UKUTA: Tathmini ya kitakachotekea baada ya hili tamko

UKUTA: Tathmini ya kitakachotekea baada ya hili tamko

"....Wapinzani waje na mbinu nyingine", mbinu ipi hiyo kama wanazuiwa kufanya shughuli za siasa na kuwafikia wananchi??? hebu atoke mtu mwenye akili atufafanulie nini kinachosemwa hapa. Je unaweza kuvizuia vyama vya siasa kufanya shughuli zake za siasa, kisha ukavishauri kuja na mbinu ipi???
watakuambia mbinu yenyewe ni kulala ndani kusubiri 2020.
 
Kazi ya vyombo vya dola si kuzuia maandamano na mikutano ya siasa. Kazi yake ni kulinda na kuhakikisha maandamano yoyote na mikutano ya siasa inafanyika kwa amani. Tuache kushabikia mambo yasiyo na maana......
 
Hoja yako hapa ni serikari kutumia polisi na kuzima hizi harakati kinyume na uhuru uliomo kwenye katiba.
Ndoto ya Tanzania yenye amani ni kupitia utawala wa katiba na maridhiano ambapo kila mmoja atajisikia kutendewa haki.
 
Mnataka kumshikisha ukuta nani? Hayo mambo ya pwani pelekeni mombasa,
 
Hii ni tathmini yangu mnaweza mkakubaliana na mimi au mkakataa.
Refer mawazo yaliyowasilishwa na profesa Kitila wa UDSM kuwa upinzani unatakiwa ukae chini na kuja na mbinu zingine kwa sababu huu sio utawala wa JK.

Naona wapinzani wamempuuza ila Kitila Mkumbo alikuwa na point muhimu sana na sio ya kuichukulia juu juu.

Sasa kuanzia sasa hivi polisi watatoA vitisho na kupiga marufuku hayo maandamano na mikusanyiko msishangae baadhi ya viongoZi kukamatwa na kuswekwa ndani..

Ukiangalia mwisho wa UKUTA sio mzuri na unaweza kuleta mtafaruku na uvunjifu wa amani kati ya serikali watawala na upinzani..

Lowasa alishauri upinzani uachane na siasa za harakati ila naona hawajamsikiliza..
Kama Makamba alivyosema kuwa anayekuja atawabatiza kwa moto, na huu ndio utakuwa mwanzo wa moto

Stay tuned and watch the end of this movie.:
Moja ya mambo ambayo JK aliwahi kuyakiri hadharani ni vyama vya upinzani kuwekeza kwa wasomi na hilo ndilo lilichangia sana kuisumbua CCM. Mm bado naamini CDM ina wasomi wengi na wabobezi/wachambuzi wa masuala ya siasa wa kutosha hasa pale top layers. Mtizamo wangu wanajua wanachokifanya, walichokilenga na watakachovuna coz siku 4 Bahari beach hawajakaa bure, hata ukitizama tamko lenyewe kuanzia contents zake, muda lilipotolewa na namna lilivyowasilishwa utagundua operation hii imekaa kimkakati sana. Wameyazungumza haya mwezi mmoja kabla ili waone reaction ya vyombo vya usalama na hatimaye wawe na muda wa plan B.
Ni mtazamo wangu lakini............
 
Wewe sema ni mnazi wa chadema uliyekubuhu!
Hao viongozi wako hawana lolote la kuwaambia watanzania, sembuse wana CHADEMA.

Viongozi wenye akili hawawezi KUSUSIA vikao halali vya Bunge , hasa ukitilia maanani kuwa wao ni wenye ushawishi mdogo Bungeni.
Hiyo si aili kabisa , na wapinzani wezao wadiriki kuuita ni utoto!
Tatizo lenu mtu akikwambia ukweli, haraka mnaenda matusi na kumkashifu, lakini akili za utoto ni kama mbio za sakafuni zinzoishia ukingoni.
Tukija kwenye suala la UKUTA, hizo ni mbio za utoto, nazo zitaishia sakafuni hadi ukingoni.
Haihitaji akili sana kuona kuwa hapa mnambeep Mzee wa Push Up, naye hajawahi kubipiwa aisjibu.

