Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,132
- 10,514
Ni jambo la kushangaza na lenye kuibua maswali makubwa kuhusu usawa katika mazingira ya biashara kati ya Tanzania na China. Mfanyabiashara wa China anapokopa katika benki za kibiashara nchini kwao hulipa riba ya takribani asilimia 3 pekee.
Lakini mfanyabiashara wa kitanzania anapokopa katika benki za kibiashara za Tanzania, anakabiliana na riba ya wastani wa asilimia 17. Hii ni tofauti kubwa ya asilimia 14.
Je, katika mazingira haya, mfanyabiashara wa Tanzania anawezaje kushindana na Mchina ambaye mara nyingi hujificha nyuma ya mgongo wa Mtanzania kuendesha biashara zake? Ni wazi kuwa mfumo huu unawaweka wafanyabiashara wetu katika wakati mgumu, ukipunguza uwezo wao wa kushindana na kuendelea kibiashara. Swali la msingi linabaki: ipo wapi sera ya usawa na ulinzi kwa wafanyabiashara wa ndani?