Ukomo wa Mpambe na Walinzi wa Rais kisheria ikoje baada ya kifo?

mwanzo wetu

JF-Expert Member
May 4, 2014
1,581
461
Nafasi za Mpambe wa Hayati Magufuli pamoja na Walinzi wake unatakiwa kukoma lini?

Au pia na wao wanakuwa na mkataba?

Je, kama wana mkataba unakoma baada ya kiongozi wao kukosa uzima wa kuishi?

Naombeni watalamu watolee ufafanuzi.
 
Kwa upeo wangu nadhani wakishazika tu ndo ukomo wa upambe wake utafika mwisho. Ngoja wajuvi waje na neno
 
Mpambe ni mpambe tu, anarudi home Kula mihogo may be hekima ya Raisi aliyepo madarakani imwangukie vyema, walinzi hao ni moja ya highly internal security. Wanarudi kwenye defence ya nchi , kitengo cha TISS au army nafikiri hayo yapo kwenye mwongozo wa wanausalama
 
Mpambe ni mpambe tuu , anarudi home Kula mihogo may be hekima ya Raisi aliyepo madarakani imwangukie vyema , walinzi hao ni moja ya highly internal security .....wanarudi kwenye defence ya nchi , kitengo cha TISS au army ......nafkr hayo yapo kwenye mwongozo wa wanausalama
Na kabla ya mazishi wanaendelea na nafasi zao mpaka pale marehemu atakapo hifadhiwa?
 
Mpambe anarudi kwenye majukumu yake aliyokua nayo awali(jeshi) kabla hajachaguliwa kuwa mpambe. Na wale wengine wanasambaa walipotokea
 
Kwa siku kadhaa kumekuwa na movement kubwa ya watu wenye mabegi na Rambo wakitoka sehemu moja kwenda nyingine nadhani wanarudi walikotoka baada ya waliyekuwa wanamtumikia kupoteza maisha
 
Kwa siku kadhaa kumekuwa na movement kubwa ya watu wenye mabegi na Rambo wakitoka sehemu moja kwenda nyingine nadhani wanarudi walikotoka baada ya waliyekuwa wanamtumikia kupoteza maisha
 
Yule mwanajeshi anarudi jeshini ambapo baada ya muda tu atapandishwa cheo na kuwa Brigedia.

Wale walinzi na wasaidizi wake wote wakishatoka Chato after 2 weeks watarudi Ikulu, na kutokea hapo ndio watapangiwa vituo mbalimbali. Wengine wataendelea na Mama, wengine watarudi kitengo chao PSU, wengine watapelekwa kuwa mwambata ubalozini na wengine utawaona kwa VP mpya n.k.
 
Wamekua naye zaidi ya miaka 5. Aliye subiria dakika za majeruhi itakuwa imekula kwake. Aombe fadhila za mpokea kijiti.
 
Wapambe wa Rais wataachana na shuguli hiyo Mara baada ya hayati kufukiwa kaburini.

So toka hapo ndo wanakuwa wamehitimisha kazi ya usaidizi kwa mwenda zake na kupangiwa kazi nyingine.

Lakini mpaka sasa wao bado Wana jukumu la ulinzi kwa Mh. Magu ndio maana tunawaona wakiwa sambamba na jeneza la muheshimiwa
 
Yule mwanajeshi anarudi jeshini ambapo baada ya muda tu atapandishwa cheo na kuwa Brigedia.

Wale walinzi na wasaidizi wake wote wakishatoka Chato after 2 weeks watarudi Ikulu, na kutokea hapo ndio watapangiwa vituo mbalimbali. Wengine wataendelea na Mama, wengine watarudi kitengo chao PSU, wengine watapelekwa kuwa mwambata ubalozini na wengine utawaona kwa VP mpya n.k.
Nafikiri mulungwa anastahili promotion ilinawe relevant huko jeshini

Rais Ni taasisi so mulungwa kaitumikia kwa uamifu arudishwe jeshini kwa promotion sio kubaki na ukanali

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Wanarudi vikosini mwao kuendelea na maisha ya duty roster za kijeshi zingine.. wanachomiss saana Ni per diem, exposure, connection, presidential experience.

Kw kifupi wanarudi vikosini kusaga na rumba, kuendelea na fatigue za jeshi. Chaka ndo linakuwa limechomwa Moto.
 
Back
Top Bottom