Ukomavu wa kisiasa; Wakati Kenya wanaonesha njia, Tanzania kama wafanyavyo mbuni, tumezika vichwa mchangani

Tumia ignore formula, mimi hutumia thanks, usipoteze muda wako wa thamani kujibishana na hawa wavuvi wa kokoro na makorokocho yao.
P
Na wewe Pascal vile vile usijifanye mbwa mwitu ulovaa ngozi ya kondoo hapa , wewe ni fitna number one na una chuki ndani kwa ndani na Wazanzibari na chuki zako ni kubwa kuliko nuclear bomb.Kalamu yako iko siku Mungu ataukataka mkono wako .Mag3 lete vitu umeleta jambo la busara sana.
 
Kwanza, Mag3 uliyosema ni kweli kabisa Jamvi letu limekuwa kokoro, hoja zinapigwa rungu.
zingine tunajiuliza zinaruhusiwaje jukwaani ima kwa mzaha wake au kwa uchechefu.
Sijui nini kimetokea katika upande wa ''contents and quality'' Maxence Melo

Pili, siku zote namuona Uhuru Kenyatta kama Gentleman. Tangu wakati aliporidhia hukumu ya Mahakama, namuona muungwana na kila siku hutenda uungwana.

Tatu, siasa zetu zilikuwa nzuri sana siku za awali. Nakumbuka NCCR Mageuzi ikifunga kampeni na CCM siku moja Dar watu wakipishana kwenda watakapo bila hofu.

Nyakati za Mkapa ikawa hivyo na alikuwa na hasira lakini alijibu hoja kwa hoja au kudharau tu
JK naye alikuja lakini kauvumilivu kalianza kutoweka baada ya matukio kama ya akina Dr Uli

Awamu ya tano siasa zikawa si malumbano bali 'misiba'. Tulianza kuhasimiana, kutoheshimiana na kupoteza maelewano kama jamii. Kwamba dawa ya hoja ni kuumizana, tukaufanya utamaduni.

Tulipo tunahitaji kurudi katika mstari. Katika hii ''derailment'' Watanzania tunaweza kurejea

swali nani wa kutupa mweleko tofauti?

Pascal Mayalla
 
Chadema bado mna ndoto ya kuitwa ikulu mkanywe juice? 😂😊😊

JK aliwadekeza mkajiona watu muhimu sana kwenye hii nchi kumbe vibaka tu watafuta fursa kujifanya mnapigania maslahi ya watu waongo wakubwa mkionyeshwa hela mnasaliti wananchi waliowaamini.
Mkuu ungeficha japo kdg aibu yako. I'm so sorry.
 
Mkuu Mag3 , kwanza karibu tena jamvini maana umeadimika sana, na pia ni kweli jamvi hili letu adhimu, siku hizi kimekuwa kama kokoro, ila wewe mvuvi wa ndoana, huwezi kuacha kuvua samaki wakubwa eti tuu kwasababu sasa ziwani wamejaa wavuvi wa kokoro.

Ziwa letu limekuwa kubwa, enzi zile wavuvi wa ukweli mlikuwa wachache na mlituvulia samaki wakubwa, lakini jf imevamiwa na wavuvi wa kokoro, hivyo wanavua kila kitu hadi vidagaa, ila lile hitaji la wavuvi wa ndoana bado lipo.

Kuacha kuvua samaki wakubwa watamu kwasababu ya ujio wa wavuvi wa kokoro sio kuwatendea haki wale wateja wako. Endelea tuu kuvua mdogo mdogo kama hivi sisi walaji wa samaki wako tupo.

Natoa wito kwa wale wavuvi wakongwe wa humu, baadhi yao ni hawa
Mzee Mwanakijiji , Nguruvi3 , Mchambuzi, Kuhani, Woman of substance, Jasusi , Nyani Ngabu , @FMES and the like
rudini, hawa wavuvi makinda wanaotumia kokoro wasiwafanye mkapotea hivi.
Tena mkikubali kurejea, hata mimi nitamwita yule pacha wangu, Pasco wa Jf naye arejee, tumsaidie... Mama..., Mama anahitaji msaada wenu.
I mean Mama Tanzania...
P
Kama uko humu kwa ajili ya kumfurahisha mtu mmoja badala ya kuishi kwa ajili ya taifa lako ni bora ukaendelea kuwa Pascal MAYALA tu.
 
Siku hizi nashindwa hata kuingia JF kwani kwa sasa hili jamvi letu pendwa limekuwa kama kokoro. Hata hivyo hili tukio huko kwa jirani zetu limenizindua kutoka usingizi mzito. Kuna wakati taifa letu lilikuwa la kupigiwa mfano na hata sisi wananchi wake tulitembea vifua mbele bila soni wala aibu.

Nasikitika kuwa hivi leo nasita hata kujitambulisha kama Mtanzania kwani hakuna tena cha kujivunia! Tunawindana, tunatekana, tunatesana, tunajeruhiana,tunapotezana na tumefikia hata pahala pa kuuuana, kisa? Siasa. Ole wako usiwe na kinga ya vyombo vya dola kama ulinzi na usalama.

Wakati wenzetu pamoja na mapungufu yao wanapiga hatua kusonga mbele wakibebana ndugu zao wanaposhindwa kutembea, sisi kama mbuni vichwa tumevificha mchangani. Hakuna adui wa amani na usalama kama kujiaminisha kuwa tuko bora kuliko binadamu wengine na eti kama hukubali, hama nchi!
Nina neno moja tu fupi kwako.
Tanzania inahtaji kiongozi ambaye pamoja na mambo mengine yote, kupaumbele chake kiwe "HAKI NA USAWA".
 
Rais wa Tanzania kupitia CCM hawezi akapata ujasiri wa kutenda alilolitenda Rais wa Kenya.
Nadhani Rais akiona kuna haja ya kufanya hivyo kwa maslahi mapana ya Chama chake lakini kubwa kabisa kabisa maslahi ya wananchi na usalama na ulinzi wa Tanzania lazima afanye kama Rais wa Kenya alivyofanya.

Hata hivyo, hivi tumesahau jinsi Rais staafu Mzee Kikwete wakati huo akiwa Rais aliwakaribisha tena Ikulu viongozi wa vyama vya Siasa wakati huo Chadema wakiwa na sigana na CCM katika hali ya juu sana.

Mzee Kikwete alikuwa Rais wa Tanzania kupitia CCM. Hii gesture ya Mzee Kikwete na Chama chake wahaiwezi kupuuzwa. Nadhani tuwe fair kidogo.
 
Siku hizi nashindwa hata kuingia JF kwani kwa sasa hili jamvi letu pendwa limekuwa kama kokoro. Hata hivyo hili tukio huko kwa jirani zetu limenizindua kutoka usingizi mzito. Kuna wakati taifa letu lilikuwa la kupigiwa mfano na hata sisi wananchi wake tulitembea vifua mbele bila soni wala aibu.

Nasikitika kuwa hivi leo nasita hata kujitambulisha kama Mtanzania kwani hakuna tena cha kujivunia! Tunawindana, tunatekana, tunatesana, tunajeruhiana,tunapotezana na tumefikia hata pahala pa kuuuana, kisa? Siasa. Ole wako usiwe na kinga ya vyombo vya dola kama ulinzi na usalama.

Wakati wenzetu pamoja na mapungufu yao wanapiga hatua kusonga mbele wakibebana ndugu zao wanaposhindwa kutembea, sisi kama mbuni vichwa tumevificha mchangani. Hakuna adui wa amani na usalama kama kujiaminisha kuwa tuko bora kuliko binadamu wengine na eti kama hukubali, hama nchi!
Kenya?kuna nini?ugomvi wa rais na naibu rais?

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Ukweli mchungu! Mbinu za kikatili ndio njia pekee ya CCM kusalia makarakani!!
Tukifika 2024 utasikia watu wanavyopigwa mapanga, kutekwa, n.k.
Kumbuka watendaji wa chama wanapewa malengo ili chama kishike hatamu kwa NAMNA YOYOTE ILE; na hapo ndio mwanya wa wahuni kukodiwa ili kutimiza adhma.
Pamoja na yule katili kuwafanyia wapinzani aliyoridhia yafanyike, makada vijana ambao ni watekelezaji wa mikakati haramu wanasema 2020 chama kisingetoboa.
 
..Ssh hakuhusika. I agree with u 100%

..ila nashauri Ssh amuombee msamaha aliyehusika.

..sababu ni kwamba aliyehusika hawezi kuomba msamaha.

..Nadhani umenielewa.
JokaKuu na Pascal Mayalla

Kuna kitu kinaitwa 'conspire' halafu kingine 'accomplice''

The late Archbishop Emeritus Desmond Tutu alisema
''If you are neutral in situations of injustice , you have chosen the side of the oppressor.
If an Elephant has its foot on a tail of a mouse and you say that you are neutral, the mouse will not appreciate your neutrality ''
 
Tulipo tunahitaji kurudi katika mstari. Katika hii ''derailment'' Watanzania tunaweza kurejea

swali nani wa kutupa mweleko tofauti?

Pascal Mayalla
Mkuu Nguruvi3 , mtu huyo yupo ndiye huyu Mama!.
Angalia alivyoanza
View attachment 2062291
P
 
Chadema bado mna ndoto ya kuitwa ikulu mkanywe juice?

JK aliwadekeza mkajiona watu muhimu sana kwenye hii nchi kumbe vibaka tu watafuta fursa kujifanya mnapigania maslahi ya watu waongo wakubwa mkionyeshwa hela mnasaliti wananchi waliowaamini.
Punguza ujinga,kua mjinga hakukusaidii kwasababu hakuna tuzo kwa wajinga.Kubwa zima unawaza juice badala yakujadili hoja.Fikiria namna yakulikomboa hili taifa sio kuwaza ujinga.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Chadema bado mna ndoto ya kuitwa ikulu mkanywe juice?

JK aliwadekeza mkajiona watu muhimu sana kwenye hii nchi kumbe vibaka tu watafuta fursa kujifanya mnapigania maslahi ya watu waongo wakubwa mkionyeshwa hela mnasaliti wananchi waliowaamini.
Actually kama ukifikiria the state of the Nation sasa hivi utaona makosa tuliyoyafanya huko nyuma.
Weka vyama pembeni halafu focus kwenye maendeleo.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Tumia ignore formula, mimi hutumia thanks, usipoteze muda wako wa thamani kujibishana na hawa wavuvi wa kokoro na makorokocho yao.
P
clap.gif
 
Chadema bado mna ndoto ya kuitwa ikulu mkanywe juice? 😂😊😊

JK aliwadekeza mkajiona watu muhimu sana kwenye hii nchi kumbe vibaka tu watafuta fursa kujifanya mnapigania maslahi ya watu waongo wakubwa mkionyeshwa hela mnasaliti wananchi waliowaamini.
Nchini inapigwa mnada soon madalali wameishapewa Tenda
 
Siku hizi nashindwa hata kuingia JF kwani kwa sasa hili jamvi letu pendwa limekuwa kama kokoro. Hata hivyo hili tukio huko kwa jirani zetu limenizindua kutoka usingizi mzito. Kuna wakati taifa letu lilikuwa la kupigiwa mfano na hata sisi wananchi wake tulitembea vifua mbele bila soni wala aibu.

