Uko wapi uzalendo wa Tundu Lissu kwa Nchi yake?

Uko wapi uzalendo wa Tundu Lissu kwa Nchi yake?

Akili imekopeshwa sehemu japo ni Dr akili

Sent using Jamii Forums mobile app
Wazungu wanasema "Tit for tat", waswahili husema "Dawa ya moto ni moto". Sasa kosa liko wapi? Kamtukana mkuu wa nchi, cha moto kakipata. What did he expect? Kupongezwa?Tujifunze kuutumia uhuru wetu wa kutoa mawazo yetu (freedom of expression) vizuri. Uhuru huu unaishia pale pua ya mwenzako inaanzia. Kwenda kinyume na hapo utajikuta kila wakati uko kokoroni.
 
Fred Mpendazoe anatafuta uDC au uDED kwa nguvu. Huyu mchumia tumbo kaanza kuyaona haya baada ya kukosa Ubunge mara mbili na baada ya kuhama chama tena. Kigeugeu na ndumilakuwili mkubwa. Bahati nzuri watu kama Fred Magufuli huwa hana time now. Wamehasiwa na ni tasa. Useless opportunists.

Tusi alilotoa Lissu ni lipi? Anayoyaongea JPM, Ndugai na Mkapa majukwaani yenyewe Fred huwa hayasikii?
 
Halafu itasaidia nini?
Itamfanya awe na tabia njema ya kuheshimu wakuu wa nchi. Maana kawasema vibaya marais Kagame, Nkurunzinza, Museveni, Kabila na Magufuli. Alishawahi kimsema vibaya sana baba wa taifa letu Mwl Nyerere hasa wakati ule wa mchakato wa katiba mpya.
 
mbona tumeitwa wapumbavu na malofa kuna kipi kimefanyika, tena watz wote milioni 52, kafanywa nini, kuna mtu alimuonya, na mbaya zaidi akarudia juzi kusema, nani kamfata, yeye alilotukana ni lipi, mie sijaona, haya mshamkamata mumule nyama,
Walioitwa wapumbafu ni wale wanaozani nchi hii haijawahi kukombolewa na kwamba wanataka wao (wapumbafu) waikomboe. Nchi hii ilikombolewa na akina Mwl Nyerere na Karume.. Sasa hawa wengine ulitaka tuwaiteje kama si malofa na wapumbavu? Si kila mtanzania aliitwa hivyo, usitake kupotosha. Ni hicho kikundi kidogo chenye mawazo ya kuikomboa Tanzania.
 
Fred Mpendazoe, post: 22381796, member: 382107"]Mimi ninajiuliza, viongozi wengine wa upinzani hawawezi kuikosoa Serikali bila kutumia matusi na kejeli ? Je hawawezi kutoa maoni bila kutoa matusi na kejeli kwa viongozi waliopo madarakani?
Hakuna kinachoitwa heshima kwa'flani,kipo kinachoitwa heshima kwa wote
Madaraka hayatoi haki ya heshima zaidi ya mkulima, mwanafunzi au kindergarten
Heshima ni 'two way traffic' unatoa kama unavyopokea, haombwi inajijenga kwa mhusika

Watanzania wanapoitwa malofa/Wapumbavu kwasababu ya maoni tofauti si heshima
Unategemea anayesema hayo atapata wapi heshima ikiwa yeye mwenyewe hakuchunga ulimi kujenga heshima
1. Madai kuhusu demokrasia kuminywa na haki na Uhuru wa kutoa maoni.Wakati Mh Lissu anadai haya kwa Serikali iliyopo madarakani angewatetea wanachadema kuhusu haki na Uhuru wa kutoa maoni na demokrasia ndani ya Chadema. Mfano Lowassa alishindanishwa na nani wakati wa kugombea urais 2015.
Unaweza kuwa sahihi kwa mtazamo wa uchama, hupo sahihi kwa mtazamo wa sheria na katiba

Demokrasia inayoongelewa ipo ndani ya katiba ya Tanzania, si ya Chadema au CCM
Je kama Taifa tunapata kile tulichokubaliana ndani ya katiba?
Wengi watakumbuka uchaguzi wa viongozi wa jumuia za Chama ndani ya Chadema ulivyokuwa umegubigwa na ubabe kwa kisingizio cha maslahi mapana ya Chama. Mh Lissu alikaa kimya.
Hayo ni mambo na matatizo yao, siasa za vyama si mwongozo wa nchi.

