super nova
JF-Expert Member
- Aug 12, 2014
- 1,479
- 1,095
Mimi ninaamini Mh Rais anastahili kuungwa mkono kwani ameonyesha kwa dhati anatetea wanyonge.
Akili ya Watanzania ni ya ajabu sana, ndiyo maana kila siku Rais anauliza hivi sisi tuna nini? Yeye hana jibu na hawa akina Mpendazoe wanaojifanya wajuaji hawana majibu!!Mpendazoe kwa umri wako hoja hii unajidhalilisha sana. Hujielewi umesimamia wapi zaidi ya kuonyesha unafiki na uchumia tumbo tuu.
Lissu ametoa hoja ambazo zilihitaji majibu na sio kusema katukana, kamtukana nani? ona hata Polisi wamechoka ndio maana wanatoa majibu kuwa NI AMRI TOKA JUU.
Hiyo kauli ukiiangalia kwa jicho la tatu ni kama kusema sisi hatuoni kosa la huyu lakini aliyeko juu ndio katoa amri.
Jambo ambalo ni kinyume na katiba na haki za kiraia. Wewe kaa kimya tuu, umejichujia na huna hoja yeyote zaidi ya njaa.
Mheshmiwa Mpendazoe, shikamoo!! Kwa sasa nitajikita katika maana ya uzalendo.
Pengine baadae nitarudi kujibu hoja zako zingine. Nimeona msingi wa hoja yako ipo kwenye neno "uzalendo" hadi umehoji uzalendo wa Tundu Lissu (TL) uko wapi.
Nijuavyo mimi uzalendo ni mapenzi ya kujitoa, kuunga mkono na kuilinda nchi yako;utii kwa taifa lako (i.e devoted love, support, and defense of one's country; national loyalty). Hapa hakuna maneno mawili "rais" na "chama cha siasa".
Kwa sababu binfasi, sababu za kisiasa, sababu za kutetea maslahi binafsi, watanzania wengi tena wengi wao ni wasomi wamekuwa wakipotosha maana ya neno "uzalendo". Wao kwenye neon "taifa" au "nchi" wanaweka neon "rais" kwenye definition ya neon uzalendo.
Mark Twain alipata kusema "patriotism is supporting your country all the time, and your government when it deserves it". Pia Edward Abbey alipata kusema "A patriot must always be ready to defend his country against his government".
Hapa utaona utofauti kati ya nini mzalendo anapaswa kutetea; Je ni serikali (including rais) au Je ni nchi/taifa?
Serikali ni watu ambao wapo wema na wabaya lakini nchi/taifa lina misingi na miiko yake ikiwemo demokrasia, utawala wa sheria, umoja, huduma bora za kijamii, amani nk. Je, anayoyafanya TL hata kuhoji uzalendo wake ana-defend nini? Unachofanya wewe Mpendazoe, JPM nk mna-defend nini?
Uzalendo ni "NDIYOOOOO" kwa kila afanyalo Rais hata kama linavunja msingi na mwiko wa taifa letu?
Uzalendo ni kuunga mkono chochote kilicho chema kwa taifa regardless kimefamywa na nani? Kinachopaswa kuungwa mkono ni MTU au KITENDO?
jibu kwanza hoja za Lisu, sio kutupa mateke kule na kule..............Hapo sasa, tena nashukuru Chademakwanza hawakuchukuwa nchi, hawa jamaa hawangekuwa madikteta, wangekuwa kama kina Museveni kama siyo kina Mugabe, wakibisha wewe angalia wanavyoendesha chama chao, kuanzia mwenyekiti wa kudumu, jinsi wanavyochaguwa wabunge wa kuteuliwa uendeshaji wa chama, mapato na matumizi n.k. n.k.
Kipande, Africa hiyo democracy ndani ya vyama ni kiini macho!! Na kama kungekuwa na hiyo democracy mtu kama Maghufuli asingekuwa Rais wa nchi hii kupitia CCM !! Kwani hakuwa na uungwaji mkono ndani ya chama. Kwa hiyo hata kwa CDM walijuwa kinachowafaa ndani ya chama na si wengi wanatakaje !! Kwa hali hiyo hoja ya Mpendazoe haina mashiko.Umeongea vizuri sana lakini jambo moja tu limeharibu uzi wako nalo ni '' USHABIKI''. yaani umepindisha maana halisi ya andiko lako ili kumtetea Lissu against Uzalendo. unapomreffer Mark Twain "patriotism is supporting your country all the time, and your government when it deserves it".
Nadhani ulielewa maana halisi ya msemo huu unless hukuelewa. alichokisema Lissu kwamba 'Nchi' inyimwe misaada, maana yake aliongelea Tanzania as country inyimwe misaada na siyo Serikali au Rais Magufuli. sasa kwa mujibu wa kauli hiyo ya Mark Twain uzalendo wa Lissu uko wapi hapo? maana he is not support his country nor the government, therefore he is not a patriotic.
Wakati mwingine tuwe waungwana kukubali pale watu wanapokosea hata kama tunawapenda au tunaunga mkono mlengo wa itikadi zao za kisiasa. vile vile, badala ya kufanya personal attack kwa mpendazoe hebu tujaribu kuzielewa hoja zake hususan demokrasia ndani ya vyama vyetu kama inaendana na kile tunachokikosoa kwa wengine.
Kipande, Africa hiyo democracy ndani ya vyama ni kiini macho!! Na kama kungekuwa na hiyo democracy mtu kama Maghufuli asingekuwa Rais wa nchi hii kupitia CCM !! Kwani hakuwa na uungwaji mkono ndani ya chama. Kwa hiyo hata kwa CDM walijuwa kinachowafaa ndani ya chama na si wengi wanatakaje !! Kwa hali hiyo hoja ya Mpendazoe haina mashiko.
Kuhusu uzalendo Tundu Lisu ni mzalendo kwa sababu hataki nchi irithishwe udikteta unaomea pole pole kupitia mikono ya JPM. Na Bahati mbaya kabisa siku hizi pro Maghufuli na government wote wanashabikia u dictator
Cairo's