Watanzania watafaidika na nini kwa upuuzi wote huo?
Ndo tunaita vyama kutawaliwa na watu wasio makini.
 
Imagine umeandamana kisa ukawa hawajaruhusiwa wafanye mikutano yao ya mipasho.. Umekutana na wazee wa osterbay wamekuwasha ya mguu... Dhambi ya woga mbaya sana ila sio kwa hapa bongo.. Hatujafikia extent ya mtu kula shaba kwa sababu ya ukawa.. Bado hamjanidanganya...
... Unakula shaba ya mguu ili Sumaye na Lowasa washike nchi .. Wakuletee maendeleo... Kwanza msinipe hasira... Sumaye wakati wa utawala wake alituweka sana njiani na vin'gora kila week end alikuwa anaelekea kibaha.. Tunakaa foleni karibi dakika 45.. Leo hii ati niandamane kisa Sumaye hajaruhusiwa kufanya mkutano.?
Siipendi ccm na mimi sio mwana ccm but sio kwa strategic hizi za UKUTA
 
Sifurahii lakini njia inayotumika sio nzuri kwa wakati huu... Tungekuwa waarabu hapo sawa.. Waarabu waki rise wanaingia kitaa wote kupinga udhalimu.. Ila kwa bongo yetubkwa woga wetu huu watakaoumia ni wachache sana ..mimi nishaingia sana kitaa na chupa langu la maji.. Ila ukipigwa au ukiumia unaenda kuuguza mwenyewe japo hio ndio price ya HAKI. Wewe si utaona.. Kuanzia wiki hii utaona matamko ya mapolisi kila mkoa..
unashauri wapinzani wangefanyaje?
 
acha kutisha watu kila mtu na anavyopokea jambo na hisia zake hapa duniani!kwani wangapi wanakufa kwa HIV bila kujilinda wanapofanya ngono tena ni dhambi kubwa! sembuse kutetea na kulinda demokrasia!kama wewe ni muoga kaa kumya !
 
Wewe sema ni mnazi wa chadema uliyekubuhu!
Hao viongozi wako hawana lolote la kuwaambia watanzania, sembuse wana CHADEMA.

Viongozi wenye akili hawawezi KUSUSIA vikao halali vya Bunge , hasa ukitilia maanani kuwa wao ni wenye ushawishi mdogo Bungeni.
Hiyo si aili kabisa , na wapinzani wezao wadiriki kuuita ni utoto!
Tatizo lenu mtu akikwambia ukweli, haraka mnaenda matusi na kumkashifu, lakini akili za utoto ni kama mbio za sakafuni zinzoishia ukingoni.
Tukija kwenye suala la UKUTA, hizo ni mbio za utoto, nazo zitaishia sakafuni hadi ukingoni.
Haihitaji akili sana kuona kuwa hapa mnambeep Mzee wa Push Up, naye hajawahi kubipiwa aisjibu.

Watanzania watafaidika na nini kwa upuuzi wote huo?
Ndo tunaita vyama kutawaliwa na watu wasio makini.
mkuu...hata kubaki bungeni unapangiwa cha kuongea na hauko huru...sasa bungeni kuna maana gani
w engine sisi tunaona kuziba watu midomo ni tatizo kubwa kuliko kuwaacha wabwabwaje...tupingane kwa hoja na utendaji wetu usindikize hoja zetu
 
acha kutisha watu kila mtu na anavyopokea jambo na hisia zake hapa duniani!kwani wangapi wanakufa kwa HIV bila kujilinda wanapofanya ngono tena ni dhambi kubwa! sembuse kutetea na kulinda demokrasia!kama wewe ni muoga kaa kumya !
Pongwa sitishi mtu.. Maneno yangu sio mnyororo.. Sept 1 si ipo hapo tu near by....
 