Lini utajenga hoja za utaifa kwa kulingana na wasifu wako?
Hili si jukwaa la Chadema au CCM wala si eneo la kutafuta 'kick'

Tuongee kama wananchi, vyama si nchi.
Nchi ni watu na ipo kabla ya vyama. Hoja yako ina mantiki gani!
Dk Slaa aliondolewa kwenye kugombea urais ndani ya Chadema kibabe, Mh Lissu alitetea ujio wa Lowassa. Mh Lissu na Chadema haiwezi ikawa msemaji wa kudai demokrasia nchini wakati ndani ya Chadema kuna udikiteta ulipitiliza.
Hili ni matatizo ya vyama vyao, hayatuhusu. Kinachotuhusu ni nchi na sheria
Mrema ni mwenyekiti wa maisha, haituhusu. CUF wanalumbana haituhusu.
Ukigusa Tanzania tutakwambia jitazame kama unachoandika kinanamtiki japo chembe
2. Kuhusu haki na Uhuru wa kutoa maoni. Uhuru na haki hiyo haijazuiwa isipokuwa lipo tatizo kubwa upande wa Lissu na wengine kwenye upinzani
Hudhani kama watakatazwa!Mikutano ilipigwa marufuku si kwasababu ya Matusi
Kama 'unadhani' ni maoni yako Kuyafanya ni facts unajidanganya!
Hakuna jambo linalokera na kuudhi kama lugha zinazotumiw na wapinzani.kama wao walivyo na haki ya kutoa maoni pia Rais nae ana haki zake kama kiongozi wa Nchi. Haikubaliki mtu atumie lugha ya kejeli, dharau, na matusi kwa Rais na kiongozi wa Nchi kwa kisingizio cha haki na Uhuru wa kutoa maoni. Hapana.
Wewe si sheria, kama hutaki tumia mkondo wa sheria kuwafikisha mbele ya sheria. Period
3. Lissu amezungumzia suala la ukabila na upendeleo wa kiukoo. Inasikitisha na ni hatari sana kwa kuanza kuleta hoja za ukabila na ukoo au undugu au udini. Ni kweli JPM analo Kabila lake, ukoo wake wa kuzaliwa na dini yake. Lakini JPM kama Rais, ni baba wa Tanzania wote.
Ni maoni yako kama yalivyo ya wengine siyo facts. wala hayanyana uzito kuliko ya wengine.
Kwa milioni 45 tegemea maoni tofauti. Muhimu ni je maoni hayo yanavunja sheria?
Hivyo, hoja alizozitoa Mh Lissu kuhusu ukabila au ukanda ni matatizo yake ya kifikra. Wengine hawaoni kama anavyoona yeye Mh Lissu. Mh Lissu ndiye mwenye ukabila, udini, na ukanda. Watanzania wengi wameondokana na fikra hasi alizonazo Mh Lissu. Inawezekana, hoja za ukabila, ukanda, udini na ukoo bado zipo Chadema.
Again, unaongelea suala la kitaifa kwa jicho la uchama.
Haya ni mawazo dhaifu kwa mtu mwenye elimu!
4. Mh Lissu ameiomba Jumuiya ya Kimataifa iinyime misaada Tanzania. Moja ya viongozi wanaozungumzwa duniani kuhusu uongozi bora ni Rais JPM.
Tupe facts, kama anazungumzwa tupe takwimu. Huwezi kuwa na hisia zako ukazifanya ni facts za 'duniani'.
Kama Chadema ilikuwa imedhamiria kweli kupiga vita rushwa na ufisadi inatakiwa imuunge mkono Rais JPM. Lakini cha kushagaza kabisa Mh Lissu kuhusu suala la ufisadi amekuwa kimya tangu Chadema wampokee Lowassa.
Mh Lissu tangu wakati huo alibadilika.Mh Lissu aligeka jiwe.
Vita ya rushwa, ufisadi n.k. ni masuala ya kitaifa

Ni hoja ya kitaifa kwa bahati mbaya watu kama wewe mnaipunguza nguvu kwa kuipa jicho la uchama. Hili si suala la CCM au Chadema, sijui kama unajua hilo!

