Ukuta katika machimbo ya Mererani wazua utata

Ukuta katika machimbo ya Mererani wazua utata

Kwa uelewa wangu eneo linawekewa mitambo ya gprs ukivuka eneo la uzio hata ukiwa kilometer tano chini ya ardhi inajulikana so kwa hili kuiba ni ngumu, japo huyu sizonje simpendi hata
Hahah unajua maana ya GPRS mkuu?
 
Mkurupukaji kama kawaida yake.

Walitakiwa kujenga Ukuta wa sheria za kuhakikisha madini yanafuata proper channels,siyo ukitaka wa Cement ya wazo.Hahahhahaha
 
Phd feki hua hazijifichi, kama ile ya Bashite.
Ukuta uzuie uibaji wa madini? Hehehe. Yanachimbwa chini ya ardhi we unaziba ukuta pembeni. Siamini dini ila kweli hapa albadri haijamuacha mtu. Haiwezekani mtu amedata kiasi hiki.
 
Anauzoefu na maduara ya dhahabu....kima cha kwenda chini shimo la dhahabu Mita 50 hadi 60
Lkn duara(shimo)la Tanzanite
Mita zaidi ya 900
 
Nia ni nzuri laki madini si kama kuangua nazi kwamba mkwezi anaonekana tangia anavyo panda hadi kushuka ,kwa hili imetumika akili ndogo niwe mkweli tu
Mkuu unabishana na muuza nyanya??
Nyanya na uchimbaji wa Madini wapi na wapi
 
hii kali machimbo kuwekewa ukuta juu ya ardhi? Ni sawa Shimo la Panya kuzibwa kwa Mkate

Mkuu umenikumbusha enzi zile ktk mgodi wa almasi mwadui,tuliwekewa electric fence(fence ya umeme)ukiigusa unakauka hapo hapo.
Lkn makaburu walikoma na sisihapo ndio ilikua maeneo yetu ya kupumzikia kwasbb mbwa wala askari wao hagusi maeneo hayo kwa kuuogopa umeme
Wakiondoka sisi ndio tunapita kilaiiiini
 
Ars mpoooo!!!
Madini ni ya Manyara sio ya kwenu.

Haijawahi wanufaisha wao. Kwanini biashara ifanyikie kwenu?

Acha soko lifanyikie huko.

Bunini na nyie vyanzo vingine vya biashara ktk mji wenu.

MNA kiburi sana.
 
mkuu cha kwanza ni kulinda raslimali zetu kwanza.....kejeli na kelele hizo zipo tuu.
Nahisi hata uchimbaji wa madini huujui unafanywaje... Kimsingi mtu anaweza akachima shimo hapa na akaenda kutoke mbali.. Kwani yale mashimo yaliyopo kwenye ikulu ndogo toka kwenye vyumba vya waheshimiwa hayatokei mbali na vyumba vilipo?

Sometimes ongeeni kwa hali halisi na si ushabiki wa aina yoyote
 
Acheni viwanda vyetu vya simenti vipumue
Yaani kama ni kupumua viwanda vya simenti, pale Kakola na ile BATCH PLANT ilikuwa inapumua haswa kwenye back filling ya mashimo underground... Sasa wamefunga mgodi, hilo gap my friend viwanda vya cement vitaliona tu....

Unjenzi wa ukuta ni ONE TIME EVENT, ukiisha ndo basi tena... lakini ile BATCH PLANT ilikuwa ni kwa litime ya mgodi...
 
Hamna wema nyie hv ukijenga nyumba yako ukiweka ukuta unakuea na maana gani?ni moja ya njia za ulinzi,njia nyingine zinafuata badae ...Tuko pamoja Mh Rais 100%
 
Habari wana jamvi,

Kama kichwa kisemavyo,

Huu ukuta wa mererani ulioagizwa na mh Magufuli umezua utata kwa namna ulivgopokelewa hasa na washikadau wa shughuli usika za madini,

Kwanza wameshangaa kutolewa maamuzi ya namna ile ambayo kwayo wamesikitika kwamba kwann nguvu hio na gharama hizo wasingejenga barabara sehemu zenye uhitaji.