Nasikitika kuwa hivi leo nasita hata kujitambulisha kama Mtanzania kwani hakuna tena cha kujivunia! Tunawindana, tunatekana, tunatesana, tunajeruhiana,tunapotezana na tumefikia hata pahala pa kuuuana, kisa? Siasa. Ole wako usiwe na kinga ya vyombo vya dola kama ulinzi na usalama.

Wakati wenzetu pamoja na mapungufu yao wanapiga hatua kusonga mbele wakibebana ndugu zao wanaposhindwa kutembea, sisi kama mbuni vichwa tumevificha mchangani. Hakuna adui wa amani na usalama kama kujiaminisha kuwa tuko bora kuliko binadamu wengine na eti kama hukubali, hama nchi!
Sasa si uhamie Kenya?
Wewe mganganjaa bora ungekaa huko huko bila kurudi humu jamvini. Nilikutoa akili tangu uchaguzi 2015 kwa kuukumbatia upumbavu wa udalali walioufanya CHADEMA. uliwashambulia sana walioongea ukweli kuhusu ubaya wa udalali ule.
Leo mpo wapi?
 
Ili mwanasiasa aridhike inabidi uondoke kwenye kiti cha mamlaka umpatie yeye.

Au unatakiwa na yeye umuite mezani naye ALE.

Anyway, sasa Uhuru kaelewana na Raila Odinga, ni lini atakuja kuelewana na Miguna Miguna, na William Ruto ?
 
JokaKuu na Pascal Mayalla

Kuna kitu kinaitwa 'conspire' halafu kingine 'accomplice''

The late Archbishop Emeritus Desmond Tutu alisema
''If you are neutral in situations of injustice , you have chosen the side of the oppressor.
If an Elephant has its foot on a tail of a mouse and you say that you are neutral, the mouse will not appreciate your neutrality ''
Mkuu Nguruvi3 , kwanza nakubaliana na hoja. Ila tuko vitani na kuna mbinu nyingi za warfare ili ushinde. Ukiona unashindwa kabisa na kamwe hutaweza kumshinda adui yako, then unatumia mbinu ya mwisho ya "If you can't beat them, join them".

Sisi wengine wenu tume wa join for a very good reasons ambazo ni justified.
Nikijitolea mfano mimi mwenyewe

P
 
Ili mwanasiasa aridhike inabidi uondoke kwenye kiti cha mamlaka umpatie yeye.

Au unatakiwa na yeye umuite mezani naye ALE.

Anyway, sasa Uhuru kaelewana na Raila Odinga, ni lini atakuja kuelewana na Miguna Miguna, na William Ruto ?
Mkuu wanasiasa wetu hawafikirii vizazi vijavyo. Wanafikiria uchaguzi ujao.
Wanawaza kutawala na si kuongoza. Mleta mada ni mmoja kati ya hao
 
Mkuu wanasiasa wetu hawafikirii vizazi vijavyo. Wanafikiria uchaguzi ujao.
Wanawaza kutawala na si kuongoza. Mleta mada ni mmoja kati ya hao
Siku zote wanasiasa huwa wanajiangalia wao tu.

Na mahitaji ya wanasiasa siku zote ni tofauti na mahitaji wa wananchi.

Hata huu ujinga wa wanasiasa kujidai wanahitaji katiba mpya ni upuuzi na kupotezeana muda.

Katiba mpya na imara ni ile itakayomdhibiti mwanasiasa, na hivyo haiwezi kuketwa na mwanasiasa.

Hata sasa hivi ikitokea CDM wameshika madaraka ndani ya katiba hii hii ya 1977, SAHAU kuhusu katiba ya warioba.

Hii katiba ya 77 hakuna mwanasiasa mwenye madaraka asiyeipenda. Hakuna.

Mfano mdogo, huko CDM katiba ya chama ina kipengele chochote kinachotoa nguvu kwa wanachama dhidi ya viongozi akiwemo mwenyekiti ?

Kama hakuna, kuna tofauti gani na hii katiba ya 77?
 
Back
Top Bottom