Tafadhali acha kuangalia Taifa kwa mboni ya uchama.
Umerudi CCM kwa masilahi yako, tunaheshimu. Utaifa wetu hauna uhusiano hilo.
Elimu haikupi nafasi kujali hoja kwa kiwango hiki!
Uko wapi Uzalendo wa Mh Lissu kwa Nchi yake ?Mimi ninaamini Mh Rais anastahili kuungwa mkono kwani ameonyesha kwa dhati anatetea wanyonge.
Uko wapi uzalendo wa wale waliotia saini mikataba hiyo!

Upo wapi uzalendo wa wale walioruhusu mchanga kuibiwa miaka 16.
Upo wapi uzalendo kwa wale walioita wabunge tumbili.
Upo wapi uzalendo kwa wale waliopitisha miswada ya dharura kwa ndiyoooo.
Upo wapi uzalendo kwa wale waliouza rasilimali za nchi kinyume na sheria

Mh Rais anastahili kuungwa mkono na Watanzania wote.
Wanaomkwaza ni kama Mpendazoe wanoligawa taifa kwa misingi ya uchama.
Kila jambo linaangaliwa kwa mboni ya uchama.

Watu wasioweza ku articulate hoja bali kulinganisha pumba na mashudu
Kwamba Chadema walifanya fyongo ni haki yao kuboronga! Pathetic

Hawa ndio tatizo kwa jitihada za Mh Rais, mitazamo yao kifikra ipo matumboni si vichwani
 
Nilisikiliza hotuba ya Mh Tundu Lissu aliyoitoa huko jimboni kwake akimshambulia Mh Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania JPM kwamba ni dikteta uchwara, ni mkabila na anaendesha nchi kwa upendeleo.

Ameomba Jumuiya ya Kimataifa iinyime misaada Tanzania na waizomee Tanzania kutokana na uongozi mbaya wa JPM unaogandamiza demokrasia nchini. Mh.Tundu Lissu alionyesha hasira na dharau kubwa kwa Rais wakati akitoa hotuba hiyo.

Kwanza nianze na masuali ya jumla :

Mimi ninajiuliza, je Mh Lissu na viongozi wengine wa upinzani hawawezi kabisa kuikosoa Serikali bila kutumia matusi na kejeli ? Je hawawezi kabisa kutoa maoni yao bila kutoa matusi na kejeli kwa viongozi waliopo madarakani?

Pamoja na Elimu aliyonayo Mh Tundu Lissu haelewi kwamba Mh John P Magufuli amechaguliwa na wa Tanzania na ni kiongozi wa Nchi na lugha anayoitumia dhidi yake inalidhalilisha Taifa ?

Naomba nitazame hoja za Mh Lissu.

1. Madai kuhusu demokrasia kuminywa na haki na Uhuru wa kutoa maoni. Wakati Mh Lissu anadai haya kwa Serikali iliyopo madarakani angewatetea wanachadema kuhusu haki na Uhuru wa kutoa maoni na demokrasia ndani ya Chadema. Mfano Lowassa alishindanishwa na nani wakati wa kugombea urais 2015.

Sikumsikia Mh Lissu akimuijia juu Mbowe wakati alipobadilisha gia angani. Wengi watakumbuka uchaguzi wa viongozi wa jumuia za Chama ndani ya Chadema ulivyokuwa umegubigwa na ubabe kwa kisingizio cha maslahi mapana ya Chama. Mh Lissu alikaa kimya.

Dk Slaa aliondolewa kwenye kugombea urais ndani ya Chadema kibabe, Mh Lissu alitetea ujio wa Lowassa. Mh Lissu na Chadema haiwezi ikawa msemaji wa kudai demokrasia nchini wakati ndani ya Chadema kuna udikiteta ulipitiliza.

2. Kuhusu haki na Uhuru wa kutoa maoni. Uhuru na haki hiyo haijazuiwa isipokuwa lipo tatizo kubwa upande wa Lissu na wengine kwenye upinzani. Wakijenga hoja na kutoa maoni yao bila matusi sidhani kama watakatazwa.

