MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,643
- 33,439
Wakuu,
Rais wetu Magufuli amekuwa akikosolewa mno na wapinzani hata anapofanya mambo ambayo ni historia kwa nchi hii.
Pamoja na madai ya msingi wakati mwingine lakini ni vizuri kumtia moyo kwenye issues za msingi ambazo ni kwa faida ya Taifa hili.
Ujenzi wa ukuta kuzunguka machimbo ya madini ya Tanzanite na kuandaa mpango wa soko kuwa pale pale ni kitu kikubwa mno! Historia itamkumbuka kwa hili na hata kama sisi tutabeza vipo vizazi vitamuelewa.
Rais Magufuli amekuwa champion wa kulinda rasilimali zetu kwa vitendo ingawa kwasasa tunaumia na matokeo ya "sabotage" against juhudi hizi kutoka kwa "wakubwa" waliokuwa wakijichotea sawa na bure.
Mbona hatusikii "wazalendo" wetu wakipongeza hatua hii ngumu na muhimu kwa kelele zile zile tunazopiga akikosea jambo. Kitu kimoja ambacho ni hakika, Rais Magufuli anaweka historia na Africa itajifunza kwake mbinu za ulinzi wa rasilimali za nchi.
Kwa hili la kujenga ukuta, kuhusisha majeshi moja kwa moja kulinda rasilimali na mkakati wa madini kuuzwa pale pale ni moja ya maamuzi ambayo Rais John Pombe Magufuli utakumbukwa na vizazi vyote.
Uwe humpendi au humuungi mkono Rais Magufuli lakini anaweka historia na mlio kinyume chake kwa hili kumbukumbu zitabaki hivyo vizazi vyote.
Ushauri kwa mh Rais Magufuli;
Vitu vidogo kama kijana Abdul kuhojiwa uraia wake vinachafua mambo makubwa na mazuri unayofanya. Hivi hatuna magenius wa kushughulika na hali ya kisiasa inayoendelea ili nchi ibaki na mshikamano kwenye mambo ya msingi unayofanya kama haya?
Mambo mengine mnayakuza wenyewe. Tunapaswa kuwa na mshikamano against mabeberu walioitafuna hii nchi kwa muda mrefu. Kelele lazima zitakuwepo lakini nyingi zinakuzwa na wenyewe.
Kumuhoji uraia kijana Abdul kipindi hiki inajenga taswira gani? Sehemu kubwa ya wananchi wakiwemo wanafunzi wenzake wanaichukuliaje hii?
Hongera sana Rais Magufuli kwa hatua hizi za kulinda rasilimali zetu ambazo zinaenda kuweka alama ya kukumbukwa nchi hii. Napendekeza swala la majeshi kulinda rasilimali zetu moja kwa moja iwe kisheria badala ya kutegemea wanasiasa wenye objectives zao kulingana na nyakati.
Sasa Tanzanite italindwa!
Soma: Raw Tanzanite exports hurting local economy
Soma: Rais Magufuli kuzindua ukuta katika migodi ya Tanzanite Mirerani
Soma: Kujenga ukuta Mererani haitaweza kutatua tatizo la utoroshaji wa madini