenda kupamba barabara atakayopita kwa miti iliyozungushiwa majani,na wakati anapokuja mnakwenda kijipanga barabarani kumkaribisha.
 
mweeee umenikumbusha mbali weeeee. tulikua na zam za kuwapikia walimu basi siku ukiwa jikoni we ni muhimu sana, kama hakuna mwalimu wa kuwasimamia kwa saaana hahahhaha msosi unapitia dirishani.....na kuanzia asubuhi ukijua uko zam hata hom hunywi chai......

kwa wale wa kazi za UK... kubebe mchanga, kuchuma kahawa, kulima vibustani vya waalimu loooh.... kwa wale waliokua wa kwanza kujiliza na deko kibao wanabaki skuli kudeki madarasa yote...

na kombolelaaaaaaaa.... duuu watoto wa siku hizi sijui kama haya mambo yako tena. utasikia mambo ya kina ben 10, super mario na vikatuni kibaaaao na game kibao hata ngoma hakuna tena......

eeehe na somo la sanaa na uchoraji.... kuchonga miiko ( ukiwa mzuri unabaki jikoni au mwalimu anaupeleka kwake), na kutengeneza magari kwa mabua.... ubunifu ule atiii. siku hizi
........ hahahahhah
Kutengeneza magari ya maboksi, kubumba vitu kwwa ule udongo mfinyanzi. nakumbuka unamuunda mdoli wa udongo w akike unamuwekea na vinyonyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom