REDEEMER.
JF-Expert Member
- Feb 22, 2015
- 8,918
- 14,894
Nimekusoma kwa makini nikijua una la maana kama "formal mwanaapolo" kumbe ni siasa tu.Mimi niliwahi kuchimba madini huko mererani, nilikuwa najaribu kujiuliza ukuta utasaidiaje? nikawa sipati picha. Labda kama huo ukuta unaweza kupunguza wizi. Sikushangaa sana kwani rais wetu anapenda kudhibiti au kulinda kwa mtazamo wake. Lakini anakosa mbinu sahihi au wanaomshauri wanamshauri anachowashauri wao.
Nilishangaa ili siku aliposema kesho jeshi likaingia na mkwara mkubwa utafakiri ni jambo lenye tija sana. Nimewahi kushauri mara nyingi humu, badala ya jeshi kukaa tu bila kuzalisha mali wakati huu wa amani, ni bora lipewe mashamba makubwa ya kulima kwa kupewa pembejeo kama tractors, combine harvestors, mbolea nk. wazalishe kwa wingi kisha wananchi tunaolima kwa nguvu zetu tuachwe tuuze tunapotaka. Hayo ya jeshi ndio yakajazwe kwenye maghala ya serekali kwa ajili ya njaa na kutunza bei elekezi. Lakini nimeona jeshi limeenda kama roketi kujenga ukuta wakati kama ni madini ndio yako ukingoni. Usishangae ndani ya mwaka huo ukuta ukaanza kuweka ufa kwani sidhani hata kama feasibility study imefanyika. Anyway ndio rais wetu huyo nia njema lakini hana mbinu.
Nikuulize swali, katika kuchimba kwako madini hapo mererani kuna shimo lolote lenye urefu wa Kilomita 2?
Alafu aina ya uchimbaji ni surface au sub-surface mining?
Ni drift, slope au shaft mining?
Sababu naona wengi wenu Mnajifurahisha na hekaya za kutengenezea underground tunnel, hivi kuchimba hatua moja huko chini kwa tindo itakuchukua muda gani sababu mnadhani kule ni udongo kumbe ni miamba.