Uko wapi uzalendo wa Tundu Lissu kwa Nchi yake?

Uko wapi uzalendo wa Tundu Lissu kwa Nchi yake?

Nachukua nafasi hii Kutangaza hadharani Kumdharau moja kwa moja Fred Mpendazoe kwa kipindi chake chote kilichosalia hapa duniani .

Eeee Mwenyezi Mungu nisaidie .
 
Aah Fred Mpendazoe katika ubora, sasa mngemjibu kwa hoja, Hoja inajibiwa kwa Hoja, Lissu kaongea mengi ambayo watz tulikuwa hatujui na hasa sie wa vijijini, sasa ilitakiwa 1 huko Lumumba asimame nae amjibu sasa wananchi tungewaelewa kuwa mchele ni upi na pumba ni zipi.

Lakini mkimkamata na kumuweka jela na kumnyima dhamana, hapo mnajenga chuki, mngemjibu kwa hoja kama polepole anavyojibu watu kwa hoja tunaomuelewa tunamuelewa na wasiomuelewa ndio hivyo lakini amejibu hoja, kitendo cha kumuweka ndani wananchi tutaamini kuwa yaliyosemwa na Lissu ni kweli.

Nadhani umeona kauli ya yule mwanasheria aliyekwenda jioni japo atoe dhamana aachiwe aende kwenye mkutano, lakini askari wamegoma na kusema wanasubiri maagizo kutoka kwa wakubwa.
Hoja gani zaidi ya hizo za mpendazoe, unachangia bila kusoma alichosema mleta hoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpendazoe kwa umri wako hoja hii unajidhalilisha sana. Hujielewi umesimamia wapi zaidi ya kuonyesha unafiki na uchumia tumbo tuu.

Lissu ametoa hoja ambazo zilihitaji majibu na sio kusema katukana, kamtukana nani? ona hata Polisi wamechoka ndio maana wanatoa majibu kuwa NI AMRI TOKA JUU.

Hiyo kauli ukiiangalia kwa jicho la tatu ni kama kusema sisi hatuoni kosa la huyu lakini aliyeko juu ndio katoa amri.

Jambo ambalo ni kinyume na katiba na haki za kiraia. Wewe kaa kimya tuu, umejichujia na huna hoja yeyote zaidi ya njaa.
Mpendazoe ni sawa na kunguru , haiwezekani kumfuga , Huyu alishindwa kura za maoni lakini chama kikamsitiri kwa kumbeba ili kumfichia aibu , lakini hizi ndio shukrani zake !
 
Umeongea vizuri sana lakini jambo moja tu limeharibu uzi wako nalo ni '' USHABIKI''. yaani umepindisha maana halisi ya andiko lako ili kumtetea Lissu against Uzalendo. unapomreffer Mark Twain "patriotism is supporting your country all the time, and your government when it deserves it".

Nadhani ulielewa maana halisi ya msemo huu unless hukuelewa. alichokisema Lissu kwamba 'Nchi' inyimwe misaada, maana yake aliongelea Tanzania as country inyimwe misaada na siyo Serikali au Rais Magufuli. sasa kwa mujibu wa kauli hiyo ya Mark Twain uzalendo wa Lissu uko wapi hapo? maana he is not support his country nor the government, therefore he is not a patriotic.

Wakati mwingine tuwe waungwana kukubali pale watu wanapokosea hata kama tunawapenda au tunaunga mkono mlengo wa itikadi zao za kisiasa. vile vile, badala ya kufanya personal attack kwa mpendazoe hebu tujaribu kuzielewa hoja zake hususan demokrasia ndani ya vyama vyetu kama inaendana na kile tunachokikosoa kwa wengine.

Kama huoni kuwa hoja za Lissu zinalenga ku support nchi, basi hata kujadili uzi huu utakuwa unapoteza muda wako bure. Kama misaada inayotolewa na hizo nchi inatumika kugandamiza wengine, kwanini misaada hiyo ije?

