Mimi niliwahi kuchimba madini huko mererani, nilikuwa najaribu kujiuliza ukuta utasaidiaje? nikawa sipati picha. Labda kama huo ukuta unaweza kupunguza wizi. Sikushangaa sana kwani rais wetu anapenda kudhibiti au kulinda kwa mtazamo wake. Lakini anakosa mbinu sahihi au wanaomshauri wanamshauri anachowashauri wao.
Nilishangaa ili siku aliposema kesho jeshi likaingia na mkwara mkubwa utafakiri ni jambo lenye tija sana. Nimewahi kushauri mara nyingi humu, badala ya jeshi kukaa tu bila kuzalisha mali wakati huu wa amani, ni bora lipewe mashamba makubwa ya kulima kwa kupewa pembejeo kama tractors, combine harvestors, mbolea nk. wazalishe kwa wingi kisha wananchi tunaolima kwa nguvu zetu tuachwe tuuze tunapotaka. Hayo ya jeshi ndio yakajazwe kwenye maghala ya serekali kwa ajili ya njaa na kutunza bei elekezi. Lakini nimeona jeshi limeenda kama roketi kujenga ukuta wakati kama ni madini ndio yako ukingoni. Usishangae ndani ya mwaka huo ukuta ukaanza kuweka ufa kwani sidhani hata kama feasibility study imefanyika. Anyway ndio rais wetu huyo nia njema lakini hana mbinu.