Hakuna jambo linalokera na kuudhi kama lugha zinazotumiwa Mh Lissu na baadhi ya wapinzani. Watambue pia kama wao walivyo na haki ya kutoa maoni pia Rais nae ana haki zake kama kiongozi wa Nchi. Haikubaliki mtu atumie lugha ya kejeli, dharau, na matusi kwa Rais na kiongozi wa Nchi kwa kisingizio cha haki na Uhuru wa kutoa maoni. Hapana.

3. Lissu amezungumzia suala la ukabila na upendeleo wa kiukoo. Inasikitisha na ni hatari sana kwa kuanza kuleta hoja za ukabila na ukoo au undugu au udini. Ni kweli JPM analo Kabila lake, ukoo wake wa kuzaliwa na dini yake. Lakini JPM kama Rais, ni baba wa Tanzania wote.

Na koo zote ni zake, watumishi wote ni wake, na wanajeshi wote ni wake. Hivyo, Mh Rais anayo haki ya kumchagua yeyote katika nafasi yoyote anayemwona ataweza kumsaidia katika kutekeleza majukumu yake bila kujali alikotoka au dini au kabila au ukoo au hata Chama.

Hivyo, hoja alizozitoa Mh Lissu kuhusu ukabila au ukanda ni matatizo yake ya kifikra. Wengine hawaoni kama anavyoona yeye Mh Lissu. Mh Lissu ndiye mwenye ukabila, udini, na ukanda. Watanzania wengi wameondokana na fikra hasi alizonazo Mh Lissu. Inawezekana, hoja za ukabila, ukanda, udini na ukoo bado zipo Chadema.

4. Mh Lissu ameiomba Jumuiya ya Kimataifa iinyime misaada Tanzania. Ni jambo La kushangaza kweli! Moja ya viongozi wanaozungumzwa duniani kuhusu uongozi bora ni Rais JPM. Jitihada za Rais JPM katika kupiga vita rushwa na ufisadi zinaonyesha matunda.

Kama Chadema ilikuwa imedhamiria kweli kupiga vita rushwa na ufisadi inatakiwa imuunge mkono Rais JPM. Lakini cha kushagaza kabisa Mh Lissu kuhusu suala la ufisadi amekuwa kimya tangu Chadema wampokee Lowassa. Mh Lissu tangu wakati huo alibadilika.Mh Lissu aligeka jiwe.

Mh JPM anapigania kwa dhati utajiri wa Nchi yetu ili uweze kuwanufaisha watanzania wote. Mh Lissu na hili limemkera mpaka anaombea Tanzania ishitakiwe na makampuni yanayochimba madini nchini !

Mh Rais JPM anapambana kwa dhati na uzembe na ubadhirifu kwenye mashirika ya umma na Serikali, Mh Lissu na hili linamkera kwani alishasema atawatetea wale wote wanaotumbuliwa ! Very sad. Kwa juhudi hizi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya 5 bado Mh Lissu anashawishi nchi na Jumuiya ya Kimataifa ziisusie Tanzania na kuinyima misaada! Inasikitisha sana.

Uko wapi Uzalendo wa Mh Lissu kwa Nchi yake ?
Mimi ninaamini Mh Rais anastahili kuungwa mkono kwani ameonyesha kwa dhati anatetea wanyonge.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yan watu wengine huwa mnaamka mkiwashwa kutaka tu mtukanwe? si heri uendelee kulala na mkeo kuliko huu upuuzi uliopoteza muda kuandika?
 
Nilikuwa namsikiaga tu huyu jamaa kumbe yasemwayo ni kweli!
 
Mi huwa sisomagi watu kama nyie mkiandika najua utaandika pumba tu sasana utaishia kusifu tu Leo hii anayeonekana mzalendo niyule anyemsifia Mkuu tu lakini ukiwa tofauti na Mkuu au ukisema ukweli tu juu ya jambo flani unaonekana wewe hufai,mchochezi na unaatarisha amani ya nchi enyi watanzani ebu acheni unafki alichokisema lisu ambacho sio chakweli nikipi?
 