Lissu anapokemea uvunjwaji wa katiba na ugandamizaji wa wazi wazi ana support nchi, hamsapoti mtu. Ila wewe na Mpendazoe mnaposhangilia Rais aanaposigina katiba hamuisapoti nchi mnamsapoti mtu.

Ni upumbavu kujadili demokrasia ya ndani ya vyama kama kinga ya kujadili usiginaji wa katiba ya nchi unaofanyika sasa. Na ni upumbavu zaidi kutumia kigezo cha Lowasa kupewa nafasi ya kugombea urais kuhalalisha vitendo vya wazi vya ukiukwaji wa katiba vinavyofanyika leo.
 
Fred, uzalendo wa Lissu uko wazi sana lakini si wote wanaweza kuuona au kuutambua, sharti uwe na siha nzuri ya ubongo ndipo uuone.

Je hujaona?
 
Pole sana mpendazoe. Mkia umeshaota tayari? Vipi zile kauli kali za mkulu za kuhusu wapinzani na kuwazuia kabisa kufanya mikutano je zenyewe hazihatarishi amani ya nchi? Vipi ulimsikia anko Ben na matusi yake ya wapinzani ni wapumbavu?

Angetamka lisu au mpinzani yeyote kuwa ccm ni wapumbavu Si siku hiyo hiyo angeswekwa lupango! Any way nina halina kabisa alichoandika unajua kabisa kuwa ni unafiki tu na Pasi na shaka nafahamu kabisa kuwa nawe unajua demokrasia Tanzania inaelekea kwa kasi kwenye korongo ila tu unajitoa ufahamu makusudi kabisa.

Subiri teuzi za udc huenda ukakumbukwa.
Usimfananishe mkapa na lisu mkapa anakinga lisu anayokinga au anatafuta kiki kwa pikipiki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fred Mpendazoe
Je wale Wajerumani walio jaribu kumua Dikteta/Fashist Reich Fuhrer Adolf Hitler kwenye usiku wa Kristalnitch' kabla ya kuanza vita kuu ya pili iliyosababisha raia wake million sita kufa walikuwa wazalendo wa nchi yao au la?

Unajifunza kitu hapo?
BTW huna sifa ya kuteuliwa wadhifa wowote na Magu,sorry to say that but it's the bitter truth

Tafuta vingine vya kulaumu mtaji wako wa pekee wa Lowassa ume expire
 
Kiongozi anatumia kejeri, lugha ya kudharilisha! unategemea ninimtu anashikiliwa na polisi sio kisheria Ila maagizo toka juu, tungejuu utanganyika wako halisi ili ueleweke, jamaàa wakili msomi hawezi kuwa ma fikra kama zako
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mheshmiwa Mpendazoe, shikamoo!! Kwa sasa nitajikita katika maana ya uzalendo.

Pengine baadae nitarudi kujibu hoja zako zingine. Nimeona msingi wa hoja yako ipo kwenye neno "uzalendo" hadi umehoji uzalendo wa Tundu Lissu (TL) uko wapi.

Nijuavyo mimi uzalendo ni mapenzi ya kujitoa, kuunga mkono na kuilinda nchi yako;utii kwa taifa lako (i.e devoted love, support, and defense of one's country; national loyalty). Hapa hakuna maneno mawili "rais" na "chama cha siasa".

Kwa sababu binfasi, sababu za kisiasa, sababu za kutetea maslahi binafsi, watanzania wengi tena wengi wao ni wasomi wamekuwa wakipotosha maana ya neno "uzalendo". Wao kwenye neon "taifa" au "nchi" wanaweka neon "rais" kwenye definition ya neon uzalendo.

Mark Twain alipata kusema "patriotism is supporting your country all the time, and your government when it deserves it". Pia Edward Abbey alipata kusema "A patriot must always be ready to defend his country against his government".