Wakaenda mbali zaaidi juu ya washauri wa mh. Magufuli kana kwamba elimu yao ni yakinadharia tuu imewanyima ujuzi wa uhalisia kufikia maamuzi yasiyo na tija au wanaamua kumpotisha tuu mh. Magufuli.

Wanasema kama mh. Magufuli hawajui wachimba madini na wadau wake atakuja shtuka shimo linachimbwa mererani wanapolo wanatokea Arusha au hata chumbani kwa mtu na hapo ndo hasara ya kamera itakapo onekana, pia patakua na njia nyingi tuu za kufanikisha wizi kwa serikali kama serikali haitokuja na sera rafiki, shirikishi katika ukusanyaji kodi.

Mimi ni mzalando!!
Sidhani hii yaweza kuwa sababu ya msingi ya kutoona umuhimu wa kujenga ukuta, changamoto zipo kwenye kila kitu.
 
Mi naamini muheshimiwa Rais ameamua kuwapa ajira JKT maana hawajawai kupata tenda kama hiyo.
Na pia anajua kabisa waliofanikiwa kwa madini kama Bostwana na SA hawajajenga ukuta na waliofeli kama sisi na DRC sio kwasababu hatuna ukuta
 
Adui wa maendeleo ya Tanzania ni mtanzania mwenyewe
 
Kwenye haya madini yote tuliyonayo Tanzania....
1. Tupo zaidi ya 45M now, lakini katika hao wanaojuwa at leat kiasi fulani ya nini kinaendela kwenye DHAHABU hawazidi laki tano (Makadilio tu)
2. Tupo zaidi ya 45M now, lakini katika hao wanaojuwa at leat kiasi fulani ya nini kinaendela kwenye ALMASI hawazidi laki nne
3. Tupo zaidi ya 45M now, lakini katika hao wanaojuwa at leat kiasi fulani ya nini kinaendela kwenye GESI hawazidi TATU

Kati idadi iliyotajwa hapo juu, wanaojua mambo ya sehemu zaidi ya moja (ALMASI NA DHAHABU NA GESI) pengine hawazidi laki mbili....

CHA AJABU, SASA KWENYE MIJADALA HUMU JF NA KWINGINEKO, WATU WANAONGEA MIVUKE YA KUTISHA.... yaani wanaojuwa wanaamuaga kujikalia KIMYA... maana kubishana na siyejua, NA KWA UWINGI WAO HUWEZI WABADILISHA, UKIZINGATIA HAWAONGOZWI NA HOJA BALI...
1. Uchama
Hawa, wanaongea kumlinda aliye kwenye chama chao... yaani hata achemke vipi, the fact kwamba wapo chama kimoja lazima amtetee... HAPA WAPO AKINA NDIYOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO WENGI SANA

2. Udini
Wengine wanalitazama kwa namna hii, yaani akiongea askofu, mchungaji, sijui shehe, sijui imamu yaani lazima amuunge mkono hata kama anachemka na hajui lolote kuhusu madini

3. Ukanda
Hapa ndo wale AKINA NYIE MNALIMA NYANYA HAMJUI MADINI... utadhani zile kamati hazikuwa na watu wanaotoka kusiko na madini... wa hivi wako wengi.. waliojitokeza kusema hadharani ni wachache

4. Umkoa
Mtu anadhani kwa vile Madini yapo Arusha, sijui Shinyanga, Sijui Gesi ipo Mtwara sijui wapo basi wengine wasiongelee suala hilo, simply because hatoki mkoa wenye madini husika
 
Nia ni nzuri laki madini si kama kuangua nazi kwamba mkwezi anaonekana tangia anavyo panda hadi kushuka ,kwa hili imetumika akili ndogo niwe mkweli tu
Unashauri wangefanyeje kwa kutumia akili yako kubwa zaidi ya waliopanga hivyo since 2002.
Any alternative suggestion?
 
Back
Top Bottom