Itamfanya awe na tabia njema ya kuheshimu wakuu wa nchi. Maana kawasema vibaya marais Kagame, Nkurunzinza, Museveni, Kabila na Magufuli. Alishawahi kimsema vibaya sana baba wa taifa letu Mwl Nyerere hasa wakati ule wa mchakato wa katiba mpya.
Kwani kiongozi kusemwa vibaya ni tatizo? Bush hakusemwa vibaya tu bali alirushiwa mpaka kiatu kwenye press conference! Kiongozi kusemwa vibaya ni jambo la kawaida sana. Anasemwa Papa sembuse akina Nkuruzinza? Kuwa kiongozi, tena wa kuchaguliwa na wananchi, haina maana kuwa unageuka malaika ghafla. Bado ni binadamu na usitarajie kuwa kila unalolisema au kulitenda litafurahisha wote. Lissu anasimama kukusaidia hata wewe pamoja na ndugu zako indirectly!
 
Haya tusubiri maamuzi ya mahakama kwani ndizo zitasema kama hayo aliyowasema Lissu hao viongozi hayana ubaya wo wote. Ndiyo maana Lissu kafikishwa kwenye mkondo wa sheria kabla hajafika huko Kigali alikokuwa akienda baada ya kumsema vibaya rais wa Kigali. Yangeweza kumpata mabaya zaidi huko Kigali maana wao hawana muda wa kupoteza kushughulikia uchizi!!

Hivyo vuta subira tu ndugu yangu. Jibu litatoka mahakamani kama tunaruhusiwa kisheria kuwasema vibaya viongozi hawa kwa namna ambavyo Lissu kawasema. Itakuwa poa kama tunaruhusiwa kwani kila mmoja sasa atawasema ile mbaya kupitia mi press conference, mitandao ya jamii, kwenye nyumba za ibada na kila mahali. Au unafikiri ruhusa hiyo itatolewa kwa Tundu Lissu peke yake? Usidanganyike.
 
Mtanzania mzalendo soma hoja aliyotoa Fred Mpedazoe (Patriotic one) kuhusu -uko wapi uzalendo wa Lissu??? Sina haja ya kusema mzakendo mwenzangu kamaliza. All the best Fred

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya tusubiri maamuzi ya mahakama kwani ndizo zitasema kama hayo aliyowasema Lissu hao viongozi hayana ubaya wo wote. Ndiyo maana Lissu kafikishwa kwenye mkondo wa sheria kabla hajafika huko Kigali alikokuwa akienda baada ya kumsema vibaya rais wa Kigali. Yangeweza kumpata mabaya zaidi huko Kigali maana wao hawana muda wa kupoteza kushughulikia uchizi!!

Hivyo vuta subira tu ndugu yangu. Jibu litatoka mahakamani kama tunaruhusiwa kisheria kuwasema vibaya viongozi hawa kwa namna ambavyo Lissu kawasema. Itakuwa poa kama tunaruhusiwa kwani kila mmoja sasa atawasema ile mbaya kupitia mi press conference, mitandao ya jamii, kwenye nyumba za ibada na kila mahali. Au unafikiri ruhusa hiyo itatolewa kwa Tundu Lissu peke yake? Usidanganyike.
Hata huna hoja. Kwa hiyo kama Rwanda hawana muda wa kupoteza kushughulikia uchizi, nyie ndio huo muda mnao? Nani alikwambia kumsema vibaya kiongozi ni kosa la jinai? Nenda kawaulize polisi ni kosa gani wanamtuhumu nalo TL ndipo urudi kwenye huu mjadala!
 
Mbona ndugu yangu bado unarudia swali hilo hilo la kumsema vibaya kiongozi kama ni kosa au si kosa la jinai. Nimekujibu kwamba jibu la swala lako hilo litatolewa na mahakama ambako Lissu atapelekwa hivi punde.

Halafu polisi hawawajibiki kukueleza wewe au mimi sababu za kumshikilia Lissu au mtu yo yote mwingine. Polisi wanawajibika kutoa sababu hizo kwa mahakama watakompeleka, na si kwako wala mwingine ye yote. Hivyo subiri utazisikia atakapofikishwa kwa Pilato. Haraka ya nini? Kwani Tundu ndiyo mtu wa kwanza kukamatwa na polisi?
 
Back
Top Bottom