Hapa utaona utofauti kati ya nini mzalendo anapaswa kutetea; Je ni serikali (including rais) au Je ni nchi/taifa?

Serikali ni watu ambao wapo wema na wabaya lakini nchi/taifa lina misingi na miiko yake ikiwemo demokrasia, utawala wa sheria, umoja, huduma bora za kijamii, amani nk. Je, anayoyafanya TL hata kuhoji uzalendo wake ana-defend nini? Unachofanya wewe Mpendazoe, JPM nk mna-defend nini?

Uzalendo ni "NDIYOOOOO" kwa kila afanyalo Rais hata kama linavunja msingi na mwiko wa taifa letu?

Uzalendo ni kuunga mkono chochote kilicho chema kwa taifa regardless kimefamywa na nani? Kinachopaswa kuungwa mkono ni MTU au KITENDO?

Dah! Nashukuru kwa elimu mkuu...
 
Nilisikiliza hotuba ya Mh Tundu Lissu aliyoitoa huko jimboni kwake akimshambulia Mh Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania JPM kwamba ni dikteta uchwara, ni mkabila na anaendesha nchi kwa upendeleo.

Ameomba Jumuiya ya Kimataifa iinyime misaada Tanzania na waizomee Tanzania kutokana na uongozi mbaya wa JPM unaogandamiza demokrasia nchini. Mh.Tundu Lissu alionyesha hasira na dharau kubwa kwa Rais wakati akitoa hotuba hiyo.

Kwanza nianze na masuali ya jumla :

Mimi ninajiuliza, je Mh Lissu na viongozi wengine wa upinzani hawawezi kabisa kuikosoa Serikali bila kutumia matusi na kejeli ? Je hawawezi kabisa kutoa maoni yao bila kutoa matusi na kejeli kwa viongozi waliopo madarakani?

Pamoja na Elimu aliyonayo Mh Tundu Lissu haelewi kwamba Mh John P Magufuli amechaguliwa na wa Tanzania na ni kiongozi wa Nchi na lugha anayoitumia dhidi yake inalidhalilisha Taifa ?

Naomba nitazame hoja za Mh Lissu.

1. Madai kuhusu demokrasia kuminywa na haki na Uhuru wa kutoa maoni. Wakati Mh Lissu anadai haya kwa Serikali iliyopo madarakani angewatetea wanachadema kuhusu haki na Uhuru wa kutoa maoni na demokrasia ndani ya Chadema. Mfano Lowassa alishindanishwa na nani wakati wa kugombea urais 2015.

Sikumsikia Mh Lissu akimuijia juu Mbowe wakati alipobadilisha gia angani. Wengi watakumbuka uchaguzi wa viongozi wa jumuia za Chama ndani ya Chadema ulivyokuwa umegubigwa na ubabe kwa kisingizio cha maslahi mapana ya Chama. Mh Lissu alikaa kimya.

Dk Slaa aliondolewa kwenye kugombea urais ndani ya Chadema kibabe, Mh Lissu alitetea ujio wa Lowassa. Mh Lissu na Chadema haiwezi ikawa msemaji wa kudai demokrasia nchini wakati ndani ya Chadema kuna udikiteta ulipitiliza.

2. Kuhusu haki na Uhuru wa kutoa maoni. Uhuru na haki hiyo haijazuiwa isipokuwa lipo tatizo kubwa upande wa Lissu na wengine kwenye upinzani. Wakijenga hoja na kutoa maoni yao bila matusi sidhani kama watakatazwa.

Hakuna jambo linalokera na kuudhi kama lugha zinazotumiwa Mh Lissu na baadhi ya wapinzani. Watambue pia kama wao walivyo na haki ya kutoa maoni pia Rais nae ana haki zake kama kiongozi wa Nchi. Haikubaliki mtu atumie lugha ya kejeli, dharau, na matusi kwa Rais na kiongozi wa Nchi kwa kisingizio cha haki na Uhuru wa kutoa maoni. Hapana.

