Ukristo unahubiri upendo, je huu ni upendo wa aina gani? Au huu ni Ukristo wa aina gani?

Kila kitu na kasoro zake.... jamaa kasoro yake ni hiyo ila kuna mengine yupo perfect ndiyo maana wanamkubali na kumuelewa.... issue ni mafundisho tu.
 
Hah haa kwani Biblia inasemaje?
Tukiachana na hiyo video ambayo sijaiona tuongelee kuchapa...hivi unapomchapa mwanao maana yake
  • Usihukumu usije ukahukumiwa. Viboko ni adhabu. Mathayo 7:1
  • Mit 23:13 Usimnyime mtoto wako mapigo - Bible.com

    Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa. Mchungaji wako sio baba yako. Na ni dhambi kumwita mchungaji kuwa baba wa kiroho.
  • Mt 23:9-12 SUV​

    Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni. Wala msiitwe viongozi; maana kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye Kristo. Naye aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu. Na ye yote atakayejikweza, atadhiliwa; na ye yote atakayejidhili, atakwezwa.
 
View attachment 2093183

Mafundisho ya dini ya Kikristo yamejikita zaidi kwenye upendo, kwani ndio amri iliyo kuu kama tulivyo agizwa na Bwana wetu Yesu Kristo.

Miongoni mwa mistari inayo onyesha kiwango cha hali ya juu cha upendo ni ule unaosema tusamehe saba mara sabini. Pia upo ule mstari unaosema ukipigwa shavu la kushoto, geuza na la pili.

Sasa hebu tazama hiyo video, kisha tujadili, ni nini kimetokea? Je huyu anayepiga wenzake na ni kiongozi wa kanisa anasimamia andiko kutoka mstari gani?

Je, huu ni upendo wa namna gani?
Upendo unaotakiwa uhubiriwe ni ule kwa Kiingereza unaitwa 'unconditional love' au 'steadfast love' (upendo wa aina hii ni mgumu sana kuuishi - [1 Wakorintho 13:1-13]) na siyo 'reciprocal love' au 'artificial/cosmetic love' (upendo wa aina hii ni rahisi sana kuuishi - [Mathayo 25:41-46]).
 
Back
Top Bottom