Ukristo unahubiri upendo, je huu ni upendo wa aina gani? Au huu ni Ukristo wa aina gani?

View attachment 2093183

Mafundisho ya dini ya Kikristo yamejikita zaidi kwenye upendo, kwani ndio amri iliyo kuu kama tulivyo agizwa na Bwana wetu Yesu Kristo.

Miongoni mwa mistari inayo onyesha kiwango cha hali ya juu cha upendo ni ule unaosema tusamehe saba mara sabini. Pia upo ule mstari unaosema ukipigwa shavu la kushoto, geuza na la pili.

Sasa hebu tazama hiyo video, kisha tujadili, ni nini kimetokea? Je huyu anayepiga wenzake na ni kiongozi wa kanisa anasimamia andiko kutoka mstari gani?

Je, huu ni upendo wa namna gani?
Si kila anayejiita Mkristo ni Mkristo kweli. Usizuzuke na bodi,check injini.
 
Hah haa kwani Biblia inasemaje?

  • Usihukumu usije ukahukumiwa. Viboko ni adhabu. Mathayo 7:1
  • Mit 23:13 Usimnyime mtoto wako mapigo - Bible.com

    Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa. Mchungaji wako sio baba yako. Na ni dhambi kumwita mchungaji kuwa baba wa kiroho.
  • Mt 23:9-12 SUV​

    Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni. Wala msiitwe viongozi; maana kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye Kristo. Naye aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu. Na ye yote atakayejikweza, atadhiliwa; na ye yote atakayejidhili, atakwezwa.
Tafsiri mbaya! Mithali 23:13 haina maana ya kumpiga mtoto as if kupiga ni tunu ya Kimungu. Isipokuwa kumwongoza mtoto katika njia nyoofu na kufanya hivi siyo lazima kumpiga mtoto. Kama watu wazima ambao walipokuwa watoto walichapwa viboko, mbona baadhi yao wamepinda kama kiboko ni tunu? Mathayo 23:9-12 nayo tafsiri yake ni mbaya kwa sababu maana hata Yesu mwenyewe alitaja...Yohane 8:56.
 
Tafsiri mbaya! Mithali 23:13 haina maana ya kumpiga mtoto as if kupiga ni tunu ya Kimungu. Isipokuwa kumwongoza mtoto katika njia nyoofu na kufanya hivi siyo lazima kumpiga mtoto. Kama watu wazima ambao walipokuwa watoto walichapwa viboko, mbona baadhi yao wamepinda kama kiboko ni tunu? Mathayo 23:9-12 nayo tafsiri yake ni mbaya kwa sababu maana hata Yesu mwenyewe alitaja...Yohane 8:56.
Hujaeleweka bado
 
hahahahaha weeee unajua kitisi ndio magheto hapo hiyo ndio mitaa yangu ya kujidai Aisee ukishuka hapo stendi ya MK Kwa nyuma tu hapo inaanzia kitisi mpaka Kule bondeni kama unaenda kahawa!
mkuu we kweli mwenyeji unakufahamu hadi kahawa. Niliwahi kuishi mitaa hiyo watu wengi ukiwaambia kahawa walikuwa hawaelewi
 
Tatizo la madhehebu mengine ya kikristo hayana liturgia ndio maana kinatokea na za namna hio, kama wangekaa chini hayo makanisa ya kipentekoste na kuwa na mwongozo mmoja wa ibada ambao sio kila mchungaji awe na mwongozo wake kulingana na anavyoamka, hapo kidogo ingekua na kueleweka katika jamii.
Pia wangetambua Karama za roho na kila mmoja akaiishi karama yake, kama mchungaji ni mchungaji na ndie mwenye kanisa, mtume nabii mwinjilisti mwalimu mwombezi hawa wote wewe chini ya mchungaji.
 
Hivi unatambua kristo= christ na asiri yake ni uzunguni sasa je ni wapi pameandikwa Waafrika asiri yao ni uzungu yaani "wa kristo""

Utawafanya watu wengi wajinga kwa muda mchache tu baadae watafumbuka macho
Ukristo asili yake ni mashariki ya kati. Na hakuna wazungu kule. Kama huwezi kuelewa kitu rahisi kama hiki unawezaje kuwa mwerevu wa kukosoa?
 
Back
Top Bottom