3. Lissu amezungumzia suala la ukabila na upendeleo wa kiukoo. Inasikitisha na ni hatari sana kwa kuanza kuleta hoja za ukabila na ukoo au undugu au udini. Ni kweli JPM analo Kabila lake, ukoo wake wa kuzaliwa na dini yake. Lakini JPM kama Rais, ni baba wa Tanzania wote.

Na koo zote ni zake, watumishi wote ni wake, na wanajeshi wote ni wake. Hivyo, Mh Rais anayo haki ya kumchagua yeyote katika nafasi yoyote anayemwona ataweza kumsaidia katika kutekeleza majukumu yake bila kujali alikotoka au dini au kabila au ukoo au hata Chama.

Hivyo, hoja alizozitoa Mh Lissu kuhusu ukabila au ukanda ni matatizo yake ya kifikra. Wengine hawaoni kama anavyoona yeye Mh Lissu. Mh Lissu ndiye mwenye ukabila, udini, na ukanda. Watanzania wengi wameondokana na fikra hasi alizonazo Mh Lissu. Inawezekana, hoja za ukabila, ukanda, udini na ukoo bado zipo Chadema.

4. Mh Lissu ameiomba Jumuiya ya Kimataifa iinyime misaada Tanzania. Ni jambo La kushangaza kweli! Moja ya viongozi wanaozungumzwa duniani kuhusu uongozi bora ni Rais JPM. Jitihada za Rais JPM katika kupiga vita rushwa na ufisadi zinaonyesha matunda.

Kama Chadema ilikuwa imedhamiria kweli kupiga vita rushwa na ufisadi inatakiwa imuunge mkono Rais JPM. Lakini cha kushagaza kabisa Mh Lissu kuhusu suala la ufisadi amekuwa kimya tangu Chadema wampokee Lowassa. Mh Lissu tangu wakati huo alibadilika.Mh Lissu aligeka jiwe.

Mh JPM anapigania kwa dhati utajiri wa Nchi yetu ili uweze kuwanufaisha watanzania wote. Mh Lissu na hili limemkera mpaka anaombea Tanzania ishitakiwe na makampuni yanayochimba madini nchini !

Mh Rais JPM anapambana kwa dhati na uzembe na ubadhirifu kwenye mashirika ya umma na Serikali, Mh Lissu na hili linamkera kwani alishasema atawatetea wale wote wanaotumbuliwa ! Very sad. Kwa juhudi hizi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya 5 bado Mh Lissu anashawishi nchi na Jumuiya ya Kimataifa ziisusie Tanzania na kuinyima misaada! Inasikitisha sana.

Uko wapi Uzalendo wa Mh Lissu kwa Nchi yake ?
Mimi ninaamini Mh Rais anastahili kuungwa mkono kwani ameonyesha kwa dhati anatetea wanyonge.

Sent using Jamii Forums mobile app
Fred, Ukowapi Uzalendo wako kwa Nchi yako? Kumbuka, uzalendo siyo kupiga makofi tu, kuchanganua hoja nao ni uzalendo.
 
Ng'ombe uliyekatwa mkia, Wewe si ulikatwa mkia, Mamluki mkuu wewe, Nenda kalambe viatu utapewa ukatibu kata, madeni umemaliza au bado interest inaongezeka
 
Ukiweka unachosema kuwa ni lugha za matusi na kuudhi,kuna ukweli katika alichosema LISU
 
Haya unayomsema nayo Lissu, ndio hayo uliyokuwa unayasema kwenye kampeni zako za kugombea ubunge jimbo la Segerea kwa tiketi ya Chadema, ukapigwa bao na sisiemu.. Wewe ni mnafiki wa kiwango cha makanikia..
Msukuma wa mbogwe. Njaa kali
 
Back
Top Bottom