Amani ikivurugika chanzo ni ccm na hakuna atakayekuwa salama
 
wenye busara wanatakiwa wawashauri waungwana wa pande zote mbili (hasa hasa watawala) kuwa kutunishiana misuli huku huwaga na mwisho mbaya.

hivi kwa nini hamjifunzi lakini? eh? kwa nini hampendi kujisomea mambo ya wengine mkajifunza ili tuepukane na maujanja ya akina bokoharamu? hivi hamjui kuwa mnaipeleka nchi kubaya?

sijui tukimbilie wapi.....mweee!
 
Chadema ni chama kilichojaa watu wabunifu sana,hii ni mbinu tosha inayoifanya Chadema kuwa kila kona husuxan kila mtanzania mpenda demokrasia na mabadiliko daima.Ndani ya masaa kadhaa tangu operation UKUTA itamkwe,tayar imejaa vinywan,kwenye mawazo,mikonon mwa watanzania kila kona mwa nchi na katika vyombo vya habar vya nje.Hii ni mbinu mbadala au chenga mzunguko kwa serikali isiyo na dira yeyote wao wanakuja hivi,Chadema wanakuja kivingine.Kiukweli tunahitaji mawazo mbadala,serikali ya ccm haijatupa dira,kila tukiamka mara tuhamie dodoma hatuelew tunakoelekea.
 
Kweli ukiwa mfuasi wa dola huoni ni kusifu na kuabudu. Mwangosi ni shujaa tayari na Jina lake litadumu .
Kifo kila mmoja atakufa hata huyo anaejiona yuko peponi
Lakini si kwa kuingizwa mjini kama mlivyofanya kwa marehemu Mwangosi.

Pamoja na ushujaa mnaompa, watoto wake mnawasomesha?
 
wenye akili timamu huwa wanaelewa wale wenzangu na mimi wanaodhani siasa ni uadui kazi kwao!
 
yani katika kitu ambacgo naona wazi wazi kuna CHADEMA wamerocha rocha ni kuendelea kutaka kutumia nguvu dhidi ya chama kilichojihami kupitia jeshi la polisi,wao wangefaa kutafuta njia nyingine za kuhamasiha watu zao juu ya kutambua haki,lakini sio kujifanya kiburi kwa huyu mtu ambaye yeye akisema anaamini katika kile anachosema tu,CHADEMA leo hii wangeweza kuwa na redio yao hata ya on line tu au you tube tv yao ambayo nadhani wangeitumia hiyo kuwafikia watu zao kokote walipo nchini tena bila hata ya kusuguana na serikali hii ya sasa,
 
Kitila ni mnafiki, upinzani hawastahili kubadili chochote kwa sababu wao hawajakosea lolote lile katika kudai haki zao ambazo zimo ndani ya katiba ikiwemo kujadili chochote Bungeni kuhusiana na mustakabali wa nchi bila kuingiliwa ba chama tawala kutaka kuwaamulia nini kinastahili kijadiliwe bungeni na upinzabi na nini hakistahili na pia kufanya mikutano yao popote pale nchini bila kuzuiliwa na polisiccm.

Mwenye kosa ni huyu dikteta ambaye anashindwa kutamka hadharani kwamba sasa utawala wake haufuati katiba na vyama vya upinzani vifutwe badala ya kuendeleza unafiki kwamba Tanzania ni nchi ya vyama vingi lakini ukweli ni kwamba tangu uanzishwe udikteta nchini Tanzania si nchi ya vyama vingi tena bali usanii tu.

Wewe unafikiria upinzani ufanye lipi!? Umpigie magoti dikteta!? Au usalimu amri katika kubakwa demokrasi nchini kwa kutoiheshimu katiba ya nchi!?

Back
Top Bottom