ukoloni ndani ya uhuru wa mtanganyika.

ukoloni ndani ya uhuru wa mtanganyika.

Angyelile99

Member
Joined
Oct 9, 2023
Posts
94
Reaction score
171
mitaba ya MANGUNGO katika jina la UWEKEZAJI

1.Waarabu wa familia ya kifalme Dubai, (DP WORLD) wamepewa kuendesha bandari ya Dar es Salaam kwa mikataba ya kiduanzi unaotajwa miaka thelathini

2.Waarabu wa familia ya kifalme ya Dubai (Blue Carbon LLC) wamepewa kusimamia na kuhifadhi misitu ya Tanzania. Hii ni hekta milioni 8.1 (8% ya ardhi yote)

3.Watu wa Korea Kusini wamekabidhiwa kipande cha bahari ya Hindi na ardhi wachimbe madini nadra. Ajabu, hawa na mkopo wametoa na TUTALIPA na riba

4.Watu wa Australia (URANEX) wamepewa ardhi nzuri wachimbe madini nadra ya kimkakati na graphite Mkoa wa Lindi. Kampuni zao tatu zitauza madini nje

5.Watu wa Canada (BARRICK GOLD) wanaondoka na dhahabu. Hawajajenga hata smelters moja. Wanaacha mashimo na watu wetu kupigwa risasi nyingi.

6.Waarabu familia ya kifalme Dubai (OBC) wameongezewa ardhi 1,500km² kutoka 4,000km² zilizokuwa kwa Maasai wao wamebaki na 2,500km²

7.Watu kutoka Netherlands (SHELL) na Norway (EQUINOR) wamepewa kuchimba gesi asilia katika bahari kuu kusini, eneo la Likong’o, Lindi, Tanzania

8.Waarabu wa Dubai, Emirates National Group (ENG) wamepewa kuendesha huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART), Jiji la Dar es Salaam.

9.Watu wa France, Maurel & Prom Exploration Production (T) Ltd. (MPEP) wamenunua hisa kitalu cha uzalishaji wa gesi asilia cha Mnazi Bay, Mtwara.

10.Kandarasi ujenzi Bwawa la Nyerere (JNHPP) kapewa Egypt. Kandarasi ya ujenzi wa SGR kapewa China na Turkey. Waswahili mtapewa Kanda Bongo
 
Back
Top Bottom